Hesabu ya Nyota Kwa Ajili ya Kujua ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hesabu ya Nyota Kwa Ajili ya Kujua Miezi Kati ya Kuzingatia na Upotevu

Question

   Sifa zote njema anazostahiki Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, na rehma na amani zimshukie Bwana wetu Muhammad, Muaminifu, na jamaa zake na masahaba zake wote, na baada ya hayo.

Ni kutokana na rehema za Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyake kwamba aliwapelekea Mitume miongoni mwao, na akaweka sheria pana ambayo itabakia wakati wote ili kushughulikia matukio mapya, bila ya wale waliokalifishwa na Sharia kuhisi tabu, na kadiri elimu na sayansi za watu zinavyokua, Sharia haizuii katika njia ya maendeleo hayo, na haikuwa kikwazo, na hatupati kitu katika Sharia kisichokubaliana na Sayansi na akili, na akili  haipingani na upeo wa elimu ya binadamu kwa zama zote na hiyo ni kwa sababu tu zote mbili Sharia Tukufu na elimu ya ulimwengu zote zimetoka katika chanzo kimoja, ambacho ni Mwenyezi Mungu Mtukufu, ambaye alimfundisha mwanadamu asiyoyajua, kwa hivyo sifa njema ni Kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliyetujaalia kuwa katika Umma  wa bwana wa watu na ametutukuza kwa Sharia hiyo Tukufu, ambayo ustaarabu mkubwa zaidi ulijengwa, ustaarabu wa Ukweli, Haki, Sayansi, Nuru na Maadili yaliyotukuka.

    Na baada ya hayo, Hakika Mwenyezi Mungu, Utukufu uwe kwake, na Jina Lake lihimidiwe, ameunganisha baadhi ya ibada na matukio kadhaa ya ulimwengu yanayotuzunguka, kwa mfano, kuunganisha Swala na mwendo wa jua machoni mwa watazamaji, kuunganisha baina kuzama kwa jua, kuchomoza kwa Alfajiri ya kweli na kutoweka kwa machweo mekundu, na kadhalika. Kwa kufunga mwezi wa Ramadhani Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha kufunga wakati mwezi wa Ramadhani unapoonekana na kufungua Saumu unapoonekana mfungo mosi (Mwezi wa Shawwal), na akafanya faradhi ya Hijja pia kufungamana na Miezi, hivyo Miezi ya Hijja huanza na Mfungo Mosi na kuishia na mwisho wa siku za Hijja katika  Mfungo tatu (Mwezi wa Dhul-Hijjah).

    Hivyo basi, tunaona kwamba Sharia tukufu imeubainisha mwanzo wa Miezi hii ya mwandamo kwa kuonekana kwa Mwezi kuwa ni faradhi ambayo haina budi kuifanya, na kwa hivyo haiwezekani kwetu kutekeleza ibada yoyote katika hizi zilizotangulia isipokuwa baada ya kuhakikisha juu ya kuonekana kwa miandamo hii ya Mwezi, kwa hivyo kuandama kwa Miezi hii imekuwa ni miongoni mwa wajibu katika dini kufuatana na msingi wa Kifiqhi usemao: “Chochote ambacho wajibu hautekelezwi bila hicho basi hicho pia ni wajibu.” Hivyo basi, Maimamu Waislamu na wenye Mamlaka miongoni mwao ni lazima wafanye kazi ili kutekekeza wajibu huu, na kurahisisha njia ya kuufikia, na hivi ndivyo ilivyokuwa tangu zama za Mtume, Waislamu walikuwa wakiandama Mwezi kisha wanamwambia Mtume (S.A.W), matokeo ya muandamo wao, ili Mtume (S.A.W) atangaze mwanzo wa Mwezi, katika Hadithi ya Ibn Abbas, (R.A), kwamba Bedui mmoja alikuja kwa Mtume (S.A.W) akasema: “Niliuona Mwezi mchanga, akasema: Je! unashuhudia kwamba hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu?” Akasema: “Ndiyo.” Akasema: “Je, unashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Ndiyo.” Akasema, “Basi ewe Bilali waache watu wafunge kesho”. Na muandamo wa macho ndicho chombo chao walichokuwa wakikitegemea katika kuandama mwezi, hasa kwa ukosefu wa zama hizi katika elimu ya kina ya unajimu na zana mpya za uchunguzi zilizobuniwa. Wajibu wa wakati huo ulikuwa ni kile ambacho Waislamu waliweza na ambacho wangeweza kutekeleza ibada na mila zao, msingi wa kisheria uliotamkwa na Qur'ani Tukufu unasema: “Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo”. [AL BAQARAH: 286] Uwezo wa Waislamu wakati huo ulikuwa ni kuandama kwa Mwezi kwa njia ya kuuona kwa macho tu, zama zinazosonga mbele na kupita kwa wakati na kufika kwa Sayansi kwa kiwango chake kinachojulikana sana katika suala la usahihi na kasi lilizuka miongoni mwa Waislamu suala kuhusu ni kwa kiasi gani inawezekana kutegemea data za Sayansi ya kisasa katika uwanja wa elimu ya nyota, ambazo zinaweza kuamua wakati ambapo mwezi huzaliwa na wakati ambao unaweza kuonekana na jambo hilo lilichunguzwa kutokana na vipengele vyake vyote vya kisheria na hata vya kisayansi vya wanaastronomia.

Kwa hiyo, suala la uwezekano wa kutegemea hesabu ya unajimu limejibiwa kwa njia tofauti. Jopo moja la Wanachuoni liliona kwamba Sharia haitegemei kuandama kwa Mwezi isipokuwa kuuona kwa macho, na kwa hiyo vyovyote thamani ya usahihi wa hesabu ya unajimu hakuna mazingatio ya kisheria kwa hilo, na kundi jingine liliona kwamba zama zetu ni zama ambazo tunapaswa kushughulika na data na zana za kisasa za kisayansi ambazo Sharia haizipingi – miongoni mwa hivyo ni kutegemea matokeo ya hesabu ya unajimu - na kwa hivyo hakuna mazingatio isipokuwa kwa hesabu ya uhakika ya unajimu na hakuna kuzingatia kwa maono ya kudhamiria, na kuna kundi tatu lililopatanisha kati yao, na kuifanya hesabu ina mchango wake katika kuthibitisha uwezekano wa kuuona Mwezi kwa macho na kisha inakuja zamu ya kuuona Mwezi kwa macho ambayo hesabu ya unajimu huamua maeneo yake ambayo ni bora zaidi pia, kwa hivyo inachanganya zana mbili na iko nje ya mzozo wa Kifiqhi, na nimechukua kila rai ya kundi la wanazuoni wa Kiislamu, na hii ilisababisha baadhi ya taratibu katika nchi zote za Kiislamu zinazothibitisha maoni thabiti kwao, na ambayo wameyapitisha, na kutoka hapa tutajaribu kupitia utafiti huu kuwasilisha kwa maoni juu ya suala hili na jaribio la kufichua baadhi ya ushahidi ambao pengine haujaonekana katika majaribio ya awali ya utafiti kutokana na mtazamo wa kisheria, na kupitia hayo tutajaribu kujibu swali kuu na kutoka nje ya utafiti huu nalo Je, hesabu ya unajimu inazingatiwa katika Sharia au haizingatiwi? Na daraja yake ni ipi wakati wa kuizingatiwa pamoja na kuuona Mwezi kwa macho? Kwa hivyo, kuuliza kwa swali hili ni jambo ambalo mwanzoni litaainisha mada ya mzozo katika suala hilo. Kwa upande mmoja, inahusika na kiwango ambacho hesabu ya unajimu inazingatiwa au haizingatiwi, na kwa upande mwingine, huainisha kiwango ambacho hesabu ya unajimu inapaswa kuwa wakati wa kuidhinishwa, na ninamuomba Mwenyezi Mungu ajaalie mafanikio katika kuwasilisha ushahidi wa kila kundi na kubainisha rai ambayo ni sahihi zaidi kati yao.

Answer

Maana ya hesabu ya unajimu katika lugha na istilahi:

Katika lugha: - Ilitajwa katika kamusi ya Al-Muhiit kwenye kidahizo cha Hasaba ina maana ya kuhesabu. 

Na katika kamusi ya Lisan Al-Arab katika kidahizo hicho hicho: “Na Al-Hisabu yaani kuhesabu kitu maalumu”.

Katika istilahi: Hesabu ya unajimu ni mojawapo ya matawi ya “Elimu ya umbo” ambalo somo lake ni kuangalia hali ya maumbo ya juu na ya chini; Ikiwa yamesimama au vinasonga.

Au ni: “Elimu inayotafuta hali ya maumbo ya mbinguni, au ni Sayansi inayosoma nyota na Sayari angani”.

