Hukumu ya makubaliano yasiyofaa kat...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya makubaliano yasiyofaa katika nchi zisizo za Kiislamu

Question

Hukumu ya makubaliano yasiyofaa katika nchi zisizo za Kiislamu 

Answer

Shukrani ni za Mwenyezi Mungu ambaye Ameteremsha Kitabu chake cha ubainifu wa kila kitu, na kikabainisha mpaka kati ya halali na haramu, na kipimo cha kina cha kufahamu mashirikiano sahihi na mabaya, kimekuwa ni Kitabu kilichokusanya mambo ya dini na ya dunia.

Rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad mwenye kubainisha mambo ya kwenye Kitabu, na kuondoa uzito kwa mwenye kukiendea pamoja na matatizo yake kwa watu wenye utambuzi, pia ziwaendee watu wa nyumbani kwake na Maswahaba zake wote.

Baada ya Utangulizi: Huu ni utafiti unaotibia moja ya matatizo ambayo yamekuwa na maneno mengi ndani ya zama zetu, nayo ni katika matatizo yaliyoeneza balaa ndani ya zama hii kutokana na wepesi wa kuenea kati ya nchi, na kufanya kazi zaidi ya kufahamiana kati ya wanadamu, hivyo Muislamu ni mwenye kuhitaji kufahamu yaliyo halali kwake na haramu katika mashirikiano yake na watu wa hiyo nchi, ikawa ni lazima kwetu kutafiti na kuleta kauli za Wanachuoni katika masuala yanayohusu makundi makubwa ya Waislamu nje ya mipaka ya nchi zao, hivyo ukawa utafiti unahusu “Hukumu za makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi zisizo za Kiislamu”, na mpango wetu katika utafiti huu unagawanyika sehemu nne, chini yake kuna masuala yafuatayo:

Uchambuzi wa Kwanza: Maana ya makubaliano kilugha na kimsamiati.

Uchambuzi wa Pili: Aina za makubaliano kwa upande wa usahihi na ubatili, na chini yake: Tafauti kati ya uharibifu na batili katika hukumu ya Kisharia:

Kwa madhehebu ya Abu Hanifa.

Kwa Jamhuri ya Wanachuoni.

Hukumu ya mkataba usiofaa ndani ya nchi ya Uislamu.

Uchambuzi wa Tatu: Hukumu ya makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi zisizo za Kiislamu na chini yake:

Madhehebu ya Wanachuoni katika masuala.

Uchambuzi sehemu ya mvutano.

Dalili za wanaosema kubatilika kwa hayo makubaliano.

Dalili za wanaosema kufaa kwa makubaliano.

Kauli yenye nguvu.

Dalili zinazopewa nguvu.

Miongoni mwa makubaliano yasiyofaa ambayo yanaelezea kuhalalisha kwa waliopitisha.

Majibu juu ya dalili za wazuiaji.

Uchambuzi wa Nne: Mambo yanayopaswa kuangaliwa katika utafiti huu.

UCHAMBUZI WA KWANZA:

Maana ya makubaliano kilugha na kimsamiati:

Makubaliano kilugha: Kiunganishi, kufunga dhamana na ahadi, ndani ya kamusi amesema: Kufunga kamba kuuza na ahadi ([1]):

Na huitwa pia mkusanyiko kati ya pande za kitu, husemwa: Kufunga kamba: Pindi pande moja inapokutana na nyengine na kufanya makubaliano kati yao ([2]).

Katika kitabu cha Miswbaah: Imesemwa: Makubaliano ya mauzo na mfano wake, na nimefanya makubaliano naye kwa maana: Nimeahidiana naye, na mwenye kufanya makubaliano ya kitu mfano wa baraza: Ni sehemu ya kufanyikia makubaliano, na makubaliano ya ndoa na mengine: Kufunga kwake na kupitisha kwake, na katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Timizeni ahadi} ([3]). Na kauli yake: و {Wala msiazimie kufunga ndoa} ([4]). Kwa maana: Wala msiazimie kufunga ndoa ndani ya kipindi cha eda ([5]).

