20- Talaka

Egypt's Dar Al-Ifta

20- Talaka

Question

 Matini ya Qurani
Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Hapana ubaya kwenu mkiwapa talaka wanawake}. [AL BAQARAH: 236]
Pia Mwenyezi Mungu alisema: {Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwingine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayo ibainisha kwa watu wanao jua} [AL BAQARAH: 230]
Maana ya jumla:
Katika Aya tukufu ni kwamba Waumini
Mdai alisema nini?!

Answer

Qur’ani inamruhusu mwanamume, kwa hiari yake, bila ya kumtegemea yeyote katika anachotaka, kuiangamiza familia yake na kuidhoofisha na kutawanya nguzo zake, hivyo kwa kumtaliki mke wake. Moja ya machozi ni kumuona Muislamu mwanamume akigombana nje ya nyumba na kula kiapo mara tatu na kumfukuza mke wake aliyekaa salama nyumbani kwake, bila ya sababu yoyote isipokuwa kuwa ameapa kwa ugomvi ambao mwanamke hana dhambi katika ugomvi huu! Kisha wanasema kwamba halali inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni talaka. Je, namna gani Mwenyezi Mungu anahalilisha jambo analochukia? Je, si sahihi zaidi kwamba anachochukia anakiharimisha? ()
Maana ya Tuhuma: Ni moja ya kanuni zilizowekwa kwa lugha ya Kiarabu kwamba"
Kujibu kwa Tuhuma:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Juhudi za wanachuoni kujibu kwa tuhuma hii:
Tuhuma hii ni miongoni mwa tuhuma maarufu zinazohusiana na wanawake katika Uislamu, na umaarufu wake unatokana na kukosekana kwa talaka katika baadhi ya sheria za zama hizi, hivyo, watu wengi wa Magharibi wakazingatia kwamba kati ya dosari ya Uislamu ni kwamba inaruhusu talaka, na wanaona kuwa hii ni dalili ya kupuuza kwa Uislamu kwa thamani ya wanawake na utakatifu wa ndoa, na baadhi ya Waislamu waliojifunza tamaduni za Magharibi waliwaiga katika hilo, na wanazuoni wengi waislamu wameitikia tuhuma hii kwa majibu mengi, ambayo muhimu zaidi yameelezwa katika yafuatayo.
Kujumlisha taswira potofu juu ya sheria yenye busara:
Muulizaji aliweka hapa hali inayoweza kutokea miongoni mwa Waislamu wasioshikamana na mafundisho ya dini, na alitaka kuhukumu kwayo sheria ya Kiislamu ya talaka kwa ujumla wake, na huu ni aina fulani ya mkanganyiko, na ni sahihi kuangalia sheria ya talaka katika muktadha wake kutoka kwa mfumo wa Kiislamu. Taswira aliyoiweka muulizaji kwa mwanaume anayegombana na mwenzie, kisha akaapa talaka inayopelekea kumfukuza mke wake nje ya nyumbani kwake, hii ni picha ya Waislamu wa kawaida na wasiokuwa na dini, na wala si sahihi kuwahukumu Waislamu wengine kwayo, wala kwa sheria zote za Kiislamu.
Haki ya Mwanamke katika Talaka:
Suala hilo halipo kabisa mikononi mwa mwanamume, kama muulizaji alivyosema, lakini mwanamke naye ana haki ya kuomba talaka ikiwa itathibitika kuwa ameumizwa na ndoa hii.
Ajabu ni kuwa muulizaji alitaja hukumu za talaka na hakuzungumzia hukumu ya (Kului) kupewa talaka ambako ni miongoni mwa hukumu za fiqhi ambapo inahukumiwa kwa mwanamke kumwacha mumewe kwa hiari yake. Basi kwa nini muulizaji alipuuza sehemu hii ya sheria ya Kiislamu? Je, yeye hajui, basi kwa nini anazungumza kuhusu sheria za Kiislamu bila ya kufahamu vizuri masuala hayo, na ikiwa anajua na hakulitaja suala hilo, je, hii ni njia sahihi ya kielimu?
