Shaka Kuhusu Maana ya Ulinganiaji.
Question
Matokeo ya hali inayoishi kazi ya ulinganiaji kunapelekea maswali mengi kwenye uwanja huo ndani na nje yake kwa mfano: Ni vipi ulinganiaji utakuwa mmoja kwenye wigo wa tofauti za marejeo ya Kiislamu? Kwa kiwango gani ulinganiaji unamgusa mwanadamu kama mwanadamu? Na kipi maalumu na cha wote kwenya ulinganiaji huu? Na je ulinganiaji wa Kiislamu unaruhusu maisha ya pamoja na wasiokuwa waislamu? Kisha swali kuhusu muundo wa ulinganiaji? Na kuhusu weledi wake? Na je ulinganiaji ni sura mpya ya ukabila? Au je ulinganiaji utakuwa ni sura ya matumizi ya mali ili kuingia kwenye dini?
Baada ya kufahamika hali inayopitia maana ya kazi ya ulinganiaji na mchango wa fikra za msimamo wa kati na kati,
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ulinganiaji ni chanzo cha kauli yao: Fulani ameita kwenye kitu, kwa maana ya kukileta kitu kwako kwa kutumia sauti na maneno yatokayo kwako ( ), na inasemwa: Nimemuita fulani, kwa maana ya nimetoa sauti na kumuita, na kulingania pia ni mara moja ya maombi au duwa ( ).
Na kulingania katika Uislamu ni mfumo usiotengana na maana hii, na pembezoni mwake hutengenezeka mfumo maana yake ni kufanya juhudi baada ya uelewa na kuamini, kufanya juhudi – kwa njia zake zote halali na zilizopo – kwenye kuelezea sifa za dini hii na kuonesha vipengele vyake na kuboresha sura yake pamoja na kuzilainisha nyoyo kwenye hilo na kuondoa shaka pamoja na kufungua sababu zenye kupelekea kwenye hilo ( ).
Qur`ani Tukufu kupitia Aya zake nyingi inaelezea mfumo wa maana za ulinganiaji ikiwa ni pamoja na ufikishaji ubainifu ukumbusho nasaha njia hekima mawaidha mazuri na mijadala kigezo chema kuamrisha mema kukataza maovu kubashiria kuonya kushirikiana kwenye mema na ucha-Mungu.
Maana ya ulinganiaji imezaliwa wakati wa kuzaliwa kwa ulinganiaji wenyewe kwa maana ya kuanza kwa ukhalifa ambapo ulinganiaji ni kutanguliwa kwa Utume, na walinganiaji na wafikishaji wa ujumbe wa Manabii na wasiokuwa Manabii pamoja na kuzingatia sifa za kila kipindi na kazi zinazofanywa na ulinganiaji, miongoni mwa Manabii waliotumwa kwa watu wao maalum, na aliyepelekwa kwa watu wake maalum jukumu lake kuwalingania wengine kumfuata Mtume wa mwisho ambaye ameletwa kwa watu wote, kisha ulinganiaji unahama kutoka kwa watangulizi miongoni mwa wale waliobeba amana yake na kuifanyia kazi vizuri mpaka ulinganiaji ukapiga hatua ndani ya kipindi ambacho nyota yake ilififia sambamba na umma kusimama kutekeleza wajibu wake kama vile Jihadi kujitosheleza kijamii mpaka ulipotokea mlipuko wa ustaarau na kufungua macho ya walinganiaji wa umma kwenye mahitaji mengine mapya yanayohitajika na kazi ya ulinganiaji.
Na Tawheed pamoja na ndugu zake ni katika mfumo wa maana ya msingi wa Kiislamu mfano wa ibada amri mbalimbali imani fikra marejeo na mengine miongoni mwa vipengele vya mfumo wa uelewa wa kitawheed, ukiwa ni muundo na mfumo unaokusanya vyote na kuzuia ambapo ulinganiaji huu hutoa sifa zake na kukutana chini ya bendera yake umma wote, umma wa ulinganiaji na wa kuitikia nao ni mfumo wa kinga na kuponya maradhi mengi ya ulinganiaji, kwani Tawheed na ndugu zake ndio mdhibiti wa marejeo na mlinzi wa upotoshaji, ni marejeo ya mtu binafsi au taasisi.
