Sanamu Lenye Sauti

Egypt's Dar Al-Ifta

Sanamu Lenye Sauti

Question

Aya ya Qur'ani: {Na baada yake walimfanya ndama kutokana na mapambo yao (kumwabudu), kiwiliwili tu kilicho kuwa na sauti. Hivyo hawakuona kuwa hawaongeleshi wala hawaongoi njia? Wakamwabudu, na wakawa wenye kudhulumu}{AL-AARAF: 148}.
Na akasema: {Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa hiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri Msamaria * Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau}{TWAHA: 87, 88}.
Maana kwa Ujumla
 

Answer

 Mola Mtukufu Anampa habari ndani ya Aya hizi Tukufu Nabii wake Musa - amani ya Mungu iwe kwake - Kwa yale yaliyotokea kwa watu wake pale walipotanguliwa na utashi wa kufanya haraka kukutana na Mola Mtukufu. Mwenyezi Mungu Akasema kuwa sisi tumewapa mtihani watu wako baada ya kuondoka kwako na Samiriy akawapoteza na Musa aliporudi kwa watu wake alikuwa ni mwenye kukasirika mno akiwa na huzuni kubwa na akafanya mazungumo na watu wake kama yafuatayo: Enyi watu wangu hivi Mola wenu hajawaahidi ahadi njema kwa kuwateremsha Taurati, hivi ni kwanini mmebadilisha kunifuata mimi na mkaenda kinyume na miadi yangu, hivi muda wa kuwa mbali na nyinyi umekuwa ni mrefu sana au mmetaka hasira za Mola wenu ziwateremkie? Watu wake wakajibu kuwa sisi hatujakwenda kinyume na miadi yako kwa utashi wetu na hiyari yetu lakini dhambi zetu zimetubebesha kwenye mapambo ya watu kwa maana ya watu wa mjini na kutuingiza motoni kama alivyofanya Samiriy.
Kisha Mwenyezi Mungu anatoa habari kuwa Samiriy aliwatengenezea ndama mwenye mwili akiwa na sauti inayofanana na ndama wa ng’ombe, pindi watu wa Musa walipomwona ndama huyu wakawa wanasemezana wao kwa wao: Huyu ndio mola wenu na ndio mola wa Musa kwani Musa alimsahau au Samiriy alisahau mafundisho ya Musa.
Kauli ya mjenga hoja ni nini?
Sisi tunauliza: Ni wapi Qur'ani imeelezea habari hii ambayo haipo kwenye historia? Na je inaingia akilini kuwa ndama wa dhahabu anatoa sauti kama ndama asili? Na je Samiriy anayedhaniwa na hilo anatamani na kumtaka Haruna amuombee kwa Mungu na Mwenyezi Mungu anakubali na kuwezesha kutengenezwa sanamu lenye kutoa sauti ili kuwatia watu kwenye mtihani wa kuliabudia kinyume na kumwabudia Mwenyezi Mungu? Je! Samiriy na Haruna pamoja na Mungu wamekuwa washirika walioungana katika kutengeneza sanamu? ( )
Yanayochukuliwa kwenye shaka
1. Ni kipi chanzo cha kisa hiki ambacho kimeelezewa na Qur'ani kisichokuwa na msingi wowote katika historia?
2. Ni vipi akili inayofikiria eti ndama aliyetengenezwa kwa dhahabu anaweza kutoa sauti kama vile ndama wa asili?
3. Je! Samiriy alitamani ndama huyu awe anatoa sauti? Na je! Alimwomba Haruna hilo?
4. Ni vipi Mwenyezi Mungu Mtukufu anawezesha kutengenezwa vizuri sanamu hili na kutoa sauti ili kuwatia watu kwenye majaribu ya kuliabudu sanamu hili?
5. Je inafaa Samiriy na Haruna ambao wametengeneza sanamu, Mungu kuwasaidia kwenye hilo?

Kuondoa shaka
Je! Historia imevihukumu Vitabu Vitakatifu?
