Ulipizaji Kisasi kwa Baba yake Mdogo Hamza.
Question
Tamko Lenye Kuleta Shaka:
Alipouliwa Hamza baba mdogo wa Mtume wa Uislamu katika vita vya Uhudi Mtume alikasirika sana na akaapa kuwa atalipiza kisasi kwa makuraishi kwa kuuwa watu sabini kufidia kifo cha Hamza.
Tunauliza: Ni vipi mwenye kudhamiria kulipiza kisasi kwa maadui anakuwa Mtume aliyetumwa? N aje kulipiza kisasi ni katika tabia na maadili ya Mitume
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Mtume wa Mwenyezi Mungu aliahidi kisasi kwa wauaji wa Hamza hasa wale waliochezea mwili wake baada ya kumuuwa kwa kumpasua tumbo lake na kumkata pua masikio na kumg’oa maini, kwani Mtume alihuzunika sana kwa hayo mpaka alilia kwa sauti, bali alisema katika yaliyonukuliwa kwake: “Hakuna tena atakayepatwa sawa na mfano wako” ( ).
Kati ya Hasira na Athari zake:
Inapaswa mwanadamu kutafautisha kati ya hasira ya lazima ambayo mwanadamu hawezi kuepukana nayo hata kama atakuwa ni Mtume, na kati ya hasira kali ambayo ni mtu kutoka kwenye maadili sahihi, ama hasira za lazima ni jambo la kawaida mwanadamu yeyote hawezi kuepukana nayo hata viongozi wa maadili mema katika Mitume, kwani mwanadamu yeyote ana asili yake silika zake na hisia zake ambazo Mwenyezi Mungu amemuumbia nazo, ama hasira kali ni mwanadamu kwenda mbali zaidi katika hasira zake na kufanya tabia isiyo sawa, hali hii kwa Mtume S.A.W ni hali ya kawaida isiyoshusha hadhi yake wala kupunguza uvumilivu wake.
Wala si katika maana ya Mitume kuzuiliwa kufanya makosa kukosekana kutokewa na mambo ya kibinadamu, bali maana yake ni kuwa Mtume anapotokewa na kitu miongoni mwa vitu vinavyowatokea wanadamu havimpelekei kufanya ubaya.
Ikiwa mtu atachukuwa maamuzi basi anatakiwa kumuiga Mtume S.A.W ikiwa mmoja wetu ametatizwa na kitu wakati wa huzuni au hasira kutokwenda mbali zaidi kwenye hasira zake na wala asitekeleza alichokusudia kukifanya wakati alipokuwa na hasira pindi akiona kutekeleza hayo kutapelekea madhara.
Maelekezo ya Mungu:
Kwa kuteremka tu Aya ikabainisha kwa Mtume S.A.W kulipiza sawa na ilivyofanywa bila ya kuzidisha akasema: Tunasubiri wala hatutesi, ndio pamoja na huzini imefika kiwango cha mwisho pale alipoona wapinaji wa Waislamu na kuchezewa kwa miili yao vitendo hivyo vikiongoza kwa baba yake mdogo basi ikateremka Aya iliyoelezea adhabu sawa na dhambi: {Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa} [AN NAHL 126].
Kisha Aya ikamuinua kwenye kiwango cha juu sana ikasema:
{Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri} katika Aya kuna hali ya kupewa hiyari kati ya kisasi na kusubiri, kisha ikahamia kwenye kusubiri lakini kuhama huku ni kukubwa na nafasi ya nafsi ya mwanadamu inahitaji msaada wa Mungu, Akasema: {Na subiri. Na kusubiri kwako kusiwe ila kwa sababu ya Mwenyezi Mungu tu} [AN NAHL 127] .