Je, Uislamu Unahalalisha Kumshawis...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je, Uislamu Unahalalisha Kumshawishi Mtu kwa Mali ili Aingie Kwenye Uislamu?

Question

 Je, Uislamu Unahalalisha Kumshawishi Mtu kwa Mali ili Aingie Kwenye Uislamu? 

Answer

 Matni yenye kuleta shaka:
Ndani ya Qur'ani Tukufu imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu uliolazimishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hekima} [AT TAWBAH 60]
Tunauliza: Je Uislamu unahalalisha kushawishi mtu kwa kutumia mali ili aingie kwenye Uislamu kwa kulipa wale wanaoitwa wa kutiwa nguvu nyoyo zao? Na je mali inazingatiwa Zaka na Sadaka au inazingatiwa ni rushwa na ufisadi?
Jibu la Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya hii Tukufu imetaja pande za kupewa Zaka ndani ya Uislamu na Zaka yenyewe inatolewa kwa watu wa makundi manane mingoni mwa hao ni pamoja na watu wanaotiwa nguvu nyoyo zao, na fungu la hao watu ni moja ya matumizi ya Kisharia ambayo hupewa mali za Zaka, nao ni Waislamu au sio Waislamu inakuwa ni katika hekima na akili kuziimarisha nyoyo zao kwa kuwapa hizi mali za Zaka.
1- Je kuzoeshwa na kutiwa nguvu nyoyo ni jambo la aibu?
Ni tofauti kubwa sana kati ya kinachotolewa kwa lengo la kupewa nguvu mioyo ya watu na kukusanywa kwenye msingi mmoja na kati ya kutolewa fedha ili mtu auze dhamira yake na kununuliwa kwa kupewa mali.
Ya Kwanza: Ni mali inayotumika ili kuzipa nguvu nyoyo zao. Ya Pili: Hiyo ni rushwa.
Mwenyezi Mungu ametuonesha ni namna gani kumesababisha utekelezaji wa matumizi haya wakati wa zama za Mtume S.A.W katika kuzipa nguvu nyoyo za baadhi ya Waarabu ambao wameacha ubedui na kukimbilia utiifu kwa kiongozi au kufuata mfumo hivyo fungu hili la matumizi ya Zaka likawa na mchango mkubwa katika kuzizoweza nafsi hizi na kuzisafisha, na kuwatoa Waarabu wengi kutoka kwenye mambo maovu na mabaya na kuwaleta kwenye mfumo wa kufuata nchi na kujichanganya kwenye mfumo, na baadhi ya nafsi huwa hazifuati mfumo uliopo isipokuwa kwa kupewa mali.
1. Mali sio kwa sababu ya Imani:
Haina maana mtu kupewa fungu hili kuwa sisi tunanunua dhamira yake ili kuingia kwenye Uislamu, kwani mali haikuwa na haitakuwa sehemu ya imani bali mtu anapopewa fungu hili halimuanzishii kuamini na kuteua kuendelea na kile anachoamini – imetokea sana – hatukuwa wa kumlazimisha kuingia katika dini yetu, ni vipi wakati Mwenyezi Mungu ametuongoza kuwa imani ya dini ni kitu cha moyoni haiwezi kuja kwa kulazimishwa wala kutenzwa nguvu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:
{Na sema: Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae. Hakika Sisi tumewaandalia wenye kudhulumu Moto ambao utawazunguka kama hema. Na wakiomba msaada watasaidiwa kwa kupewa maji kama mafuta yaliyo tibuka. Yatayo wababua nyuso zao. Kinywaji hicho ni kiovu mno! Na matandiko hayo ya kupumzikia ni maovu mno!} [AL KAHF 29 ].
Miongoni mwa waliotiwa nguvu kiimani na Mtume S.A.W walikuwa ni pamoja na wanafiki walioridhika wao wenye kuonesha kuwa ni Waumini pamoja na hayo Mtume S.A.W hakuwalazimisha chochote ili waamini ( ).
Miongoni mwa wanaozoeshwa imani zao ni pamoja na walioingia katika Uislamu hivi karibuni, mmoja wao anapewa ikiwa ni kumsaidia ili kuthibiti zaidi kwenye Uislamu, kwani aliyesilimu hivi karibuni na kujitoa muhanga kwa wazazi na ndugu zake, wengi wao huwa wanaingia kwenye mvutano na ndugu zao pamoja na koo zao na kuhatarishiwa riziki zao, hivyo hakuna shaka kwa huyu ambaye ameiuza nafsi yake na akaacha dunia yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni muhimu kumuhamasisha kumthibitisha kiimani na kumsaidia.
2. Anayestahiki kupewa katika fungu hili baadhi ya sura zake inakuwa mfano wa kama nchi nyingi zinatoa ikiwa sura yake itakutwa imeharibiwa kwenye akili za watu basi hupelekwa mali kwenye mpango wa kuboresha sura ya kiakili kwenye nafsi za watu, wakati huo hupelekwa matumizi haya kwenye fungu la kuondoa matatizo ya kisaikolojia na kuvunja mlima wa theluji unaojengwa kwa harakati na juhudi za sekta ya habari kitamaduni na kihistoria zinazojaribu kuchafua sura ya dini hii kwenye akili za watu.
