Haya katika Mfumo wa Maadili ya Ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Haya katika Mfumo wa Maadili ya Kiislamu

Question

 Nini mafasi ya maadili ya kuona Haya katika mfumo wa Maadili ya Kiislamu?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Dini imekuja na ikahimiza kuwa na haya kwa kuzingatia kuwa ni katika maadili mema yanayosemwa vizuri ngazi ya Mtu mmoja mmoja na ngazi ya jamii nzima mpaka ikawa ni kawaida kumsema mtu vibaya kwa kumwambia ni (mchache wa Hayaa) katika matumizi ya kila siku pamoja na kuondosha Hamza katika neno la kiarabu la Hayaa badala ya Hayaau kwa sababu waarabu hupunguza herufi katika kila neno lenye Mada mwishoni sio lazima kulivuta kila neno lililofupishwa.
Na katika Hadithi ya Mtume S.A.W: pale mtu mmoja alipomkalipia nduguye kwa kuwa na Hayaa nyingi, Mtume S.A.W, akamwambia: "Hayaa yote ni Kheri" . Na akasema: "Hakika maneno waliyoyapata watu kutoka katika Utume wa Awali, kama hukuwa na haya basi fanya utakavyo" .
Na Hayaa ilikuwa inazalisha utamaduni wenye kutawala unaozuia kwenda kombo kimaadili na kudhibiti utendaji wa matendo ngazi ya Mtu na ngazi ya Jamii, na ukosefu wa Hayaa unatupeleka kwenye ukosefu wa Kigezo kinachonyoosha maadili na kukubali au kukataa na kile ambacho kinahitaji maboresho na makatazo. Na kukikosa Kigezo hiki kunapelekea katika hali inayofanana na machafuko, nayo ni hali ambayo kama iliendelea mtu haifikii mwisho wake na Jamii ya Kibinadamu itapotea na Mwishowe kuanguka kwa staarabu kwa kuwa hakuna udhibiti wala mfungamano.
1- Na kwa ajili hiyo, na miongoni mwa Ibara zilizoenea nayo ni Kauli yao yenye makosa: (Hakuna Hayaa katika Dini) na wanakusudia kwamba mtu anapaswa kuulizia chochote bila aibu yoyote inayomzuia kujifunza, basi asione aibu kwa kutojua kwake na wala asione aibu kwa anapotaka kujua kitu chochote katika nyanja zote za maisha, hakuna mipaka ya kutafuta elimu. Na sentensi sahihi Iliyovurugwa kutoka katika asili yake na kuwa sentensi hii mpya yenye makosa, ni: (Hakuna uzito -msimbulio- katika Dini). Na kuna tofauti kubwa sana baina ya sentensi mbili. Na iliyo sahihi ni hii isemayo kwamba hakuna uzito (msimbulio) katika Dini, Hakika wepesi unaushinda Ugumu, na mtu yeyote atakayeitekeleza Dini basi hatapata ugumu wowote au Unyanyasaji basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi. Hakika pamoja na uzito upo wepesi}. [AS SHARH 5,6]
2- Na katika Hadithi ya Mtume S.A.W: Hakika hakuwahi kuchagulishwa baina ya mambo mawili isipokuwa huchukua lililo jepesi . Na Msingi Mama wa Kifiqhi unasema: "Mazito huleta wepesi" Kwa hiyo Uwepesishaji ni Asili katika Dini. Na hukusanya upole katika mtangamano. Anasema Mtume S.A.W: "Hakika Upole hauwi katika kitu isipokuwa hukipendezesha, na hauondolewi katika kitu isipokuwa hukifanya kichukize" . Na Urahisishaji unakusanya pia Huruma. Anasema Mtume S.A.W: "Wenye Huruma Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka anawahurumia, wahurumieni walio ardhini
watakuhurumieni Walio Mbinguni" . Na hukusanya pia uondoshaji wa madhara, ambapo anasema Mtume S.A.W: "Hakuna Kudhurika au kuleta madhara" . Na hukusanya pia Uendelevu wa Kazi. Na katika Hadithi ya Mtume S.A.W: Matendo ya Mtume S.A.W, yalikuwa ni ya kudumu.
