Kutumika Kitenzi cha Wakati Uliopi...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutumika Kitenzi cha Wakati Uliopita Badala ya Kitenzi cha Wakati Uliopo.

Question

Kutumika Kitenzi cha Wakati Uliopita Badala ya Kitenzi cha Wakati Uliopo. 

Answer

 Matni ya Qur'ani:
{Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa} ( ).
Nini madai ya mjenga hoja?
Ilikuwa inapaswa kuzingatiwa sehemu ambayo inapelekea muundo wa kitenzi cha wakati uliopita na wala si kitenzi cha wakati uliopo na kusema: Akamwambia kuwa basi alikuwa ( ).
Kuondoa Shaka:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Muulizaji ameshindwa kuelewa yale yanayofungamana na dhati iliyo juu zaidi nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu yupo nje na muda na wakati kwani kwake ni sawa nyakati zote, hivyo wala haiwezi kusemwa kwa upande wake wakati uliopita na wakati uliopo na kuwa ni kama vile inavyosemwa kwa upande wa wengine wanaoambiwa.
Pia muulizaji ameshindwa kuelewa ni katika kawaida za Qur'ani kutumia kitenzi cha wakati uliopo badala ya kitenzi kilichopita ili kuleta sura halisi “Kuileta akili kana kwamba inaona kwa macho” na kwa kanuni hii zimekuja Aya nyingi ndani ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa Aya hizo ni pamoja na Aya aliyoitaja muulizaji na pia kauli ya Mwenyezi Mungu inayosema:
{Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma Pepo ziyatimue mawingu} ( ). Na miongoni mwa kawaida za Qur'ani Tukufu pia kuelezea jambo lililofikiwa kwa kitenzi cha wakati uliopita ikiwa ni kuleta msisitiza wa kutokea kwake na hilo ni mfano wa kauli ya Mola Mtukufu: {Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize} ( ).
Wala hakitumiki kitenzi cha wakati uliopo katika hali kama hii isipokuwa kwenye maana kama hii….. na kutumika hapa tofauti na hivi haina maana ( ).
Tafsiri: Maelezo kuanza upya: Imeelezwa kwa Wakristo mambo yanayotokana na uzushi kuhusu sifa ya Isa kuwa ni neno litokalo kwa Mungu, wakapotea kwa uzushi wao kuwa yeye si binadamu halisi, hii imeingiza ubatilifu katika imani ya Kikristo ya kumfanya Isa ni mungu, wakajibiwa ndani ya Uislamu nayo ni dalili ya moja kwa moja, kwa sababu wao wamesema Isa ni mungu kwa sababu ameumbwa na neno litokalo kwa Mungu na wala hana baba, wengine wakasema: Yeye ni mtoto wa mungu, basi Mwenyezi Mungu akawaonesha kuwa Adam ni bora zaidi kuitwa hivyo kwani Adamu ikiwa hawezi kuwa mungu pamoja na kuwa ameumbwa bila ya kuwa na wazazi wawili basi Isa ni bora zaidi kuwa kiumbe kuliko Adam.
Sehemu ya kufanana ni kuwa wote wawili wameumbwa wakiwa hawana baba, lakini Nabii Adam anazidi kwa kuwa kwake bila ya mama, hivyo imejengwa hoja ya kutajwa eneo la kufanana kwa kauli yake Mola Mtukufu: {Amemuumba kwa udongo} Aya, kwa maana amemuumba bila ya baba wala mama bali ni kwa neno kuwa, pamoja na kubainisha kuwa kwake na nguvu zaidi ya kufananishwa kwa hali ya kawaida bali alisema kwa Mwenyezi Mungu kwa maana ya kunasibishwa kwa Mwenyezi Mungu hakuzidishi chochote kwa Adamu kuwa kwake ni kiumbe kwa sababu wamefanya kuumbwa kwake kwa ajabu kumewajibikia Masihi unasibishwaji maalumu kwa Mwenyezi Mungu nao ni mtoto kwa maana kuwa mtoto wa Mungu. Na Ibn Atwiyah amesema: Amekusudia kwa kauli yake {Mbele ya Mwenyezi Mungu} ni hali hiyo hiyo.
Na dhamiri katika neno kuumbwa kwake inarejea kwa Nabii Adamu na wala si Nabii Isa, ambapo watu wote wamefahamu kuwa Nabii Isa hakuumbwa kwa udongo, sehemu inayofanana ni kauli yake: {Kisha akasema kuwa basi inakuwa}.
Na jumla ya neno {Amemuumba} na herufi kiunganishi chake inabainisha jumla inayosema {Ni kama mfano wa Adamu}.
Kisha kwa ajili ya kuinua cheo na nafasi, kuumbwa kwake kwa amri ya {Kuwa!} ni nafasi ya juu zaidi ya kuumbwa kuliko kuumbwa kwa udogo, nako kuumbwa huko ni kwa muda mrefu zaidi na ndio kuumbwa kulikoashiriwa kwa neno Kuwa!: Nako ni kuumbwa kwa sifa inayokusudiwa, hivyo Mwenyezi Mungu hakusema: Amemtengeneza kutokana na udongo, na wala hakusema: Alimwambia Kuwa kutokana na udongo kisha akampa uhai, bali amesema amemuumba kisha akamwambia Kuwa!. Na kauli yake Kuwa! Ni kuelezea kuhusu uwezo wa kumuumba kwake hai mwenye roho ili kuwafundisha wasikilizaji kuwa kuumba sio kazi ya kufanya kwa mkono wala kuchonga kwa mashine lakini ni utashi na kufungamana na uwezo na kuwezesha viumbe ambavyo vimekuwa na athari katika kutengeneza kusudio, mpaka kupelekea kuonekana aliyeumbwa yote hayo ni kutokana na muelekeo wa utashi wa kufanikisha, kwa neno hilo Adamu pia alikuwa ni neno kutoka kwa Mwenyezi Mungu lakini hakusifika kwahilo ni kwa sababu hapakuwa na kuhitajika hilo kwa kupita muda wake.
Tafsiri: Wafasiri na wasomi wa sarufi wameelezea kauli yake Mola Mtukufu {Kuwa basi akawa} Zamakhshary akafupisha na akasema: Hiyo ni simulizi ya hali ya wakati uliopita, kauli hii ya Zamakhshary imechukuliwa pia na Imamu Al-Baidhawy na wala hakuzidisha kitu, nayo ni ibara inayohitaji ufafanuzi ni ipi hiyo simulizi ya hali ya wakati uliopita?
Maimamu wawili wanakusudia kuwa kitenzi cha wakati uliopo {Anakuwa} maana yake katika Aya ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaelezea wanaoambiwa mpangilio wa kutokea Kiyama kutokea kwake ndani ya wakati ambao Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu, hii ndio maana ya kitenzi cha wakati uliopo pindi kinapowekwa sehemu ya kitenzi cha wakati uliopita kwa Wanachuoni wa maana ya Kibalagha ni kuletwa kitenzi cha wakati uliopita na kuelezewa katika sura ambayo kinatokea hivi sasa.
Haya ndio waliyotaka kusema Masheikh wawili: Zamakhshary na Al-Baidhawy katika ibara inayosema “Simulizi ya hali iliyopita” ili kubainisha siri ya kugeuka kutoka “Ilikuwa” kuwa “Inakuwa” katika Aya Tukufu ambayo amedai huyu mleta shaka kuwa ndani yake kuna makosa kisarufi na wao wanauelewa sahihi na makosa.

 

Share this:

Related Fatwas