Sehemu ya kwanza

Madhehebu yaliyojadili kupitishwa kwa suala la hesabu ya unajimu na kutopitishwa

Maoni ya Wanachuoni wa Fiqhi yalitofautiana baina ya kukataa na kuzingatia kupitishwa kwa hesabu ya unajimu. Wanachuoni wa Fiqhi wengi wa zamani walikataa kuzingatiwa kwa hesabu ya unajimu kabisa, na wachache waliiona kuwa ni dalili ya mwanzo wa Mwezi wa mwandamo. Katika yale yanayofuata, tutapitia matini za Madhehebu hayo, kisha tutawasilisha katika sehemu inayofuata ushahidi wa kila kundi, na kumalizia kwa kauli ya kile tunachochagua kutoka kwao.

1 - Madhehebu ya wale wanaokataa kupitishwa kwa hesabu ya unajimu katika kubainisha mwanzo wa miezi ya kiarabu na dalili zake:

Wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi wa Hanafi, Shafi, Maliki na Hanbali, walikuwa na mtazamo wa kutozingatia hesabu ya unajimu. Yafuatayo ni matini za Wanachuoni wa Fiqhi wanaokataa mazingatio haya:

Madhehebu ya Hanafi:

Al-Sarakhsi amesema katika kitabu cha Al-Mabsout:

 (Akasema): Iwapo watu wa mji mmoja watafunga bila ya kuandama Mwezi, na mmoja wao hakufunga mpaka uandame Mwezi kesho yake, basi watu wa mji huo wakafunga siku thelathini, na yule mmoja akafunga siku ishirini na tisa tu. basi hatakiwi mtu huyo kulipa chochote, kwa kuwa watu wa mji wamekosea kwa kufunga bila ya kuona Mwezi kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W.): {Fungeni Saumu kwa kuuona (Mwezi), na fungueni Saumu kwa kuuona,  na kama mawingu yatawakinga msiuone, basi kamilisheni Mwezi wa Shabani siku thelathini.} Basi watu wa mji wamekwenda tofauti na amri ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) na walikosea, na baadhi yao wakasema itarejelewa kauli ya watu wa hisabu wakati wa kutia shaka, na hili liko mbali kwa Mtume (S.A.W.), aliyesema: “Mwenye kumuendea KUHANI (mganga, mpiga-ramli, mtabiri, mnajimu) akamwamini anayoyasema basi amekufuru alichoteremshiwa Muhammad”.

Katika maelezo ya Ibn Abidin:

 Kauli yake: (Kauli ya watu wa muda haizingatiwi) yaani katika faradhi ya kufunga Saumu kwa watu, bali katika kitabu cha Al-Miraaj kauli yao haizingatiwi kwa maafikiano ya wanachuoni wengi, na haijuzu kwa mnajimu kufanya hesabu kwa nafsi yake mwenyewe, na katika kitabu cha An-Nahr, sio lazima kwa kauli ya watu wa muda, kwamba Mwezi uko angani kwa usiku maalumu hata wakiwa ni sawa tu kama ilivyo katika kitabu cha Al-Idhah.

• Madhehebu ya Maliki:

Amesema katika kitabu cha Minah Al-Jaliyl:

Ramadhani haithibitishwi (kwa) hesabu ya (mnajimu) amebebeshwa haki ya wengine na haki ya nafsi yake. Na iwapo ukweli wake ungetokea moyoni, angemwamrisha mtunga sheria kumkana, yeye ndiye mwenye kukokotoa safu ya Mwezi na nuru yake, na ikasemwa kuwa yeye ndiye anayeona kuwa Mwanzo wa mwezi ni kupanda kwa nyota inayojulikana, naye ni  mwenye kuhesabu mwendo wa jua na mwezi na kwa kila hali hakuna yeyote anayefunga kwa kusema kwake na yeye hategemewi juu ya hilo.”

Al-Qarafiy anasema katika kitabu cha Al-Dhakhirah:

Ama kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W): “Kama kuna mawingu mengi, basi kadirieni siku za Mwezi, kwani haikusudiwi kukadiria mwendo wa Mwezi, kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W) katika Sahihi ya Imam Muslim: “Basi kadiria kwake siku thelathini, na kwa sababu maana yake ni hesabu siku zake, ambazo ni siku thelathini, na kwa hiyo kama kuna Mwezi mmoja siku zake ni siku ishirini na tisa tu, basi Mwezi huu haujakamilika.”.

 Vile vile Al-Qarafiy akasema, Mwenyezi Mungu amrehemu: “Na kutokea kwa Mwezi mwandamo nje ya miale siyo kwa sababu maalumu, bali ni kuonekana kwake kwenye fahamu, basi mwenye kumsababishia kitu kisichokuwa na kuona, kwa kutegemea hesabu, basi sababu haipatikani katika haki yake, na wala haitawekwa hukumu juu yake, na dalili ya hivyo ni kauli yake Mwenyezi Mungu  kuhusu Swala:{Shika Swala jua linapo pinduka} [AL ISRAA: 78] Na wala hakusema: “Fungeni Saumu kwa mwandamo”. Bali alisema: “Basi atayekuwa mjini katika Mwezi huu naafunge.” [AL BAQARAH: 185].

Kwa hiyo akafanya sababu ni kuuandama Mwezi siyo kitu kingine, Sanad akasema: Lau Imamu mmoja akiona hesabu ya unajimu ni bora na akathibitisha Mwezi mwandamo kwake, hafuatwi na yeyote kwa sababu ya makubaliano ya waliotangulia kinyume chake.

Madhehebu ya Shafi:

Al-Nawawi alisema katika kitabu chake Rawdhatul Talibiin:

Si wajibu kufunga Saumu kufuatana na hesabu ya mnajimu, wala kufuatana na mtu mwingine yeyote. Al-Ruyani amesema: kadhalika mwenye kujua vituo  vya Mwezi si wajibu kwake afunge saumu kwa mujibu wa rai sahihi zaidi.

Ama kuhusu kuruhusiwa, amesema katika kitabu cha  Al-Tahdhiib, haijuzu kumuiga mnajimu katika hesabu zake, si katika kufunga wala kufuturu.

Katika maelezo ya Al-Bahja na Sheikh Zakaria Al-Ansari, imetajwa kuwa:

 Kauli yake: “(au kuona kwa uadilifu) inajumuisha kama ikiwa hesabu inaonesha kuwa haiwezekani kuona, na inaunganishwa na ukweli kwamba Mwezi umetua katika usiku wa tatu kwa matakwa ya uoni huo kabla ya wakati wa Isha; Kwa kuwa  Sheria hakupitisha hesabu, bali iliifuta kabisa, na ni hivyo hivyo, kama Walid alivyotoa Fatwa kinyume na Al-Subki na waliomfuata.”.

Madhehebu ya Hanbali:

Ibn Qudamah amesema katika kitabu chake Al-Mughni:

Kadhalika lau angetegemea kauli za wanajimu na watu wa elimu ya hesabu, na ikawa ni sahihi, Saumu yake isingekuwa sahihi, hata kama kupatia kwao kumekuwa kwingi, kwa sababu hakuna dalili ya kisheria ambayo inajuzu kutegemewa kwa hilo. wala kuifanyia kazi, hivyo kuwepo kwake kumekuwa kama kutokuwepo kwake.

Katika Fatwa kubwa za Ibn Taymiyyah, imetajwa:

Hapana shaka kuwa imethibitishwa kwa Sunna sahihi na makubaliano ya Maswahaba kwamba haijuzu kuegemea katika kuhesabu ya nyota, kwani imethibitishwa kutoka kwake katika Sahihi mbili kwamba amesema: {Sisi ni umma usiojua kusoma, na hatuandiki wala hatuhesabu, fungeni mnapouona Mwezi na fungueni mnapouona Mwezi}. Na Mwenye kuegemea hesabu katika Mwezi, sawa na kupotoshwa kwake katika Sharia, yeye ni mzushi katika dini, amekosea katika akili na hesabu, Wanasayansi wanajua kuwa uoni umbo haudhibitiwi na hesabu, lakini lengo la hesabu kwa wao likiwa sawa hufahamika ni kiasi gani kati ya Mwezi na Jua kiwango cha wakati wa kuzama kwa Jua kwa mfano.

Muhtasari wa maneno ya Kifiqhi kuhusu Maimamu wa Madhehebu ambao hawakuzingatia hesabu ya unajimu:

- Inaweza kusemwa kwamba Maimamu ambao hawakuzingatia hesabu ya unajimu katika muandamo wa Mwezi, walielekea katika maoni haya, wakitegemea hoja kadhaa ambazo zote zinasababisha mwishoni kwamba Sharia tukufu haikufanya hesabu ya unajimu kuwa sababu ya kisheria  ya kujua mwanzo wa Mwezi mwandamo, lakini ilifanya kuona kwa macho ni sababu ya kisheria ambayo tulikalifishwa, na  kwamba hesabu hii ni ya kidhana, haipandi ngazi ya kuona kisheria, na walitegemea idadi ya dalili, ambazo tutaorodhesha zote na kisha tutajadili kila moja baada ya hapo.