Muulizaji ameelezea shaka yake kwa kuuliza kuhusu chanzo cha kisa hiki Kitukufu, na kisa hiki Kitukufu ni ufunuo wa Mungu ambao ni sehemu kati ya ufunuo wa Mitume ya Mungu, kwani Qur'ani Tukufu ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho Mwenyezi Mungu amekiteremsha kwa Mtume wake Muhammad S.A.W. kama vile Taurati ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha kwa Mtume wake Musa - Amani ya Mungu iwe kwake - na Injili ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu alichokiteremsha kwa Mtume wake Isa - Amani ya Mungu iwe kwake - na kama hivyo kwa Mitume wengine waliobaki ambao Mwenyezi Mungu aliwateremshia Kitabu chake.
Na Aya zinaashiria kile wana wa Israili walichokifanya pindi Musa alipowaacha kwa ajili ya miadi na Mola wake, pale Samiriy alipoamua kuwatengenezea sanamu kutokana na mapambo yao likiwa kwenye umbile la ndama na kuwa na sauti kisha watu wakaliabudia badala ya kumuabudia Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kwanza kabisa: Shaka hii imekusanya ndani yake makosa ambayo ni kukanusha uthibiti wa “Kiakili” kwa sababu ya kupoteza uwepo na kutokubali akili hakuna maana ya kutokuwepo kwani muulizaji hapa amechukuwa dalili ya kutokuwepo habari hii na kutokuwepo kwa kisa hiki Kitukufu kwa kutothibiti katika marejeo ya Historia bali dalili hii inawezekana kumbadilisha muulizaji kwa kusema kuwa Aya Tukufu zimethibitisha kisa hiki kitukufu basi ni dalili ya kutokea kwake, na mwenye kudai kutokuwepo basi huyo ni mwongo kwenye hilo kwa sababu mthibitishaji hutangulizwa badala ya mkanushaji, kwani mthibitishaji anakuwa na ongezeko la elimu kama Wanachuoni walivyosema.
Marejeo ya histori pamoja na kuwa na faida nyingi isipokuwa yenyewe huwa na kama yanayokuwa kwa mwanadamu miongoni mwa kasoro usahaulifu na mambo mengine yanayokuwa kwa mwanadamu pamoja na marejeo ya historia yanakuwa na athari za mwanahistoria kwa kile anachoamini hivyo inawezekana kufahamu tukio moja kwa sura tofauti, na hii ni katika mlango wa kuathirika kwa mwanahistoria na sababu mbalimbali, ikiwa itaongezwa kwenye hilo umbali wa muda na uchache wa wanahistoria ndani ya zama hizi hilo linakuwa ni uthibitisho wa hoja ya Qur'ani Tukufu na ukweli wa Mtume mfikishaji, hivyo ni vipi ameweza fahamu habari hii na kuinukuu na yeye hajui kusoma na kuandika, na Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema kweli pale anaposema: {Namna hivi tunakuhadithia habari ya yaliyotangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa} {TWAHA: 99}.
Pamoja na yote haya, je? Vitabu vya historia vilivyoandikwa vimekusanya matukio mengine ndani ya nyakati zilizopita? Uwepo wa kisa hiki ndani ya Qur'ani Tukufu ni dalili kubwa ya ukweli wa Qur'ani Tukufu na muujiza wake pamoja na ukweli wa Mtume Mtukufu S.A.W.
Lakini sisi hatufuati chochote katika hili kwani msingi wa habari upo ndani ya vitabu vya historia bali na ndani ya Vitabu Vitakatifu vyenyewe, na tumetaja maeneo mwanzoni mwa jibu.
Kutengenezwa kwa ndama wa dhahabu ni jambo lililotajwa kwenye Vitabu Vitakatifu ambapo imekuja ndani ya Kitabu Kitakatifu – juzuu ya 1 uk. 169 – Kitabu cha Kutoka 4:32.
“Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri”.
Na ndani ya Kitabu Kitakatifu juzuu ya 2 uk. 269. Kitabu cha Nehemia 9: 18.
“Naam, hata walipojifanyia ndama wa dhahabu iliyomiminwa na kusema huyu ndiye mungu wako aliyekupandisha kutoka Misri, tena walikuwa wamefanya machukizo makuu”.
Na Kitabu Kitakatifu juzuu ya 1 uk. 170. Kitabu cha Kutoka: 32: 8.
“Wamepotea upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli iliyokuwa katika nchi ya Misri”.
