Maneno ya Kigeni

Egypt's Dar Al-Ifta

Maneno ya Kigeni

Question

Aya ya Qur'ani:

Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Amemteremsha Roho muaminifu * Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji * Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi} ([1]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

{Qur'ani ya Kiarabu isiyo na upogo} ([2]).

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena:

{Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako ili wapate kukumbuka} ([3]). Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema tena:

{Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bayana} ([4]).

Nini amesema mjenga hoja?

 

[1] Ashuaraa: 193 – 95.

[2] Zumar: 28.

[3] Dukhaan: 58.

[4] Nahli: 103.

Answer

Sisi tunauliza: Ni vipi Qur'ani ya lugha ya Kiarabu iliyowazi inakuwa na maneno mengi ya lugha za kigeni kuanzia Kifursi, Kiashuri, Kisiria, Kiebrania, Kigiriki, Kimisri, Kihabeshi na lugha zingine? Tunataja idadi ya maneno na Sura zake nayo ni kama ifuatayo: Adam. Al-Baqarah 2: 34 Kiabrania: Neno Abaariiq. Al-Waaqia 56: 18 Kifursi: Ibrahim. An-Nisaa: 4: 4. Kiashuri: Neno Araaik. Kahf 18: 31. Kiarabu au Kifursi: Neno Istabraq. Kahfi 18: 31. Kifursi kilichofanywa Kiarabu. Neno Injili. Aal-Imraan 3: 48. Kigiriki: Neno Taabuut. Al-Baqarah 2: 247. Kimisri: Neno Taurat. Aal-Imraan 3: 50. Kiebrania: Neno Jahannam. Al-Anfaal 8: 36. Kiebrania: Neno Hibru. At-Tawbah 9: 31. Kifoiniki: Neno Huur. Ar-Rahman 55: 72. Kibahlawy: Neno Zaka. Al-Baqarah 2: 110. Kiebrania: Neno Zanjabir. Al-Insaan76: 17. Kibahlawy: Neno Sabti. An-Namli 27: 124. Kiebrania: Neno Sijjiil. Al-Fiil 105: 4. Kibahlawy: Neno Saraadiq. Al-Kahfi 18: 29. Kifursi: Neno Sakiinah. Al-Baqarah 2: 248. Aramaic: Suratul-Tawbah 9: 124. Kisiria: Neno Swaraatw. Al-Fatihah 1: 4. Kilatini: Neno Twaghuut. Al-Baqarah 2: 257. Kihabeshi: Neno Aden. At-Tawbah 9: 72. Kisiria: Neno Firaun. Al-Muzammil 73: 15. Kisiria: Neno Firdaus. Al-Kahfi 18: 107. Kibahlawy: Neno Maau’un. Al-Maau’un 73: 7. Kiarabu: Neno Mishkaat. An-Nuur 24: 35. Kihabesh: Neno Maqaaliid. Az-Zumar 39: 63. Kibahlawy: Neno Maaruut. Al-Baqarah 2: 102. Kiaramaic au Kibahlawy au Kiarabu: Neno Haaruut. Al-Baqarah 2: 102. Kiaramaic au Kibahlawy au Kiarabu: Jina Allah. Al-Fatihah 1: 1. Kiebrania linalotokana na neno Aluuh na Kisiria linalotakana na neno Ilaahah ([1]).

Shaka:

  1. Qur'ani ndani ya Aya nne inaelezea imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu pamoja na hayo msomaji atakuta ndani yake kuna maneno mengi ambayo ni ya lugha zingine si ya Kiarabu, na kwa hali hii Qur'ani ina makosa kwa kujieleza kuwa ni ya Kiarabu na uwepo wa makosa kunapelekea kuondoka muujiza wake na kuwa kwake kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu.

