Kuoa Wake Wengi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuoa Wake Wengi

Question

Aya yenye shaka
Ndani ya Qur'ani imekuja: {basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} {AN-NISAA: 03}.
Sisi tunauliza: Hivi kuoa wake wengi sio kwenda kinyume na mwenendo wa Mungu tokea kuanza kuumba kiongozi? Kwani Mwenyezi Mungu Alimuumba mmoja tu kwa Adamu mmoja.
Katika kuoa wake wengi ni kuharibu tabia za mwanamume kwa dhuluma na kuchelewesha mafanikio ya watoto na ni dharau kwa wanawake, na kunaharibu maendeleo ya kijamii pamoja na amani ya taifa, na sisi tunaheshimu uanaume kwa kuwaheshimu wakina mama, wakina dada, watoto wa kike pamoja na wake, na mwenye kuharibu nyumba basi anaharibu ubinadamu.

Answer

 Mwenyezi Mungu kutoumba mke mwingine wa baba yetu Adam amani ya Mungu iwe kwake asiyekuwa Mama yetu Hawa si dalili ya kuharamisha ndoa ya wake wengi kwa sababu baba yetu Adamu na Mama Hawa walikuwa peke yao wawili tu na hapakuwa na mwingine yeyote pamoja nao duniani, na wala Mwenyezi Mungu hakumwamrisha yeyote katika waja wake kuwafuata wao kwenye kuacha kuoa ndoa ya wake wengi.
Katika ndoa ya wake wengi muulizaji hakutaja ubaya uliopo kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya Qur'ani Tukufu ameruhusu ndoa ya wake wengi bali hata ndani ya Taurati hautakuta andiko linalozuia ndoa ya wake wengi, bali ndani yake kuna uthibitisho wa ndoa ya wake wengi kwa Mitume mingi ya Mwenyezi Mungu miongoni mwao akiwemo Nabii wa Mwenyezi Mungu Ibrahimu ( ) na Yakoub ( ) na Daud ( ) Amani ya Mwenyezi Mungu iwe kwao na kwa Mitume wote, ama Injili hatakuta andiko linaloharamisha ndoa ya wake wengi, hivyo Kanisa halikuwa linaharamisha ndoa ya wake wengi mpaka ndani ya karne ya kumi na saba ( ), bali kuna makundi ya Kikristo mpaka hivi sasa yanayofunga ndoa ya wake wengi kama vile dhehebu la Maronite na baadhi ya wafuasi wa Luther – Waprotestant – Ukristo haukuharamisha ndoa ya wake wengi isipokuwa kwa kupitia sheria za kiraia na wala si kwa andiko la Kitabu Kitakatifu ( ).
Na dalili ya hekima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kuhalalisha ndoa ya wake wengi ni pamoja na ile ulimwengu unavyoshuhudia matatizo yasiyo na ufumbuzi zaidi ya ufumbuzi uliopo kwenye Sharia za Mungu, na katika yanayosisitiza hayo ni takwimu hizi:
Tuangalie nchi ya Marekani:
• Mwaka 1982 80% ya wanawake walioolewa ndani ya kipindi cha miaka 15 walikuwa wameachika, ni upi ufumbuzi sahihi wa matatizo hayo? Na je ni bora wanawake hawa kuolewa na wanaume wengine wanaoendana nao au waishi kwenye matatizo ya upweke na useja?
• Ndani ya mwaka wa 1984 wanawake milioni 8 walikuwa wanaishi peke yao na watoto wao bila ya msaada wowote wa nje.
• Mwaka 1982 kumekuwa na kesi 65 za ubakaji wa mwanamke mmoja katika kila wanawake elfu 10.
• Mwaka 1995 kulikuwa na makosa ya uhalifu wa ubakaji elfu 82 miongoni mwayo 80% ni kwa upande wa familia na marafiki lakini polisi wanasema idadi hii sio sahihi ni zaidi.
