Kinga kwa Manabii

Egypt's Dar Al-Ifta

Kinga kwa Manabii

Question

Vipi inasemwa kuwa Manabii ni wenye kukingwa? Ipo mifano mingi ya makosa ya Manabii katika Qur'an, mfano wa Surat Abasa, pale kipofu alipomjia Mtume (S.A.W.) na akajitenga naye. kwa sababu alikuwa anashughulika kuwalingania Waarabu wakubwa, na katika Surat Yusuf aliposema Mola Mtukufu: (Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi.) Na katika sura hiyo hiyo, bwana wetu Yusuf, (A.S), alimwambia yule kijana aliyejua kuwa atavuka katika wale wawili: “Nikumbuke kwa bwana wako.” Basi Mwenyezi Mungu akamweka gerezani kwa miaka michache kwa sababu alielekea kwa mwingine na kuomba upatanishi wa mnyweshaji wa mfalme, na pia bwana wetu Yunus alipoondoka kijijini kwake kwa sababu hawakumwamini na akasafiri. Basi Mwenyezi Mungu akamtahini kwa nyangumi aliyemla majini, na lau si yeye, alimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumuomba msamaha hakunusurika kutoka kwenye nyangumi huyo, na Musa alipompiga Mmisri na kumuua? 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kinga kwa Mitume:
Dalili zimethibitisha kwamba Manabii walikuwa maasumin wakati wa bishara kutokana na kufanya madhambi kwa makusudi, na miongoni mwa dalili hizo ni hizi zifuatazo, kauli ya Mola Mtukufu kuhusu shetani: Akasema: (Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote. Isipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliokhitariwa). Basi shetani hana mamlaka juu ya waja wa Mwenyezi Mungu waliokhitariwa, na Mwenyezi Mungu mwenyewe akasema hivyo: (Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao) na Manabii wa Mwenyezi Mungu ndio waliokhitariwa, Mwenyezi Mungu akawateuwa na akawachagua ili wawe mifano hai kwa mwanadamu safi na mchamungu, ili kuwa mifano ya haki katika kauli na matendo yao, na ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya Mitume. Mwenyezi Mungu anasema: (Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu.)
Vile vile akasema: (Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake.) na akasema baada ya kuwahesabu Manabii: (Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera, Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.). Lau wangefanya madhambi kwa makusudi, wangestahili kulaaniwa mapema na adhabu baadaye, na ingeharamishwa kuwaiga. Lakini Mwenyezi Mungu aliwasifu na akatuamuru tuige wao. Mwenyezi Mungu akasema baada ya kutaja majina ya manabii wake: (Hao ndio tuliowapa Vitabu na hukumu na Unabii.) Kisha MWenyezi Mungu akasema: ( Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao.) Na Mwenyezi Mungu Mtukufu haamrishi kufanya uchafu. Mwenyezi Mungu anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu.) Vile vile anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani,na kuwapa jamaa; na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma). Ama yaliyotokea kutoka kwa Adam ni kutokana na kusahau na kabla ya bishara, kama inavyothibitishwa na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “lakini alisahau” na kusema kwake: “Kisha Mola wake Mlezi akamteuwa.” Hali kadhalika, yaliyomtokea Musa, yalitokea bila kukusudia na kabla ya bishara. Ngumi haikusudiwa kuua, lakini uwezo wa Mwenyezi Mungu unashinda na amri yake inatekelezeka, kwa hivyo Musa alitubu na akaomba msamaha kwa Mola wake Mlezi, naye akamsamehe. Akamkimbia, kwa kutaka uokovu, basi Mwenyezi Mungu akamuokoa, kisha akauona moto: (akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto. Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la T'uwa. Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa.) Na yaliyotokea kwa manabii wa kile kinachoonekana kuwa kosa yanajibiwa katika vitabu vya Itikadi kwa undani.

Share this:

Related Fatwas