Fikra kali.

Egypt's Dar Al-Ifta

Fikra kali.

Question

Ni zipi fira kali na sura zake zipoje.

Answer

fikra kali huzingatiwa moja ya hatua ya kwanza ambayo hutengeneza muundo wa kwanza katika miundo ya fikra kali, na katika hatua hiyo mwenye msimamo mkali huchukuwa msimamo wa kifikra kitabia kuvuka mpaka wa maana inayofahamika kwenye jamii yake, au kikundi kikuu ambacho anakifuata, mwenye fikra kali huanza kukinai kwake binafsi na fikra zake katika kuwa mbali na mipaka ya ukati na kati na usawa, na kuwa karibu na vitendo vya misimamo mikali na hukumu za kimakabiliano, kwa mfano mtu mwenye muelekeo wa kibaguzi kwa watu weusi huchukuwa msimamo wa kifikira na kitabia unaovuka mpaka wa msingi wa pamoja wa jamii yake ambayo inapinga ubaguzi na msimamo mkali kwenye hili na kwa mwenye msimamo mkali kwenye dini na mengine.

Fikra kali ni uadui wenye mwelekeo wa mtu binafsi au kundi wenye kuakisi kwa mtu mwenyewe au kwa mwingine, ni sawa sawa huyu mwingine akiwa ni mtu binafsi au kundi au serikali au jamii au jimbo au nchi au jamii ya Kimataifa, na fikra kali zanalenga kueneza fikra zisizo na mrejeo yanayokubalika na Sharia au sheria za kiraia au kimataifa ili kuleta shaka katika malengo masilahi mifumo na imani kwa ajili ya mapato madogo au makubwa kwa njia isiyo halali, fikra kali huathiri vibaya usalama wa mtu kundi nchi na jamii ya Kimataifa, kama vile hupelekea mtikisiko wa usalama wa kifikira kitamaduni na wakati mwingine huleta vitendo vya matumizi ya nguvu na ugaidi.

Share this:

Related Fatwas