Kuondoa Shaka:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Kwanza: Wanachuoni wamekubaliana kuwa Qur'ani Tukufu ni Kiarabu ndani yake hakuna maneno wala matamashi ya kigeni yaliyokuja ndani ya Qur'ani Tukufu, ambayo yanadhaniwa tofauti na lugha ya Kiarabu yanamaelezo ya aina tatu:

  • Yenyewe yameingia kwenye lugha ya Kiarabu kutokana na Waarabu kuyatumia, kwa maana yemewekewa kanuni na sarufi za lugha ya Kiarabu hivyo yenyewe ni Kiarabu.
  • Yenyewe ni kutoka lugha zingine au lugha ya Kiarabu hivyo hakuna ubora kuyaita si maneno ya Kiarabu kuliko kuyaita maneno ya Kiarabu.
  • Ni kuwa yale yaliyokubaliana na lugha ya Kiarabu kutoka lugha zingine au yaliyosahaulika kutoka lugha ya Kiarabu hivyo Qur'ani Tukufu ikaja na kuyafufua baada ya hapo.

 Pili: Hapa muulizaji ametumia asilimia nyingi kwenye baadhi ya maneno ambayo ameyataja na kuyahusisha si ya Kiarabu, kwa maneno kama: Zaka, Sakiinah, Adam, Huur, Sabti, Suurah, Maqaaliid, Aden na Allah, maneno yote haya yenye asili ya lugha ya Kiarabu na yenye misingi mikubwa ya lugha ya Kiarabu, kwani yamo kwenye makamusi ya lugha ya Kiarabu na kwenye vitabu mbalimbali vya Fiqhi ya lugha na vyinginevyo asili ya maneno haya ni Kiarabu ([2]).

Tatu: Miongoni mwa madai ya uwongo kusema: Neno Tukufu “Allah” ni la Kiebrania au Kisiria na Qur'ani imelichukuwa kutoka kwenye lugha hizi mbili, ambapo tamshi hili Tukufu “Allah” halipo kwenye lugha isiyokuwa ya Kiarabu: Kwa mafano lugha ya Kiebrania hutumia neno Takatifu “Allah” kwa maneno mengi, mfano wa neno Ail, Al-Wahiim, Adunay, Yahwa au Yahova, maneno haya yapo wapi kwenye tamshi la “Allah” ambalo lenyewe ni neno kuu lenye wajibu wa kuwepo linastahiki sifa zote njema, katika lugha ya Kiarabu na katika lugha ya Kigiriki ambayo kutoka lugha hiyo imefasiriwa Injili kwenye lugha ya Kiarabu ambapo tunakuta Jina la Allah ndani yake likiwa “Hallow” na imekuja ndani ya baadhi ya Injili zikimtaja Nabii Isa Amani ya Mungu iwe kwake akitaka msaada kwa Mola wake kama hivi “Hallow Hallow” na kufasiriwa “Ilahiy Ilahiy”.

Nne: Ni kipimo kipi kinachopimiwa Qur'ani kuwa ni Kiarabu au si Kiarabu ni lugha ya kigeni? Na je ikitokea ndani ya Qur'ani Tukufu kuwepo baadhi ya maneno yakasemwa kuwa si maneno ya Kiarabu ndio Qur'ani nzima inachukuliwa kuwa si ya lugha ya Kiarabu? Na Aya ambazo zinaelezea kuwa Qur'ani ni Kiarabu cha wazi si za kweli!

Qur'ani Tukufu pindi inapokusanya maneno elfu sabini na mbili mia nne thelathini na tisa ([3]) na miongoni mwa maneno haya maneno mia moja yakazungumzwa kuwa ni asili ya lugha ya Kiarabu au yenyewe yamehamishwa kutoka lugha zingine na kuingizwa kwenye lugha ya Kiarabu je hii inakana kuhusu Qur'aniTukufu kuwa ni ya lugha ya Kiarabu kilicho bayana?

Hakuna shaka kuwa idadi hii ni ndogo tena ndogo sana ya maneno ambayo ni kiasi cha asilimia moja katika elfu kwa hali yeyote ile hayawezi kufanya wasifu wa Qur'ani Tukufu kuwa Kiarabu kuwa si kweli.