Amesema mtunzi wa kitabu cha Manaar “Tumeelezea mara nyingi kuwa matukio ya historia na udhibiti wa kutokea kwake na nyakati zake pamoja na sehemu zake sio makusudio ya Qur'ani na yaliyomo miongoni mwa visa vya Mitume na watu wao ni ubainifu wa mwenendo wa Mwenyezi Mungu kwao na yanayofungamana miongoni mwa misingi ya dini( ), ni yenye manufaa kwa Waislamu mpaka Siku ya Malipo”.
Jambo lililo zuri ni kuwa sauti ya huyu ndama haikutajwa ndani ya Vitabu Vitakatifu nayo ndiyo iliyompelekea kupinga sana huyu mtu wa shaka akisema: Hivi inaingia akilini kuwa ndama wa dhahabu kutoa sauti kama vile ndama wa kweli?
Kana kwamba muulizaji hana habari ya yaliyofikiwa ya kutengenezwa kwa masanamu ndani ya zama hizo, na yanashuhudiwa hayo na ustaarabu uliopita wa kifarao kwa kutengenezwa masanamu mazuri miongoni mwayo ni sanamu la Ramsis wa pili, haukuwa ujuzi wa watu waliotangulia na ambao umeelezwa na Qur`ani sehemu ya ujuzi huo na kuthibitishwa na historia ya zamani na bado inathabitishwa na kugundulika katika utengenezaji wa masanamu tu bali imekusanya yaliyokuwa makubwa zaidi ya hayo miongoni mwa changamoto za kuandikwa historia ya wafalme kwenye kuta za mahekalu yao na wakatengeneza makaburi mwanadamu anashindwa kutafasiri namna ya ujenzi wake na kuishi kwa miaka mingi mpaka leo hii mfano wa ujenzi wa piramidi za zamani za Kimisri na makaburi ya wafalme wa miji ya Luxor na Aswan bali athari hizi zimekusanya kwa uwazi kushindwa kwa elimu na mwanadamu bado elimu inashindwa kufasiri kwa tafasiri ya mwisho kwa mfano kama kuelekea moja kwa moja miyale ya jua mara mbili kwa mwaka kwenye sura ya sanamu la Ramsis wa pili, siku ya kwanza ni ishara ya siku aliyozaliwa na siku nyingine ni siku ya kutawadhwa kwake, na zingine miongoni mwa athari na masanamu yaliyotengenezwa vizuri, haikuwa utengenezaji wa sanamu hili ambalo Qur'ani imetaja kisa chake isipokuwa ni mfano mdogo wa ujuzi huu ambao walikuwa nao Wamisri wa zamani na ambao Samiriy alikuwa anaishi nao, na kauli yenye nguvu ni Samiriy alijifunza kutoka kwao na akafanya vizuri utengenezaji huo wa sanamu ndipo akatengeneza hilo sanamu la ndama wa dhahabu ambalo Qur'ani imeelezea na kuelezewa na Vitabu Vitakatifu, akatengeneza na kuweka uwazi mfano wa filimbi au akaweka ndani yake kitu kinachofanana na filimbi hivyo kila hewa inapoingia inakuwa ni kama mchoma vyuma au upepo unatengeneza hii sauti, nalo ni jambo lilienea sana kwa watu wa Kanaan kwenye masanamu yao ambayo walikuwa wanayatengeneza.
Na katika hilo wameelezea wafasiri:
Kama ilivyokuja kwenye kitabu cha Tahriir wa Tanwiir juzuu ya 8 uk. 292:
Na kutoa sauti ilikuwa ni sauti ya ng’ombe, mtengenezaji wa ndama aliweka ndani ya tumbo la ndama uwazi mdogo maalumu na kuweka chombo cha kupuliza kwa ndani hivyo kila kinapotikisika chambo cha kupuliza hukandamiza hewa ndani yake na kuitoa kupitia sehemu nyembamba na kutoa sauti kama ya ng’ombe, na utengenezaji huu ni kama utengenezaji wa filimbi na zumari, na watu wa Kanaani walikuwa wanafanya mfano wa hivyo kwenye vitengenezwa vyao vinavyoitwa ndama.
Akasema tena mtunzi wa kitabu cha Tahriir wa Tanwiir juzuu ya 6 uk. 167.
