Kwa nini Mtume wa Uislamu Alioa Wak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwa nini Mtume wa Uislamu Alioa Wake Wengi?

Question

Matni ya shaka:
Imekuja katika Qur`ani: {Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana} [AN NISAA: 3]
 

Answer

Na vitabu vilivyotungwa kuhusu Mtume S.A.W. vimetaja kwamba yeye alioa zaidi ya wake kumi na mmoja, basi vipi Mtume katika Mitume wa Mwenyezi Mungu anakuwa na sifa kama hii?
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Muulizaji amechanganya kati ya tabia ya mazingira tofauti tofauti, kila zama zina tabia yake ambazo zinamuathiri aishie kwenye zama hizo, na zama za Mtume ilienea tabia ya kuoa mke zaidi ya mmoja, na kupumzika na watumwa wa kike, pamoja na hilo Mtume S.A.W. hakuoa kwa kupenda wanawake wengi kama alivyouliza muulizaji, bali alikuwa akioa kwa sababu za kijamii, kisheria na kisiasa, tunaweza kuzibainisha kama ifuatavyo:
Kwanza sababu za kijamii:
Kumwoa Bi. Khadija R.A. uwelevu wa kijamii ambapo mwanamume anamwoa mwanake mwenye akili ongofu, na Mtume S.A.W. alikuwa na miaka ishirini na tano, na aliishi naye mpaka alipofariki akiwa na umri wa miaka hamsini.
Baadaye alimwoa Bi. Sauda binti Zamaa na alikuwa mjane kutokana na mabinti zake wanne walihitaji mama mwingine wa kuwalea na kuwaongoza kama mama anavyowaongoza mabinti zake.
Hafsa binti Umar bin Khatab alimwoa baada ya kufariki mumewe ili kumkirimu baba yake mwaka wa tatu Hijiria.
Bi. Zaynab binti Khuzayma mumewe alikufa katika vita vya Uhud akamwoa mwaka wanne Hijiria.
Bi. Ummu salama Hind bint Umaya mumewe alifariki akamwacha na watoto akamwoa mwaka wa nne Hijiria.
Imebainika kwamba wake waliotajwa Mtume S.A.W. amewaoa wajane wa mashahidi ambao wamekufa katika Jihad kati ya Waislamu na washirikina ili azitulize nafsi zao na kuwalea watoto wao, na mbadala huu ulitoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Pili: Sababu za kisheria:
Kumwoa Bi. Aisha R.A. ilikuwa kwa Wahyi, ambapo aliota kwamba anamwoa, na ndoto za Mitume ni Wahyi.
Zaynab bint Jahsh mke wa Zayd bi Harith ambaye alikuwa akiitwa Zayd bin Muhammad kwa kumfanya mwanaye, ikashuka kauli ya Mwenyezi Mungu: {Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa }[AL AHZAAB: 4] {Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu} [AL AHZAAB: 5] na baada ya kutofautiana na mumewe aliachwa, akaamrishwa Mtume S.A.W. amwoe ili kusimamisha dalili ya kivitendo juu ya ubatili wa mtoto wa kupanga, hilo lilikuwa mwaka wa tano Hijiria.
Tatu: Sababu za kisiasa:
Baadhi ya ndoa za Mtume S.A.W. zilikuwa zina sehemu za kisiasa ili kuunganisha nyoyo na kupunguza uadui na kuwaachia huru mateka … n.k. miongoni mwazo:
Kumwoa Bi. Juwayriya binti Al-Harith, mkuu wa kabila la bani Mustalaq kutoka Khuzaa, alitekwa, alimwoa mwaka wa sita Hijiria.
