Miujiza ya Musa kwa Wamisri ni Kumi Siyo Tisa
Question
Matini ya Shaka:
Imetajwa katika Qur'ani: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa! Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ilikuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwishaangamia. Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na walio kuwa pamoja naye wote. Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi. Itapo kuja ahadi ya Akhera tutakuleteni nyote pamoja}. [AL ISRAA 101 – 104] Basi Qur'ani hapa imekwenda kinyume na yaliyokuja katika Kitabu Kitakatifu; kwani Kitabu Kitakatifu kimesema kuwa: Mapigo ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwapigia Watu wa Isarili ni kumi siyo tisa: na hayo ni: Damu [Kutoka 20:7], Vyura [Kutoka 8:6], Vidudu [Kutoka 17:8], Nzi [Kutoka 24:8], Kifo cha Mifugo (wanyama), Vipele [Kutoka 10-9], Baridi [Kutoka 23: 9], Nzige [Kutoka 4:10], Giza [Kutoka 23:10], Kifo cha Wenye Bikira [Kutoka 29,30: 12]
Answer
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Musa A.S, ni miongoni mwa Manabii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetumwa kwa wana wa Israeli na Mwenyezi Mungu alimuunga mkono kwa miujiza mingi, na miongoni mwa miujiza ya mwanzo mwanzo ni kuwapa changamoto watu wa Firauni kwa kile walichokuwa wamekizoea na kimeenea katika zama zao ambacho ni uchawi, na miujiza hiyo ya awali ni fimbo ya Musa iliyogeuka na kuwa nyoka anaekimbia na kumeza, na muujiza wa pili ni kuingiza mkono wake mfukoni ukageuka na kuwa na rangi nyeupe inayomeremeta kama mwezi bila ya kuwa na ugonjwa wa ukoma au ugonjwa mwingine wowote ule, kwa miujiza hiyo miwili Mwenyezi Mungu alibatilisha uchawi wa wachawi na kusimamisha hoja kwa Firauni na watu wake.
Na Qur'ani Tukufu iliiashiria kwa Miujiza hiyo katika kauli yake: {Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizowazi}, na yanayokusudiwa kwa kauli yake: {Ishara tisa zilizo wazi}, yaani hizo ni Aya zinazouashiria Unabii wa Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa A. S., ambazo alitumiwa kwa Firauni na jamaa zake.
Nayo ni fimbo ambayo iligeuka na kuwa nyoka, na mkono ambao aliutoa kutoka mifukoni mwake ukiwa mweupu, na watu wa Firauni iliwachukua miaka mingi, na upungufu wa mali, watu kufariki na matunda kupungua, kisha walipokanusha kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu akawateremshia gharika, nzige, chawa, vyura, na damu, na hii ni miujiza tisa maalumu iliyotokea baina ya Musa na Firauni.
Na kusudio la kauli yake: bayyinaati maana yake miujiza iliyo wazi wazi kwa maana ilitokea mbele za watu wakishuhudia. Na hii inaenda sambamba na yale yaliyokuja katika Kitabu Kitakatifu katika kauli yake: Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, Firauni hatakusikiliza, ili maajabu yangu yapate kuongezeka katika ardhi ya Misri, na Musa na Harun walikuwa wakifanya maajabu hayo yote mbele ya Firauni [Kutoka11:9-10]
Na Aya hizo tisa tu ni miujiza ya Bwana wetu Musa A.S., basi wanavyuoni walisema: Hakika kwamba kuihusisha idadi hiyo kwa kutaja, haiwi dalili ya kukanusha idadi zaidi ya hiyo. [Tazama: Tafsiri ya Roh Al Maaniy 603/4, Na At Tafsiir Al Muniir 182/15, At Tafsiir Al Kabiir 64/21, Tafsiir Ibn Kathiir 66/3]. Ibn Kathiir amesema baada ya kunukuluu Aya hizo tisa: Na hakika Musa A.S, alipewa miujiza mingi, na miongoni mwayo ni: Kulipiga jiwe kwa fimbo yake na maji kutoka katika jiwe hilo, kuwawekea kivuli cha mawingu, kuteremshimwa chakula cha Manna na Salwaa,, na mingine mingi aliyopewa Musa A.S, na Watoto wa Israeli, baada ya kutoka kwao Misri, lakini hapa imetajwa miujiza tisa ambayo Firauni aliishuhudia yeye na watu wake wa Misri ikawa hoja dhidi yake na watu wake na wakaamua kwenda kinyume nayo na wakaleta na ubishi na ukafiri na kuupinga Uislamu. [Tafsiir Ibn Kathiir 66/3, na yaliyo baada yake].
Tunaweza kusema kwamba Aya hizo zinataka kuleta sura ya hali na msimamo katika wakati huohuo ambao yametuka mazungumzo baina ya Bwana wetu Musa A.S. yeye na Mtume wetu S.A.W, na baina ya adui wa Mwenyezi Mungu Firauni, na kwamba wakati wa kutokea mazungumzo hayo baina yao wawili, Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa amewateremshia Aya hizo tisa Watu wa Israili, dalili ya usadikishaji wa Musa A.S., na Aya hizo ni ambazo zilitajwa hapo awali. Basi yaliyo wazi katika muktadha wa Aya hiyo Takatifu ni muhtasari wa yaliyotokea baina ya Musa A.S. na Firauni –Mwenyezi Mungu Mtukufu amlaani – wakati wote na miaka yote.
Au tunasema: Kwamba kuna tofauti baina ya Aya zinazotoa ujumbe usio na mipaka na Aya za adhabu ambazo aliteremshiwa Firauni na watu wake kwa kumsadikisha mtume wa Mwenyezi Mungu, Musa A,S, na kwamba makusudio ya miujiza tisa ni sehemu ya pili katika hizo, na tunatoa Aya zinazomaanisha ujumbe usio na mipaka ili ututolee sisi miujiza tisa tu, au kwamba Aya hizi ndizo Aya ambazo alienda nazo na hakuna mfanowe zilizowahi kuendelea au kuenea kinyume na zingine, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.