Ni sauti ya ng’ombe, na aliyewatengenezea ndama alikuwa ni mwenye kujua utengenezaji wa mbinu ambayo walikuwa wanatengenezea masanamu na kuweka ndani yake na kwenye shingo matundu kama ya zumari hutokea humo sauti pindi inapopulizwa na upepo wa puto la mpuliza vyuma na mfano wake.
Samiriy aliwatengenezea sanamu kwa sura ya ndama kwa sababu walikuwa wamezoea nchini Misri kuabudia ndama Ibis, pindi walipoona kilichotengenezwa na Samiriy katika umbile la kitu cha kuabudiwa walichokifahamu tokea hapo zamani, na wakaona anaongeza kuwa na sauti, ndani ya fikra zao walijenga ufahamu kuwa huyo ndio mungu wao wa kweli ambaye walimuelezea kwa kauli yao {Huyu ndio mola wenu na ndio mola wa Musa} kwa sababu walimwona akiwa ametengenezwa kwa dhahabu au fedha, wakadhani kuwa ni bora zaidi kuliko ndama ya Ibis, na tahamaka walikuwa wanathibitisha mungu asiyeonekana kwa macho na walikuwa wanatafuta kumwona ndipo wakasema kumwambia Musa: {Tuoneshe Mungu kwa uwazi} wakati huo wakadhani kuwa huu ni upotovu wao uliowekwa, na kisa cha kumfanya ndama ya Kitabu cha Taurati hakiendani na mtazamo salama.
Bali Taahir Ibn Ashuur alielezea kwenye tafsiri ya Aya hizi maana hii ambapo alisema:
Kutoa: Ni kuonesha kile kilichokuwa kimezuiliwa, na kielelezo cha kutolewa ni ishara kuwa ametengeneza njama iliyojificha machoni mwao mpaka alipokamilisha.
Kitabu cha Tahrir wa Tanwir juzuu ya 16 uk. 174.
Neno kurusha: Ni kutupa kilichokuwa mkononi.
Na neno athari, ukweli wake: Ni alama zinazoachwa na mtu mwenye kutembea ikiwa ni alama ya nyayo kwenye mchanga au udongo, na imeelezewa hapo nyuma kwenye kauli ya Mola Mtukufu: {Akasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuatia}.
Pindi maneno haya yanapotumika kwenye maana inakuwa ni nimeona kwa maana ya nimejifunza na nimefuata, kwa maana ya nimefuata elimu ambayo hawajaifundisha nayo ni elimu ya kutengeneza masanamu na sura ambazo zimetengenezewa ndama, na elimu ya njama ambayo imetengeneza sauti ya ndama, na ikawa uminyaji wa hewa kwa maana ya sehemu ndogo, na athari ilikuwa kwa maana ya kujifunza kwa maana ya Sharia, na ilikuwa kutupa kwa maana ya kupuuza kwa maana nilikuwa ni mwenye maarifa ya jumla ya mwongozo wa Sharia, hivyo inafaa kutumika neno Mtume kwa maana iliyoenea na kufahamika naye ni aliyeteremshiwa ufunuo wa Sharia itokayo kwa Mungu na akaamrishwa kufikisha.
Na maana ikawa: Mimi kwa kazi yangu ya kutengeneza ndama wa kuabudiwa nimewakatisha wafuasi wa Sharia ya Musa, na maana ni kuwa: Amekiri mbele ya Musa kumtengeneza ndama na akakiri kuwa huyo ndama ni ujinga, na kuomba radhi kuwa hilo alipotoshwa na nafsi yake.
Timu ya wafasiri wamefasiri neno sauti kwa tafsiri nyingine sawa na yaliyopokelewa kutoka kwa Samiriy aliyepewa uelewa na Malaika Jibril - amani ya Mungu iwe kwake - nikakamata sehemu ya athari yake katika kutengeneza mapambo na kuwa na sauti hii baada ya kutengeneza ndama.
