Kwa nini Sharia ya Kiislamu Imerurhusu kwa Mwanamume Kuoa Wake Wengi, na Haikuruhusu kwa Manamke Kuolewa na Wanaume Wengi?
Question
Matni ya shaka
Imekuja Aya katika Qur`ani Tukufu isemeyo: {basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu" ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} [AN NISAA: 3]
Answer
Nasi tunauliza: Kwa nini Sharia ya Uislamu imerurhusu kwa mwanamume kuoa wake wengi, na haikuruhusu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wengi pamoja na kwamba kuoa wake wengi ni kinyume na mwenendo Aliouweka Mwenyezi Mungu tangu Alipoanza kuumba? Mwenyezi Mungu Amemuumba Hawa mmoja na Adam mmoja.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kuna sababu nyingi za msingi ambazo zinapelekea kuoa wake wengi; miongoni mwazo ni kwamba idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume, miongoni mwazo, wanaume ni wachache kuliko wanawake kutokana na vita au majanga. Miongoni mwazo pia: mke anaweza kuwa tasa hazai na mume anapenda kupata watoto na ana uwezo wa hilo, na nyinginezo miongoni mwa mambo ya msingi.
Vilevile kuna faida nyingi zinarudi kwa jamii katika kuoa wake wengi, miongoni mwazo: Kuongezeka kizazi ambapo jamii inanufaika, na Mtume S.W.A amesema: “ Oeni wanawake wanaowapenda sana, wazaaji sana, kwani hakika mimi hakika mimi nitajifaharisha kwa uma mkubwa siku ya kiama” na faida nyingine mbalimbali.
Baada ya hayo, swali linakuja lenyewe ni, Je, kuna mambo ya msingi yanayopelekea kuoa wake wengi? Au kuna madhara katika kuoa wake wengi?
Kwanza: Wataalamu wa elimu ya seikolojia wamethitisha kwamba mwanamke anapenda mmoja tu, wakati ambapo mwanamume anaweza kupenda zaidi ya mmoja.
Pili: Inajulikana kwamba mwanamke ndio mfuko wa mbegu za mwanamume, kama ataolewa na mume zaidi ya mmoja hakutasaidia kuongeza uma; kwa sababu mwanamke hashiki mimba isipokuwa kwa tendo moja kipindi cha mzunguuko wake wa kila mwezi, kuolewa na mwanamume zaidi ya mmoja hakutasababisha isipokuwa kuchanganya koo na maradhi, wakati ambapo ni muhali kuongeza uwezo wake wa kuzaa kama tulivyoeleza.
Hivyo basi, kuoa mke zaidi ya mmoja kuna masilahi kwa mwanamke kwa kutokosa kuolewa, na kwa mwanamume kutochelewa manufaa yake kama mwanamke atakuwa na udhuru, na masilahi kwa uma kwa kuongezeka idadi ya watu, hilo ni Sharia ya Mwenyezi Mungu Mwenye hekima na mjuzi, ama mwanamke kuwa na wanaume wengi, hakuna masilahi au faida yoyote, wala hakuna ulazima wa kutaka hilo, bali tabia iliyosalama na maumbile yanakataa hilo na kulipinga.
Na katika ambayo yanapasa kutanabahisha ni kwamba Uislamu ulipohalalisha kuoa mke zaidi ya mmoja, umeweka kikomo mwisho wanne, na ukaweka vidhibiti kwamba mume awe na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa wake zake, aweze kufanya uadilifu kati yao, Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu} [AN NISAA: 3]
Na imepokewa Hadithi kutoka kwa Abu Hurayra R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao, atakuja siku ya kiama na ubavu wake umeegemea ubavu mmoja”
Usawa kati ya mwaume na mwanamke katika jambo la mume zaidi ya mmoja ni muhali kiasili, kimaumbile na kiuhalisia. Na inajulikana kwamba haki ya uongozi katika familia katika Sharia zote za ulimwengu ni thabiti kwa mwanamume, tukihalalisha mwanamke kuwa na mume zaidi ya mmoja nani ataongoza familia? Atakuwa chini ya waume wote? Hilo haliwezekani kwa kutofautiana mahitaji ya kila mmoja wao, kwa hili ikadhihiri hekima ya Sharia ya Kiislamu katika hukumu yake hii, na kwamba kupinga hili kwa yaliyotajwa hakukubaliki na hakuna sababu ya hilo.