Katika maana ya kimsamiati: Huitwa makubaliano kwa maana mbili:

Maana Jumla: Ni kila kinachofanyiwa makubaliano, mtu ana azimia kufanya yeye, au anafanya makubaliano na mwengine kufanya kwa ulazima, kama anavyosema Al-Jaswaswu ([6]), kutokana na hilo huitwa mauzo ndoa na makubaliano mengine ya fidia ni makubaliano, kwa sababu kila mmoja katika pande mbili za makubaliano hulazimika kutekeleza hayo makubaliano, na yameitwa pia kiapo juu ya mustakabali wa makubaliano, kwa sababu mwenye kuapa hulazimika kutekeleza alichoapa ikiwa kufanya au kuacha, vile vile ahadi na amani, kwa sababu mtoaji wake amelazimika kutekeleza hilo, vile vile kila kitu mwanadamu alichoweka sharti kwake mwenyewe atakifanya hapo baadaye basi hicho ni makubaliano, vile vile nadhiri na yanayoendana nayo ([7]).

Kutokana na maana jumla, kauli ya Al-Aalusy kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Timizeni ahadi} amesema: Kusudio lake linakusanya yote aliyolazimisha Mwenyezi Mungu waja wake na kuwapa amri na hukumu za kidini na yale wanayofanya makubaliano kati yao miongoni mwa makubaliano ya uaminifu mashirikiano na mfano wake miongoni mwa yanayopaswa kutekelezwa ([8]).

Maana maalumu: Kwa maana hii huitwa makubaliano au mkataba kwa kila kilichoanzishwa kutokana na tashi mbili ili kuonesha athari yake Kisharia, Al-Jarjani amesema: Makubaliano ni kuunganisha sehemu na matendo kwa uzuri na kukubalika ([9]).

Kwa maana hii imeelezwa na Zarkashy kwa kauli yake: Mfungamano mzuri kwa kukubali ulazima kama vile makubaliano ya mauzo ndoa na mengineyo ([10]).

Hapa maudhui ya tafiti ni makubaliano kwa maana maalumu.

UCHAMBUZI WA PILI:

Aina za makubaliano kwa upande sahihi na upande batili:

Makubaliano ima yatakuwa sahihi kwa asili yake na wasifu wake, ima kutokuwa sahihi si kwa asili yake wala kwa wasifu wake, ima yatakuwa sahihi kwa asili yake pasi ya wasifu wake au kinyume.

Aina ya kwanza, ni sahihi kwa makubaliano, aina ya pili ni batili kwa makubaiano, ama aina ya tatu ni yenye tafauti kati ya Wanachuoni, je sawa sawa yanaitwa makubaliano si sahihi na batili, au kuna tafauti kati yake ([11]).

Jamhuri ya Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Maliki Imamu Shaafi na Imamu Hambaly wao hawatafautishi kati ya batili na kutofaa, ambapo kwao maneno hayo mawili ni visawe isipokuwa katika baadhi ya masuala ya hija kuandikishiana na mambo ya (khuluu) mwanamke kujivua kwenye ndoa, na sababu ya tafauti hii ni kuwepo dalili ya hilo ([12]).

Ama watu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wao wanatafautisha kati yake, kwani makubaliano yasiyosahihi ni ya Kisharia kwa asili yake bila ya wasifu wake, na makubaliano batili yasiyo ya Kisharia kwa asili yake wala wasifu wake ([13]).

Jibu la madhehebu yao ni kuwa: Makubaliano yasiyofaa ni yaliyokuwa sahihi katika asili yake yameharibika katika wasifu wake, kwa maana kasoro hapa hutokea kwenye sifa miongoni mwa sifa za makubaliano pamoja na kubakia salama asili yake na nguzo zake.

Mfano wa hilo: Mauzo ya riba, kama vile kuuza dirhamu moja kwa dirhamu mbili, hapa asili ya makubaliano kufidia mali kwa mali, nayo ni mauzo sahihi, bila ya kupatikana kasoro kwenye nguzo yeyote katika nguzo zake, lakini tumesema makubaliano yasiyofaa kwa kuwepo wasifu uliojitokeza, nao ni ziada isiyo na fidia ([14]). Inawezekana kusahihisha makubaliano haya kwa kuondoa kilichozidia.