2- Madhehebu ya wanavyuoni wa Fiqhi wanaozingatia hesabu ya Unajimu:

Kundi la Wanavyuoni wa Fiqhi wanaona kuwa inajuzu kuzingatia hesabu kwa ajili ya kubainisha mwanzo wa Mwezi (mwandamo), na hao ndio tutanukuu kutoka maneno yao kama yafuatayo:

• Umdat ul-Qari na Al-Badr Al-Aini imetajwa kuwa:

Wengine, akiwemo Ibn Shuraih, Mutarrif bin Abdullah na Ibn Qutaybah, walisema kuwa maana yake: Walikadiria kwa kuhesabu vituo, kwa maana ya vituo vya mwezi.

Kisha akamnukuu Al-Qushayri, Mwenyezi Mungu amrehemu, akisema: “Ikiwa hesabu inaonesha kwamba Mwezi umetokeza kwenye upeo wa macho kwa njia inayoonekana lau si kwa kuwepo kizuizi, kama mawingu kwa mfano, hii inalazimu uwajibu wa kuwepo kwa sababu ya kisheria, na sio uhalisia wa kuona ambapo kuna masharti ya ulazima.”

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Daqiiq Al-Iyd, kama katika kitabu cha Ihkam Al-Ahkam:

Ninachosema ni kwamba: Hesabu haiwezi kutegemewa katika kufunga Saumu, kwa sababu Mwezi hutoka kwenye jua, kwa kuzingatia wanajimu wanavyoona, kwa kuwa Mwezi unatangulia hesabu ya Mwezi kwa kuona siku moja au mbili, kwa sababu huko ni kuzusha sababu ambayo Mwenyezi Mungu hakuiwekea sheria yake. Lakini ikiwa hesabu inaonesha kuwa Mwezi umetokeza kutoka kwenye upeo wa macho kwa namna inayoweza kuonekana, lau si kuwepo kwa kizuizi - kama vile mawingu kwa mfano, basi hii inalazimu kuwa ni wajibu, kwa sababu kuna sababu halali, na ukweli wa muandamo sio sharti la lazima; Kwa sababu maafikiano ni kuwa kufanya bidii kwa ishara: Kwamba leo ni siku ya Ramadhani, basi analazimishwa kufunga Saumu hata kama haoni Mwezi.”

• Anasema Imamu Al-Nawawi, akifafanua kipengele cha pili cha masaala ya Imamu Shafi katika suala hilo:

(Suala la nne) Mtunzi amesema: Iwapo Mwezi umefichika na alijua mtu wa hesabu na vituo vya Mwezi, na alijua kwa hesabu kuwa ni siku ya Ramadhani, basi kuna mitazamo miwili. (Amesema) Ibn Surayj ni wajibu afunge Saumu kwa sababu aliujua mwezi kwa dalili, hivyo anafanana na aliyejua kwa ushahidi wazi (na akasema) wengine hawafungi kwa sababu sisi tunaabudu kwa muandamo tu. Haya ni maneno ya Mtunzi na kundi fulani likaafikiana naye juu ya maoni hayo, na Al-Darami akasema: “Hafungi kwa kauli ya mnajimu. Na baadhi ya watu wakasema ni lazima kufunga. Akasema, akifunga kwa kauli yake, je, inatosha kwa faradhi yake? Kuna mitazamo  miwili: na akasema mtunzi wa kitabu cha Al-Bayan: Kama akijua kwa hesabu za vituo kuwa kesho ni Ramadhani, au akaambiwa na mwenye ujuzi kwa hilo, na akaamini na akakusudia na akafunga kwa kauli yake, basi kuna mitazamo miwili (Moja ya mitazamo hii) inatosha. Mtazamo huo umesemwa na Ibn Surayj, na Al-Qadhi Abu Al-Tayyib aliichagua rai hiyo kwa sababu ni sababu iliyomfanya kuwa na dhana iliyotangulia, hivyo ni sawa na vile akiambiwa na mtu muaminifu kuhusu kuushuhudia Mwezi (na mtazamo wa pili) haitoshi, kwa sababu nyota na hesabu haviingii katika matendo ya ibada.

• Imaam Ibn Al-Subki anasema katika Fatwa zake:

Kauli yake Mtume (S.A.W): “Fungeni mnapouona Mwezi na fungueni mnapouona Mwezi, kama kuna mawingu mengi, basi kadirieni siku za Mwezi.” Na katika Hadithi ya Al-Bukhari, “Timizeni siku thelathini za Shabani.” Na inaweza kusemwa: Wanakusudiwa wale wanaosema kuwa Saumu inajuzu au ni wajibu ikiwa hesabu inaashiria muandamo wake, na ni sura ya udhuru kwake ikiwa itaonesha kufunga kwa kukamilisha thelathini bila ya kuona Mwezi, tuliielewa maana yake nayo ni kuchomoza kwa mwezi na uwezekano wa kuuona, na hali hizi mbili hupatikana kwa Mwezi katika usiku wa thelathini katika nyakati fulani, kwa hivyo mzozo unatokea katika hilo kwa mujibu wa kanuni inayojulikana sana kwamba kuangalia ni kwa matamshi au kwa maana, anayezingatia matamshi anazuia maana ya maneno yake Mtume: (S.A.W)

{Basi timizeni siku za Shabani ili ziwe siku thelathini} na mwenye kuzingatia maana ya neno akasema: Hadithi ina maana ya hali iliyopo na akaashiria sababu, na ikipatikana, hata ikiwa ni kwa nadra, inafuatwa, na kauli yake “Mmeuona” haikusudiwi kuona wote kwa dalili ya uwajibu kwa kipofu kwa kauli moja. Na Ibn Umar alipomfahamisha Mtume (S.A.W) juu ya uono wake, aliwaamrisha watu kufunga, basi kinachokusudiwa ni kuona baadhi na kuthibitisha ima kwa hisia au kwa habari za yule ambaye ushahidi wake umekubaliwa. au ushahidi wa yule ambaye ushahidi wake umekubaliwa pamoja na masharti yake. Na kauli yake: “Mwezi ni hivi na hivi” tumeitaja, na makusudio yake ni kubainisha Mwezi wa kisharia wa Kiarabu na kupingana na wanachokifahamu watu wa hesabu, haibatilishi hesabu yao kabisa, bali badala ya kufafanua kuwa wakati mwingine ni thelathini na mara nyingine ni ishirini na tisa, kwa hivyo hakuna jibu ndani yake kwa wale waliosema kuwa Saumu inajuzu kwa hesabu kwa sababu haikutoka katika ukweli wa kwamba ni ishirini na tisa.”.

Na akasema mahali pengine:

 Na hapa kuna hali nyingine, ambayo ni kwamba hesabu inaonesha kuwa haiwezekani kuuona mwezi, na inatambulika kwa misingi ya uhakika, na iko karibu sana na jua. Katika hali hii, haiwezekani kulazimisha kuuona kwa busara, kwa sababu haiwezekani, kama tukiambiwa na mtoa habari mmoja au zaidi ambaye habari zake ni za uwongo au za makosa, basi yule ambaye anaelekea kutoikubali habari hii na kuifahamu kuwa  ni uwongo au ni makosa, hata kama mashahidi wawili watashuhudia, ushahidi wao hautakuwa ni wenye kukubaliwa, kwa sababu hesabu ni ya uhakika, na ushahidi na habari ni wa dhana, na dhana haipingani na uhakika, ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa kwake  ushahidi wazi na sharti lake kwamba kilichoshuhudiwa kinawezekana kwa maana, akili. na Sharia. Iwapo dalili ya hesabu hiyo imewekwa juu ya kutowezekana kwa kutokubalika katika Sharia kwa sababu ya kutowezekana kwa kinachoshuhudiwa, na Sharia haileti lisilowezekana, na hakuna matini yoyote ambayo imetujia kutoka katika Sharia kwamba kila mashahidi wawili ambao ushahidi wao umekubaliwa ikiwa shahidi ni wa kweli au wa uwongo, na faradhi ya Saumu na hukumu za Mwezi hazitegemei habari tu au ushuhuda, hata tukisema: dalili hapa ni kama ilivyosemwa na Mtunzi  kauli ya Sharia: “Fungeni akikuambieni mtoa taarifa, kwani lau tukipokelewa jambo hilo tunalikubali kwa mikono miwili, lakini hilo halikutajwa kabisa katika Sharia. Bali ni lazima tuthibitishe katika kuzikubali habari hizo ili tuujue ukweli wake kwanza, na hapana shaka kuwa baadhi ya wale wanaoshuhudia Mwezi huo huenda wasiuone na kuushuku, au anaona anachokidhania kuwa ni Mwezi na huo sio Mwezi, au macho yake yanamuonesha isipokuwa anaona au kushuhudia baada ya siku, na kosa likatokea katika usiku aliouona, au ujinga wake ni mkubwa unaompeleka kuamini kuwafanya watu wafunge kwa ajili ya malipo, au ni mwenye kutaka kuthibitisha uadilifu wake, basi anaichukua hiyo kuwa ni njia mpaka asifiwe na akubalike kwa watawala, na aina zote hizi tumeziona na kuzisikia. kwa hivyo mtawala lazima akipatwa na jambo kama hilo na akajua kutoka kwake au kwa habari ya mtu anayemwamini kwamba dalili ya uhesabu juu ya kutowezekana kuona ni kwamba hakubali ushahidi huu wala hathibitishi wala hahukumu kwa huo, na. kuambatana na asili katika kukaa kwa Mwezi, huu ni ushahidi wa kisharia uliothibitishwa mpaka kinyume chake kipatikane, na hatusemi kwamba Sharia imefuta hesabu zote.".

