ISS (Daish) ni Kundi la Kigaidi

Egypt's Dar Al-Ifta

ISS (Daish) ni Kundi la Kigaidi

Question

Je! ISS (Daish) ni Kundi la Kigaidi?

Answer

Kundi linalojulikana kwa Jina la ISS (Daish) si la kigaidi tu, bali ni alama ya mfano wa wazi wa waliofikia sifa hii, nani atakuwa gaidi kama si ISS (Daishi) si magaidi? Kumekuwa na Habari, matukio mengi, na kuna vitabu vingi vilivyotungwa na kuandikwa na wao wenyewe ambavyo vinaondosha aina yoyote ya shaka kwamba wao ndio wanahaki zaidi ya kuitwa magaidi katika zama hizi, wamewakufurisha Waislamu, wamehalalisha na kumwaga damu zao, wamevunja heshima zao na kuwapora mali zao, na kwamba nchi isiyowakubali basi ni nchi ya kikafiri – kwa madai yao - wamewalazimisha waliobeba itikadi zao kuhamia ardhi wanazozitawala!

Kama kwamba Mtume S.A.W. anawasema wao aliposema: “Zama za mwisho watakuja watu wadogo kiumri, akili zao dhaifu, wanasoma Qur’ani lakini imani zao dhaifu, wanatoka katika Uislamu kama unavyotoka mshale katika upinde, popote mtakapokutana nao, basi wauweni, kwani kuwaua kwao ni malipo kwa waliowaua siku  ya Kiyama” [Muttafaqun Alayhi]

Share this:

Related Fatwas