Mtume, S.A.W, na Malaika wa Mauti

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtume, S.A.W, na Malaika wa Mauti

Question

 Malaika wa mauti alipomshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu, alimwambia kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Kama ungetaka kuishi milele, tungekuacha kuishi milele. Na ikateremshwa katika Qur’ani kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwingi kurehemu, “Kwa hakika wewe utakufa, na wao watakufa”, Ikiwa Bwana wetu Muhammad aliomba kutokufa, ni vipi Aya za Qur’ani zilishuka kabla ya kuulizwa yeye? Natumai kuelewa, asante. Je, maswali ya aina hii yamekatazwa kwa sababu inachukuliwa kuwa ni kuingilia mambo ya Mungu? Natumai mmenielewa ili niwaeleweshe wanangu. Asante?

Answer

 Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu peke yake, rehema na amani zimwendee Mtume wa mwisho naye ni Mtume Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Masahaba zake na mwenye kumfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.
Kwanza: Usiogope chochote, uliza chochote unachotaka, kwani hakuna swali lililokatazwa katika dini ya Kiislamu
Pili: matini hii uliyotaja “Akamwambia kwa amri ya Mwenyezi Mungu: Ukitaka kuishi milele, tutakuacha kuishi milele.” Matini hii sio sahihi, na matini ambayo ni sahihi, na ambayo nadhani unayotaka, ni ile iliyopokelewa katika Sahihi ya Al-Bukhari kutoka kwa Abu Said Al-Khudri, R.A., kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu-S.A.W.- alikaa katika membari na kusema:
“Hakika mja Mwenyezi Mungu amempa chaguo baina ya kumpa ua la dunia chochote apendacho, na baina ya kile alicho nacho Mwenyezi Mungu, basi akakichagua alicho nacho Mwenyezi Mungu.” Abu Bakr akalia na akasema, “Tunakufidia baba zetu na mama zetu.” Tulishangaa kwake, watu wakasema Angalieni Sheikh huyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu – S.A.W. anazungumzia mja mmoja ambaye Mwenyezi Mungu amempa chaguo baina ya kumpa ua la dunia chochote apendacho, na baina ya kile alicho nacho Mwenyezi Mungu. Naye anasema: “Tunakufidia baba zetu na mama zetu.”, Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. alikuwa akisema: yeye ndiye aliyechaguliwa, na Abu Bakr alikuwa ndiye aliyetufahamisha.
Hii ndiyo Hadithi unayotaka kuuliza, na maana ya Hadithi hii haiashirii kuishi milele katika dunia hii, na kwa hiyo hakuna upinzani baina ya Hadithi sahihi na Aya tukufu. Asante sana.

Share this:

Related Fatwas