Mukhtasari wa Madhehebu za wale wanaozingatia hesabu za unajimu miongoni mwa Wanachuoni  wa Fiqhi:

Kwa kukagua maneno ya wale wanaozingatia hesabu za unajimu, tuligundua kuwa maneno yao yanaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

1 - Kwamba hesabu ya unajimu inapingana na unajimu, na baadhi yao, kama Ibn Al-Subki, wanaiona hivyo kwa uhakika.

2 - Haikatazwi kufanya hesabu za unajimu katika Sheria, mradi tu inafanywa na wataalamu na watu katika suala hili.

3 - Maono ya macho macho ni aina ya ushuhuda ambao uko chini ya masharti yake yote, na kwa hiyo sharti yake ni kwamba haijakiukwa kwa uhakika; Ushahidi juu ya muandamo wa Mwezi unarudishwa ikiwa hesabu itaonesha kutowezekana kwa kuonekana kwa mwezi, kama alivyosema Imam Ibn Al-Subki.

4 - Kuna viwango viwili vya hesabu ya unajimu:

 Kwanza: Tunapaswa kuifuata peke yake ilimradi tu ithibitike kuwa Mwezi unaweza kuonekana katika wakati maalumu katika sehemu maalumu bila kusubiri matokeo ya muandamo wa macho.

Ya pili: Itiliwe maanani katika kukanusha, sio katika kuthibitisha, maana yake ni kwamba hatutakubali muandamo wa macho isipokuwa kama unaafikiana na hesabu, na ikiwa inapingana na hesabu, haikubaliwi na ushahidi wa aliyeshuhudia muandamo wa Mwezi hazingatiwi kwa sababu anapingana na hesabu ya unajimu.

Sehemu ya pili katika ushahidi wa wale wanaopinga

Kutokana na kuzingatia hesabu ya unajimu katika kubainisha mwanzo wa Miezi ya mwandamo, wanavyuoni wanaopinga hesabu ya unajimu waligundua yafuatayo:

Dalili ya kwanza:

Hadithi ya Imamu Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah: “Fungeni mnapouona Mwezi na fungueni mnapouona Mwezi, ukifichikana basi timizeni thelathini”. Katika Hadithi nyingine Mtume (S.A.W) alisema:  “Kama kuna mawingu mengi, basi kadirieni siku za mwezi.”

Hadithi hii inathibitisha kama Sheikh Bakr Abdullah Abu Zaidi, mmoja wa watu wa zama hizi, anavyosema: “Hadithi kwa pamoja zinaonesha ukomo wa kupata yakini iliyotajwa hapo juu kwa njia mojawapo kati ya hizo mbili. Kufunga ni hukumu sababu yake ni: Kuuona Mwezi na kuukamilisha, baadhi yao huashiria ulazima wa kufunga na kufuturu baada ya kuuona au kuumaliza, kama Mtume (S.A.W) alivyosema: “Mkiuona Mwezi, basi fungeni, na mkiiona, fungueni, na ikiwa ni mawingu mengi kwenu basi timizeni mwezi siku thelathini.

Miongoni mwa Hadithi hizi ni ile iliyomaanisha kukataza kwa Saumu na kufuturu kabla ya kuona na kukamilisha, kama Mtume (S.A.W) alivyosema: “Msifunge mpaka mnapouona Mwezi, wala msifungue mpaka mnapouona. Ikiwa kuna mawingu kwenu, basi kamilisha hesabu ya siku thelathini.” Na kwamba hakuna Hadithi yoyote inayohusiana na hukumu ya kisharia na hesabu ya unajimu, na kuuita Mwezi kwa jina hilo.

Kwa hivyo, tafsiri ya Hadithi na kuiweka kuwa ni dalili  kutoka kwa wale wanaoipinga kwa kuzingatia sharti ya hesabu ya unajimu ni kuona kwa macho peke yake au kukamilika kwa idadi ya siku wakati wa mawingu.

 Na jambo jingine lililokuja katika muktadha wa kuiweka Hadithi hii ni kama dalili inapaswa kurejelewa, nayo ni tafauti ya maneno yake yaliyomo katika kauli yake “Mkadirie.” Baadhi ya mapokezi ya Hadithi hii yalikuja kwa kuitaja namna hii ya umoja, na baadhi yao yalikuja na kutajwa kwa mipaka, kama vile katika Hadithi isemayo “Ihesabu siku thelathini”, na baadhi yao yanasema kamilisheni mwezi ili uwe siku thelathini na kadhalika, jambo ambalo limelifanya kundi hili kubeba baadhi yao juu ya baadhi nyingine.” Kwa mujibu wa baadhi ya watu, hitimisho la yale waliyoyasema Maimamu katika tafsiri ya Hadithi hii ni tafsiri mbili:

Tafsiri ya kwanza:

 Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Omar kwamba yeye huwa hafungi ikiwa mbingu iko wazi na hufunga ikiwa ni mawingu mengi, kwa sababu anafasiri maneno yake Mtume, (S.A.W.), kwamba maana yake ni kukamilika kwa mwezi ili uwe siku thelathini, na huu ndio mtazamo wa Abu Hanifa, Malik, Al-Shafi, na wengi wa waliotangulia na waliokuja baadaye, wakabeba ibara hii: “Basi kadirieni kwake” kwa ajili ya kukamilisha hesabu ya siku thelathini.

Tafsiri ya pili:

Nayo ni kwa maana ya kupunguza idadi ya siku za mwezi, kwa hivyo wale wanaosema "Hesabu kwake" wameifasiri kwa maana ya kwamba wameipunguza idadi kwake kutoka kwa Aya ya Mola Mtukufu: {na mwenye dhiki} [AT-TALAAQ:7] Miongoni mwa walioshikilia rai hii ni Ahmad Ibn Hanbal na wengine ambao miongoni mwao wanaoruhusisha kufunga siku ya shaka ikiwa mbingu ni ya mawingu, na imepokelewa kutoka kwa Ibn Umar, (R.A). Mtume (S.A.W) amesema: {Sisi ni umma usiojua kusoma, wala hatuandiki wala hatuhesabu Mwezi hivyo na hivyo}. Yaani mara moja Mwezi ni siku ishirini na tisa na mara nyingine ni siku thelathini.

Dalili ya pili:

 Makubaliano ya Maswahaba juu ya kutoruhusiwa kufanya kazi kwa hesabu za unajimu kama ilivyoelezwa na Al-Qarafi, Ibn Abidin na Ibn Taymiyyah, na imepokelewa kutoka kwa Ibn Al-Mundhir, na kutoka kwa Maliki na Ibn Rushd Al- Qurtubi, na Ibn Taymiyyah pia amesema: “Hakika sisi tunajua katika Dini ya Kiislamu kwamba kufanya kazi katika kuandama Mwezi kwa ajili ya kufunga saumu au Hijja, au Eda, au hukumu nyinginezo zinazohusiana na mwandamo wa Mwezi kwa mujibu wa habari ya mwenye kuhesabu - kwamba anaona Mwezi au hauoni - haijuzu. Matini juu ya hili kutoka kwa Mtume (S.A.W) ni mengi, na Waislamu wameafikiana kwa kauli moja juu ya hilo, na hakuna hitilafu ya zamani kuhusu hilo hata kidogo, wala hakuna hitilafu ya hivi karibuni isipokuwa tu kwamba baadhi ya wanachuoni wa Fiqhi ambao wamekuja baadae walidai kwamba ikiwa Mwezi una mawingu, inajuzu kwa mwenye kuhesabu kufanya kazi kwa kuhesabu. Ikiwa hesabu inaonesha uoni wa Mwezi, anafunga Saumu, au vinginevyo hafungi. Kauli hii, hata kama ina manufaa katika hali ya kuwa na mawingu mengi na ni mahususi kwa mwenye kuhesabu, basi ni rai isiyo ya kawaida ambayo Wananvyuoni wameafikiana  kinyume chake. Ama kufuata hilo katika bayana, au kusimamisha kanuni ya jumla, hivyo ndivyo alivyosema Imamu Muslim.”.