Ama batili: Ni makubaliano yasiyofaa kwa asili yake na wasifu wake, na linakuwa hilo kwa kupitwa na nguzo katika nguzo za makubaliano, au kuwepo kizuizi cha kufikiwa makubaliano.

Mfano wa hilo: Kuuza vilivyomo matumboni mwa kina mama, na kuuza vilivyokwenye mgongo wa mnyama dume, na hilo ni mtu kusema: Nimekuuzia mtoto wa ngamia huyu, au ujauzito, mauzo haya yanafahamika kwa Waarabu.

Mfano wa mauzo haya ni batili, na hilo ni kwa sababu kilichofanyiwa makubaliano – nacho ni ujauzito – si cha kufanyiwa makadirio ya kukabidhiwa hivi sasa, ikawa ni sawa na kisichokuwepo, hivyo haifai kufanya makubaliano ([15]).

Na mfano wa uwepo wa kizuizi: Ni uuzaji wa mwendawazimu, ni makubaliano batili, kwa kukosekana uhalali wa muuzaji, mfano wa makubaliano haya ni batili kwa asili yake, wala hakuna njia ya kuyasahihisha ([16]).

Tafauti kati ya kutofaa na batili katika hukumu ya Kisharia:

Watu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wametafautisha kati ya uuzaji usiofaa na uuzaji batili kwa upande wa hukumu za Kisharia zinazohusiana na hilo, inawezekana kujumlisha hilo katika maelezo yafuatayo: Kinachofanyiwa makubaliano katika makubaliano yasiyofaa kinamilikiwa kwa kuwanacho tofauti na kinachofanyiwa makubaliano batili.

Kwa maana makubaliano yasiyofaa humiliki kwa kuwa nacho tofauti na makubaliano batili, bali ni haramu kwake mpaka utakapondolewa wasifu usiofaa, hapa kukatazwa kitu kwa wasifu wake huondolewa sifa ya kitu hiki, nayo ni kuwa kwake halali, lakini kubakia asili ya Kisharia kunawajibisha umiliki, hivyo kitu hiki cha kuuzwa kimekuwa haramu na makubaliano batili.

Makubaliano yasiyofaa yanaweza kusahihishwa kwa kuondoa wasifu usiofaa, ama makubaliano batili yenyewe hayana njia ya kuyasahihisha ([17]).

Katika hilo anasema Ibn Najiim: “Hukumu ya kwanza – kwa maana ya batili – ni huwa hamiliki kwa kuwa nacho, na hukumu ya pili – kwa maana ya kutofaa – yenyewe humiliki” ([18]).

Na Al-Asmandy amesema: “Kwa hakika tumeelezea mauzo yaliyokatazwa, kama vile mauzo ya riba na mengineyo kwa kutofaa, pamoja na kuwa kwake yenye faida kwa umiliki, kwa njia ya upanuzi kwa sababu ya ujirani uliopo wa jambo lisilofaa si kwa kitu kinachouzwa hakifai” ([19]).

Madhehebu ya Jamhuri ya watu wa Asili:

Jamhuri ya Wanachuoni wamesema kuwa hakuna tofauti kati ya makubaliano yasiyofaa na makubaliano batili katika ibada na mashirikiano – kwa kuondoa yaliyotajwa – maneno hayo mawili ni visawe vyenye maana moja, hivyo hakuna tafauti kati ya kauli yetu: Makubaliano haya hayafai, na kauli yetu: Makubaliano haya ni batili.

Al-Ghazaly amesema ndani ya kitabu cha Al-Mustaswfi: “Makubaliano yasiyofaa ni sawa na makubaliano batili, makubaliano ima yatakuwa sahihi ima yatakuwa batili, na kila batili ni kisichofaa” ([20]).

Ibn Qudama amesema katika kitabu cha Rawdha: “Makubaliano yasiyofaa ni sawa na makubaliano batili, maneno hayo mawili ni majina mawili kwa maana moja” ([21]).