• Mwaka 1997 kwa mujibu wa kauli za jumuia za kutetea haki za binadamu zinasema: Wanawake watatu walitekwa kila sekunde moja, wakati ambapo pande rasmi zilijibu kwa kusema idadi hii imeongezwa wakati ambapo idadi sahihi ni uwepo wa hali za ubakaji kwa kila sekunde 6.
• Mwaka 1980 – 1990: Marekani ilikuwa na wanawake wanaokaribia milioni moja ambao wanafanya kazi za ukahaba( ).
Idadi hizi ni matokeo ya kawaida yanayotufanya tuchukuwe nafasi ya mfumo wa ndoa za wake wengi na kuheshimika mwanamke ndani ya Sharia ya Kiislamu badala ya mfumo wa mpasuko wa maadili na maisha ya kimada na wapenzi kwa wanaoshambulia Sharia ya Kiislamu na kudai kuwa ndoa ya wake wengi ni jambo linalo haribu familia na maisha, je mfumo huu ni mzuri au kufungua mlango wa ndoa za wake wengi ili kuondoa matatizo haya? Kutokana na hayo serikali ya Ujerumani iliwasilisha ombi Makao Makuu ya Al-Azhar kuandika kitabu cha mfumo wa ndoa za wake wengi kwa sababu serikali inafikiria kunufaika na Azhar kupata ufumbuzi wa tatizo la kuongezeka kwa wanawake ( ).
Inaongezwa kwenye hilo kuwa jambo la ndoa ya wake wengi sio Sharia ya dini za mbinguni tu kama ilivyoelezwa bali ni jambo linalopatikana kwenye staarabu zingine pia, kwani kilichothibiti kihistoria ni kuwa ndoa ya wake wengi ni tukio ambalo limefahamika kwa mwanadamu tokea enzi za zamani sana, bali tukio hili lilikuwa limeenea kwa mafarao, na firauni maarufu kabisa ni Ramsis wa pili, alikuwa na wake wa nane vimada na vijakazi, na alizaa watoto zaidi ya mia na hamsini wakiume na wakike, na majina ya wake zake na watoto wake yameandikwa kwenye kuta za mahekalu mpaka leo hii.
Ndoa ya wake wengi ilikuwa imeenea sana kwa watu wenye asili ya “As-Salaafy” nao ni watu wa maeneo yanayofahamika hivi sasa kwa majina ya Warusi, Waserbia, Wacheki na Waslovakia, na yanakusanya pia wakazi wengi wa Lithuania, Estonia, Macedonia, Romania na Bulgaria.
Lakini Uislamu umeweka kiwango na idadi maalumu ya idadi hii ya wanawake wa kuolewa kutozidi wake wa nne, na ukaweka sharti la uadilifu kati ya wake hao, na wala haujaamrisha kila Mwislamu aoe wake wa nne, lakini umefanya kuoa wake wa nne ni halali, kwa mwenye uwezo wa kuwa na hao wake wa nne na ana uwezo wa kutekeleza haki zao ipasavyo na kwa hivyo basi inafaa kwake.
Hivyo Uislamu haukuanzisha ndoa ya wake wengi bali wenyewe umeweka idadi ya wake, wala haukuamrisha ndoa ya wake wengi kwa mfumo wa lazima bali umeruhusu ndoa hizo na kuziwekea idadi ya wake.
Uislamu umeweka Sharia ya ndoa ya wake wengi hata hivyo haukusahau madhara yanayoweza kutokea kwa mke wa kwanza kutokana na mtiririko wa idadi hii ya wake, lakini hata hivyo umeweka uwiano kati ya masilahi yanayopatikana kwenye ndoa ya wake wengi na masilahi ya kubakia kwenye ndoa ya mke mmoja na ukaondoa madhara makubwa zaidi kati ya madhara mawili na kuleta masilahi makubwa zaidi kati ya masilahi ya aina mbili.