Dalili ya tatu:

 Kutokuwa sahihi kwa hesabu za unajimu na kuhusishwa kwake na unajimu, jambo ambalo tuliamrishwa tuukanushe, na hilo ndilo lililowafanya Wanachuoni wa Fiqhi wengi wanaopinga kupitishwa kwa hesabu za unajimu kuchanganya kati ya mnajimu na mwenye kuhesabu kama inavyobainika kupitia maneno yaliyopita pamoja nasi na Wanavyuoni wa madhehebu ya Hanafi na Shafi, ambapo Imamu As-Sarkhasi alikataza kuchukua kwa hesabu ya unajimu kufuatana na kauli yake Mtume, (S.A.W): “Mwenye kwenda kwa mpiga ramli, na akamsadiki anayoyasema, basi atakufuru yaliyoteremshwa kwa Muhammad”.

Na kauli hii, ijapokuwa ilinukuliwa kutoka kwa Wanachuoni wa Fiqhi waliotangulia, lakini baadhi ya watu wa zama hizi wanaoona uharamu wa kuzingatia hesabu za unajimu nao wanasema hivyo kwa kuzingatia baadhi ya mambo, ikiwa ni pamoja na:

 1- Kwamba uhakika wa hesabu haukubaliwi isipokuwa kwa matokeo ya ambayo yanaonesha ujuzi wa hakika kwa ukweli wa matokeo yake na uthabiti wake, na kuwafahamisha wale wenye utambuzi wa kutunga sheria kwa hili na kurahisisha njia yake kwa ripoti kutoka kwa watu wa elimu kwa ajili ya kujua kiwango cha usalama wa tangulizi zake kwa mujibu wa Sheria, ikiwa Sheria ndio iliyofanya majaaliwa ni kwake.

Kwa hakika, hatuna dalili yoyote inayopatikana kwa namna hii ili kupata uhakika wa ushuhuda wake isipokuwa kwa ushuhuda wa baadhi ya wanaastronomia kwao wenyewe kwamba hesabu yake ni ya hakika, na dalili ya kimaada ifuatayo inadhoofisha utendaji wa ushuhuda wao, na unatia nguvu kukanusha kwa mifano yao katika elimu ya nyota kutokana na ukosefu wa yakini kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Sheria ya Al-Azhar katika maamuzi yake yaliyochapishwa, licha ya kuwa Sheria haizingatii ukweli wa habari na ushahidi isipokuwa kwa wale ambao ni mashuhuri kwa uadilifu wao wa kisheria.

2- Kuna dalili ya kimaada katika medani ya sasa kwamba hesabu ni jambo linalokisiwa, lenye jitihada na linaloingizwa na makosa - na hiyo ni katika matokeo ya hesabu ambayo wenye kuhesabu wanavichapisha kwenye magazeti kutokana na kutowezekana kwa kuona Mwezi wa Ramadhani au Mwezi wa Eid Al-Fitr, kwa mfano, katika usiku fulani, basi muandamo wa Mwezi unathibitishwa kwa ushuhuda wa kisheria uliorekebishwa, au muandamo katika usiku huo huo ambao waliamua kuwa haiwezekani kuandama Mwezi.
 

Sehemu ya tatu: kujadili dalili za wanaokaa suala hilo

1- Kujadili ufahamu kwa Hadithi:

- Ufahamu wa wale waliokataza kuzingatia hesabu ya unajimu kwa Hadithi, kama ilivyotajwa, unategemea nguzo mbili:

• Ya kwanza ni kauli yake Mtume (S.A.W), “Fungeni mnapouona Mwezi.” Ushahidi ni kwamba walifahamu kuwa Hadithi imefanya sababu ya kisheria ya kujua mwandamo wa Mwezi ni muandamo tu.

• Ya pili ni kauli yake Mtume (S.A.W), “Basi kadirieni” kwa mujibu wa rai ya Mwanachuoni mmoja, yaani “punguzeni” au “kamilisheni.”

- Kuhusu maudhui ya kwanza, inaweza kusemwa kwamba kuzingatia kuona ni kama sababu ya kisheria ya kujua mwanzo wa Mwezi hali hii haikuzuii kuzingatia hesabu ya unajimu na kujua mwanzo wa Mwezi pia. Hii ni kwa sababu Maimamu wa Usuul Al-Fiqhi walitaja kuwa sababu za kisheria ambazo maana yake inaeleweka zinaweza kupimwa juu yake, na hiyo ni kwa sababu wao walizichukulia sababu za kisheria kuwa ni dalili za hukumu na sio zile zinazolazimu kwake. Al-Zarkashi, Mwenyezi Mungu amrehemu, anasema katika Al-Bahr Al-Moheet: “Nayo katika lugha: ni kitu ambacho hukumu inatokea kwake na sio kwa sababu yake. Yaani,  kwa sababu kitu hicho sio mshawishi katika kuwepo, bali ni njia yake tu. Kwa mfano, kamba ni zana ya kuchota maji kutoka kisimani, na sio athari katika utoaji, bali ni harakati ya yule anayechota maji.

Na katika Sheria: wengi walisema: Ni maelezo ya wazi na yenye nidhamu ambayo kusikilizwa kulionesha kuwa ni dalili ya hukumu ya kisheria, kama vile kuifanya miale ya jua kuwa ni dalili ya uwajibu wa Swala.

Kwa hiyo, sababu hapa, ambayo ni kuona, haihusiani na hukumu yenye kiungo cha ushawishi, bali ni ufafanuzi tu, na ipasavyo, uthibitisho wa maana ya kuona katika sehemu nyingine unahalalisha kuifanya kuwa sababu ya kisheria pia, nayo ni chaguo la kundi la Wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi kama vile Al-Ghazali na Alkiah. Ifuatayo ndiyo inayounga mkono hili kutokana na maneno ya Wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi:

Amesema katika kitabu cha Al-Bahr Al-Moheet: “Suala la [kupima katika sababu] kama hukumu ikiongezwa kwenye sababu na ila ya sababu inajulikana ndani yake, ikiwa inapatikana katika maelezo mengine, je, inajuzu kuiweka sababu? Ni suala la kupima katika sababu, hivyo imepokelewa kutoka kwa Abi Zaid Al-Dabousi na wengineo kuwa katazo, wakasema: hukumu inafuata sababu bila ya kujua hekima ya sababu hiyo, haijuzu kufanya ulawiti kuwa ni sababu ya adhabu kwa kulinganisha na uzinifu, wala kufukua makaburi ni sababu ya kukata kiganja cha mkono kwa kulinganisha na wizi, na Al-Amidi, Ibn Al-Hajeb na Al-Baydawi wamechagua hivyo. Al-Isfahani, mfasiri wa kitabu cha Al-Mahsul, amesema kuwa rai hiyo ni dhahiri zaidi, lakini kilichopokelewa kutoka kwa wenzetu ni kuwa inajuzu, na Al-Ghazali na Alkiah waliichagua, na ibara yake ni: Tunaamini kwamba inajuzu kuzingatia sababu kwa sababu, sharti ni sababu hizo mbili hazitofautiani katika maana inayozingatiwa....”

Kisha akasema, Mwenyezi Mungu amrehemu: “Na baadhi yao wakasema: Tukisema kwamba: Sababu, vikwazo, na masharti ni hukumu za kisharia ambamo kupima kumetokea, na tukisema: Sio hukumu ya kisharia, basi kuna mazingatio katika mtiririko wa kupima kwake. Al-Qurtubiy, Mwenyezi Mungu amrehemu, alisema: Bora zaidi ni kutokea kwake, kwa sababu tulifikiri kuwa zinaa imenasibishwa na sababu ya adhabu ya kupigwa mawe, na tukaikuta katika kulawiti, kwa mfano, hivyo basi ni muhimu kuthibitisha sababu yake, na pia ni katika hali ya wizi hadi kufuatiwa na kufukua makaburi na kuchukua sanda. Hii ni ikiwa masharti yanatimizwa kwa usahihi. Ikaisha, na wakawajibisha anayekataza kuzuia kufahamu mvinyo kuwa ni pombe kwa kuwa umaalumu wa kuelezea mahali pale, kama pangezingatiwa mahali pa hukumu, ingelazimu kuharamishwa kupanua hukumu, na kuzuia kupanuka kwake mlinganisho huo uliondolewa kabisa. Na iliyochaguliwa ni kuwa inajuzu kubainisha sababu ya hukumu kwa mlinganisho kwa sababu nyingine, basi Mwenyezi Mungu akiamrisha kupigwa mawe mzinifu anaweza kuuliza sababu ya hilo mpaka aijue sababu yake ambayo ni zinaa. Ikithibitika kuwa uzinifu ndio sababu ya kupigwa mawe, ni sahihi kuifafanua kwa sababu ya kupitia kwake kitu kisichokuwa zinaa, na pia inajuzu kuifafanua hukumu iliyothibitishwa kwa Zayd na inapitia kwa Amr wakati wa kuelewa maana inayolazimisha kupitiwa, hali hiyo inajuzu kwa kauli moja, na kadhalika yale yaliyotangulia.."

