Kwa sababu Uislamu Unawaruhusu Wana...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kwa sababu Uislamu Unawaruhusu Wanaume Waislamu Kuwaoa Wanawake Waliopewa Kitabu, na Hauwaruhusu Wanaume Wasio Waisalmu Kuwaoa Wanawake Waislamu?

Question

Matni ya Shubha:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha walio pewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapo wapa mahari yao, mkafunganao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba. Na anayekataa kuamini bila shaka a'mali yake imepotea, naye katika Akhera atakuwa miongoni mwa wenye khasara}. [AL MAIDAH 5]
 

Answer

Aya hiyo inaruhusu kwamba Muslamu kumuoa mwanamke asiye Muislamu kutoka watu wa kitabu, wakati ambao Uislamu hauruhusu kuolewa mwanamke Muislamu na mwanamume mkristo, na katika hayo ni ushiriki wa viwili katika vigezo.
Kujibu Shaka:
Kila Sharia miongoni mwa Sharia za Mwenyezi Mungu au za Kutungwa, ndani yake kuna mkusanyiko wa kanuni za kipekee zenye sifa maalumu, na ufuasi wa sharia za wenye dini mbali mbali inategemeana na imani yake kwa Misingi ya Dini hizo. na Suala la kumzuia mwanamke wa Kiislamu kuolewa na asiyekuwa Muislamu pamoja na kuruhusu jambo hilo la ndoa kwa Muislamu mwanaume kumuona mwanamke wa kiskrito au kiyahudi ni suala la Sharia ya ibada inayotokana na imani katika itikadi za Uislamu na vyanzo vyake ni Qur`ani Tukufu na Sunna.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muuminini bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Mwenyezi Mungu anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake. Naye huzibainisha Aya zake kwa watu ili wapate kukumbuka}. [AL BAQARAH 221] Yaani haifai kwa Muislamu kuoa mwanamke mshirikina, na haifai mwanamume mshirikinaa kuoa mwanamke Muislamu.
Na sisi tunapotaja baadhi ya visingizio vya kiakili katika hukumu hiyo, hakika sisi hatusemi kwamba visingizio hivyo ni sababu za kweli ambazo kwa ajili yake hukumu hiyo imewekwa, bali ni hukumu tu ambayo tunaitaja na inaweza kuwa katika hali moja bila ya kuwa katika hali nyingine, na katika wakati kinyume na mwingine, lakini hapana shaka kwamba kuichunga ni katika mazuri ya Sharia Tukufu.
Kwa hiyo ndoa ni jukumu na usimamizi, na mke analazimika kumtii mumewe, na kama ataolewa na mume asiye Muislamu basi ukinzani utajitokeza katika utiifu wake kwa mumewe na utiifu wake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake S.A.W, na inawezekana Muislamu akawa Walii na Msimamizi pia kwa mke wake Mtu wa kitabu, lakini asiyekuwa Muislamu hana uwezo wa kuwa Walii na Msimamizi juu ya mwanamke wa Kiislamu.
Na mume anapokuwa Muislamu basi hakika miongoni mwa nguzo za imani yake ni kuwaamini Mitume wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati ambapo asiyekuwa Muislamu haamini kwamba Bwana wetu Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyetumwa na Mwenyezi Mungu, kwa hiyo Muislamu hawezi kufanya kitendo chochote kibaya kinachowagusa Mitume wa Mwenyezi Mungu bali yeye anawaheshimu Mitume wote wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ama kwa upande wa asiyekuwa Muislamu yeye hakanushi tu Ujumbe wa Mtume wetu S.A.W, bali anachupa mipaka na kumtusi au kumvunjia heshima yake, na katika mazingira kama hayo, vipi ataishi mwanamke wa kiislamu chini ya ulezi wa madaraka ya mwanaume asiyeamini Dini yake bali anaichukia?
Na hukumu hii sio maalumu kwa ajili ya Sharia ya kiislamu tu, na huu hapa ukristo hauwaruhusu wafuasu wake wa kike kuolewa na wanaume wasiokuwa wafuasi wake. Basi imetajwa katika Kitabu Takatifu: {Msiwe chini ya nguo moja (washirika) na wasiokuwa waumini; kwani hiyo ni alama ya mchanganyiko wa wema na uovu na ni alama ya mchanganyiko wa nuru na giza, na ni alama ya maafikiano baina ya Isa na Bliali, na ni alama ya sehemu ya muumini na asiyekuwa muumini, na ni alama ya kuwafikiana baina ya Hekalu la Mungu na Upagani kwani hakika nyinyi ni hekalu la Mungu aliye hai kama alivyosema Mwenyezi Mungu; Hakika Mimi nitaishi ndani yao na nitatembea miongoni mwao na nitakuwa wao Mungu na wao watakuwa watu wangu kwangu kwa hivyo jitengeni nao na anasema Mungu: Na wala siiguse najisi itakupateni}. [Wakorinto: 6:14-17]

 


 

Share this:

Related Fatwas