Yaliyomuhimu kataja hapa ni kuwa, watu wa madhehebu ya Abu Hanifa wamekubaliana pamoja na Jamhuri ya Wanachuoni kuwa makusudio ya Kisharia katika ibada ni kuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, wakati wowote katika ibada hii inapotokea kasoro ni sawa sawa kasoro hiyo ikiwa katika asili au sifa basi ibada inabatilika, kwa kukosekana makusudio yake ya Kisharia, hivyo hawakutafautisha kati ya kukosekana asili na kukusekana sifa, kwa sababu hupelekea sehemu moja tafauti na mlango wa mashirikiano, kwani hutokea kushinda upande wa masilahi dhidi ya kuabudu, kwani makusudio ya kwanza ni masilahi ya waja ya kidunia, wakati wowote inapowezekana kufikiwa hayo masilahi tunahukumu kufaa kwa makubaliano, kutokana na hilo ikiwa kutatokea kasoro kwenye sifa ya makubaliano, basi wanahukumu kwa asili ni sahihi na kutofaa kwa sifa, wala hawabatilishi mkataba wote bali wakati ambapo sifa isiyofaa inapokosekana basi usahihi wa mkataba au makubaliano yanawezekana ([22]).

Hukumu ya mkataba usiofaa katika nchi ya Uislamu:

Hukumu ya kuingia katika mkataba au makubaliano yasiyofaa kwa ujumla Wanachuoni hawajatafautiana, mpaka kwenye madhehebu ya Abu Hanifa ambapo wamethibitisha kwa kusema: “Kwa hakika makusudio ni usalama wa dini ambao umewekewa sharia ya makubaliano, kuondoa kushindwa na kufikia kwenye mahitaji ya kidunia, yote hayo mawili kwa makubaliano sahihi, ama makubaliano yasiyofaa yanakwenda kinyume na dini, kisha yenyewe hata kama umiliki utanufaisha lakini haunufaishi kwa utimilifu, ambapo haki ya muuzaji kwenye bidhaa haijakatika, wala haki ya mnunuzi katika thamani, ambapo kila mmoja kati ya wawili hao ana haki ya kuvunja makubaliano bali ni lazima kwake” ([23]).

Hivyo baadhi ya watu wa madhehebu ya Imamu Hambali wamesema: “Ni haramu kufanya makubaliano yasiyofaa ya kuuza au yasiyokuwa kuuza” ([24]).

Na baadhi ya watu wa madhehebu ya Imamu Shaafi wamesema: “Makubaliano yasiyofaa kuyafanya ni haramu” ([25]).

Zarkashy amesema: “Ibn Rafaa amesema: Makubaliano yaliyokatazwa kuyapitisha ni haramu” ([26]).

Maana ya haramu hii kwa Jamhuri ya Wanachuoni ni kuwa makubaliano yasiyofaa ambayo Sharia imeyakataza ni haramu kufanywa wala umiliki hauhami ikiwa wataridhiana walioingia makubaliano, kauli yao: Hilo ni haramu wanamaanisha kuwa: Mwenye kufanya hilo anapata dhambi, kwa sababu amefanya kitu kisichofaa kwake kukifanya, kwa uwepo wa dhambi pia umiliki haukamiliki, ili mtu asiyefahamu asidhani kuwa mwenye kufanya hilo si yameharibika makubaliano yake tu bali inasemwa anapata dhambi na makubaliano kutofaa, wala hawezi kumiliki, hivyo ni lazima kurudisha bidhaa kwa muuzaji, na aina za makubaliano yasiyokubalika ni nyingi, ndani yake yanaingia kila mauzo yaliyokatazwa ni sawa sawa yakiwa ni katika mauzo yenye riba au yasiyo na riba kama vile chakula ambacho kinauzwa kabla ya kumilikiwa ([27]), na ikiwa atakusanya kati ya mkopo na kuuza, au kuuza kitu asichokuwa nacho.

