Je. Waislamu Wote Wataingia Motoni?...

Egypt's Dar Al-Ifta

Je. Waislamu Wote Wataingia Motoni?

Question

Je. Waislamu Wote Wataingia Motoni? 

Answer

 Matni yenye Shaka:
Imekuja ndani ya Qur'ani Tukufu kauli ya Mwenyezi Mungu:
{Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipoahidiwa wote * Ina milango saba, na kwa kila mlango ipo sehemu waliotengewa} Al-Hijri: 43 - 44. Imekuja katika baadhi ya tafasiri kuwa tabaka la kwanza ndani ya moto wa jahannam ni sehemu ya Waumini ambao wataingia motoni na kuadhibiwa humo sawa na dhambi zao kisha watatolewa.
Tunauliza: Ni vipi Muumini anaingia kwenye moto wa jahannam? Hivi maisha ya Waislamu hayakutanda hofu ya kifo na hukumu? Na ipi tofauti kubwa kati ya maisha haya yaliyozungukwa hofu na kati ya maisha ambayo anayapenda kuyaishi duniani ili kuwa pamoja na Masiha na kusubiri siku ya Kiyama kwa furaha ambapo atapata mashada mazuri ya maisha!
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Aya Tukufu imezungumzia mwisho wa wadanganyifu ambao wanafuata njia ya shetani, na pindi ukisoma Aya katika muundo wake itakuwa wazi kuwa Aya zinazungumzia mazungumzo kati ya shetani na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutufikia sisi Aya mpaka shetani anasema akiwa anampinga Muumba wake:
{Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi na hakikisha nitawapambia hapa duniani na nitawapoteza wote} [AL HIJRI: 39]. Jibu linakuwa kwenye kauli ya Mola Mtukufu:
{Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa wale wapotofu walio kufuata * Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipoahidiwa wote * Ina milango saba; na kwa kila mlango ipo sehemu walio tengewa} [AL HIJRI: 42 – 44]. Kisha hakuna katika Aya Tukufu mazungumzo kuhusu Waumini waja wema wataingia motoni bali mazungumzo ni kuhusu kuingia motoni wakosaji wafanyao maasi.
Kati ya rehma na uadilifu:
Lakini ikiwa itatokea kwa baadhi ya Waumini kufanya makosa baadhi ya nyakati na kuendelea kubakia kwao kwenye asili ya imani yao wakafanya mambo ya dhambi na bila ya kufanya toba kwa maana ya kutubia dhambi walizofanya basi katika yanayopelekea uadilifu wa Mungu wafanyao dhambi kuadhibiwa kwa kuingia motoni kwa muda ili kutakasika na dhambi zao, na hii ndio maana ya yaliyokuja kwenye baadhi ya mapokezi yenye kuonesha kuingia motoni kwa muda kwa baadhi ya Waumini waasi ili kutakasika na dhambi zao, pamoja na kufahamu kuwa usamehevu wa Mungu utawakuta na kusamehewa na hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye.
Waumini kati ya hofu na mategemeo:
Jambo hili linamfanya Muumini siku zote kuwa kati ya hofu ya kupata adhabu na kuiogopa shari yake na kati ya mategemeo ya rehma na usamehevu hivyo hakati tamaa bali anaishi katika wigo wa matumaini ya msamaha wa Mola Karimu.
Na kati ya rehma, na vipi Muumini akate tamaa na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Hakika hawakati tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu makafiri} [YUSUF: 87]. Na akasema tena:
{Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale waliopotea} [AL HIJRI: 56].

Share this:

Related Fatwas