Kwa nini Mwenyezi Mungu alifanya suala la talaka mikononi mwa wanaume?
Ya kwanza: kwamba yeye ndiye mwenye kutumia pesa, basi Mwenyezi Mungu amemgharamishia gharama za kuisimamisha nyumba hii, na pia amemlazimu kuendelea kuitumia pesa kwake, kwa hivyo yeye huitunza nyumba hii zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Na wakati Uislamu ulipokuwa na shauku juu ya kuendelea kwa familia kukaa, ulimkabidhi mwanamume jambo hili.
Ya pili: kwamba anadhibiti hisia zake zaidi kuliko mwanamke; Wanawake wengi hawawezi kudhibiti hisia zao katika hali nyingi, hasa za maisha ya ndoa. Kwa sababu mwanamke anahitaji uzoefu mwingi, na anahitaji aina ya fikra inayotawaliwa na akili, si hisia, ambayo ni sifa ya mwanamke, na mara nyingi wanawake hawaelewi hilo. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu ameweka uwakili mikononi mwa wanaume.
Na sio kila talaka, kama muulizaji alivyosema, inaharibu familia na kudhoofisha misingi yake, badala yake, talaka inaweza kuwa suluhisho la pekee la faraja ya pande zote mbili.
Faida ya Talaka katika Uislamu:
Mwenyezi Mungu ameiruhusu talaka kutatua matatizo mengi yanayoweza kutokea baina ya wanandoa na hayana suluhu isipokuwa kutengana. Mwanaume anaweza kuoa mwanamke kisha ikadhihirika kuwa kati yao kuna khitilafu katika maadili, au kutofautiana kimaumbile, na inaweza kuonekana kuwa mwanamke ni tasa ambayo kwayo malengo ya juu zaidi ya ndoa hayafikiwi, na mume hataki mitaala, au hawezi, na sababu zingine na sababu ambazo hazitoi mapenzi kati ya wanandoa, na ushirikiano katika mambo ya maisha, na utimilifu wa haki za ndoa kama Mwenyezi Mungu alivyoamrisha, hivyo talaka ni lazima kwa ajili ya wokovu kutoka katika kifungo cha ndoa ambacho kimekuwa hakitekelezi kusudi lake, na kwamba ikiwa wanandoa wawili walilazimika kubaki pamoja, chuki ingekula nyoyo zao, na kila mmoja wao angepanga mpango kwa mwenziwe, na akataka kumuondoa kwa njia iliyoandaliwa kwa ajili yake, na hii inaweza kuwa ni sababu ya upotofu wa kila mmoja wao, na pazia la maovu na dhambi nyingi, kwa ajili hii aliweka sheria ya Mwenyezi Mungu talaka ni njia ya kuyaondoa maovu hayo, ili kila mmoja wao ambadilishe mke wake na mume kwa mwingine, ambaye atapata pamoja naye alichopungukiwa na wa kwanza, kwa hivyo kauli yake Mwenyezi Mungu itatimizwa: {Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima.} [An-Nisaa: 130].
Uislamu na Sheria iliyo kabla ya Talaka:
Imepokelewa ktoka kwa Ibn Umar, (R.A): Kutoka kwa Mtume (S.A.W) amesema: “Halali inayochukiwa zaidi na Mwenyezi Mungu ni talaka.” Maana ya Hadithi ni kwamba Mwenyezi Mungu ameiruhusu talaka na akawataka waja wake wasiwe na haraka kutamka talaka, bali waifanye kuwa ndiyo suluhisho la mwisho, hivyo wasiielekea isipokuwa pale inapobidi.
Maana ya chuki iliyotajwa katika Hadithi hii ni sitiari ya kuwatenga Waislamu na kuelekea talaka, kwa hivyo, Mwenyezi Mungu amewaepusha talaka na kuichukia nafsi zao, basi Mtume (S.A.W) akasema” “Mwanamke yeyote anayemuomba mume wake talaka pasipo na sababu, basi harufu ya peponi ni haramu kwake.” Pia Mtume (S.A.W) akaonya kuhusu kutamka neno la talaka ovyo ovyo, akisema: “Mbona mmoja wenu anachezea mipaka ya Mwenyezi Mungu, akisema: Mimi nimetaliki, nimerudi mke wangu”