Na Bi. Ummu Habiba Ramla binti Abi Sufyan, mumewe aliiingia kwenye ukristo yeye akabaki katika Uislamu, na kumuo kwake kulikuwa na athari kubwa ya kupunguza uadui wa Abuu Sufyan kuuchukia Uislamu mpaka Mwenyezi Mungu Akamwongoza. Na Bi. Saffiya bint Yahya bin Akhtab alitekwa katika viaa vya Khaybar Mtume alimwachilia huru na akamwoa mwaka wa saba Hijiria.
Bi.Maymouna bint Al-Harith mwaka wa saba Hijiria.
Katika hawa wawili walikufa katika uhai wa Mtume S.A.W.: ambao ni Khadija, na Zaynab bint Khuzayma, Mtume S.A.W. alifariki akiwa ameacha wake tisa.
Ama watumwa ni Mariya Al-Qibtiya ambaye ni mama wa Ibrahim aliyefariki akiwa mdogo, na Rayhana bint Zayd Al-Qiratiya.
Hivyo basi alioa wake wengi akiwa na miaka hamsini na tatu je, hii ni dalili ya kuoa kwa matamanio? Mtu mwenye matamanio ataoa wanawake walikwisha olewa na ni wenye watoto na wajane? Basi iweje hilo hali yakuwa alipewa wanawake wazuri wa kikurash na akakataa?!
Hakika yeye kuoa wake wengi ilikuwa kwa hekima pamoja na yaliyotangulia ikiwemo kubainisha yanayotokea katika nyumba ya Mtume miongoni mwa hekima za kufanyia kazi kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari} [AL AHZAAB: 34] na ili makabila ya Kiarabu yapate heshima kwa kuwepo ukwe naye, na kuongeza ukaribu na ndugu kwa upande wa wake zake ii kuongezaka wasaidizi wake kinyume na wanaompiga vita na ili kuhamisha hukumu za kisheria ambazo hawazijui wanaume; kwa sababu mengi yanayotokea na mke huwa yanajificha.
Kuoa mke zaidi ya mmoja ni Sunna ya Mitume kwa Matini za kitabu kitakatifu (Bibilia):
Kitabu kitakatifu kimetaja idadi kadhaa ya Mitume na imewaelezea kuhusu kuoa mke zaidi ya mmoja, miongoni mwao:
 Nabii Ibrahim A.S. Bibilia takatifu imetaja kuwa alikuwa na wake watatu; Sara (Sarai) Mwanzo (12: 20), Hajar Mmisri, Mwanzo (16:3), Qatura, mwanzo (25:1), pia alikuwa na wajakazi Mwanzo (25:6).
Nabii Yakoub A.S. alikuwa na wake wanne kwa wakati mmoja; imekuja katika Mwanzo “Usiku huohuo Yakoub akaamka, akawachukua wake zake wawili, wajakazi wake wawili na watoto wake kumi na mmoja, akapita kivuko cha Yaboki.” (32:22)
 Nabii Dawud A.S. Agano la kale limesema kuwa ana wake tisa:
1- Ahinoam kutoka Jezreel.
2- Abigail, mjane wa Naba kutoka Carmel.
3- Maakah, binti wa Talmai, mfalme wa Geshur.
4- Haggith.
5- Abital.
6- Eglah,.( 2 Samweli: 3:1-6)
7- Ahimeleki, ,.( 1 Samweli: 23:6)
8- Batshabaa mke wa Uria (2 samweli: 11:26)
9- Abishagi, Mshunami; (1 wafalme: 1-5)
 Nabii Sulayman A.S. Agano la kale limesema kuwa alikuwa na wake elfu moja, mia saba huru na mia tatu ni wajakazi. “Solomoni akawa na wanawake 700, wote mabinti wa kifalme; na masuria 300. Hao wanawake wakampotosha” (1 wafalme: 11-3).
Mitume wote hawa Ibrahim, Ishaq, Yakoub, Daoud na Sulayman Agano la kale limetaja kuwa wameoa wake wengi, hivyo basi kuoa wake wengi ni Sunna ya Mitume miongoni mwao ni bwana wetu Muhammad S.A.W.


 

Share this:

Related Fatwas