Kisa cha Watu wa Jumamosi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kisa cha Watu wa Jumamosi

Question

Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Na waulize habari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko) Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu} [AL-A'ARAAF: 163].
Ni vipi tunaleta hisia Mungu anawajibu waja wake kwa uovu, na kuwapesishia uovu kwa kuonekana samaki siku ya Jumamosi?
Wakati Injili inasema: “Mtu ajariwapo asiseme, Ninajaribiwa na Mungu maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu * lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa” [Yakobo. 1: 13,14].
 

Answer

 Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kituo cha tafiti za mambo ya Kisharia Ofisi ya Mufti wa Misri.
Uthibiti wa kihistoria wa kisa cha watu wa jumamosi:
Kisa hiki kwa upande wa uthibiti wa kihistoria bila ya kuangalia Qur`ani hakuna kinachosukuma na kuunga mkono kutopinga Wayahudi wa Madina na waliofuata baada yao mpaka leo hii, pamoja na kuwa wamekisikia mara nyingi kutoka kwa Waislamu, na katika hili kuna muujiza wa kihistoria wa Qur`ani Tukufu.
Majaribu ni mwenendo wa Mungu:
Katika mwenendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuwajaribu waja wake ili kuonekana Muumini katika wanafiki, na wala hakuna yeyote katika watu wa dini sahihi anayepinga mwenendo huu wa Mungu ambao mara nyingi huelezea kwa ufafanuzi wa maisha ya Manabii na Waumini, kwa mfano Nabii Yusuf A.S Nabii Ayub Yahya na Isa A.S wamejaribiwa kwa mitihani migumu na Waumini wengi pia, na huenda majaribu haya kwa wanafiki na makafiri ili iwe hoja dhidi yao siku ya kiyama wakati wa kuingia kwao motoni, jambo ambalo tunaweza kuliita ni hatua ya kuchukuwa pole pole ikiwa kuifanyia kazi kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na wale walio kadhibisha Ishara zetu, tutawachukuwa pole pole kwa namna ambayo wenyewe hawaijui} [AL-A'ARAAF: 182].
Na juu ya hili hufasiri kila yanayotokea kwa wapingaji katika mambo ya heri kwa uwazi naye kwa ndani ni mpingaji wa Sharia ya Mwenyezi Mungu.
Kati ya Qur'ani na Injili:
Sura ambayo ameichukua kama dalili huyu mwenye kudai kukiukwa kwa mwenendo huu wa kilimwengu, kisha Qur`ani Tukufu kukiuka ni ujumbe wa Nabii Yakub kwa makundi kumi na mawili ambayo yapo tofauti, katika hili hakuna hoja dhidi ya Qur`ani Tukufu ambapo Wakristo kwa kukiri kwao wenyewe ujumbe wa Nabii Yakob ni wa kutengenezwa na wanadamu kama vile vitabu vyao vyingine, na wala si ujumbe ulioteremshwa toka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hata usiwe na mgongano kati ya maana yake na kisa cha watu wa siku ya Jumamosi kwa sababu maana ya pamoja ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu huwafanyia majaribu baadhi ya waja wake kuanzia kuelezea na kubainisha madaraja yao katika mema na kuthibiti kwa amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na huwafanyia majaribu baadhi ya waja wake ili kubaini waovu wao na wavunjaji wa ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na jaribu hili hutokea kwa sababu za mapungufu yao na matumizi mabaya ya matamanio yao, na wala sio ibara ya jaribu tu kama ilivyotangulia katika aina ya kwanza kwa maana ya jaribu la kuinua na kuapndisha, na haya ndio makusudio ya kauli ya Mola Mtukufu kwenye Aya Tukufu: {Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu} vile vile kauli ya Mola Mtukufu: {Na tukawatesa waliodhulumu kwa adhabu mbaya kwa vile walivyo kuwa wakifanya upotovu} na kusudio la Nabii Yakub katika ujumbe wake huu ambao aliutuma ni kuufanya kwao watuhumiane mapungufu wao wenyewe, kwani njia hii ni kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu na kuinuliwa kwake, kwani Mwanachuoni Twahir Aashur anasema katika tafasiri ya kauli ya Mwenyezi Mungu: {Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu} kwa maana ya tunaupa mitihani utiifu wao kwa kuwaingiza kwenye maasi nayo ni kuwepo kwa tamaa iliyokatazwa, na jumla Aya inayosema: {Kwa maana hiyo tuliwajaribu} imeanza tena kwa kubainisha jibu la mwenye kusema, ni nini faida ya Aya hii pamoja na Mwenyezi Mungu kufahamu kuwa wao hawajari kukiuka uharamu wa siku ya jumamosi ( ).
Imamu Al-Aluusy anasema: “Maana yake tunatendeana nao kwa utendaji wa kuwafanyia majaribu ili kuonesha miongoni mwao wanayo yaonesha hivyo tunawachukuwa kwa hayo, na umekuja muundo wa kitenzi cha wakati uliopo ili kuelezea hali iliyopita na kuileta sura yake pamoja na kushangaza ( ).

Share this:

Related Fatwas