Hud-Hud Mwanafalsafa!

Egypt's Dar Al-Ifta

Hud-Hud Mwanafalsafa!

Question

  Aya ya Qur`ani:
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simuoni Hud-hud, au amekuwa miongoni mwa walio kosekana? * Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya kutosha * Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea habari za yakini * Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa * Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka * Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza * Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa Arshi Tukufu * Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo * Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha nini} [ANAML 20 – 28]
Maana ya jumla:
Mlalamikaji amesema nini?
Qur`ani imesema kuwa Suleiman alikuwa anafahamu lugha inayozungumzwa na ndege pamoja na wadudu wadogo, majini watu na ndege walikuwa ni askari wake, na yeye alikwenda na hawa majeshi yake mpaka kwenye bonde la sisimizi, ndipo hao sisimizi wakafahamu kuwa Suleiman ni mfalme na Nabii na hawa wote ni askari wake, hivyo wakawatahadharisha sisimizi wenzao na kusema: Enye sisimizi ingieni kwenye nyumba zenu ili Suleiman na askari wake wasije wakanyaga bila ya wao kuhisi! Na Suleiman alipotelewa na ndege akasema: Kuna nini mbona simuoni Hud-Hud? Kama hayupo kwenye kikao chetu basi nitamuadhibu kwa kumnyonyoa manyoa yake au nitamchinja ili awe zingatio kwa wengine au aje aombe radhi! Wakati huo huo Hud-Hud akafika akiwa anaruka juu ya Suleiman akasema: Nimefahamu mambo usioyajua, na nimekujia kutoka Sabai na habari ya kweli, na mimi nikiwa na nafasi ndogo sana na elimu yako ni kubwa zaidi ya elimu yangu, hivyo ninakueleza kuwa mfalme wa Sabai anaabudia jua badala ya Mwenyezi Mungu Muumba wa mbingu na ardhi na Mwenye kufahamu mambo yote yaliyojificha ulimwenguni! Suleiman akasema kumwambia: Nenda kwake na barua yangu hii ili nipate kufahamu kama utakuwa ni mkweli au muongo! Ndipo Hud-Hud alipoenda na hiyo barua na akaikabidhi kwa mfalme wa Sabai! Ndipo mfalme akataka ushauri kwa watu wake wa namna ya kufanya ili kujibu barua kisha akatuma akatuma zawadi kwa Suleiman lakini hakuipokea! Na Suleimani akawauliza watu wake nani atakaye enda kumletea kiti cha mfalme wa Sabai kwa siri? Ndipo jini mmoja akasema: Mimi nitakuletea kabla hujasimama kutoka sehemu yako na mimi kwenye kukibeba na kukilinda ni mwenye nguvu na muaminifu sana! Suleimani akakataa isipokuwa kiti cha enzi kiletwe sasa hivi, mmoja wao akasema ambaye huenda akawa ni Aswif Ibn Barkhaya Waziri wa Suleiman, au Malaika Jibril: Mimi nitakuletea kabla ya hujafunika jicho lako! kilipoletwa kiti Suleiman alibadili baadhi ya alama za kiti, na alipokuja mfalme wa Sabai Suleiman alimuuliza: Je hiki ndio kiti chako? Akajibu: Ni kama chenyewe! Akamtaka mfalme aingie kwenye Kasri, pindi alipokunja miguu yake ili kuelezea kile alichodhania kuwa ni maji, akakuta ni kioo kinagongana na miguu yake ndipo alipomuamini Mola wa Suleiman na akawa miongoni mwa Waislamu.
Sisi tunauliza: Ni namna gani akili inaweza kufikiria kuwa wafuasi wa Suleiman Mfalme mwingi wa hekima ni majini na ndege? Ni namna gani ndege Hud-Hud kuwa na busara zaidi na elimu na kumpa changamoto Suleiman akisema: Nina mambo usiyoyajua na nimekujia nikitokea Sabai nikiwa na habari kubwa? Ni namna gani Hud-Hud amejifunza na kujua ibada za kuabudia asiye mungu na kusifia upekee wa Mungu? Ni vipi Hud-Hud anafanya kazi ya upelekaji habari? Na namna gani Hud-Hud anatumia mamlaka ya Suleiman kwa matumizi ya zaidi ya wafalme mawaziri na wanafalsafa? ( ).
Kuondoa shaka:

