Kusujudu kwa Maryamu.
Question
Amesema Mola Mtukufu: {Enyi mlioamini Rukuuni na msujudu}….. Na amesema Mola Mtukufu:
{Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao} ni kwa nini neno Sujudu limekuja mwisho kwenye Aya ya kwanza na limetangulia kwenye Aya ya pili?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Imekuja Aya ya kwanza: {Enyi mlioamini Rukuuni na msujudu} kwa utaratibu wa kawaida katika ibada ya Swala, hivyo inafahamika kuwa kurukuu kunatangulia kisha kunakuja kusujudu.
Na swali linasema ni kwanini imetangulia amri ya kusujudu katika amri ya Mwenyezi Mungu kwa Bibi Maryamu pamoja na kuwa hilo lipo kinyume na hali ya kawaida ya ibada ya swala?
Jibu ni kuwa Aya Tukufu imemuamrisha Bibi Maryamu kusujudu baada ya “Maombi” kwa sababu sehemu inayozungumzia Aya Tukufu ni sehemu ya kushukuru juu ya neema za Mwenyezi Mungu ambazo amemneemesha nazo, na kusujudu ni kielelezo chenye nguvu zaidi kuelezea shukrani, nayo ni katika kuelezea shukrani ina nguvu zaidi ya kurukuu, basi ni kwa nini imetangulizwa kisha ikaja baada ya “Maombi” kisha ikaja baada ya maombi na sujudu rukuu, ni kuwa Aya hii Tukufu sio sehemu ya kuelezea utaratibu na mpangilio wa nguzo kwenye ibaba ya Swala.