Anasema Ibn Kathiir katika tafasiri yake juzuu ya 3 uk. 475.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Anaeleza upotovu wa wana wa Israeli katika kuabudia kwao ndama, ambaye walitengenezewa na Samiriyy kutokana na mapambo yao, ambayo miongoni mwayo waliyazima, hivyo akawatengenezea ndama kisha akamwekea udongo ambao aliuchukuwa kutokana na athari za farasi wa Jibril - amani ya Mungu iwe kwake - hivyo ndama akawa ni umbile lenye sauti ya ng’ombe.
Wafasiri wametofautiana kwenye huyu ndama: Je! Alikuwa na nyama, damu, na sauti? Au aliendelea kuwa kwake wa dhahabu isipokuwa ndani yake anaingiziwa hewa na kutoa sauti kama ya ng’ombe? Kuna kauli mbili, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi. Tafasiri ya Imamu Alusy juzuu ya 6 uk. 365.
Imepokelewa kuwa Samiriy alipotengeneza ndama aliweka kwenye mdomo wa ndama udongo wa alama ya farasi wa Jibril - amani ya Mola iwe kwake - na kuwa hai, na wengine wakasema katika siri ya hilo jambo ni kuwa Jibril - amani ya Mungu iwe kwake - kwa kuwa kwake ndio roho tukufu nguvu zake zilipelekea udongo huo kuleta athari hiyo kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa jambo alilolitaka Mola Mtukufu, hali hiyo hailazimishi kuwa na uhai wa kile anachokifanya yeye mwenyewe Jibril - amani iwe kwake - kwa sababu jambo limefunganishwa na ruhusa nayo inakuwa kwa mujibu wa hukumu ambayo hakuna anayeijua isipokuwa ni Mwingi wa hekima na habari, na kuhusu kauli ya uhai wafasiri wengi wameelezea, na kuunga mkono kuwa sauti ilikuwa ni ya ng’ombe na wala si umbile la ng’ombe.
Ama kauli iliyoingia kwenye shaka zake
Je Samiriy anadhaniwa kuwa alimtaka Haruna kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akakubali kutengeneza sanamu zuri na kutoa sauti ili kuwaingiza watu kwenye majaribu ya kuabudu sanamu badala ya Mwenyezi Mungu?
Ndani yake kuna ishara ya kuleta shaka ambayo ilishajibiwa hapo nyuma kwa anuwani: Ni nani aliyetengeneza ndama ni Haruna au Samariy.
Ama ishara ya Mwenyezi Mungu kukubali na kauli yake baada ya hapo:
Je! Samiriy, Haruna, na Mungu walikuwa ni washirika wa pamoja katika kutengeneza sanamu! Kunakuza kasoro ya wazi katika kufahamu imani hukumu na kadari kwa huyu mtu mjenga shaka, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu Anaumba heri na shari anaumba mfalme na shetani anaumba Mtume mtiifu na kafiri mpingaji na kuandaa kwa kila Muumini na kafiri hiyari ya kukufuru na kuamini, si kwa sababu kuwa Yeye Mola Mtukufu anapenda ukafiri na kuuridhia lakini ni kwa lengo la kutoa mtihani.
Kwani imani ya Kiislamu inaamini kuwa mtihani au majaribu ni katika mwenendo wa Mungu Mtukufu ndani ya ulimwengu wake kumfanyia mtihani amtakaye katika waja wake na hukadiria shari kama anavyokadiria heri kwa sababu katika vyote hivyo viwili kuna masilahi.
Pili: Ama kauli yake kuwa Haruna ndiye aliyemtengeneza ndama, hili ni jambo la uzushi kwa Manabii na sisi hatukubaliana nao, kwa sababu Haruna ni Nabii na nyinyi mnakiri hilo basi ni vipi Nabii alinganie kwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kuwaita watu wake kwenye kuabudia ndama! Imamu Tahir amesema: “Imeandikwa kwenye Kitabu cha Kutoka cha Taurati katika sura ya thelathini ya mbili tatizo kubwa pindi walipodhani kuwa Haruna ndio aliyewatengenezea ndama pindi walipomwambi kuwa tutengenezee sisi mungu atakayekuwa anatembea mbele yetu kwa sababu sisi hatufahamu kitu gani Musa kimemfika huko mlimani, ndipo akawatengenezea ndama wa dhahabu na kuzingatia kuwa huyu ni katika athari za kufuata Taurati ya kweli baada ya kutekwa kwa Baably na ambaye aliyeandika tena hakufanya vizuri katika kuelezea kisa hiki, na miongoni mwa tunayoamini moja kwa moja ni kuwa Haruna ni mwenye kuzuiliwa kufanya makosa na hilo ni kwa sababu ni Mtume( ).
