Kuja kwa Muundo Unaopelekea Mgonga...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuja kwa Muundo Unaopelekea Mgongano wa Maana

Question

Swali: Nini amesema mjenga hoja? 

Answer

Hapa unaona mgongano wa maana kwa sababu ya kugeuza maelezo kutoka kuambiwa Muhammad na kwenda kwa mwengine, kwa sababu dhamiri iliyoelekezwa kwenye kauli ya Mola Mtukufu {Mumsaidie na mumheshimu} inarejea kwa Mtume aliyetajwa mwisho, na kauli ya Mola Mtukufu {Mumtakase} inarejea kwenye jina Tukufu lililotajwa mwanzo, hii ndio maana, na katika tamko kuna kinachosaidia kuondoa sintofahamu, ikiwa kauli {Mumsaidie, mumheshimu na mumtakase asubuhi na jioni} inarejea kwa Mtume inakuwa ni kufuru, kwa sababu utakaso ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, na ikiwa kauli {Mumsaidie, mumheshimu na mumtakase asubuhi na jioni} inarejea kwa Mwenyezi Mungu inakuwa ni ukafiri, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hahitaji yoyote wa kumsaidia na kumuongezea nguvu( ).
Kuondoa shaka
1. Katika Aya Tukufu kuna somo la kilugha la kina ambapo muulizaji ameshindwa kuelewa, nalo ni somo la kukunja na kukunjua na faida yake ni kuwa Qurani Tukufu katika Aya hii imeweka wazi ulazima wa kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kisha ikaunganisha ulazima wa kuamini mambo mengine matatu la kwanza likirejea kwenye “Kusaidia” la pili “Mtume” la tatu “Kutakasa” kwanza tamko Takatifu “Allah” pili inarejea katika sifa tatu kwa sifa mbili pamoja ni kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa Mtume wake S.A.W. na aina hii ni katika aina kubwa za kukunja na kukunjua.
2. Hapa kuna maelezo mengine ya kifasaha au kilugha nayo ni neno “Kumheshimu” lenyewe linabeba ndani ya wakati mmoja kumheshimu Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumheshimu Mtume wake S.A.W. na katika hili kuna muujiza wa hali ya juu na muujiza balagha kama wanavyosema, na wabebaji wa maana hii wanazingatia upande wenye kuleta shaka ya kitamko au ushirikiano wa kitamko kama anavyosema Imamu Al-Ghazaly R.A.( )
3. Qurani Tukufu kuifahamu kwake kunategemea akili kwa msaada wa Sharia, kwani Qurani inaizungumzisha akili na vinavyomilikiwa na akili, hivyo utakuta Aya nyingi ambazo zinahimiza matumizi ya akili kuzingatia na kufikiri kwa kina na Sharia inakuja na kunyoosha hatua zake, dhamiri katika neno “Na mumtakase” inarejea kwa Mwenyezi Mungu moja kwa moja bila ya shaka yoyote, kwa sababu kutakasa ni ibada, na wala Mwenyezi Mungu hajaruhusu kwa waja wake kuabudu mwengine asiyekuwa Yeye: {Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu}[AL ISRAA: 23]. Ama marejeo ya dhamiri katika kauli ya “Na mumtie nguvu” ni kwa Mtume kwa sababu katika mazingira yake ni pamoja na kuhitaji kutiwa nguvu, ama dhamiri katika kauli ya “Na mumheshimu” hakuna kiziwizi kiakili wala Kisharia kuwa inarejea kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu kumuheshimu Mwenyezi Mungu ni kumtukuza na kumwadhimisha, kwani Nabii Nuhu alisema kuwaambia watu wake akiwa anawalaumu: {Mna nini nyinyi hamuweki heshima kwa Mwenyezi Mungu?}[NUH: 13]. Na inafaa kuwa ni yenye kurejea kwa Mtume, na kumheshimu Mtume ni kumuweka sehemu yake katika kumtukuza na kumtii. Na inafaa kubeba maana mbili kwa pamoja ( ). Na huu mfano wa tafasiri ya kauli yake Mola Mtukufu: {Na mtakapo wapa wanawake talaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema}.
Unaona maelezo ni ya aina moja “Kuwapa talaka. Kuwazuia” na kuangalia kwa haraka kunazingatiwa kuwa mwenye kuambiwa kwenye sehemu mbili ni mmoja kwa upande wa wanaume lakini akili – kwa msaada wa Sharia – haraka inatofautisha kati ya wale walioambiwa “Kuwapa talaka” na wale walioambiwa “Kuwazuia” wa kwanza wanaoambiwa ni wanaume ambao wanawapa talaka wake zao, na wa pili anayeambiwa ni wale wasimamizi wa mambo ya watalakiwa, Qurani inawaambiwa ikiwa mume anataka kumuacha mkewe talaka ya kurejea katika eda au baada ya eda kumrejea mke wake au kwa kufunga ndoa mpya na mke akawa ni mwenye kutaka hilo, hivyo wasimamizi wa mambo yao hawapaswi kukwamisha hilo.
Ambacho kimetafautisha hapa kati ya marejeo ya dhamiri mbili ni akili kwa msaada wa Sharia baada ya Mwenyezi Mungu kusema: {Hakika tumekutuma wewe uwe Shahidi, na Mbashiri, na Mwonyaji} akabainisha faida na mfumo wa kutuma unaofungamana na herufi ya Laam ya sababu ili kumfahamisha Mtume na watu wote kuwa sababu ya kutumwa kwake kwenye hilo Amesema: {Ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumheshimu, na mumtakase asubuhi na jioni}.
Maelezo hapa ni kwa ajili ya Mtume katika kutumwa kisha yakaelekea kwa Waumini wa ujumbe huo ili kuwabainishia sababu ya kutumwa kwake Mtume huyu.


 

Share this:

Related Fatwas