Suala hili limepitishwa kwa mapana na marefu kutokana na umuhimu wake katika utafiti wetu hapa, na kwa sababu Al-Zarkashi, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikusanya ndani yake kile ambacho hakikukusanywa na ushahidi mwingine, na kwa hiyo kundi la Wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi wanaruhusu kupima katika sababu maadamu masuala mawili yalikuwa yameungana kimaana, na maana katika suala letu hapa ni dhahiri na ni kuthibitisha mwanzo wa Mwezi, maadamu Sayansi ilithibitisha ukamilifu wa matokeo ya hesabu ya unajimu, hii ilikuwa ni sababu ya kuzingatia hesabu ya unajimu kwa jumla ya kubainisha mwanzo wa Mwezi katika kila hali. miongoni mwa hali hizi ni njia ya kubainisha mwanzo wa Mwezi, na kila hali ina sababu ya wazi na ya nidhamu kwa kile kitakachooneshwa baadaye katika majibu ya ushahidi wa tatu kwa wanaopinga hivyo.

Ama kuhusu ufahamu wa neno "basi kadirieni", jibu lake ni kama ifuatavyo:

Ukadiriaji katika lugha una maana tofauti, miongoni mwao tumetaja kupunguza na ukamilisho, na pia yale yaliyotajwa katika lugha ya sheria, na Ibn Surayj kutoka kwa wanavyuoni wa madhehebu ya Shafi aliitaja kuwa ni ushahidi kwamba waliikadiria kwa hesabu ya vituo, kama tutakavyotaja kwa undani hivi punde.

Haya ni pamoja na kuwa waliokataza kuzingatia hesabu ya unajimu wamehitalifiana katika maana ya kukadiria kwa rai mbili zinazopingana, moja wapo inayolazimisha kufunga saumu siku ya shaka kuwa ni kutokana na Ramadhani kwa tahadhari, nao ni Wanavyuoni wa Madhehebu ya Imamu Ahmad Ibn Hanbal iwapo mawingu yanazuia kuona Mwezi, na wengine wakafanya ukamilisho wa Mwezi wa Shabani kuwa ni jambo lisiloepukika, na hao ndio waliobakia. .

Hakuna makubaliano katika kuamua maana ya kuthamini.

Hasa kwa vile makadirio hayo yametajwa katika hotuba ya Mtume (S.A.W) kwa maana ya hesabu, kama ifuatayo kuhusu dalili za wanaozingatia mahesabu ya unajimu.

2. Kujadiliana kwa dalili za makubaliano:

     Ili kujadili ufahamu wa wale wanaozuia hivyo kwa kauli moja, ni lazima kwanza tuelewe maana ya makubaliano, kisha tutaona kiwango cha utambuzi wake katika suala letu.

Makubaliano hayo yanafafanuliwa na Wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi kama: “Ni makubaliano ya Wenyekujitahidi katika umma wa Muhammad katika zama miongoni mwa zama juu ya hukumu ya tukio”

Katika kueleza maana ya makubaliano hayo, Wanachuoni wa Usuul Al-Fiqhi walitaja kuhusu kubainisha maana ya makubaliano ni kushirikishana rai, ikiwa wenyekujitahidi waliikubali kwa maneno yao yote au kwa vitendo vyao vyote, au kwa maneno ya baadhi yao au vitendo vya wengine kama katika makubaliano yaliyo wazi, au kwa maneno au vitendo vya baadhi yao pamoja na ukimya wa baadhi yao, kama katika makubaliano ya kimya / kunyamaza ya wale wanaoyaona kuwa ni hoja.

     Kwa hivyo, ni wajibu wetu hapa, baada ya kufahamu maana ya makubaliano, kubainisha nafasi ya makubaliano katika suala letu, kama inavyodaiwa na wapingaji. Na kwa mujibu wa yale yaliyotajwa katika maneno ya wapingaji, basi kauli moja inayodaiwa hapa ni: kupinga kwa kufanya kazi kwa kutumia hesabu katika kubainisha mwanzo wa Miezi ya mwandamo, kwani mapokezi yanayopita yametoka kwa Sheikh Ahmed Ibn Taymiyyah, ambapo anasema: “Hapana shaka kwamba imethibitishwa kwa Sunna sahihi na makubaliano ya Maswahaba kwamba haijuzu kutegemea hesabu ya unajimu”

    Kwa hiyo, swali ni: Je, makubaliano yanayodaiwa hapa yanawekwa chini ya aina gani ya makubaliano yaliyotajwa na Wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi? Je, ni mapatano kwa namna ya kauli zinazotolewa na Maswahaba kwa kukataza kuzingatia hesabu ya unajimu katika kubainisha mwanzo wa Mwezi wa mwandamo?

Jibu, bila shaka, ni kwamba hili halijathibitishwa katika suala letu, kwa sababu hakuna makubaliano juu ya ukatazaji huu. Kwa sababu ili hili liweze kufikiwa, ni lazima suala hilo litokee kwanza katika zama za Maswahaba kwa njia ya Fatwa au uchunguzi kuhusu hukumu ya kutumia hesabu ya unajimu, hivyo basi mmoja wa Maswahaba anajibu hilo, kisha kunakuwa na makubaliano juu ya uharamu wa kutumia hesabu, au mtu anafuata hesabu, na mmoja wa maswahaba watukufu akaikanusha, basi waliosalia wakaafikiana juu ya hilo na hivyo ndivyo makubaliano ya Maswahaba yanayojulikana kwa watu wa fiqhi na elimu, kama tulivyoona katika makubaliano yao juu ya urithi wa bibi na makubaliano yao juu ya mkusanyiko wa Qur'ani na makubaliano yao juu ya kwamba Maimamu wanatoka kwa Maquraishi, na hivyo katika yote haya, suala lazima litoke na kauli kutoka kwa mmoja wa maswahaba wa maoni yake hutokea. Baada ya hayo, kunakuwa na makubaliano ya wazi au makubaliano ya kimyakimya / kunyamaza  juu ya yale ambayo mmoja wao aliyaonesha. Kwa hivyo ni nini kilifanyika katika suala letu hapa, ni kama hivi? Jibu ni kwamba hili ndilo ambalo hakika halikutokea hapa, halikutokea swali au hakukuwa na utafutaji wa hukumu ya kuchukua kwa hesabu ya unajimu, na lengo la kinachoweza kudaiwa hapa ni kwamba kilichotokea ni makubaliano tu juu ya kufanya kazi kwa kuuona mwezi, ama kuhusu hali ya kufanya kazi kwa hesabu ya unajimu, haikutajwa katika maneno ya Maswahaba kukanusha au kuthibitisha. Kwa hiyo, makubaliano hapa, ni kutenda kwa kuona Mwezi, hali ambayo inatofautiana na mabishano, nayo ni hukumu ya kufanya kazi kwa mahesabu katika kuthibitisha mwanzo wa Miezi.

    Kunaweza kuwa na pingamizi hapa kwamba sio tu makubaliano yao ya kutenda kulingana na kuona na kuacha hesabu ya unajimu ni makubaliano juu ya uharamu wa kufuata hesabu?

    Jibu ni kwamba imeamuliwa na wanavyuoni wa Usuul Al-Fiqhi kwamba kuacha kufanya jambo fulani si uharamu wa kufanya kazi na jambo hilo kama alivyolithibitisha hilo na akafafanua katika ushahidi wake Sheikh Abdullah Ibn Al-Siddiq (Mwenyezi Mungu amrehemu), pale anaposema,: “Hali ya kuacha ikiwa haikuambatanishwa na matini kwamba kitendo kilichoachwa ni haramu si hoja katika hilo, bali makusudio yake ni kuashiria kuwa kuacha kitendo hicho ni halali, ama kitendo kilichoachwa ni haramu, maana hii haifahamiki kutoka kwa hali ya kuacha peke yake, lakini inafahamika kutokana na  dalili inayothibitisha hivyo”.

- Iwapo mtu atasema kuwa dalili ni ile iliyotajwa katika Hadithi sahihi iliyopokelewa kutoka kwa Al-Bukhariy na wengineo ambamo Mtume, (S.A.W), anasema: “Sisi ni umma usiojua kusoma, na hatuandiki wala hatuhesabu.” Maana yake ni kukataa kwa kufanya kazi ya hesabu, kwa hivyo jawabu la hilo ni kwamba tafsiri ya ibara ya “hatujui kuandika wala kuhesabu” Maimamu walihitalifiana kuhusu kauli hiyo, je ni habari tu kuhusu ukweli wa Waarabu wakati wa Utume wake Mtume (S.A.W), na kwa sababu hiyo haina amri yoyote ya kuacha hesabu ikiwa Sayansi ya Kiislamu inasonga mbele baada ya hapo, vinginevyo ingehitaji hivyohivyo Hadithi pia imekatazwa kuandikwa na hakuna Mwanachuoni hata mmoja amesema hivyo. Katika tafsiri nyingine, maana ya Hadithi hii ni Mtume (S.A.W.), ni mwenyewe, anapoeleza juu ya nafsi yake kwani yeye hajui kuandika wala kuhesabu.