Tatu: Ama kauli yake kuwa Mji wa Samiriy haukuwepo ndani ya wakati huu na kutosheka na maelezo haya mapana na wala hakutaja dalili, naye katika hili hana haki ambapo marejeo mengi yanataja ukweli huu kama utakavyokuja katika tafsiri ya Aya Tukufu, ama kuwa kwake hafahamu hilo hili ni jambo halina umuhimu, ama kudai kuwa Qur'ani Tukufu ina makosa huu ni ujinga, ametaja mwenye kamusi ya Lisaan Al-Arab kuwa Samiriy ni kabila katika makabila ya wana wa Israeli na kunasibishwa na Samiriy amesema: “Samiriy ni kabila katika makabila ya wana wa Israeli ni watu ambao Mayahudi wanakwenda kinyume nao katika baadhi ya dini zao hunasibishwa na Samiriy ambaye aliabudu ndama ambaye alisikika kuwa na sauti” ( ), vilevile ametaja muandishi wa kitabu cha Taaji na amesema: Na Samiriyy na Samra ni kundi la Mayahudi ni katika kabila miongoni mwa makabila ya wana wa Israeli wanakwenda kinyume nao kwa maana ya Mayahudi katika baadhi ya hukumu zao ( ).
Vilevile ametaja Ibn Hazmi katika kitabu chake kuwa miongoni mwa Mayahudi kuna kundi kubwa linaloitwa Samiriyy, amesema hayo kwenye kitabu cha Mgangano wa wazi na uwongo wa wazi ndani ya kitabu ambacho Mayahudi wanakiita Taurati “Mwanzo wa hilo ni kuwa mikononi mwa Samiriyy ana taurati tofauti na Taurati iliyopo mikononi mwa kila Myahudi wanaelezea kuwa yenyewe ina nafasi kubwa na wanaamini kuwa ambayo ipo mikono ni mwa Mayahudi imetengenezwa na kubadilishwa, na Mayahudi wengine wanasema kuwa ambayo ipo mikononi mwa Samiriyy imetengenezwa na kubadilishwa” ( ).
Na mfano wa hayo anataja Shahristan katika kitabu ha mila na madhehebu kuwa wao ni kundi kubwa lenye mafundisho na ibada lakini ni lenye kugawika sana katika Mayahudi, na akasema: “Hawa Samiriy ni kundi linaloishi Jerusalem na baadhi ya vijiji nchini Misri…. Wamethibitisha Utume wa Musa na Haruna pamoja na Yuushaa Ibn Nuun – amani iwe kwao - na wakapinga utume uliofuata baada yao… na wakasema Taurati haikubashiri isipokuwa Nabii mmoja” ( ), angalia namna gani kabila hili linafahamika na namna gani ni kundi kubwa katika makundi ya Mayahudi na kujinasibisha kwa huyu Samiriy katika moja ya kauli kama ilivyofahamu na mjenga hoja amekua mjinga wa kutofahamu ukweli wote huu na kudai kuwa Qur'ani Tukufu ina makosa basi laana za Mwenyezi Mungu ziwashukie watu madhalimu. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi.
Ikiwa anataka kuwa mji haukuwepo basi hii pia ni kupinga kwake marejeo, mwandishi wa kamusi ya Al-Buldan anasema “Saamiraa ni lugha ya siri ya mwenye kuona… na ndani yake kuna lugha za saamiraa … Ikasemwa kuwa mji umejengwa na Saam na kunasibishwa na yeye kwa lugha ya Kifursi Saam raah” ( ), yote haya yanaonesha kuwa mji huu ni mkongwa sana na wala sio mpya kama anavyosema mjenga hoja.
Na kwa ujumla jina hili linaweza kuwa linanasibishwa na mji wa zamani sana au na kabila la zamani au halinasibishwi na kitu chochote bali ni jina la mtu, na katika makadirio yote hakuna shaka yoyote kwenye Aya Tukufu. Mwenyezi Mungu anajua zaidi.