Kama vile Tawheed ndio kitenganishi kinazuia kuto yayuka kwa ulinganiaji kwa kitu kingine, kwani kulingania bila ya mfumo wa Tawheed ni chombo kilicho wazi hakina mfikishaji kwa walinganiwa, kama vile Tawheed ni maana inayokusanya kwa upana wake watu ndani ya umma haikosekani kukuta kinachowaunganisha ili kukifanyia kazi kwenye marejeo yake na makusudio yake au katika kugawa nafasi zake.
Mizani ya ulinganiaji wa kati na kati unaofungamana na mfumo wa makusudio, uwiano kati ya kuleta masilahi na kuondoa maovu ndio usalama wa ulinganiaji kutokana na misimamo mikali ya mfumo wa upande wa kuume au wa kushoto, na makusudio ndio mizani ya kukadiria vipaombele vya ulinganiaji ( ), hivyo kazi za ulinganiaji pamoja na makusudio hulinda na hulindwa haiwezekani kutenganishwa kimoja na chengine.
Kumlinda mwanadamu ni muhimili wa kazi za ulinganiaji kama vile ni muhimili wa makusudio ya Sharia, ulinganiaji unaanza kwa kutengeneza maana ya uhai. Mola Mtukufu Anasema:
{Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi mnasikia * Wala msiwe kama wale wanao sema: Tumesikia, na kumbe hawasikii * Hakika wanyama waovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi na bubu wasio tumia akili zao * Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao angewasikilizisha, na lau ange wasikilizisha wangeli geuka wakapuuza * Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa} [AL-ANFAAL: 20 – 24].
{Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya} [AL-AN'AAM: 122]. Hivyo mwenye kuitikia wito huyo yupo hai na mwenye kupuuza wito huyo ni mfu, na muongozo wa mwanadamu na mafanikio yake hufungamana na ulinganiaji huu. Mwenyezi Mungu Anasema:
{Na yule aliye amini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni mimi, nitakuongozeni njia ya uwongozi mwema * Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya kudumu * Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake, na anaye tenda wema, akiwa mwanamme au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hesabu * Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uwokofu, nanyi mnaniita kwenye Moto? * Mnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami nakuiteni kwa Mwenye nguvu Mwenye kusamehe? * Bila ya shaka mnaye niitia kumuabudu hastahiki wito duniani wala Akhera. Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanao pindukia mipaka ndio watu wa Motoni! * Basi mtayakumbuka ninayo kuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja wake} [GHAAFER: 38 – 44].
Ulinganiaji hulinganiwa mwanadamu kwa pande zake zote za kiakili kimwili na kiroho na kujibu maswali ya mwanadmu wa aina zote na watofauti zote za kimajukumu.
Maana ya kumlingania mwanadamu inafungamana na aina mbambali miongoni mwazo:
• Maana ya Ulinganiaji na Umma ni ndugu, ulinganiaji na Tawheed ni vipimo viwili vya kutafautisha watu wao kwa wao, na kwa msingi wa maana ya ulinganiaji watu hugawanyika katika Umma mbili: Umma wa kwanza ni Umma wa kulingania, na Umma wa pili ni Umma wa kuitikia ulinganiaji, na pande zote mbili ndio kusudio la kumlingania Muislamu, kisha hutengenezeka mtazamo wa Muislamu kwa ulimwengu, kwani ulimwengu wote unatokana na Umma wake na kwa kiwango cha kuungana na Tawheed kiwango cha mazungumzo na ulinganiaji huanza kwa kuanzia mazungumzo ya Kiacademi na kupanda kutoka kwenye busara na hekima kwenda kwenye mawaidha mazuri na kufikia majadiliano mazuri mpaka kufika mwisho wa kulinda kazi za ulinganiaji kwa kupambana “Jihadi”.
