Kwa nini Uislamu Umeweka Sheria kwa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwa nini Uislamu Umeweka Sheria kwa Mwnamke Aliyeachwa na Mumewe Aolewe na Mume Mwingine?

Question

Asili ya shaka;
Imekuja Aya katika Qur`ani inasema: {Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine}. [AL BAQARAH 230]
 

Answer

Imekuja katika tafsiri yake: Mke wa Rifaa alimwambia Mtume S.A.W.: Hakika Rifaa ameniacha talaka isio rejea, na Abdurrahama bin Zubayr amenioa, na hakika alicho nacho ni kama nyuzi za nguo. Akasema Mtume S.A.W. unataka kurejea kwa Rifaa? Akasema: ndio. Alasema: hapana, mpaka uonje kiasali chake na aonje kiasali chako (papatikane tendo la ndoa).
Na mara nyingi mwanamke anaweza kuwa na mume mzuri na watoto wa kiume na wa kike ambao ni wakubwa katika jamii yao, na anapoghadhibika anamwacha mumewe, kisha anajuta kwa alichokitenda, kwa hiyo sharia katika Qur`ani inamlazimisha mwanamke huyu aingiliwe na mume mwingine kabla ya kumrejea.
Kuondoa shaka;
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Maana ya Aya na Hadithi zilizotangulia:
Makusudio ya kauli ya Mtume S.A.W. “mpaka uonje kiasali chake na aonje kiasali chako (papatikane tendo la ndoa).” Maana yake: haiwi halali kwa aliyemwacha mke wake talaka tatu kumrejea mpaka aolewe na mume mwingine ndio iliyo sahihi, akisha aachike bila ya kukusudia ndiyo hii ya pili kuhalalisha kuoelewa na mume wa kwanza, mke akitaka kurudi kwa mume wa kwanza kunajuzu kwake.
Muulizaji amekosea aliposema: “kwa hiyo sharia katika Qur`ani inamlazimisha mwanamke huyu aingiliwe na mume mwingine kabla ya kumrejea”, ili idhaniwe maana isiyokuwepo kwamba makusudio: aingiliwe na mwanamume mwingine asie mumewe, wakati Aya na Hadithi zimesema aingilie na mume wa pili katika ndoa yake, na amemwoa kwa ndoa ilio sahihi.
Mwenyezi Mungu Anasema: {Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine} kwa maana: mpaka aolewe na mume mwingine ndoa ya mapenzi, ndoa ya kawaida inayokusudiwa kudumu na kuendelea, si ndoa ya kuonesha hakuna ndani yake ndoa isipokuwa muonekano tu, ama maana yake na uhakika wake ni utulivu wa kila mmoja, mapenzi na huruma, mapenzi haya hayana maana ya udogo wala wingi, na linajulisha hilo kwamba miongoni mwa makusudio ya kisheria ni kumlinda mwanamke.
Na wanazuoni wamekubaliana kwamba ndoa yake kwa mume wa pili inakuwa batili kukiwa na makubaliano ya awali na mume wa kwanza, ili ahalalishe kumrejea, imekuja katika Hadithi sahihi: “Amemlaani Mwenyezi Mungu mwenye kuhalalisha na mwenye kuhalalishiwa”.
kwa maana ambaye anamwoa mwanamke kwa makubaliono naye au na mumewe wa kwanza, kisha amwache ili awe halali kwa mume wa kwanza.
Na wamekubaliana wanazuoni pia kwamba talaka ya aliyekasirika haiwi talaka, kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Hakuna talaka wakati wa ghadhabu kali” muulizaji amaekosea kataka kauli yake: “Na mara nyingi mwanamke anaweza kuwa na mume mzuri na watoto wa kiume na wa kike ambao ni wakubwa katika jamii yao, na anapoghadhibika anamwacha mumewe, kisha anajuta kwa alichokitenda”.
Na muulizaji hajui kwamba kuheshimu hukumu za dini ni jambo la wajibu na kwamba mtu huyu ambaye ni kiongozi katika jamii ni vyema kwake kuheshimu hukumu za kisheria wala hadaharau hukumu za talaka.
Kwa nini Mwenyezi Mungu Ameweka talaka na Akazifanya kuwa tatu:
Mwenyezi Mungu Ameweka sharia ya talaka ili kubatilisha yale yaliyokuwa yakifanywa katika zama za ujinga, mtu alikuwa anamwacha mke wake kisha anamrejea, anafanya hivyo mpaka anakuwa kama hana pakushika, hana mume wa kutulia naye wala hayupo huru ili aolewe na mume mwingine, Mwenyezi Mungu Akabatilisha hilo, na akabainisha kwamba mwanamume asimwache mkewe isipokuwa mara mbili, akimwacha mara ya tatu harudi kwake isipkuwa baada ya kuolewa na mwanamume mwingine, amaesema Imamu wa waumini Aisha R.A.: Mwanamume alikuwa anamwacha mke wake mara anazotaka kumwacha na anaendelea kuwa mke wake akimrudia akiwa katika eda, hata kama atamwacha mara mia moja, mpaka mwanamume mmoja alimwambia mke wake: Wallah sikuachi ukaondoka kwangu wala sikuweki kwangu? Akasema: kivipi? Akasema: Ninakuacha, kila eda inapokaribia kuisha ninakurejea. Yule mwanamke akatoka mpaka kwa Aisha R.A. akaingia ndani akamweleza akanyamaza mpaka alipokuja Mtume S.A.W. akamwelezea, akanyamaza Mtume S.A.W. mpaka iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu: {T'alaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri}[Al-Baqara: 229] amesema Aisha: Watu wakaanza upya talaka kwa mustkabali, aliyekwisha acha na ambaye hakuacha.
Akiachwa na mume wa pili anakuwa halali kwa mume wa kwanza, na sharia hii ni katika kumhurumia mwanamke, na kuondosha laana ya waume. Na hili ndani yake kuna kukata tamaa ya mwanamume kwa mwanamke, ambapo kumeshurutishwa katika kuwa halali kwake awe mbali naye, anakuwa ameolewa, na huenda akaishi naye maisha yake yote na asimpate tena, hilo litapelekea kutoharakia talaka na kutopetuka mpaka katika hilo.
Na hakuna dini yoyote Aliyoweka Mwenyezi Mungu kwa waja wake isipokuwa inakuwa na ukalifishaji ambao Mwenyezi Mungu Anawakalifisha waja wake, nayo bila ya hili haiitwi dini, hata falsafa za kisasa ambazo zinataka kuchukua nafasi ya dini nazo zinawakalifisha wafuasi wake mambo mengi.
Na lengo la Uislamu kuweka sharia ya talaka: Kumzoesha mwanadamu kudhibiti nafsi yake, na kutokuwa na maamuzi ya haraka, akichukua maamuzi ya haraka na akafanya hilo anasemehewa mara ya kwanza na ya pili bila ya kuzidisha juu ya hapo.


 

Share this:

Related Fatwas