Je! Mtume S.A.W. Alikuwa na Dhambi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je! Mtume S.A.W. Alikuwa na Dhambi Inayovunja Mkongo?

Question

 Je! Mtume S.A.W. Alikuwa na Dhambi Inayovunja Mkongo?

Answer

 Asili ya shaka
Imekuja ndani ya Qur`ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hatukukunjulia kifua chako? * Na tukakuondolea mzigo wako * Ulio vunja mgongo wako} [AS-SHARH: 1– 3].
Na kauli yake Mola Mtukufu: {Hakika tumekufungulia Ushindi wa wazi * Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yajayo, na akutimizie neema zake, na akuongoe katika Njia Iliyo Nyooka * Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu} [AL-FAT-H: 1–3].
Na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba msamaha kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pakukaa} [MUHAMMAD: 19].
Na kauli ya Mola Mtukufu: {Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi} [GHAFIR: 55].
Tunauliza: Aya hizi zote zinathibitisha kutokea makosa kwa Mtume wa Uislamu S.A.W. je inafaa kudai kuwa yeye ni muombezi hali ya kuwa yeye mwenyewe ni mwenye kufanya mambo ya dhambi?
Kuondoa shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Manabii ndio watu bora kabisa kwa makubalino ya Wanachuoni wote, na Nabii Muhammad S.A.W. ndio Nabii mkubwa zaidi na mbora wa wabora na wenye nafasi za juu, wanaangalia mambo yasiyozingatiwa na watu wengine kuwa ni dhambi lakini wao wanayaangalia kuwa ni dhambi, kama ilivyosemwa: Matendo mema ya waja wema ni mabaya kwa waliokaribu.
Kwa huyo kutaka msamaha hawa Manabii wakubwa hakuzingatiwi ni kuomba msamaha wa makosa waliyoyafanya, kwa sababu kwao hakuna makosa kabisa.
Lakini kunazingatiwa ni kuomba kuinuliwa daraja na kufikishwa nafasi kamili ya juu kabisa, na viwango vya ukamilifu na utukufu havina mwisho.
Uwingi wa kutaka msamaha ni katika sifa za watu wa ibada hufikia kwa mja kupanda katika nafasi ya ukamilifu na utukufu ambao hauna mwisho, kutaka msamaha kwenyewe ni ibada hutekelezwa na mja hata kama hajafanya dhambi ya kuitakia msamaha, kwani kuhisi hali ya kuwa na upungufu ni sifa ya waja wema hata wafikie daraja ya kiwango gani.
Hivyo utaona Mtume S.A.W. alikuwa anasimama usiku kuswali mpaka miguu yake inavimba ikiwa ni kutekeleza wajibu huu na kutambua neema ya kuwezeshwa na Mola, kutoka kwa Mughiirah Ibn Shaabah R.A. amesema: Mtume S.A.W. alisimama usiku kuswali mpaka miguu yake ikavimba, alipoulizwa: Kwanini hali ya kuwa Mwenyezi Mungu amekusamehe dhambi zako zilizotangulia na zitakazokuja. Mtume S.A.W. akasema: “Hivi siwezi kuwa mja wa kushukuru”( ).
Akili historia na tafasiri ya Qur`ani vinapinga Mtume S.A.W. kuwa amefanya dhambi.
Ama Akili: Ni kwa sababu Manabii ni wenye kusifika na sifa ya uaminifu katika kauli zao matendo yao na hali zao, hawana kabisa tabia ya usaliti wala kufanya makosa, uaminifu wao umeungwa mkono na miujiza, na Mwenyezi Mungu akawabebesha Ujumbe wake ambao hakuna anayeubeba isipokuwa ni mwenye kuwa muaminifu mkweli wa kuaminika, na kwa haya Mwenyezi Mungu ametuamrisha sisi kuwafuata bila ya kutaka ufafanuzi wowote, na katika hili ni ukanushaji wa uwezekano kwao kufanya makosa, kwa sababu ikiwa kutawezekana kwao kufanya makosa basi Mwenyezi Mungu atatutenganisha na makosa hayo na kutuongoza kwake na hatotuamrisha kuwafuata tu bila kigezo wala sharti.
Upande wa Historia: Ni kuwa Vitabu sahihi vya Historia kwa ujumla wake vianaeleza kuwa maisha ya Mtume S.A.W. yamekuwa ni mfano kamili wa uaminifu, wala hakuna ndani yake makosa wala dhambi, bali Qur`ani Tukufu yenyewe imemsifu Mtume S.A.W.: {Na hakika wewe una tabia tukufu} [AL-QALAM: 4],
Na akaamrisha kumfuata, na Aya inayoelezea kuwa Mtume S.A.W. hafanyi makosa: {Wala hatamki kwa matamanio} [AN-NAJM: 03], ni namna gani Mtume anadaiwa kuwa ni mwenye makosa? Na inadaiwa kuwa Qur`ani Tukufu ambayo imemtakasa ni yeye mwenyewe ndiye anayeyasema hayo?
Ama kwa Upande wa Tafasiri za Aya ambazo ndani yake kuna sifa ya Mtume S.A.W. ni mwenye makosa, tafasiri sahihi ambayo imeelezewa na vitabu vya tafasiri vinaweka wazi kuwa “Neno Mzigo” katika kauli ya Mola Mtukufu: {Na tukakuondolea mzigo wako} ina maanisha ni Haraji, na neno Haraji ni kuhisi dhiki na tabu ambayo imesababishwa na kutoitikiwa kwa baadhi ya wito wa Mtume S.A.W. au kwa maana ya shida na matatizo ambayo yanakwamisha muelekeo wa kazi za ulinganiaji.
Na maana ya neno ((وضعنا Wadha’anaa: Maana yake, tumetoa, hivyo Aya inaelezea hali ya kuondoa shida na matatizo kwa hali ya mwenye kuondoa uzito kwa mbebaji, kwa maana ya kumuondolea ili kumpumzisha kutokana na tatizo la uzito( ).
Miongoni mwa tafsiri sahihi pia ya Aya:
Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na tukakuondolea mzigo wako} ni fumbo kuhusu kuzuiliwa kwake Mtume S.A.W. kufanya matendo ya dhambi na kusafishwa kutokana na uchafu, ni Aya imeelezea hivyo kwa neno la kuondoa ikiwa ni kwa njia ya ufikishaji kukanusha Mtume kufanya makosa na matendo ya dhambi.

 

 

Share this:

Related Fatwas