Ama maana ya hilo kwa Abu Hanifa ni kuwa: Makubaliano yasiyofaa ambayo Sharia imeyakataza ni haramu kufanyika hata kama wenye kukubaliana wataridhia, pindi akiwa nayo au akiwa nacho inakuwa ni umiliki usiofaa lazima uvunjwe na anapata dhambi katika kumiliki kwake, hapa tunakuta kuwa kuna makubaliano kati ya Jamhuri ya Wanachuoni na madhehebu ya Abu Hanifa nayo ni kuharamishwa kufanyika na ubaya wake pamoja na wajibu wa kuvunjwa hayo makubaliano na bidhaa kurudishwa ([28]).

Pamoja na kuwa hii ni hukumu ya kuingia kwenye makubaliano yenyewe inaweza kufaa wakati mwingine, na hilo ni wakati wa dharura, kwani dharura uhalalisha kilichokatazwa.

UCHAMBUZI WA TATU

Hukumu ya makubaliano yasiyohalali katika nchi si ya Waislamu:

Jambo muhimu la kutajwa kwanza kabla ya kuelezea tafauti za Wanafiqhi katika hukumu ya makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi si ya Waislamu ni kuelezea kuwa matumizi ya Wanafiqhi Waislamu neno nchi ya kufuru, na matumizi ya neno nchi ya vita, ni matumizi ya wakati, ambapo nchi hizo zilikuwa zikiwafanyia uadui Waislamu, na kuzipiga vita nchi zao, au kuwaondoa Waislamu kwenye nchi yao kama ilivyotokea kwenye vita vya kimsalaba, na kama ilivyotokea huko Andulus miongoni mwa mauji ya kimbari ya Waislamu, na kuwalazimisha kuacha Uislamu pamoja na kuwaondoa nchini mwao ambapo waliishi humo kwa miaka mingi.

Baadhi ya nchi zimeitwa nchi za kufuru, kwa sababu walikuwa wanazuia kufanyika kazi za kulingania Uislamu, na Waislamu kuishi ndani ya hizo nchi, ama hali imebadilika, kwani tunaona ulimwengu haukatai Waislamu kuishi kwenye hizo nchi, wala haupingi kazi za kulingania Uislamu, kuelezea uhuru wa imani zao, kuendeleza mambo ya dini yao na wala hakuna vita vilivyotangazwa kati ya nchi fulani na nchi ya Waislamu.

Hivyo katika hali hii inapendeza kutumika neno nchi si ya Waislamu, ikiwa ni kusisitiza kuwa mgawanyo huu si mgawanyo wa Kisharia bali ni mgawanyo wa kinyakati, ni lazima kuchunga hilo wakati wa kusoma maandiko yaliyonukuliwa kutoka vitabu vya waliotangulia, na kutoleta hukumu zinazopelekea mvutano au kupelekea ulinganiaji wa Kiislamu au dini ya Waislamu kuwa ni dini ya mvutano, kwa sababu hawajakimbilia kwenye hilo isipokuwa kwa sababu wengine wameshambulia Waislamu na kuwafanyia uadui.

Miongoni mwa yanayopaswa kuangaliwa pia katika hili ni kuwa, kusudio la Wanafiqhi hapa la kuita nchi ya vita na nchi ya kufuru, ni sawa sawa vita vilipiganwa au hapana, kwa dalili kuwa, dalili nyingi ambazo wametumia watu wa madhehebu ya Abu Hanifa zilikuwa ni nchi ya kufuru na wala si nchi ya vita, nao ni mji wa Makka kabla ya kuhama kwa Mtume S.A.W na kabla ya kukombolewa, ambapo wakazi wake wengi walikuwa ni makafiri, wala hapakuwa na hukumu ya Uislamu, kisha sura ya dalili ilikuwa kuingia katika hukumu zote.