Ndoa ya wake wengi ndani ya Uislamu ni sehemu ya mfumo mkubwa wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameubana kidogo upande mmoja kwa waja wake na kuwakunjulia upande mwingine, hivyo akaharamisha kumuangalia mwanamke aliye halali kwako kumwoa na akaharamisha kukaa naye peke yake, pia akaharamisha uzinzi na akahalalisha ndoa ya wake wengi.
Ama mfumo mwingine wenyewe hauamini isipokuwa uhuru wa mwanadamu na kuzidisha kwenye uhuru huu wala hauamini Mwenyezi Mungu wala hukumu zake na Sharia zake, kwani Uislamu unakuja na mfumo unaochojenga na mifumo mingine inakuja na muundo unaobomoa.
Hekima ya wake wengi katika mtazamo wa Uislamu
Kuna faida nyingi kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu Ameweka Sharia ya wake wengi, miongoni mwa faida hizo: Ni faida ya kijamii, pia kufikia masilahi ya kidini na kijamii pamoja na kulinda maadili mema.
Ama faida ya kijamii huonekana katika hali mbili hakuna yeyote anayepinga uwepo wake:
1. Wakati wa hali ya kuongezeka kwa wanawake zaidi ya wanaume, kama hali ilivyo ndani ya nchi nyingi duniani.
2. Wakati wa wanaume kuwa wachache zaidi ya wanawake ikiwa ni matokeo ya hali za kivita au majanga ya umma.
Ama faida ya kufikiwa kwa masilahi ya dini na jamii pamoja na kulinda maadili hufikiwa kwa sura zifuatazo:
1. Mke kuwa mgumba na mume anapenda na kuwa watoto, katika hali hiyo hakuna kizuizi kwake kuoa mke zaidi ya mmoja.
2. Mke kufikwa na maradhi sugu au yenye kuambukiza au kutengwa ambapo mume hawezi kumwingilia uingiliaji wa wanandoa, hivyo hapa mume anakuwa kati ya hali mbili: Ima kumuacha kwa talaka au kuoa mke wa pili na huyu wa kwanza kubakia kwenye usimamizi na ulezi wake, hakuna shaka kwa yeyote kuwa hali ya pili ina heshima zaidi na bora, na inaleta furaha zaidi kwa mke mgonjwa na kwa mume pia.
3. Mume kutokana na asili ya kazi yake kuwa na safari nyingi na ni ngumu kwake kusafiri na mke wake pamoja na watoto kila anapo safiri.
4. Mume kuwa na nguvu za kiume zaidi kiasi kinachopelekea kutotosheka na mke wake mmoja ima kwa utu uzima wa mke au udhaifu au kwa kuwa na siku nyingi ambazo haifai kufanya naye tendo la ndoa - nazo ni siku za hedhi, ujauzito, nifasi, na maradhi na mengineyo yanayofanana na hayo.
5. Mume kuwa na utashi wa kweli na dhamira thabiti ya kuwa na watoto, na kuwa na familia kubwa na kwa sababu hiyo jicho la Mtume S.A.W. litatulia katika kujifaharisha kwake mbele ya uma zingine siku ya Kiyama kwa ukubwa wa umma wake, kwani Mtume S.A.W. amesema: “Oeni wanawake muwapendao wenye kizazi kwani mimi kwa uwingi wenu huo nitajifaharisha nao kwa uma zingine siku ya Kiyama” ( ).
Ndoa ya wake wengi imekuwa yenye kufahamika na kuenea zaidi maeneo mbalimbali ya dunia kabla ya kuletwa kwa Mtume S.A.W. kuwa ni rehema kwa walimwengu.
Ndoa ya wake wengi ilikuwa haina mipaka wala udhibiti wa idadi ya wanawake, kama mifano inayoonesha hapakuwa na kiwango cha mwisho cha idadi ya wake wa kuoa.
Wala hapakuwa na sharti kwa mume kufanya uadilifu kati ya wake zake, au kugawa kati yao sawasawa kama ilivyo ni amri katika Uislamu.

Share this:

Related Fatwas