Maji yanayobaki baada ya mbwa kuyan...

Egypt's Dar Al-Ifta

Maji yanayobaki baada ya mbwa kuyanywa

Question

 Wallahi ni swali ambalo simaanishi kuwa na shaka nalo, kwani mimi nina yakini na maneno ya Mwenyezi Mungu na mwongozo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W). Najua kwamba maji yanayobaki baada ya mbwa kuyanywa yanawajibisha kuosha chombo mara 7, kwanza kwa uchafu kwa sababu ni najisi ... Je, mbwa wa kuwinda hunajisi mawindo ambayo mbwa humwindia mmiliki wake?
Nauliza kwa ajili ya kupata elimu au udadisi, na narudia kusema kuwa ninakufuru udunia na ninaamini mafundisho ya dini yangu ya kweli ya Kiislamu na.... Lau dini ingeegemezwa kwenye akili, basi kufuta chini ya viatu kungekuwa bora kuliko juu.

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Inajulikana sana kwamba sheria ya Kiislamu hairuhusu kuwinda isipokuwa kwa aina fulani za mbwa, ambao ndio mafakihi huwaita "mbwa waliofunzwa." Mbwa hawa wana sifa maalum na wana masharti na taratibu ili uwindaji pamoja nao ni sahihi, na jambo hilo halieleweki kutoka kwa swali la muulizaji.
Pili: Ikiwa idadi ya mbwa ni maelfu, basi idadi ndogo sana ya wale wanaofaa kwa uwindaji haizidi asilimia kumi.
Swali sasa ni: Kwa nini Sunnah inaruhusu kuwindwa kwa asilimia ndogo na mbwa?
Jibu: kwamba Sheria iliangalia hitajio la watu kuwinda wakati kuna aina nyingi za ndege anazohitaji mtu na hawezi kuzipata isipokuwa kwa kuwafundisha mbwa na mawindo mengine mfano mwewe, matokeo yake ni katika uchafuzi wa ndege wanaowindwa na ndege hawa wanaowindwa wanaweza kuoshwa kwa maji baada ya kuwinda, kwa hivyo faida ni kubwa zaidi kuliko madhara, na kanuni inayojulikana ya kifiqhi ni kwamba kuzuilia uovu mkubwa zaidi kati ya maovu mawili ni wajibu, na kutambua manufaa makubwa zaidi kati ya hayo mawili ni wajibu.
Aliyeruhusu kuwinda kwa mbwa aliyefunzwa ni kwa ajili ya ujumla wa masilahi haya, ambayo ndiyo yanayojulikana kwa wanavyuoni wa fiqhi kuwa ni ujumla wa balaa, kumaanisha kuwa hayo ni masilahi ya umma ambayo watu wengi wanayapata, hivyo inafaa kwa Sheria tukufu kuyapunguza. Hivi sivyo kwa chombo alicholambwa na mbwa, hakuna ujumla wa balaa katika hali hiyo, na inaweza kuepukika na kuna uwezo wa kukisafishwa, kinyume na ndege ambaye hawezi kufanywa kwake hivyo isipokuwa kwa njia hizi zilizopita.

Share this:

Related Fatwas