Tafsiri:
Qur'ani Tukufu ni yenye kusadikisha na upingaji huu umeibuka baada ya kutokuwepo, kwani walifuata watangulizi wao Qur'ani, ubainifu wa hayo ninasema Mwenyezi Mungu Ameteremsha Kitabu chake kusadikisha Vitabu vilivyotangulia na kuvilinda. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:{Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda}{AL-MAIDAH: 48}. Pindi Kitabu kilipokuwa kinasadikisha na kulinda yaliyokuwa kabla yake, hilo ndilo lililopelekea mazungumzo kuhusu watu wa kitabu, Mayahudi na Wakristo, kwani Mwenyezi Mungu Amewataja kwa uwingi katika Aya nyingi na akataja kila kundi katika makundi hayo mawili kwa Aya mbalimbali, na ikawa katika Aya maalumu zilizowataja Wakristo ni Aya za Suratul Aal-Imran zikizungumzia kuhusu familia hii takatifu, na ilikuwa sababu ya kuteremka kwa Sura hii Tukufu ni Wakristo wa Najran, pindi walipotuma wajumbe woa kwenda kwa Mtume S.A.W. baada ya Mtume kuwatumia barua akiwalingania kuingia kwenye Uislamu na Mwenyezi Mungu Akamteremshia Sura hii na akawasomea kwani Mwenyezi Mungu Amesema kwa kuwazindua kuhusu kuwa na chanzo kimoja na lengo moja: {Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili Kabla yake, ziwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani}{AAL-IMRAAN: 3, 4}. Na Mwenyezi Mungu akakata kabisa utata wao kuhusu Nabii Isa na roho mtakatifu akasema: {Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye elimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila YeyeMwenye nguvu na Mwenye hikima}{AAL-IMRAAN: 18}. Na akamsomea Mtume wake jibu pale walipomjengea hoja Mola Mtukufu Akasema: {Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na pia walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu?} {AAL-IMRAAN: 20}. Kisha akawahadithia habari ya Aal-Imraan kwa kuanza na habari ya Mwenyezi Mungu kuwateulia wao akasema: {Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote. Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua}{AAL-IMRAAN: 33, 34}.
Akataja kisa hiki mwanzo wake ambao Wakristo hawana katika Vitabu vyao kwani Imamu Tahir amesema: “Hakuna ndani ya Vitabu vya Wakristo utajo wa jina la Baba wa Bibi Maryam Mama wa Nabii Isa wala mtoto wake lakini kimeanza kwa mstukizo kuwa bikira Maria akiwa kwenye kijiji cha Nasrah alichumbiwa na Yusuf Najjar akapata ujauzito pasi na kuwa na mume” ( ), nayo ni maombi ya Mke wa Mzee Imran ambaye ni Mama wa Bi. Maryam: {Pindi mke wa Imran aliposema. Ewe Mola hakika mimi nimeweka nadhiri kwako kile kilichomo tumboni mwangu awe ni mtumishi wa dini, hivyo naomba unikubalie maombi yangu hakika yako Wewe ni Msikivu Mjuzi}.
Pamoja na ujumbe huu wa Wakristo kusikia ukweli huu kuhusu Bi. Maryam wao hawakupinga na wakajisalimisha kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa na uwezekano wa kupinga na kuwa hawalazimiki kumuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu lakini hata hivyo walijisalimisha na kuwa wanyenyekevu, hivi walikuwa na Injili inaeleza hivyo wakawa wameipoteza au watangulizi wao walitengeneza ukweli huu hivyo wao hawakuukuta! Kama kawaida yao ya kupoteza Vitabu vyao na kuweka maneno yao si katika sehemu yake, au anataka kushawishi juu ya Qur'ani ikiwa ni kuthibitisha kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur`ani hii, na timueni zogo, huenda mkashinda}{FUSWILAT: 26}. Sura hii imetuhadithia pia kisa cha Mama yake Bi. Maryam pale alipojifungu, na mfano wa hilo alifanya Jafar Ibn Abi Talib huko Habasha wala hakupingwa na yeyote pamoja na kuwa watu wa Habasha walikuwa ni Wakristo.

 

 

Share this:

Related Fatwas