Madhehebu ya Wanachuoni katika masuala haya:

Wanafiqhi wametafautiana katika makundi mawili juu ya hukumu ya makubaliano yasiyofaa kwa nchi si ya Waislamu:

Kundi la Kwanza: Wanasema kutofaa makubaliano haya, kisha haizingatiwi athari ya kuwanacho na kumiliki, miongoni mwa waliosema kauli hii: Watu wa madhehebu ya Imamu Maliki, Imamu Shaafi na Imamu Hambali katika usahihi wa madhehebu yao, na Is’haq, pamoja na Al-Auzaai na Abu Yusufu kutoka madhehebu ya Abu Hanifa ([29]), vile vile Ibn Hazmi katika madhehebu ya Dhahiriya ([30]).

Kundi la Pili: Linasema kufaa kwa makubaliano haya na athari zitokanazo, msemaji kwenye hilo: Ibrahimu An-Nakhai, Sufyani At-Thawry, Abu Hanifa, Muhammad Ibn Al-Hassan As-Shaibani ([31]), Ahmad Ibn Hambal katika upokezi wake, na kupewa nguvu na Ibn Taimia ([32]).

Kauli hii ndiyo inayozingatiwa kwa watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa na iliyotolewa Fatwa, ambapo wamesema katika Fatwa kuwa ndio sahihi, kama ilivyokuja katika kitabu cha As-Sarajiyah, na vitabu vingine kwa Fatwa ya kauli ya Abi Hanifa, kisha kauli ya Abi Yusufu, kisha kauli ya Muhammad, kisha kauli ya Zafar na Al-Muhasinu Ibn Ziyad, na ikasemwa: Ikiwa Abu Hanifa kwa upande mmoja, na rafiki yake upande mwingine, kwa Umufti wa hiyari, wa kwanza ndio sahihi zaidi kama hatokuwa Mufti wa Jitihada, kinachoelezwa ni kuwa ikiwa watakutana Muhammad na Imamu Abi Hanifa basi hakuna Fatwa kwa kauli isiyokuwa yao, lau Mufti atakuwa ni mwanajitihada katika Madhehebu, kwa maana ni mtu wa mtazamo katika dalili.

Kuongezea, vitabu vyote vya watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa vinaeleza kauli hii na kuleta masuala na aina mbali mbali ambayo wanajengea, kama vile katika milango ya riba, matumizi, kamari, kuuza nguruwe na pombe – mambo ya mudharaba, muzaaraa na kuacha huru mtuwa, kama tutakavyoeleza baada ya dalili za watu wa Abu Hanifa.

 Mvutano kati ya makundi mawili:

Kwa asili kumekuwa na mvutano kati ya makundi mawili kuhusu tafauti ya nchi mbili na athari zake katika hukumu za Kisharia, na Fatwa je hubadilika kwa kubadilika sehemu?

Jamhuri inaona kuwa, kila kilichokuwa haramu kwa Muislamu ndani ya nchi ya Uislamu ni haramu kwake ndani ya nchi isiyo ya Kiislamu, mazingatio kwa upande wao ni makubaliano, wala hakuna athari ya nchi katika hilo, kisha haitofautiani sifa ya sehemu kwa kutofautiana watu.

Wakati huo huo watu wa Abu Hanifa wanaona kuwa mazingatio ni nchi na wala si makubaliano, kwa dalili kuwa yanayofanywa kwa Muislamu hufanywa kwa mwingine ndani ya nchi ya Uislamu miongoni mwa uharamu wa makubaliano yasiyofaa ([33]).

Hivyo Zailai anasema: “Chenye kuathiri - kwa maana katika hukumu – ni kutofautiana hukumu kati ya nchi mbili ili ukweli usibadilike kwa kitu kingine ([34]).

Kusudio la tafauti ya hukumu ni tafauti kati ya watu wawili katika ufuasi, kwa maana utaifa, na wala si ukazi, kwa mmoja wao kuwa ni mfuasi wa nchi fulani, na mwingine mfuasi wa nchi nyingine tofauti na ya kwanza kwa tafauti ya hukumu, na wote wawili wanaishi ndani ya nchi moja na tofauti ya kweli ni tofauti kati ya watu wiwli katika ukazi tu bila ya utaifa.