Na Hayaa ni Maadili yanayomzuia mtu mwenye nayo machafu katika kauli na katika vitendo na kwa hiyo hakika mambo yalivyo hii ni kinyume cha baadhi ya maana za uwazi zitamkwazo zinazolinganiwa na baadhi katika zama zetu hizi. Na uwazi unaweza kumaanisha ukweli wa maneno na ukweli katika vitendo nazo ni tabia njema bila ya shaka yoyote, na inaweza kumaanisha kujigamba na machafu na kudhihirisha maasi na maovu kwa kisingizio cha Uhuru ambao kwa wakati wake huo unamaanisha kukengeuka na kuvuruga, na sisi tumezuiwa na kujigamba huku. Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. amsema: " Umma wangu wote umesamehewa isipokuwa wenye kudhihirisha makosa yao, na hakika katika kudhihirisha ubaya wao ni mtu kufanya jambo Usiku kisha akapambazukiwa huku Mwenyezi Mungu akiwa amemsitiri na akasema: Ewe fulani, jana nilifanya hivi na vile. Na alilala huku Mwenyezi Mungu Mtukufu akiwa amemsitiri na anaamka na kuifichua siri ya Mwenyezi Mungu aliyomfichia" . Kwa hivyo, mdhihirishaji makosa anajigamba kwa maasi Hakika mambo yalivyo, mtu huyu anataka kueneza kitendo chake hicho kwa watu mpaka wawe kama yeye na wao watumbukie katika hali hiyo. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema; { Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walioamini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera.Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui}. [AN NUURI 19]
Na hakika tumejaribiwa kwa kuwa na aina hii ya watu wanaotaka kueneza maovu kwa walioamini.
3- Na Hayaa iliyotajwa katika Qur’ani imekuja katika pande tatu za mwanzo: Ni kile kinachoegemezwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. {Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano hatawa mbu na ulio wa zaidi yake. Ama wale walio aminihujua ya kwamba hiyo ni haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, lakini wale walio kufuru husema: Ni nini analokusudia Mwenyezi Mungu kwa mfano huu? Kwa mfano huuhuwapoteza wengi na huwaongoa wengi; lakini hawapoteziila wale wapotovu} [AL BAQARAH 26].
Na hivyo ni kwa kuwa hii sio hali ya Hayaa; kwani hizo ni nyanja za kujifunza kama ilivyotangulia. Na Hayaa hakika yake kwamba ni Maadili mema yanayomzuia maovu mwenye kuwa nayo na kudhihirisha maasi na kupenda kuenea kwa machafu na wala haina Uhusiano wowote na Aibu ya kutaka kuuliza wakati wa kujifunza na kutafuta elimu; kwani hakika Elimu na kuisaka kwake ni katika Haki. Na Hayaa ya Pili imenasibiwa Mtume S.A.W., Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapoitwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapowauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyozenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu}. [AL AHZAAB 53]
Na yeye ni Haya na ni katika ukamilifu wa Maadili yake na huruma yake kwa Wafuasi wake; ambapo anawaambia: "Mimi kwenu nyinyi nina nafasi ya Mzazi" . Na ya tatu imekuja kwa kunasibishwa na Wanawake wanaojilinda waliolelewa karika nyumba za Utume. Kama katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema: Baba yangu anakwita akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipo mjia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwishaokoka kwenye watu madhaalimu}. [AL QASAS 25].
Na athari ya Ulinganiaji katika Upungufu wa Hayaa, tunaiona katika vitendo vya kimataifa, ambapo Mvamizi wa Ardhi za Wapalestina anazuia kheri nyingi na anaiba nyaraka na vielelezo vya kihistoria na anawaadhibu wafungwa na anawapiga picha wakati wa kuwaadhibu ili azitume kwa Jamaa zake huku akijigamba kwamba yeye ameadhibu watu. Na Uduni wa Maadili yake ambapo Haya imetoweka. Na vyombo vya habari na nchi vinadanganya wazi wazi tena mchana kweupe kwa madai ya uwepo wa silaha angamizi na zilizokamilika kisha inagundulika kwamba hakuna maangamizo wala ujenzi na Uongo pamoja na Uzushi vinaendelea, na kwenda kinyume na uhalisia bila ya Hayaa, kwa hiyo Manabii wamesema kweli waliposema: Kama huoni Haya basi fanya utakavyo.
Hakika sisi tulikuwa tunategemea ya kwamba Hayaa inamzuia mwenye nayo kudhihirisha ubaya na anapoudhihirisha basi Hayaa humzuia asiendelee nao na akiendelea nao basi Hayaa humzuia asibaki nao, na kuwadharau walio karibu naye kuhusu hiyo Hayaa, lakini Uchache wa Haya umewawezesha hawa kufanya yote hayo.