      Sayyid Ahmed bin Siddiq Al-Ghamariy anasema katika ujumbe wake (Tawjiih Al-Andhar litawheed Al-Muslimiin fi As-Saumi wal-Iftaar): “Ikisemwa basi nini maana ya Hadithi hii? Tukasema: Maana yake ni kwamba Mtume (S.A.W), amekusudia kwa kauli yake: “Sisi ni umma usiojua kusoma” amekusudia nafsi yake, na kueleza juu ya kwamba yeye Mtume (S.A.W) hajui kusoma wala kuandika, wala kuhesabu kama ukweli ulivyo, na kwa hivyo itatosha kueleza idadi kwa kunyooshea vidole vyake, wala hataji neno la “idadi” ili afuatwe na watu waliokuwa kama yeye miongoni mwa umma wake.”.

Ibn Hajar, kwa kauli iliyotangulia, alionesha kauli nyingine kuwa Wale waliokanushwa kutoka kwao kuandika na kuhesabu ni wengi wa Waislamu waliokuwa pamoja na Mtume (S.A.W) wakati wa kuhadithiwa Hadithi hii.

Kwa hivyo, hakuna dalili katika Hadithi au katika makubaliano ya Maswahaba juu ya ukatazo unaodaiwa, kwa hivyo imebakia tu kujadili dalili ya tatu.

3. Majadiliano ya dalili ya kutokuwa sahihi kwa hesabu za unajimu:

     Ni lazima kutofautisha mwanzoni mwa mjadala wetu hapa kati ya hesabu zote mbili za nyota na unajimu, ambazo zilikuwepo katika kipindi fulani cha wakati uliochanganywa na elimu ya nyota. Mwandishi wa kitabu [Tahdiid Awail Ash-shuhur Al-Qamiriayh Royah Elmiya Shariah] anasema: “Hapana shaka kwamba mtazamo wa kuiga usio na fahamu kwa rai ya kundi la wanazuoni waliotangulia na wasiosema maoni yao kuhusu rai ya wanavyuoni wa hesabu. - yaani wanaastronomia – mtazamo huo ndio uliozalisha makosa makubwa kama haya, na watu wa kale wasiosema maoni yao kuhusu jambo hilo walikuwa na sababu kadhaa, Baadhi ya sababu hizi ni halali na kuzingatiwa, na zinaweza kuwa na udhuru kwa ajili yao, na baadhi yao haziwezi kuwa na udhuru kwa hali yoyote. Mchanganyiko uliopatikana katika vitendo vya kundi la watu wa zama zao baina ya elimu ya nyota na unajimu, uliwafanya baadhi yao kuwa na mashaka katika taarifa zote wanazozitaja, na huenda baadhi yao walifikiri kwamba kuainisha mwanzo wa Miezi na nyakati za Swala, au nyakati za kupatwa kwa jua na Mwezi, ni kama unafiki na upotofu wa wanajimu, na madai yao kwa elimu ya ghaibu na matukio yajayo.

   Kwa hivyo, yaliyo sahihi kwa Wanachuoni wa Fiqhi waliotangulia kueleza juu ya dhana ya hesabu hayana nafasi hata kidogo katika zama zetu hizi baada ya kuwaona wanaastronomia wakithibitisha kutokea kwa kupatwa kwa Jua au Mwezi katika wakati maalum, hivyo ni kwa mujibu wa yale wasemayo, na hayo ni kwa sababu tu Mwenyezi Mungu Mtukufu aliujaalia mwendo wa jua na mwezi kuwa ni hesabu isiyobaki nyuma; Kwa hiyo, Sayansi katika wakati wetu ina uwezo wa kutambua hesabu hii na kuitegemea katika mambo mengi, ambayo ndiyo inafanya kuzungumza juu ya usahihi wa hesabu ya unajimu sio sahihi yenyewe.

Sehemu ya nne

Dalili za wale wanaozingatia hesabu ya nyota katika kutambua mwanzo wa Miezi ya mwandamo.

Dalili za kikundi hiki zinaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

Dalili ya kwanza:

 Kauli yake Mtume, (S.A.W), katika Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Muslim: “Ukiuona Mwezi, basi fungeni Saumu, na ukiuona, fungueni Saumu, na ikiwa ni mawingu mengi basi kadirieni kwake.” Ibn Surayj anasema kwamba “kadirieni kwake” neno hilo linaelekezwa kwa mwenye elimu ya hesabu, na kauli yake Mtume, (S.A.W) katika Hadithi nyingine: “Basi kamilisheni idadi ya siku thelathini”. Maneno hayo yanaelekezwa kwa umma.

Hadithi hiyo ilikuwa ni dalili kwa watu hawa juu ya uhalali wa kuhesabu kwa ajili ya kubainisha mwanzo wa miandamo ya Mwezi.

- Pia, tunaona kuwa usemi huu: “kadirieni” umekuja katika baadhi ya Hadithi zenye maana ya kuhesabu, kama katika Hadithi ya Mpinga Kristo (Al-Masihi Ad-Dajaal) iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Muslim na ambamo Maswahaba walimuomba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), wakisema: Siku hiyo, ambayo ni kama mwaka, inatutosha sisi kuswali Swala ya siku moja,  Mtume (S.A.W), akasema: “Kadirieni kwake tu.”, ni wazi kwamba kwa kuwa dalili zilizowekwa zitavurugika katika wakati huu – tunamuomba Mwenyezi Mungu atulinde – Mtume, (S.A.W), ametuelekeza kukadiria kwa hesabu katika Swala, inawezekana kwamba hii ni amri kwa kuhesabu inayohusiana na Saumu, kwani muda wa kukaa kwa Mpinga Kristo ni mwaka na zaidi ya kile kinachopaswa kuambatana na ujio wa mwezi wa Ramadhani. Na Mwenyezi Mungu Anajua Zaidi hali hiyo.

Dalili ya pili:

- Muandamo huo sio sababu pekee ya kisheria ambayo hukumu inaegemezwa, nayo ni ulazima wa kufunga Saumu au kufuturu, kwa dalili ya makubaliano yao kwamba aliyefunga na hajui muandamo wa Mwezi anapaswa kujitahidi maadamu asipate mtu wa kumjulisha mwandamo wa Mwezi, na kwa sababu hiyo, hesabu ya nyota badala ya kuandama katika baadhi ya hali inawezekana; Ni lazima tufanye bidii kwa aliyefunga, na ni jambo lisilokuwa muandamo ambalo linachukua nafasi yake, kwa hivyo, ikiwa makusudio ya Sheria yamefikiwa kutokana na muandamo kwa hesabu, tunaweza kuufanya kuwa ni dalili ya kujua mwanzo wa Mwezi, ni kama kuandama.

Dalili ya tatu:

     Amri ya kuandama peke yake na kutosheka nayo ilitajwa kwa sababu yake katika Hadithi tukufu na kuhusishwa na dari ya elimu ya zama za ufunuo mtukufu kutokana na kuenea kwa ujinga uliokithiri na kadhalika, iwapo sababu hii itabadilika na elimu itapanuka, inawezekana kutegemea zaidi ya kitu kingine isipokuwa kuandama, kama vile hesabu, nayo dalili hii ya mwisho ni ile ambayo imechukuliwa na kundi la watu wa zama hizi, akiwemo Mwanachuoni Sheikh Ahmed Shakir, anasema (Mwenyezi Mungu amrehemu) katika ujumbe wake mwanzoni mwa miezi ya kiarabu: “Hapana shaka kwamba Waarabu kabla ya Uislamu na katika siku za mwanzo za Uislamu hawakujua elimu ya nyota kwa maarifa thabiti ya kisayansi, Walikuwa ni umma usiojua kusoma na kuandika, wala hawakuandika wala hawakuhesabu, na yeyote aliyekuwa na ujuzi miongoni mwao alijua machache tu, alijua hivyo machache kwa kuangalia kwa makini, au kufuatilia, au kusikia habari, bila kuzingatia kanuni za hesabu, wala kwa uthibitisho wa uhakika ambao unarudia tangulizi za awali. Kwa hivyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akafanya rejea ya kuthibitisha mwezi katika ibada zao kwa amri ya uhakika na inayoonekana iliyo ndani ya uwezo wa kila mmoja wao, au ndani ya uwezo wa wengi wao, nayo ni kuandama Mwezi kwa macho. Hali hii ndiyo ni sahili zaidi kwa nyakati za ibada zao, nayo ndio hali ambayo yakini na kujiamini hufikia katika uwezo wao, na Mwenyezi Mungu haibebeshi nafsi kupita uwezo wake, na hiyo haikuwa kwa mujibu wa hekima ya sheria kwamba msingi wa uthibitisho katika miandamo ya Mwezi ni hesabu na nyota, na wao hawajui lolote katika hayo katika miji yao, na wengi wao ni watu wa majangwani, na habari za maeneo ya miji mikuu haziwafikii, isipokuwa katika vipindi ambavyo wakati mwingine huwa karibu na wakati mwingine mbali. Lau angewatengenezea kwa hesabu na nyota, ingewasaidia”.

