Waarabu na Waislamu Wanafanya Bias...

Egypt's Dar Al-Ifta

Waarabu na Waislamu Wanafanya Biashara ya watu Weusi

Question

Assalamu Alayikum!
Ningependa kukuonesha moja ya sehemu za video, ambayo inawasilisha utafiti wa mtaalamu wa Mambo ya Mwafrika aliyebobea Anthropolojia aitwaye Tidian Nadia, ambapo utafiti huu unahusu utumwa au hasa zaidi "Waarabu na Waislamu wanafanya biashara ya watu weusi" katika kitabu chake. Ningependa ufanye utafiti wa dhati na ulioandikwa ujibu yaliyomo katika kitabu hiki. Ninakaribia kupata nakala ya kitabu hiki ili nikutumie. Je, maneno hayo ni sahihi?

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ukweli ni kwamba kuzungumza juu ya watumwa hakuwakilishi shaka juu ya Uislamu, kwani biashara ya utumwa ilikuwa imeenea katika zama zote na katika staarabu zingine zote za kale, na iliendelea biashara hiyo hadi hivi karibuni, wakati mikataba ya kimataifa ilipoumaliza utumwa katika karne ya kumi na nane.
Iwapo kuna mazungumzo juu ya utumwa katika Uislamu, basi Uislamu umemtukuza mtumwa kwanza kwa kuvikausha vyanzo vya utumwa, kutunga sheria zinazotaka kukombolewa kwa watumwa, kuita kwa kuwepo usawa baina ya watu huru na watumwa, kukataza ubaguzi dhidi ya watumwa, kuita kwa kuwaheshimu watumwa, wapunguze kazi zao, na wasiwagawie kazi ila kwa yale wanayoyaweza, na wala si kuwapangia kazi mchana na usiku na kuwasaidia kuikamilisha kazi yao kwa kufanya pamoja nao kazi hii.
Lakini Uislamu haukuamuru kukomeshwa kwa utumwa moja kwa moja kwa kuzingatia desturi ya Sheria ya Kiislamu ya taratibu katika hukumu, na kukomesha utumwa mara moja kulikuwa ni upotevu wa mali na upotevu wa watumwa hawa ikiwa hawakuwa na kile ambacho wangeweza kuishi nacho.
Kuna utafiti mzuri kuhusu utumwa yenye kichwa "Mfumo wa Utumwa katika Uislamu" na Dk Abdullah Nasih Aloun, ambao inaweza kuurejelea katika kuelewa hukumu za Kiislamu juu ya utumwa na kukanusha tuhuma za maadui wa Uislamu juu ya suala hili.
Kila kitu ambacho maadui wa Uislamu waliandika juu ya jambo hili kinatokana na chuki yenye kulaumiwa, dhulma, kughushi, na kuchanganyikiwa kwa makusudi kati ya mafundisho ya dini ya kweli na matendo mabaya ya baadhi ya wadai na wasio Waislamu. Na katika hili kuna dosari katika mkabala wa kushughulikia historia na matini ambazo hazifichiki kwa mtu mwadilifu na mwenye akili timamu.
Na Mwenyezi Mungu anajua zaidi
Kuna maandishi mengi kuhusu tuhuma hii na makala zilizochapishwa kwenye mtandao wa Internet.

Share this:

Related Fatwas