4- Na Uchache wa Hayaa tunauona pia kwa wale waliochafua maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetukuka, na Uchafuaji na utungaji bado vinaendelea. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Mnatumai watakuaminini na hali baadhi yao walikuwawakisikia maneno ya Mwenyezi Mungu, kisha wakayabadili baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua?} [AL BAQARAH 75].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani,na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilishamaneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema}. [AL MAIDAH 13]
Kwa hiyo tiba ya upungufu wa Haya ni Kusamehe na Kufuta makosa na kufanya mema na kuivumilia Mitihani aliyotutahini Mwenyezi Mungu Mtukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Ewe Mtume! Wasikuhuzunishe wafanyao haraka kukufuru, miongoni mwa wanaosema kwa vinywa vyao: Tumeamini, na hali nyoyo zao hazikuamini, na miongoni mwa Mayahudi, wanao sikiliza kwa ajili ya uwongo, wanao sikiliza kwa ajili ya watu wengine wasiokufikia. Wao huyabadilisha maneno kutoka pahala pake. Wanasema: Mkipewa haya basi yashikeni, na msipo pewa haya tahadharini. Na mtu ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumfitini huwezi kuwa na madaraka naye mbele ya Mwenyezi Mungu. Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu hata kikuzitakasa nyoyo zao. Watakuwa na hizaya duniani, na Akhera watakuwa na adhabu kubwa (41). . Hao ni wasikilizaji kwa ajili ya kusema uwongo, nani walaji mno vya haramu! Basi wakikujia, wahukumubaina yao au jipuuze nao. Na ukijipuuza nao, basi wao hawatakudhuru kitu. Na ukiwahukumu, basi hukumu baina yao kwa uadilifu. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda waadilifu}. [AL MAIDAH 42-42].
Na Uchache wa Hayaa umeenea kwa Wanafiki walioamini kwa midomo yao huku nyoyo zao zikiwa zinakataa, na imeenea kwa Makafiri pia, ambao wajipamba kwa ukafiri wao pia, na tiba ya watu hawa ni kujitenga nao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kukaza maana hayo: {Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemezahujibu: Salama!} [AL FURQAAN 63].
5- Na kwa uchache wa Hayaa, ngazi ya Jamii, ni pale watu waovu katika Jamii wanapoyataka madaraka baada ya kufanya kila aina ya machafu na kuwa na sifa mbaya, na Kauli yake Mtume S.A.W, inayohusu alama za ufisadi wa zama na watu wake inayasadikisha wayafanyayo. "Itawajia watu miaka ya kudanganyika, Mwongo ataaminika na msema kweli atakadhibishwa, na Mhaini ataaminiwa, na Mwaminifu atafanya uhaini, na msemaji atakuwa mtu mpuuzi. Akaulizwa Mtume S.A.W, na ni nani huyo Mpuuzi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni mtu asiye wa maana analizungumzia suala la Watu wote" .
Basi huu ndio mfano wa anayeutaka Uongozi kwa kutumia demokrasia na mifano wa hawa Nzi wako wengi. Na Mheshimiwa Mufti anasimulia kwamba Mmoja wao alijadiliana naye katika moja ya Mamlaka za kielimu akaamua kuuacha mjadala na mmoja wa wajumbe walioketi na ambao walipelekwa masomoni Marekani kwa njia ya kujifakharisha kwa kuwa na uchache wa Hayaa na Dini, na kwa kudharau kila Maadili na tabia njema: "Ewe fulani, baada ya maonano nitakupa anwani za mchango wa uovu katika nchi ya Marekani, kwani iko katika mkoba wangu". Na Masikini yule akasahau ya kwamba uchache wa Hayaa hauzalishi kheri, na haumzidishii mwenye nao Isipokuwa utovu wa adabu na kuwa chini kimaadili na kuporomoka mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Watu.
Na inaonekana wazi kwamba njia pekee ya kuepusha upungufu wa Hayaa ni Malezi endelevu na kudumu nayo, na kurejesha Maadili yanayozuia kupotea, na kuifanya ile aya kuwa ni Katiba ya Malezi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Marejeo: kitabu cha: (Sifa za Zama hizi) kwa Mheshimiwa Mufuti wa Misri Dkt. Ali Jumaa.

 

 

Share this:

Related Fatwas