Tano: Mwenyezi Mungu amesema Qur'ani Tukufu kwa lugha bayana ya Kiarabu na wala hakusema kwa matamshi ya Kiarabu kwani maneno yote yaliyomo ndani ya Qur'ani yenye asili si ya Kiarabu ni neno moja moja nayo ni majina maarufu mfano wa jina la Ibrahim, Yakobo, Isaka na Firauni, na haya majina maarufu ya watu, au sifa mfano wa Twaghuut na Hibru, ikiwa tutasema neno “Twaghuut” ni neno la lugha ya kigeni ([4]), na sifa tofauti kati ya lugha na matamshi, lugha maana yake ni muundo na mfumo, hivyo Qur'ani Tukufu imeachana kabisa na muundo wowote usiokuwa wa Kiarabu, kwani ndani yake hakuna jumla hata moja ya jina au kitenzi isiyokuwa ya Kiarabu.

Sita: Matumizi ya majina maarufu yasiyokuwa ya Kiarabu ndani ya lugha ya Kiarabu hayapingani na lugha hii kuwa yenyewe ni Kiarabu kwa sababu majina maarufu ni sawa sawa yakiwa majina ya watu au sehemu au vyombo au majina ya watu ya kutungwa, yote hayo hayafasiriwi wala kuwekwa Irabu na kutumika kwake ndani ya lugha ya Kiarabu hakukanushi Uarabu wake, na kanuni hii si kwa lugha ya Kiarabu tu bali kila lugha, kwani mzungumzaji wa lugha ya Kiingereza pindi anapohitaji kutaja jina kutoka lugha isiyokuwa lugha yake huwa analitaja kwa urasmi wake na utamshi wake katika lugha yake ya asili, kutokana na hili yale tunayoyasikia hivi sasa katika taarifa za habari kwa lugha za kigeni kuhusu habari za Misri majina ya Kiarabu hutamkwa kwa Kiarabu, na wala haisemwi kwa mfano taarifa ya habari si kwa lugha ya Kifaransa au Kiingereza kwa sababu tu baadhi ya maneno yametamkwa kwa lugha ya nyingine.

Na vitabu vya kisasa vya kisayansi na kifasihi ambavyo huandikwa kwa lugha ya Kiarabu na ndani yake kunakuwa na waandishi wake wengi wakitajwa kwa majina ya kigeni na vyanzo ambavyo wamenukuu, na huandikwa kwa herufi za kigeni na utamkaji wa kigeni lakini hata hivyo haisemwi kuwa vyenyewe havijaandikwa kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu kwa sababu tu ya kuwemo baadhi ya maneno ya lugha ya kigeni na kinyume chake sahihi.

 

[1] Ukurasa 157 kitabu cha je Quran haina makosa?

[2] Hakaiku Al-Islaam 54.

[3] Wametofautiana katika jumla ya idadi ya maneno ya Quran Tukufu katika mapokezi ya Atwaa Ibn Yasar  ni maneno elfu sabini na saba mia nne thelathini na tisa nayo ni upokezi wa watu wa Madina. Na katika upokezi wa Abi Rabiah kutoka kwa watu wa Makka kuwa ni maneno elfu sabini na saba mia nne sitini. Na katika upokezi wa Yahya Ibn Al-Harith ni maneno elfu sabini na tisa na kumi. Kutoka kwa Abi Ady ni maneno elfu sabini na tisa thelathini na tisa, sababu ya tafauti ni kuwa baadhi yao wamehesabu mfano wa neno Ardhi, Akherah, Al-Anhaar na Al-Abraar maneno mawili kw aupande  wa madhehebu ya watu wa Kufa kwa sababu wao  hufanya herufi ya Waw na Laam neno kwa sababu zinaleta maana ya kufahamisha, na baadhi yao wamezingatia ni neno moja ni madhehebu ya watu wa Basra kwa sababu wanafanya herufi ya Laam peke yake ni kwa ajili ya kufahamisha na herufi ya Alifu ni kwa ajili ya kuanza

[4] Kitabu cha Hakaik Al-Islaam katika kupambana na shaka za wenye shaka ukurasa wa 54.

Share this:

Related Fatwas