Ikiwa kuwafanyia watu wema ni ushawishi wa wao kuingia kwenye Uislamu, basi inakuwaje kwa wasiokuwa Waislamu wanaanzisha mahospitali na taasisi mbalimbali za mambo ya heri ndani ya nchi za Waislamu na zisizo za Waislamu kwa lengo la kueneza ukristo na kupambana na njia ya Mwenyezi Mungu?
107- Je. Qur'ani Inahalalisha kumpinga Mwenyezi Mungu?
Matni yenye Shaka:
Ndani ya Qur'ani imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao hasira za Mwenyezi Mungu zipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa} AN-NAHLI: 106. Na imekuja katika baadhi ya habari kuwa Imara alitamka maneno ya kufuru baada ya kuadhibiwa.
Tunauliza: Je ni katika imani mtu kuleta udanganyifu katika imani yake na kuukana Uungu wa Mwenyezi Mungu ikiwa lengo ni kuwaridhisha watu?
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Kwanza: Aliyoyafanya Swahaba Mtukufu Imara Ibn Yasir si katika kuridhisha watu bali ni kuokoa nafsi, na ufafanuzi wa hilo ni kuwa Imara alifahamu ukweli nao ni kutoka kwenye Uislamu na kuzingatiwa si Muislamu hakuwi kwa neno analotamka mwandamu pasi ya kuliamini, bali kutoka kunakuwa kwa kuamini imani inayokaa moyoni, na alifahamu kuwa neno hili ambalo halimtoi kwenye Uislamu linawaridhisha hawa watu wajinga hivyo wataacha kumfanyia maudhi ndipo akafanya hivyo, na akapata masilahi ya aina mbili, kwanza kuikoa nafsi yake na kuendelea kubaki kwenye imani.
Pili: Kuna jambo muhimu nalo ni kuwa: Uislamu unasamehe kwa mtu mwenye kulazimishwa au kutenzwa nguvu, wala hauwachukulii watu isipokuwa kwa kile walichofanya kwa hiyari, hii haina maana kuwa Uislamu unapiga vita ukweli na watu wakweli, hapana bali mwenye kuwa na uwezo kisha akasubiri dhidi ya maadui wala hakutamka neno la kukufuru basi huyo anakuwa ni shahidi, kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ana malipo makubwa, ikiwa mtu ataingia kwenye matatizo kwa sababu ya yanayomkuta ikiwa ni pamoja na kutenzwa nguvu basi imehalalishwa kwake kutoka kwenye fitina hii kwa kutamka neno ulimini mwake bila ya kuliamini, hivyo anafaulu kwa kuikoa nafsi yake na moyo wake ukiwa umetulizana kwenye imani yake sahihi.
Tatu: Angalia yaliyojirudia kwa wingi ndani ya Taurati na Injili mfano wa yaliyokuja kwenye sura ya kumi na tatu katika kitabu cha Wafalme wa Kwanza: “Kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana. Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia * Akamwambia mini ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la Bwana, kusema mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako ale chakula akanywe maji lakini alisema uongo * basi mtu yule akarudi pamoja naye akala chakula akanywa maji nyumbani mwake”.
Alitumia hila katika njaa yake na akaongopa, na ndani ya Injili ni kuwa Paul alikuwa ni mtu mwenye ndimi mbili na sura mbili kwani anapojibu husema: “Mimi ni mwenye utaifa wa Roma na nimezaliwa nikiwa huru”. Na akasema: “Mimi ni Myahudi kutoka ukoo wa Benjamin”. Pindi alipokuwa mbele ya kiongozi wa Makuhani na akapigwa mdomoni akasema Paul: “Mungu atakupiga ewe ukuta mweupe”. Pindi alipomtukana kwa kauli hii na ndani ya Torati ni kuwa haifai kumtukuna kiongozi wa Makuhani na kumuelekezea lawama kwa kwenda kwake kinyume na Taurati. Paul akasema: “Enyi ndugu sikuwa nafahamu kuwa ni kiongozi wa Makuhani, kwa sababu imeandikwa: Kiongozi wa Makuhani usimwambie neno baya”.
Ndani ya Torati kutenza nguvu kwenye kuvunja hukumu katika hukumu za Kisharia kunaondoa adhabu ya kuvunja hukumu, binti bikra aliyechumbiwa na mwanamme ikiwa atakutwa shambani na akachukuliwa na mwanamme na kulala naye basi mwanamme anauwawa peke yake, ama kwa upande wa mwanamke hatofanywa lolote “Kwa msichana hakuna makosa ya kifo kama inavyokuwa kwa mwanamme anauliwa, hali ni kama hivi.
Nne: Mwenye kufahamu maana ya huruma ya Mungu anafahamu kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kujua hali ya mwanadamu, naye ndiye ambaye amemuumba katika hali ya udhaifu ambapo wakati mwingine anafikwa na hali ya kusahau na wakati mwingine hukosea, na baadhi ya watu hawana kusimama imara wakati wa matatizo, hivyo amewapunguzia mfano wa hali hii.

Share this:

Related Fatwas