     Kisha anasema baada ya hayo, Mwenyezi Mungu amrehemu: “Amri ya kuthibitisha hali ya kuandama peke yake ilikuja kwa sababu iliyobainishwa, nayo ni kwamba umma huu (umma usiojua kusoma wala kuandika wala kuhesabu), na sababu inazunguka kwenye athari, kuwepo na kutokuwepo. Kwa hiyo umma ukitoka katika hali yake ya kutojua kusoma na kuandika na kuanza kuandika na kuhesabu, namaanisha, unakuwa kwa ujumla wake miongoni mwa wale wanaozijua Sayansi hizi, na watu - wa kawaida na wasomi - wanaweza kufikia yakini na uhakika katika kuhesabu mwanzo wa Mwezi, na wanaweza kuamini hesabu hii kama wanavyoamini kuandama au zaidi, ikiwa hali hii itakuwa hali yao katika kundi lao na haipo tena sababu ya kutojua kusoma na kuandika ni lazima warejee kwenye uhakika uliowekwa, na wachukue uthibitisho wa miezi kwa kuhesabu peke yake.”

Hitimisho la utafiti na maoni yaliyochaguliwa:

     Baada ya kuchunguza ushahidi wa wale wanaopinga na wanaozingatia hesabu na kujadili ushahidi wa wale wanaopinga hesabu, inaweza kupatikana kwetu kwamba madhehebu ya wale wanaozingatia hesabu ya nyota katika kubainisha mwanzo wa Miezi ndiyo yenye nguvu zaidi katika suala la ushahidi na kufaa zaidi kwa uthabiti wa Sheria na taarifa za Sayansi ya kisasa, na kwa hivyo Madhehebu ya wale wanaozingatia hesabu ya nyota umeamuliwa kwa viwango viwili: Cha kwanza ni kuwa kuthibitisha mwanzo wa Mwezi wa mwandamo inatosha kuthibitisha hesabu ya nyota peke yake, na ya pili ni kuchukua hesabu ya nyota kwa maono ya kimacho, yaani, katika hali ya kukanusha siyo katika hali ya uthibitisho, kiwango cha pili hicho ndicho tunachochukua na kukichagua katika suala hili; kwa sababu kukichukua ni njia ya kutoka katika mzozo kwani kinachanganya kuandama Mwezi kwa macho hali ambayo imeamriwa nayo na hesabu sahihi ya nyota kwa wakati huu. Chaguo hili lilichaguliwa na kundi la Wanazuoni wa zama hizi, akiwemo Mwanachuoni Sheikh Yusuf Al-Qaradhawi, ambaye anasema katika kitabu chake: (Kaifa Nataamal Maa As-Sunnah An-Nabawiyah): “Nimekuwa nikitoa wito tangu miaka tuzingatie hesabu ya uhakika ya nyota - angalau - katika hali ya kukanusha na sio katika hali ya uthibitisho, ili kupunguza tofauti kubwa inayotokea kila mwaka mwanzoni mwa Saumu na katika Eid Al-Fitr, hadi kikomo kinachofikia siku tatu baina ya baadhi ya nchi za Kiislamu, na maana ya kuchukua hesabu katika hali ya kukanusha ni kwamba tunaendelea kuthibitisha Mwezi kwa kuandama kwa mujibu wa mtazamo wa wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi wa zama zetu, lakini ikiwa hesabu inakanusha uwezekano wa kuandama, na inasema kwamba haiwezekani kwa sababu Mwezi haukuzaliwa mahali popote katika ulimwengu wa Kiislamu, ilikuwa ni wajibu kwamba ushahidi wa mashahidi usikubalike kwa hali yoyote; kwa sababu Ukweli - ambao umethibitishwa na elimu ya uhakika ya hesabati – unawakadhibisha, na katika hali hii, muandamo wa Mwezi mpya hautakiwi kutoka kwa watu hata kidogo, na wala mahakama za kisheria wala Ofisi za Fatwa au mambo ya kidini hazifungui milango yake kwa yeyote anayetaka kutoa ushahidi kuhusu kuandama kwa Mwezi mpya.”.

Rai hii pia ndiyo iliyokubaliwa na Ofisi ya kutoa Fatwa ya Misri, tangu miaka kadhaa ambapo kuingia kwa mwezi kunathibitishwa na hesabu zote mbili za unajimu pamoja na kuandama kwa kuona pia, kama ilivyotangazwa na Mufti Mkuu wa Misri katika taarifa ya kuthibiti kuandama kwa Mwezi wa Ramadhani kila mwaka.

- Kwa hiyo, haya ni maoni ambayo ni karibu na roho ya Sheria na inafaa zaidi kupitishwa kwa wakati wetu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye Kufanikisha kila jema.

Marejeleo

Al-Ijmaa Inda Al-Usuliin, Prof. Ali Juma, Al-Quds kwa Uchapishaji na Utangazaji.

Ihkam Al-Ahkam cha Al-Amidi, Dar Al-Sumai.

Ihkam Al-Ahkam, Sharhu Umdat Al-Ahkam kwa Ibn Daqiq al-Eid, Al-Muhammadiyah Sunnah Press.

Awail Ash-Shuhuur Al-Arabiah, Ahmed Shaker, Maktaba ya Ibn Taymiyyah.

Al-Bahr Al-Moheet cha Al-Zarkashi, Dar Al-Ketbi.

Bughyat Ar-Raid Bitahqiq Majmaa Az-Zawaid wa Manbaa Al-Fawaid kwa Nour Al-Din Al-Haythami, Dar Al-Fikr.

Tahdid Awail Ash-Shuhur Al-Qamariyah Roiay Elmiyah Shariyah, Dk. Mustafa Abdel Basset, mchapishaji wa Chuo cha Kiislamu cha Utafiti wa Kisayansi.

Tawjih Al-Andhar litawhiid Al-Muslimiin Fi As-Swaumi wal Iftaar, As-Said Ahmad Ibn As-Siddiq Al-Ghamari, Dar An-Nafais.

Haashiyat Ibn Abidin, Dar al-Kutub al-Ilmiyya.

Al-Hukumu Ash-Sharii li-Roiat Al-Hilal bil Absaar, Dk. Muhammad bin Abdul Karim Al-Jazaery, iliyochapishwa na Al-Maaref Foundation kwa uchapishaji.

Al-Thakhira kwa Imam Al-Qarafi, Dar Al-Gharb Al-Islami.

Ar-Rad Al-Muhkam Al-Matiin kwa As-Said Abdullah Ibn Al-Siddiq Al-Ghamari, i: Maktaba ya Cairo.

Rawdat At-Talibin kwa Imam An-Nawawi, Dar Alam Al-Kutub.

Sunan Abi Dawood, Jamiyat Al-Maknaz Al-Islami.

Sharhul Bahja Al-Wardiya Bihawashi Ash-Sheikh Ibn Al-Qasim Al-Abadi, Al-Maimani Press.

Sahih Muslim, Jamiyat Al-Maknaz Al-Islami.

Ilmul Falak, kwa Dk. Yahya Shami, Dar Al-Fikr Al-Arabi.

Umdat Al-Qari, Dar al-Kutub al-Ilmiyya.

Al-Fatawa Al-Kubra kwa Ibn Taymiyyah, Dar al-Kutub al-Ilmiyya.

Fatawa Al-Subki, Dar Al-Maarif.

Fiqhi An-Nawazil, Sheikh Bakr Abdullah Abu Zaid, Dar Al-Resalah.

Fath Al-Bari, Sharh Sahih Al-Bukhari kwa Ibn Hajar al-Asqalani, Salafiyyah.

Kamusi Al-Muheet kwa Firouzabadi, Shirika la Vitabu vya Kimisri.

Kashaf Al-Qinaa an Matn Al-Iqnaa kwa Sheikh Mansour Al-Bahouti, Dar Al-Kutub Al-Ilmiyya.

Kaifa Nataamal Maa As-Sunnah An-Nabawiyah, Dk Yusuf Al-Qaradawi, Toleo la Dar Al-Wafa’a.

Lisan al-Arab cha Ibn Manzur al-Afriqi, Dar Al-Maarif.

Al-Mabsout kwa As-Sarakhsi, Dar Al-Maarifa.

Al-Majmoo’ Sharhu  Al-Muhadhdhab kwa Yahya bin Sharaf Al-Din Al-Nawawi, Al-Muniria Press.

Majmuu Al-Fatawa kwa Ibn Taymiyyah, King Fahd Complex.

Al-Mughni kwa Ibn Qudamah Al-Maqdisi, Dar Ihyaa At-Turath Al-Arabi.

Manah Al-Jalil, Sharhu Mukhtasar Khalil, kwa Sheikh Alaish, kilichochapishwa na Dar Al-Fikr.

Share this:

Related Fatwas