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kukosekana kusudio na kugeuka ukweli:
Hakuna yeyote aliyesema kuwa wafuasi wa Nabii Suleiman walikuwa ni majini na ndege, wala Aya haijasema kuwa Hud-Hud alikuwa ni mwenye busara zaidi na elimu kuliko Nabii Suleiman A.S wala Hud-Hud hata siku moja hajawahi kumfanyia changamoto Nabii huyu Mkubwa Nabii Suleiman, na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kupitia ulimi wa Hud-Hud:
{Nimegundua usilo gundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea habari za yakini * Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho kiti cha enzi kikubwa} ndani yake hakuna changamoto kwa Nabii Suleiman A.S na wala vitendo vinavyofanywa na Hud-Hud vinavyofanana na wafalme na mawaziri pamoja na wanafalsafa kama alivyofahamu muulizaji, lakini jambo halizingatiwi kisa kuwa kimetokea kati ya Nabii wa Mungu na huyu ndege dhaifu aliyeleta habari ya kile alichokiona wakati wa kutembelea kwake ambapo alipewa jukumu hilo na Nabii huyu mkubwa…
Muulizaji amefahamu kuwa Hud-Hud alifahamu ibada za kuabudia asiyekuwa mungu na kuelezea upekee wa Mungu, na jambo sio hivyo bali alielezea kwa Nabii wa Mungu kile alichokiona na ikawa ni sababu ya kuchelewa kwake ndani ya wakati, hivi yote hayo mwanadamu hayaoni au hafikirii uwepo wake hivyo ni lazima kukosekana kwa swali hili kwenye tukio hili, na akili ya sasa inaelekea kuwa mwanadamu anapaswa kutoamini isipokuwa kwa anachokiona na kusikia au kinachotokea kwenye moja ya hisia zake za wazi, na ukweli wa jumbe za mbinguni zina zinakwenda kinyume na jambo hili, kwani mwanadamu kutofahamu kitu si dalili ya kutokuwepo kwake, kukosekana kwa ufahamu hakuoneshi kukosekana kuwepo na kukosekana ujuzi hakumaanishi kukosekana, kwani vitu vingi mwanadamu havioni lakini anaamini kwa imani kubwa kuwa vipo, kwani mwanadamu hawaoni Malaika wala hawaoni majini lakini anaamini uwepo wao.
Na hisia za mwanadamu ni dhaifu zaidi kufahamu ukweli wote wa ulimwengu ikiwa pamoja uwepo wa viumbe wengi hisia zenyewe mpaka hivi sasa zinashindwa kufahamu vitu vingi kama vile ukweli wa roho na ukweli wa mbingu na kila elimu au sayansi inapogundua kitu mwanadamu anashindwa kufahamu vitu vingine, na hali ya mwanadamu itaendelea kama Qur`ani inavyosema:
{Nanyi hamkupewa katika elimu ila kidogo tu} [AL ISRAA 85].
Pia kuna vitu vimejificha nyuma ya ulimwengu unaoonekana mwanadamu havifahamu.
Miujiza iliyothibiti kwa Manabii:
Waislamu wanaamini kuwa Nabii Suleiman – amani ya Mungu iwe kwake – alikuwa Nabii katika Manabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mwenyezi Mungu alimpa ufalme pembezoni mwa Utume, na Mwenyezi Mungu alipokea maombi yake katika kauli yake:
{Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji} [SWAAD 35]
Ufalme wake ambao haufanani na ufalme wa yeyote haukuwa ni sehemu tu ya ardhi ambayo alikuwa anaitawala, kwani kuna wafalme wengi wametawala sehemu kubwa zaidi ya ardhi, wala haukuwa pia kwa idadi ya waliohukumiwa ambao walikuwa chini ya utawala wake, kwani kuna wafalme wengi waliotawala watu wengi zaidi, bali ulikuwa chanzo cha utofauti wake na sababu ya upekee wake na falme zote zilizotangulia au zilizofuata ni kule Mwenyezi Mungu kumrahisishia majini ndege na upepo na haya yapo nje ya uwezo wa mwanadamu vyovyote atakavyokuwa kwani yenyewe ni katika fadhila zitokazo kwa Mwenyezi Mungu kwake, hili si jambo la kushangaza kwa sababu ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake Suleimani yenyewe ni katika wigo wa miujiza na lazima muujiza kuwa ni jambo kinyume na kawaida na kama si hivyo basi isingefaa kuwa muujiza.
Tafasiri ya Vitendo vya Hud-Hud:
Ama Hud-Hud kuwa na hekima nyingi na elimu kuliko Nabii Suleimani na kuwa alimpa changamoto Suleimani, hili si sahihi kabisa, kwani Hud-Hud kuwa amefahamu jambo asilo lifahamu Suleimani haioneshi hata kidogo kuwa Hud-Hud anajua zaidi ya Nabii Suleimani bali kinachomaanisha ni kuwa Hud-Hud alijua jambo moja lilijificha kwa Suleimani, na hili halina mgongano wowote wa uwezo wa Suleimani au kuwa juu uwezo wa Hud-Hud bali ni dalili ya nafasi ya upungufu wa wanadamu na ukamilifu ni wa Muumba Mwenye nguvu na Uwezo, ama kupewa changamoto Nabii Suleimani ni tofauti na uhalisia kwa sababu hakumpa changamoto bali alimpa habari halisi ya kile kiichomchelewesha ndege kwani alisema “Nimefahamu kile usichokifahamu” kwa sababu ana yakini kuwa Suleimani lau angelikuwa na ujuzi wa hawa ambao wanaabudia asiyekuwa mungu basi asingewanyamazia na angeliwalingania kwenye kumpwekesha Mungu, hivyo maneno ya Nabii Suleimani ni kwa njia ya kusimulia ukweli na wala si kwa njia ya changamoto.