Talaka ilichukuliwa kuwa ni nia ya mwisho, hivyo kwamba inawezekana kuielekea tu wakati azma inapofikiwa, tatizo linapokuwa kubwa, na wakati hakuna tatuo lengine isipokuwa talaka tu, na Mwenyezi Mungu akaagiza kuchukua njia nyingi kabla ya kuielekea talaka, hivyo alimhimiza mume asubiri na kustahimili, hata kama akimchukia mke wake kuhusu baadhi ya mambo kutoka kwake, ili kuhifadhi maisha ya ndoa, Mwenyezi Mungu akasema: {Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake} [An-Nisaa: 19]. Vile vile Mwenyezi Mungu alimuelekeze mume, akiona uasi wa mkewe, kwa yale anayomuadhibu polepole: mawaidha, kisha kuacha, kisha mapigo yasiyo makali. Mwenyezi Mungu anasema: {Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu} [AN NISAA: 34].
Mwenyezi Mungu aliwaamuru wanandoa pia ukitokea mzozo wasuluhishe kati yao kwa ajili ya kupatanish kati yao na kuhifadhi familia. Mwenyezi Mungu alisema: {Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari.} [AN NISAA: 35]. Taratibu na njia zote hizi zinachukuliwa kabla ya talaka kufanyika, na kutokana na hili inakuwa wazi umuhimu mkubwa wa mahusiano na maisha ya ndoa kwa Mwenyezi Mungu.
Sio lazima kuvunja kile ambacho Mwenyezi Mungu amekifunga na kutawala, isipokuwa kama kuna sababu kubwa na ya hatari ya kutenganisha, na hii inaweza tu kufanywa baada ya kumaliza njia zote za upatanisho.
Na kutokana na muongozo wa Uislamu katika talaka, na kutokana na kufuata sababu zinazopelekea talaka, inadhihirika kuwa kama kwamba talaka ina maslahi ya mume, pia ina manufaa ya mke katika mambo mengi. Mke anaweza kuwa ni yule anayeomba talaka anayeitamani, hivyo Uislamu hausimami katika njia ya matamanio yake, na katika hali hii nfasi yake huinua, na kuithamini hali yake, huku sio kudharau hali yake, kama wadai wanavyodai, bali ni kudharau hali yake ni kwa kupuuza matamanio yake, na kumlazimisha kufungwa na kifungo ambacho anachukia na kudhuriwa nacho.
Sio kudharau kwa utakatifu wa ndoa, kama wanavyodai, bali ni njia ya kupata ndoa sahihi na iliyo bora, ambayo inafanikisha maana ya ndoa na malengo yake ya hali ya juu, na sio ndoa ya udanganyifu isiyo na maana zote na madhumuni ya ndoa. Sio makusudio ya Uislamu ni kudumisha kifungo cha ndoa, chochote kile, bali Uislamu uliweka malengo kwa kifungo hicho, ambayo lazima yafikiwe kutokana nayo, vinginevyo sivyo, na badala yake kuwekwa yale yanayofikia malengo na makusudi hayo.
Uislamu na sheria baada ya talaka:
Uislamu uliporuhusisha talaka, ulishughulikia matokeo yake, hivyo ikathibitisha kwa mama ulezi wa watoto wake wachanga hadi watakapokuwa wakubwa, na ikamlazimu baba kugharamia watoto wake, na ada za kuwalea na kuwanyonyesha, hata kama mama ndiye anafanya hivyo.
Hali sahihi katika talaka kwa vizazi:
Mtazamo sahihi ni kwamba Waislamu wote wanatahadhari juu ya talaka na wala hawawi na haraka kwa kutamka neno la talaka, kama muulizaji alivyotaja, na kwamba talaka si chochote ila ni kama mkataba wa ndoa inayohitaji maandalizi, subira na kusoma wajibu wake. kisha mwanachuoni wa Faqihi Mwislamu huwaongoza watu kwa mambo hayo.
 

Share this:

Related Fatwas