Kisimamo cha Ibrahim

Egypt's Dar Al-Ifta

Kisimamo cha Ibrahim

Question

Matini ya shaka:
Imetajwa katika Qur'ani Tukufu Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika Nyumba ya kwanza walio wekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyo barikiwa na yenye uwongofu kwa walimwengu wote. Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu simhitaji kwa walimwengu}. [AAL IMRAAN 96-97]
 

Answer

Inajulikana kwamba Wapagani ndio walioijenga Kaabah; kwa ajili ya Kuyaabudu Masanamu. Na Waarabu walikuwa wanahiji Kaabah kwa ajili ya kuyatukuza Masanamu yao ndani yake, kwa dalili ya kwamba Mtume wa Uislamu S.A.W, alipofanikiwa kuwashinda Makureshi aliyavunja masanamu hayo.
Na inajulikana kwamba Ibrahim alikuwa akiishi katika ardhi ya Kanaan, na hajawahi kwenda katika ardhi ya waarabu. Kwa hiyo ni kosa kusemwa kwamba Kaabah ni nyumba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu au Kisimamo cha Ibrahim. Na kuna uhusiano gani kati ya nyumba ya Mwenyezi Mungu na nyumba ya Masanamu? Na kuna uhusiano gani kati ya Kihibru na Kiarabu? Na kuna uhusiano gani kati ya Palestina na Hijazi (Makkah)?
Kujibu shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Ya kwamba Wapagani ndio walioijenga Kaabah; kwa ajili ya kufanya Ibada ya Masanamu, ni jambo lisilo sahihi na halina dalili yoyote. Ama walioijenga Kaabah ni Malaika – kwa kauli sahihi zaidi – kwa Amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kazi ya Bwana wetu Ibrahim A.S, ilikuwa ni kunyanyua tu misingi ya Kaabah. Kwa dalili ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi} [AL BAQARAH 127]
Na katika alama, za wazi katika nyumba hii ni Kisimamo cha Ibrahim, nalo ni jiwe ambalo Mtume Ibrahim alikuwa akilitumia kumamia hapo ili aweze kunyanyua Kuta za Kaaba juu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameendelea kukihifadhi Kisimamo hiki pamoja na muda mrefu kupita.
Ama kwa upande wa kauli yao: kwamba Ibrahim alikuwa akiishi katika ardhi ya Kanaan, na hajawahi kwenda katika ardhi ya waarabu, hili jambo sio sahihi kwani Ibrahim A.S, ambaye Dini zote za Mwenyezi Mungu zimeafikiana juu ya Utume wake, kama vile Uislamu, Wakristo na Wayahudi, kwamba Ibrahim alihama hama sehemu nyingi mpaka alipoamua kutulizana katika mji wa Hamruun, kule Kanaan Palestina, kisha mji huo ukanasibishwa naye na ukaitwa Mji wa Khalili.
Na katika Ulinganiaji wake alikutana na ukaidi pamoja na mateso, na bidii ya watu - akiwemo baba yake – za kutaka kumchoma moto kama malipo ya kuwakana miungu yao lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alimwokoa na akamwamrisha aende kwenye ardhi iliyobarikiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya Walimwengu wote, na Makkah akiwa na mkewe Haajar na mwanaye Ismaili na wakasimamisha Misingi ya Kaaba, na akaweka misingi ya Dini ya kumtakasia Mwenyezi Mungu Mtukufu ambayo Waarabu walirithiana baada yake.
Na ama kauli ya kwamba: Waarabu walikuwa wanahiji Kaaba kwa ajili ya kuyapanga Masanamu yao ndani yake, na dalili ni kwamba Muhammad S.A.W, alipowashinda Makureshi aliyavunja Masanamu hayo, tunasema: Makureshi walikuwa wameshaathiriwa na nyadhifa kubwa kubwa za Kidini kabla ya Uislamu ndani ya Makkah Mukarramah kama vile kulihudumia Kaaba na kuwanywesha maji Mahujaji na nyingine nyingi.
Na Makkah ikawa Kituo Kikuu cha chenye uzito wa Kidini na mkusanyiko wa Misimu ya Kidini kwa makabila mengi ya Kiarabu, na pakachanganyika kati ya urithi wa Dini Takatifu inayotokana na Mila ya Ibrahim na mabaki mbalimbali ya upagani na pindi Ushirikina ulipozidi na kuenea dhidi ya Imani ya Umoja na Upweke wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ndipo Uislamu ulipodhihiri na Qur’ani kuteremshwa kwa Mtume Mwarabu, Bwana wetu Muhammad Bin Abdillah, S.A.W, na Risala yake ikawa ndiyo hitimisho la Risala ya Kipenzi cha Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuiunga mkono, na akavunja Masanamu hayo baada ya kuifungua Makkah.


 

Share this:

Related Fatwas