• Ulinganiaji ni moja ya mfumo wa lazima unayotosheleza ambao Umma umeambiwa ili kuifanya kazi hiyo kwa kutoshelezana na kwa ubora zaidi.
• Kazi za ulinganiaji hazijitengi na mlinganiaji mwenyewe, hivyo kumlinda mlinganiaji ni makusudio ya ulinganiaji na njia miongoni mwa njia zake, na kumlinda mlinganiaji ni kusimamia malezi yake na uwezo wake, kisha ulinganiaji unafungamana sana na maana ya Maarifa na Wasifu mzuri kwani ni mambo mawili yanayosimamia kumuwezesha mlinganiaji, ulinganiaji ni elimu na sanaa, na elimu inahitaji utafiti nao ni uwanja wa kiweledi unahitaji uzoefu, na katika ukati na kati wa ulinganiaji ni kuwa kati ya weledi na umahiri wa kazi, kwani vyote huzungumzishwa kwa vitendo kulingana na uwezo wa mtu na uzoefu wake.
• Ikiwa ulinganiaji ni ubainifu wa kile anacholinganiwa mtu kwa sura yenye mvuto na utakelezaji wa wajibu wa kufikisha wala isichukuliwe kwa njia ya kutenza nguvu kwani yenyewe ni haki ya kueleza na haki ya kutafautiana lakini pia ni haki ya ufikishaji.
• Maana ya ulinganiaji inafungamana kihistoria na kilugha na maana ya kiufanisi, kwani ulinganiaji ni ndugu wa kazi za kuamrisha mema na kukataza maovu vile vile kuathiri kisha kubadilika.
• Ikiwa kazi za ulinganiaji ni chombo cha mabadiliko ya kibinadamu kijamii bali kisiasa na kiuchumi, yenyewe haiwezi kugawika – kwa hali yeyote – na utendaji kwani ulinganiaji ni juhudi za kuendewa na mlinganiaji kati kati, hiyo kati kati ni uhalisia wa ulimwengu wake tofauti na kuufahamu kwake na kuwa na umahiri nao ni jambo muhimu sana kwa mlinganiaji.
• Ukweli ni maana yenye mabadiliko makubwa, na haki ya mabadiliko lazima iambatane na harakati kubwa za kuleta mitazamo mipya na jitihada kwa kiwango cha yanayotokea kwa jamii za watu, na kwa kiwango cha kupatia fikra mbalimbali kwenye ulimwengu halisi na taasisi mifumo na watu kwa hali ambayo hasa fikra mpya za ulinganiaji na jitihada pamoja na mifumo, kwani mifumo ni mingi kulingana na jitihada na fikra mpya, hivyo maana ya jitihada ni fikra mpya ni maana mbili zenye kulinda na kusimamia kazi za ulinganiaji na harakati zake pamoja na uwezo wake wa kuvuka zama na sehemu.
Na katika utu wa ulinganiaji ni kunufaika na kila jaribio la kibinadamu katika upana wa majaribio ya kibinadamu kidini kisiasa na kijamii pamoja na kuzingatia marejeo makuu na mifumo ya kimaarifa ni sawa sawa kwa upande wa nadharia au vitendo.
Maana ya ulinganiaji inakamilishana na maana ya jitihada ili kupanua ulinganiaji wa misingi ya kati na kati, kwani walinganiaji ni watu wanaofanya jitihada kubwa ambayo wanaifanya katika kufikia makusudio baada ya kufikia jitihada za kiulinganiaji ni wenye kulipwa malipo mema wakipatia au wakikosea, kwa mwenye kupatia ana malipo ya aina mbili na mwenye kukosea ana malipo ya aina moja, kisha hakuna kupinga kwa mfanya jitihada kwenye kujitahidi kwake, kwani jambo la jitihada ni lenye kukubali tofauti ambapo ulimwengu wa dhana na fikra ni mpana sana na watu wote wanabaki katika wigo wa kukosea na kufanya vizuri, na ili ulinganiaji kulinda nafasi yake na kuwa kazi ya ulinganiaji ni kubwa zaidi ya mlinganiaji, na Uislamu mkubwa zaidi ya wanajitihada.
