Je, Uislamu Umeharamisha Kutaka Msaada kwa Wengine? Na Je, Kutaka Msaada kwa Wengine Kunalazimika Adhabu ya Mwenyezi Mungu?
Question
Matni ya Shaka:
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu:
{Na akamwambia yule aliye jua kuwa atavuka katika wale wawili: Nikumbuke kwa Mola wako. Lakini Shetani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf akakaa gerezani miaka kadhaa} Yusuf: 42.
Answer
Na imekuaja kuwa Mtume wa Uislamu S.A.W amesema: “Mwenyezi Mungu amemfanyia huruma ndugu yangu Yusuf lau kama asingesema nikumbuke kwa Mola wako basi angekaa jela miaka saba badala ya mitano” sisi tunauliza hivi ni haramu wakati wa shida mtu kutaka msaada kwa ndugu yake?
Jibu la shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Udhaifu wa Hadithi.
Ama Hadithi aliyoitumia muulizaji ni kwamba Hadithi dhaifu kama inavyopelekea hivyo kwa mujibu wa kanuni za wazungumzaji wa Hadithi. Ibn Katheer R.A amezungumza kuhusu Hadithi hii na akasema: “Hii ni Hadithi dhaifu sana kwa sababu Sufian Ibn Wakii ni mtu dhaifu kimapokezi na Ibrahimu Ibn Yazidi pia ni dhaifu zaidi ya Sufian” ( ).
Aya inathibitisha kinyume na madai
Kisha Aya inathibitisha kinyume na madai ya mwenye kudai kuwa Yusuf A.S alielekea kwa mmoja wa vijana wawili ambao walikuwa pamoja naye gerezani kwamba huyo kijana amtaje vizuri Yusuf kwa mfalme wake atakapotoka gerezani, lakini hata hivyo huyo kijana akasahau alichomuahidi Yusuf, hivyo haikuwa kwa Yusufu isipokuwa kuishi gerezani miaka mingi akiwa mwenye kuridhia na kupokea maamuzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ni kinyume na madai ya mwenye shaka, kwani Aya inatuongoza kufahamu kuwa Yusuf alichukuwa sababu alimtaka kijana amsaidie lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuzidi kumsafisha Yusuf wala matokeo hayafikiwi moja kwa moja baada tu ya maombi, hivyo haikuwa isipokuwa Yusufu kukaa akiwa mwenye kuridhia maamuzi ya Mwenyezi Mungu.