Jawabu la Lamma Halikuja

Egypt's Dar Al-Ifta

Jawabu la Lamma Halikuja

Question

Matini ya Qur`ani:
Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui} [YUSUF:15]
Muulizaji amesemaje?!
 

Answer

Liko wapi jawabu la LAMMA? Lau ingeondoshwa WAAW iliyo kabla ya AWHAYNAA maana ingesimama sawa.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Muulizaji hana elimu ya kutosha katika fani ya Nahwu na Balagha elimu hizi zina athari kubwa katika tafiti ya Ijaz (kufupisha) katika lugha ya Kiarabu. Anasema mwanazuoni Alltahir “Na Jawab la (Lamma) limeondolewa kilichojulisha ni neno {wamtumbukize ndani ya kisima} na kukadiria ni wakatumbukiza ndani ya kisima. Na mfano wa hili ni mingi ndani ya Qur`ani. Na hili ni katika Ijaz (kufupisha) maalumu kwa Qur`ani huko ni kupunguza maneno ili kudhihirisha maana”.
Miongoni mwa dalili za kuondoshwa jawabu la LAMMA katika Aya Tukufu:
Kuondoshwa jawabu la “LAMMA” kinachokusudiwa hapa kuyakuza na kuonesha ubaya wa kile walichokifanya ndugu wa Yussuf kwa Yussuf baada ya baba yao kuwaruhusu kwenda naye jangwani, na imepokewa kwamba walikuwa wanamkera kwa maneno na vitendo wakiwa njiani kuelekea sehemu waliyoitaka mpaka walikaribia kumwua, na dalili ya hilo ni neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu likisimulia aliyosasema mmoja wa ndugu zake: “ Akasema msemaji kati yao: Msimwue Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima. Wasafiri watakuja mwokota; kama nyinyi mna sharti ya kufanya jambo.” Kukataza kuua kunakuja baada ya kuazimia kufanya hivyo na kuchukua sababu, hivyo likaondoshwa jawabu la “LAMMA” ili kila nafsi iwe na mtizamo wa kila mwelekeo, na kuondoshwa jawabu kuna dalili kwa urefu wa yaliyotokea kwao na kwa kushangaza kwake na ubaya wake, hivyo basi, Imamu Al-Zamakhshary amesema: “Walimfanyia waliyomfanyia miongoni mwa maudhi… na wakamdhihirishia uadui, kumtesa na kumpiga, akiomba msaada kwa yeyote hamsaidii isipokuwa kwa kipigo …” Imamu Al-Badhawiy amesema hivi pia. Na wengine wamesema njia nyingine katika kukadiria jawabu, na kilichopelekea tofauti hii katika kukadiria jawabu lililoondoshwa ni huko kuondoshwa kwake.
Je! kuondoshwa WAAW kunasahihisha maana:
Ama pendekezo la aliyeuliza utata huu kuondoshwa heru WAAW katika neno “WAAWHYNAA” ili maana inyooke ni kosa kubwa, kwa sababu “AWHYNAA” sio jawabu la “LAMMA” bali imeunganishwa katika jawabu lilikadiriwa, kwa sababu jawabu la “LAMMA” ni kile kilichomtokea Yussuf kutoka kwa ndugu zake baada tu ya kutoka naye kwa baba yake kusogea naye mbali kidogo. Na dalili ya hilo ni kuunganisha kwa herufi ya FEI katika “FALAMMA” kwa sababu hiyo inajulisha uharaka na mpangilio.
Imamu Abdulqadir Al-Jarjany sheikh wa elimu ya balagha katika kuielezea kuondoshwa huku kibalagha na uzuri wa faida zake: “ Ni tafiti ya ndani sana, nzuri, na ya ajabu inayofanana na uchawi, kwa sababu unaona kwamba kuacha kutajwa ni fasaha zaidi kuliko kutajwa, kunyamaza kutoitaja kumeongeza faida, na unakuta imetamkwa pale ambapo haikutamkwa, ipo wazi zaidi ikiwa haikubainishwa”.
Sheikh Al-Mut’any Allah Amrehemu anasema: “Utata huu unafungamana na fani ya kuondosha, na huu ni upande wa kibalagha zaidi kuliko kinahwu… na hii ni nafasi ya kuondosha katika elimu ya Bayani ya Kiarabu, kulikozoeleka katika maneno ya kila siku, ni maarufu sana katika Qur`ani Tukufu, hakuna Sura iliyokosa hilo takriban, wala Aya kati ya Aya zake, na maana ambazo zimeondoshwa katika Qur`ani zinakaribia kuwa sawa na robo ya maana zote za Qur`ani. Na huu ni Mtaala mpana sana na wa hekima katika Mitaala ya lugha ya Kiarabu isiyo na mfano.
Hivyo basi, tunaona mwanachuoni mkubwa wa Lugha Ibdu Janaa ameiita katika kitabu chake cha “Al-Khasais” jina la kimzaha, nalo ni “A-Shujaa Al-Arabiya”. Na kuondoshwa kunanasibiana na fani ya Balagha, baadhi ya wanazuoni wameifanya fani hii, ni “Fani ya Al-Ijaaza” ikiwa na maana maneno macheche yenye maana nyingi, na ina nafasi ya juu na vitu vinavyotosheleza malengo yake”

 

Share this:

Related Fatwas