Kwa ufafanuzi huu ambao unalenga maana ya jitihada na kwa kuifanyia kazi kanuni ya Kisharia ambayo inaelezea kuwa jitihada inakubali kugawika hivyo walinganiaji wenye kufanya juhudi kubwa wanapaswa kuchunga kuwa mahusiano kati ya juhudi zetu kwenye mfumo wetu wa kimaarifa zimejengwa kwa msingi wa mashirikiano na wala si mvutano, hivyo jitihada hulinda ulinganiaji kuzalisha harakati au taasisi au kujibu ulinganiaji bila ya kitu kingine na vyote vikafanya kazi kupitia mwanya wa kinadharia ambao kila mmoja anasimamia kulinda na kuchukuwa tahadhari ya kuingizwa Uislamu kwa upande wake.
Na katika ukati na kati wa ulinganiaji ni kulinda njia zake, hivyo ni lazima kwa wanaofanya kazi kwenye sekta hiyo ya ulinganiaji kujitengea muda mwingi katika kubuni njia na mifumo itakayofikia makusudio ya ulinganiaji yanayoendana na wakati wa ulinganiaji na sehemu ya ulinganiaji pamoja na watu walinganiwaji, na njia zake haziishii kwa mlinganiaji tu bali zinaendelea na kufikia kwa upande wa vitu na watu mifumo na taasisi, kisha kulinda kubakia ulinganiaji kuendelea kwake ndani ya zama zote na kuvuka maeneo yote, kisha kulinda mwisho ambapo njia humalizikia kwa kufikia makusudio yake au kutokubaliana na wakati na sehemu ( ), kwani Fiqhi halisi ya uwiano na vipaombele hulinda kazi za ulinganiaji kutokana na uovu wa njia za kuendea makusudio.
Na katika ukati na kati pia wa ulinganiaji na kufanya juhudi ni kuto haribu urithi wa kibinadamu ikiwa ni kama sehemu ya jaribio la kibinadamu na kutokana na urithi huo umezaliwa urithi wa dini kwa ujumla ambao unashirikiana na urithi wetu katika kiwango kisicho na ubaya, kisha urithi wa Kiislamu kwa pande zake za kauli ya moja kwa moja au kauli inayokubali dhana na tofauti ambapo zenyewe ni jaribio litokanalo na nadharia na utekelezaji wa marejeo yetu yenye kuchanganyika na mfumo wetu wa kimaarifa, hivyo kuuharibu ni kuharibu uwezo wa kulinda urithi kwa kulinda kiwango cha kazi za ulinganiaji.
Kama vile miongoni mwa ukati na kati wa ulinganiaji ni pamoja na kusikiliza wito wa mwingine na kukubali wito wa kwenye kheiri na kumsaidia kwenye hilo ikiwa ni kuhudumia jengo zima au kuhudumia wasifu mzuri au ibada. Mwenyezi Mungu Amesema:
{Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia * Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za watawa, na Makanisa, Masinagogi na Misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu} [AL HAJJ: 39, 40].
Tunafanyia kazi yale tuliyokubaliana na kusameheana sisi kwa sisi katika yale tuliyotafautiana jambo lililofanya kuwepo ushirika kati ya walinganiaji na watu wote.
Baada ya maelezo hayo na kwa namna hii utaona ni namna gani mfumo wa makusudio ya Sharia unatujengea maana ya ulinganiaji kwa kuonesha upande wa kibinadamu kuwa ni moja ya maana na uelewa wa Uislamu wa huruma kwani pindi kiungo kimoja kinapopata maumivu basi mwili mzima huhisi homa ikiwa kulinda ukati na kati wa ulinganiaji kutofikwa na walinganiaji wa misimamo mikali na kuulinda kutokana na maradhi ambayo hufikwa ulinganiaji ambao haujavaa vazi la makusudio yake.