Kufanya muamala na Benki
Question
Ni ipi hukumu ya kukodisha mali maalumu kwa benki?
Answer
Kukodisha mali isiyohamishika - kwa mikataba iliyoidhinishwa ya kukodisha - kwa mabenki na kuchukua malipo ya kukodisha ni kama vitu vingine vyote vinavyoruhusiwa kisheria. Vile vile, matumizi yake - yaani, kodi - katika nyanja zote za matumizi hali hiyo inaruhusiwa; na hakuna ubaya kwa hilo kwa mujibu wa Sharia. Kwa sababu ni haki zinazotokana na mkataba halali. Imethibitishwa kisheria kuwa asili ya mikataba na shughuli inaruhusiwa, isipokuwa kama kuna dalili ya kisheria ya kukataza hivyo. Kukodisha ni halali kwa mujibu wa Qur’ani, Sunna, na makubaliano ya wanachuoni.