Mtume S.A.W. na Kuharimisha Halali...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtume S.A.W. na Kuharimisha Halali.

Question

Aya yenye shaka:
{Ewe Nabii! Kwa nini unaharamisha alichokuhalilishia Mwenyezi Mungu? Unatafuta kuwaridhisha wake zako. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu * Hakika Mwenyezi Mungu kakupeni Sharia ya kufungua viapo vyenu, na Mwenyezi Mungu ni Mola wenu. Na Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye hekima} [AT TAHRIIM 1-3].
Katika baadhi ya marejeo ya Kiislamu ni kuwa Mtume S.A.W siku moja alikuwa nyumbani kwa Hafswah Bint Omar ni mmoja wa waki zake, hivyo Bi Hafswa alimuomba ruhusa mme wake ya kwenda kumtembelea baba yake ndipo Mtume alipompa ruhusa, kisha akaja Bi Maria nyumbani kwa Hafswah na kukakaa, aliporudi Bi Hafswah alimuona Bi Maria akiwa na mume wake nyumbani kwake hivyo Bi Hafswah hakuingia nyumbani kwake mpaka alipotoka Bi Maria kisha ndio akaingia na kumwambia mume wake: Nimemuona aliyekuwa na wewe ndani ya nyumba, bi Hafswah alikasirika sana na kulia na akamwambia tena: Umenifanyia kitu ambacho hujawahi kumfanyia mkeo yeyote, kwenye zamu yangu ndani ya siku yangu kitandani kwangu! Mtume akamwambia: Nyamaza, hivi utaridhia nijizuie naye au kuwa naye karibu siku zote? Akajibu Bi Hafswah: Ndio naapa usiwe naye karibu, kwani pindi upendo ulipomzoea Maria uliapa kwa uwongo, ndipo akafunga mlango wa kulalamika kwa Hafswah kwa kufuta kiapo chake kwa kusema: Hakika Mwenyezi Mungu amemfungulia ufunuo wa Aya hizi. Sisi tunauliza: Ni kwa nini Nabii wa Kiislamu aliharamisha kitu kilichohalalishwa kwake na Mwenyezi Mungu? Na ni vipi anashirikiana na wake zake kwa namna hii?
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza kabisa: Kisa hiki kilichopita ni dhaifu sana wala hakifai kuwa sababu ya kuteremka kwa Aya, usahihi wa kuteremka Aya hii ni habari iliyopokelewa na Masheikh wawili kutoka kwa Bi Aisha R.A kuwa amesema: “Mtume S.A.W alikuwa anapenda sana asali na haluwa, na alikuwa pindi anapoondoka wakati wa Al-Asri akienda kwa wake zake, anakaa kwa Bi Zainab Bint Jahsh na anakunywa asali, nikakubaliana mimi na Hafswah kuwa yeyote kati yetu atakapoingia Mtume tumwambie: Ninasikia harufu ya maghafiri, je umekula maghafiri? Akasema Mtume: Hapana bali nimekunywa asali kwa Zainabu Bint Jahsh na sitoirudia tena na nimeapa hivyo usimwambie mtu yeyote” ( ).
Hii ndio sababu sahihi ya kuteremka Aya kama ilivyopitishwa na jopo la Wafasiri wa Qur`ani miongoni mwao ni Abubakri Ibn Al-Araby ( ) na Qurtwuby ( ) na Ibn Katheer ( ) na Twahir Ibn Aashuur ( ) na wengine.
Ibn Al-Araby amesema: “Hakija andikwa – kwa maana kisa cha Maria kilichotajwa kwenye swali – kwenye Vitabu vya Sahihi wala kutajwa uadilifu wa wapokezi wake” ( ).
Pili: Huenda imekuwa wazi kuwa alichokifanya Mtume S.A.W hajazingatiwa kuwa kujizuia na jambo halali kwake, na kitenzi cha Kiarabu “Harrama” hutumika kwa maana ya kujizuia na kitu, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu Alivyosema kuhusu Nabii Musa:
{Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia watakuwa wema kwake} [AL QASWAS 12].
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: {Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharamisha mwaka mwingine} [AT TAWBAH 37].
Na kwa hili haijifichi Aya kuwa si katika maana yake kuwa Mtume S.A.W alibadilisha halali na kuwa haramu – kama ilivyotajwa kwenye swali – hilo haliwezekani kwa Mtume S.A.W ( ) bali ni malekezo ya Mwenyezi Mungu kuwa huruma ya Mtume S.A.W kwa wake zake imemfanya kuzuia kile alichohalalishiwa na Mwenyezi Mungu ikiwa kupendezesha mawazo yao, na njia ya huruma huenda haikubaliani – wakati mwingine – na yale aliyoyafanya Mwenyezi Mungu kwa Nabii kigezo cha kuigwa na walimwengu, na Mwenyezi Mungu hataki kwa watu wote kujizuia na halali, hivyo Aya zikamuelekeza kuchukuwa njia nyingine na kufuta kiapo chake ili watu wasipate ugumu pale watakapo taka kushikamana nacho bila ya kukiacha.

 

Share this:

Related Fatwas