Kwanini Ushahidi wa Mwanamke ni Nus...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwanini Ushahidi wa Mwanamke ni Nusu ya Ushahidi wa Mwanamume?

Question

Matini ya Shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaumewawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine}. [AL BAQARA 282]
 

Answer

Basi, Qur'ani haikusawazisha baina ya mwanamume na mwanamke; kwani Qur'ani imeufanya ushahidi wa mwanamke uwe nusu ya ushahidi wa mwanamume, na tofauti hiyo inamfanya mwanamke ahisi kuangamizwa, kudhalilishwa na kupuuzwa, na historia inathibitisha kwamba wanawake wengi walikuwa bora zaidi kuliko wanaume wengi.
Jibu la shaka hii:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Uislamu umempa heshima Mwanamke na umempatia haki zake ambazo Sheria zingine zilizotangulia hazijawahi kumpatia, na Uislamu umemfanya Mwanamke kuwa mshirika wa mwanaume katika Maisha, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amemjaalia kila mmoja wao maumbile maalumu ya mwili tofauti na mwenzake na yanayonasibiana na nyadhifa maalumu anazotakiwa kuzitekeleza, na akawalinganisha katika maamrisho ya Sharia, na kwa hivyo uhusiano baina ya mwanaume na mwanamke ni uhusiano wa kukamilishana na kuambatana na sio wa kupambana na kuwa maadui kama wadhaniavyo baadhi ya watu, kisha wanajaribu kutekeleza dhana yao hii kwenye Sharia za Kiislamu.
Na Aya aliyoitumia Muulizaji kwa ushahidi, inazungumzia kutoa ushahidi, na itambulike kuwa kutoa ushahidi ni tofauti na Ushahidi kwani Ushahidi hauchukui kigezo chake kutokana na uume au uke; bali unategemea Kuona wazi, ama kwa upande wa kutoa ushahidi unaokusudiwa na Aya ni maalumu katika matangamano au mahusiano yanayohusu vitu kama vile madeni na malipo ya fidia, jambo ambalo linahitaji aliyeona achanganyike na Jamii.
Na mara nyingi, Mwanamke hana aina hii ya mahusiano; na kwa hivyo anakuwa hatarini kusahau kutokana na akili yake kutoshughulishwa na mambo hayo shime yake kuelekea zaidi katika kuendesha mambo ya nyumbani kwake, na pale mambo yanapolazimu ushahidi wa mwanamke katika mahusiano haya na mwanaume mmoja tu basi na awe na Mwanamke mwenzake mwingine.
Na sharia ya Kiislamu inaelekea kuimarisha ushahidi katika kesi za kimali kwa ujumla, kwa ushahidi wa mwnamume mwengine kando ya mwamume wa kwanza, ili ushahidi usiwe mahali pa tuhuma. Na hakuna mtu yeyote anaeuzingatia usanifishaji wa ushahidi wa mwanamume hapa na kuuimarishia kwa ushahidi wa mwanamume mwingine ni jambo linaloipuuzia heshimu yake, ikiwa uimarishaji huo ni kwa ajili ya himaya ya haki za watu.
Kwa hiyo Suala la Ushahidi halina ndani yake kumtanguliza mwanaume dhidi ya mwanamke; kwani kubeba jukumu la Ushahidi ni kubeba mzigo mzito na tabu na hakuna ndani yake cha kugombania, na Ushahidi wa wanawake wawili unasimama nafasi ya mwanaume mmoja katika baadhi ya mambo, kwa lengo la kumpunguzia mzigo mwanamke na sio kwa maana ya kudharau uwezo wake.
Na kuna mambo ambayo hayasikilizwi isipokuwa Ushahidi wa Mwanamke, nayo ni mambo maalumu ya wanawake ambayo asiyekuwa mwanamke hayajui, na kuna baadhi ya mambo ushahidi wa mwanamke mmoja tu unakubaliwa na ushahidi wa wanaume haukubaliki ndani yake, na je jambo hili linamaanisha kuwa ni kuwadharau wanaume?
Basi sharia ya Kiislamu imezingatia ushahidi wa mwanamke peke yake na iliukubali katika mambo hasa ya wanawake. Ibn Qudama alisema katika kitabu cha: [Al Mughniy], "(suala) "Alisema –yaani Imamu Al Kharaqiy- na inakubaliwa katika mambo yasiyodhihirika kwa wanaume; kama vile: Kunyonyesha, Uzazi, Hedhi, Eda, na kadhalika, ushahidi wa mwanamke mwadilifu)". Halafu Ibn Qudama akaelezea maneno ya Al Kharaqiy kwa kauli yake: "Hatujui baina ya wana elimu hitilafu katika kukubaliwa kwa ushahidi wa wanawake peke yao kwa ujumla.
Al Kadhi alisema: Mambo ambayo Ushahidi wa mwanamke mmoja mmoja unakubalika ni matano: Uzazi, Ukelele wa Uhai wa Kichanga, Kunyonyesha, kasoro za nguoni kama vile Kuziba kwa Utupu, Kuota kipembe, Bikira, na kutimiza Eda.
Na sababu iliyotajwa na Qur'ani Tukufu katika kuuweka ushahidi wa Mwanamke kuwa nusu ya mwanume sio upungufu wa akili yake, Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwingine} [AL BAQARAH 282]. Na upotofu hapa ni kwa maana ya usahaulifu; na hiki ni kizuizi cha kisheria kinachozuia kuuharibu ushahidi nacho ni kwa kuchelea mkanganyiko na usahaulifu kwani mara nyingi mwanamke ni mnyonge zaidi kuliko mwanaume kwa asili ya maumbile.
Ama ushahidi ambao kwa kawaida hakuna hofu ya upotofu, ni wenye kuambatana na mambo hasa ya wanawake, basi ushahidi wa mwanamke haukuwa ni nusu ya ushahidi wa mwanamume. Bali ushahidi wake unakubaliwa peke yake, kwani hivyo ni vitu, mwanamke anaviona kwa macho yake, au anavigusa kwa mikono yake, au anavisikia kwa masikio yake kama vile; Uzazi, kunyonyesha, Hedhi na kasoro zilizo nguoni. Basi kwa kawaida, vitu kama hivyo havisahauliki, na kuvijua kwake havihitajii mambo ya kutumia akili.


 

Share this:

Related Fatwas