Uhusiano wa Daish na kundi la kigai...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhusiano wa Daish na kundi la kigaidi la Ikhwanul Muslimin

Question

Uhusiano gani uliopo kati ya Daish na kundi la kigaidi la Ikhwanul Muslimin?

Answer

Daish si chochote ila ni mfano unaotumika na unaotokana na mawazo ya kundi la kigaidi la Ikhwanul Muslimin, na hii inaashiria kwamba kanuni ya “ Upweke wa Mwenyezi Mungu katika utawala” nao ni mojawapo ya kanuni mashuhuri ambazo itikadi za makundi ya kigaidi zimeegemezwa humo bila ubaguzi. , na maana yake ni kwamba kutotawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ni kufuru, nayo hii ni dhana potofu ambayo haisemwa na mmoja wa maimamu wanaoheshimika, basi maana ya kufuru katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri}[Al-Maidah: 44]. Yaani ukafiri sio ukafiri unaomtoa mtu kutoka Uislamu, au unaonasibishwa na mwenye kuukataa utawala kwa ukamilifu wake, kama iliyopokelewa kutoka kwa Al-Tabari na wengineo katika tafsiri. Pamoja na upotofu mwingine wa watu wenye misimamo mikali, ambao ni imani yao kwamba kanuni zinapingana na sheria ya Kiislamu, na kwa hiyo wanawakufurisha watu wa umma wa Waislamu, watu na serikali kwa ujumla, na wa kwanza wa kuunda kanuni hii ni Abu Al-A'la Al-Mawdudi kisha Sayyid Qutb akaifasiri kwa Kiarabu na kuitangaza katika idadi ya vitabu vyake, hususan “Adhilaal”, na kwa hiyo “Adhilaal” kinachukuliwa kuwa ni miongoni mwa vitabu mama vya makundi ya kigaidi, kuanzia kundi la Ikhwanul Muslimin, kupitia kundi la Takfir wal-Hijrah, kundi la Jihad, Al-Qaeda, na kumalizia na Daish.

Share this:

Related Fatwas