Kama vile muundo wa swali ndani yake kuna hali ya ujinga wa kutojua Qur`ani kwani ndege Hud-Hud alisema “Nimekuja kutoka Sabai na habari ya kweli” na wala hakusema nimekuja na habari kubwa kama ilivyokuja kwenye swali, na tofauti ipo wazi ambapo Hud-Hud ana hakika na habari isipokuwa hawezi kuhukumu kwani hukumu katika hilo inasimamiwa na Nabii Suleimani na yeye ndio ata ainisha kustahiki kwa Hud-Hud kusamehewa au kutosamehewa.
Ama Hud-Hud kuwa anachukia ibada za kuabudia asiyekuwa mungu na kufahamu pamoja na kupenda upwekeshaji wa Mwenyezi Mungu na kumsifia hili ni jambo la kawaida na wala sio Hud-Hud peke yake kwenye hilo bali viumbe vyote vinafahamu hilo, kwani Mola Mtukufu Amesema:
{Na hapana kitu ila kinamtakasa kwasifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake} Lakini kwa vile hatufahamu maneno ya viumbe bali lilipoondoka hili pazia kwa Nabii Suleimani na akawa anazungumza na wanyama na kuwafahamu ndipo pazia hili likaondoka na kufahamika kwetu yale yaliyokuwa yamejificha miongoni mwa utakaso wao na kumfahamu kwao Mwenyezi Mungu Mtukufu hivyo hakuna sababu kabisa ya kupinga hilo.
Ama Hu-Hud kuwa amechukuwa kazi ya mjumbe wa kupeleka taarifa hii pia ni kitu cha kawaida kwa sababu hakufanya kazi asiyoiweza kufanya mwingine yeyote bali alichofanya ni kufikisha ujumbe kwa mfalme kisha kuja na habari ya majibu yake kwa Sueimani, na hili ni jambo la kimuujiza kwani msingi wa jambo lote ni kuwa Nabii Suleimani anafahamu lugha ya ndege Hud-Hud na hii ndio tulielezea sababu yake, na pindi Hud-Hud alipokuwa ndio mwenye habari ilikuwa ni jambo la kawaida Nabii Suleimani kumpa jukumu ambalo alilianza mwenyewe ni kawaida kulikamilisha.
Ama kauli ya swali kuwa, Hud-Hud anaitumia mamlaka ya Nabii Suleimani matumizi ya zaidi zaidi ya wafalme mawaziri na wanafalsafa hii ni kauli batili wala haiashiriwi na kisa kama kilivyokuja ndani ya Qur`ani wala kumaanisha hivyo, basi viko wapi vitendo vyake ambavyo vinakaribia vitendo vya wafalme au zaidi? Je aliamrishwa na akakataa? Je alipewa na akazuia? Je alisimamia tukio na jeshi likaenda nyuma yake? Sifahamu kutoka wapi amefahamu huyu mjenga shaka kuwa Hud-Hud alifanya kama wafanyavyo wafalme na mawaziri bali ni ubaguzi wenye chuki unaopelekea kwa watu wake na kuwafanya wanasema yale yasiyokuwa na msingi wowote wa ukweli.
Wanyama na Milima yazungumza katika Kitabu Kitakatifu:
Na mwisho huyu muulizaji tunamwambia: Je unaondoa uwezekano wa Hud-Hud kuzungumza kwa lugha yake anayoifahamu Nabii Suleimani? Ni unasemaji kwenye Aya ya Kitabu Kitakatifu ambayo inazungumza kwa uwazi maneno ya wanyama mfano wa maneno ya wanadamu, ndani ya Kitabu cha Hesabu: 22: 27: 28:
“Yule punda akamuona Malaika wa Bwana, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaam ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake. Bwana akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, nimekutendea nini, hata unakipiga mara tatu hizi?” punda alizungumza na kumlaumu nabii Balaam”.
Na Peter anasema katika barua yake ya pili 2:16
“Lakini alikaripiwa kwa uhalifu wake mwenyewe; punda asiyeweza kusema, akinena kwa sauti ya kibinadamu”.
Bali zaidi ya hayo vitu vigumu navyo vinazungumza kwenye Kitabu Kitakatifu ndani ya kitabu cha Waamuzi 9: 8 – 16.
“Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu * Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayongeyonge juu ya miti? * kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu * Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? * Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu * Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge yonge juu ya miti? * Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu * Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumani kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni”.
Uhalisia wa kisa na ukweli wake kinafuata uchambuzi uliotajwa ndani ya Aya Tukufu: Na kufuatiwa pia na Suratul Sabai ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya ni ishara kwa waja wake, na imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu Sura kamili Mwenyezi Mungu ameita kwa jina la ufalme huu.

 



 

Share this:

Related Fatwas