Na kwa vile kiwango cha makubaliano yasiyofaa kinakuwa kwa mali ya mtu wa kivita katika utafiti wetu, watu wa madhehebu ya Abu Hanifa wanaona kuwa kuzuiliwa mali yake kunathibiti kwa kufanikiwa, na kufanikiwa ni kwa nchi si kwa dini, kwa sababu dini ni kizuizi kwa mwenye kuamini ukweli wa Sharia tofauti na asiye amini, na nguvu ya nchi huzuia mali yake kwa mwenye kuamini uharamu wake na kwa asiye amini ([35]).

Hivyo ikiwa Muislamu ana makubaliano yasiyofaa na mtu wa nchi ya vita ndani ya nchi ya vita kisha mtu wa nchi ya vita akasilimu na akatoka kwenda nchi ya Uislamu kabla ya kukabidhiana, basi mgonvi wake katika hilo akielekea kwa hakimu atabatilisha, na wakiwa wamekabidhiana ndani ya nchi ya vita kisha wakagombana, hakimu hatoliangalia kabisa ([36]).

Tofauti kati ya mashirikiano ndani ya nchi ya Uislamu na nchi ya vita kwa upande wa Muislamu na mtu wa nchi ya vita ni umiliki, kwa maana ushirikiano usiofaa unapokosa maana ya umiliki wenyewe kwa upande wa ushirikiano ni sawa sawa kwa Muislamu ndani ya nchi ya vita na nchi ya Uislamu, ama kwa upande wa kuwa kwake sababu ya kupata umiliki wa mali ya mtu wa nchi ya vita kwa ridhaa yake, basi inafaa ndani ya nchi ya vita na haifai ndani ya nchi ya Uislamu, kwa kuwa nchi ya kwanza ni sehemu ya umiliki bila ya nchi nyingine ([37]).

Dalili za wasemao kubatilika makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi si ya Waislamu:

Hapa inapaswa kuelezea kuwa asili katika utafiti huu ni hukumu ya mkataba au makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi si ya Waislamu, lakini kama yalivyo makubaliano yote yasiyofaa – kama Sarkhassy alivyosema – katika maana ya riba, dalili kubwa ya pande mbili imekuwa kwenye masuala ya riba kati ya Muislamu na mtu wa nchi ya vita ndani ya nchi ya vita ([38]).

Wanaosema kuzuiliwa hayo makubaliano na uharamu wake, wameleta dalili za Kimaandishi na zile za kiakili.

Ama dalili za Kimaandishi nazo ni:

Dalili ya Kwanza: Maana jumla ya Aya inaonesha uharamu wa riba bila ya kutofautisha, miongoni mwa hizo Aya ni:

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Wale walao riba hawasimami ila kama anavyo simama aliyezogwa na Shetani kwa kumgusa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba. Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu} ([39]).

Kauli ya Mola Mtukufu:

{Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo baki, ikiwa nyinyi ni Waumini * Basi ikiwa hamtofanya basi jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe} ([40]).

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa} ([41]).

Sehemu ya dalili ni kuwa: Ahadi ya adhabu na amri ya kuacha riba na kukataza kuila ndani ya Aya zilizotajwa inaonesha moja kwa moja maana jumla, wala haijahusisha sharti ya sehemu bila ya sehemu nyingine au wakati bila ya wakati mwingine, wala haihusishwi maana jumla ya Aya isipokuwa kwa dalili, na kutokana na hayo anasema mwenye kitabu cha Al-Bahru Al-Zukhar: “Riba si halali ndani ya nchi ya vita, ikiwa hakuna dalili” ([42]).

Dalili ya Pili: Hadithi zinazonesha uharamu wa riba, katika hizo Hadithi ni Hadithi ifuatayo:

Kutoka kwa Jabiri amesema:

“Mtume S.A.W amemlani mwenye kula riba na mwenye kusaidia riba mwenye kuandika riba na mashahidi wa riba. Na akasema: Wote hao ni sawa” ([43]).

Kutoka kwa Abi Said Al-Khudry kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:

“Msiuze dhahabu kwa dhahabu, wala sarafu ya karatasi kwa karatasi, isipokuwa uzito kwa uzito, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, basi mwenye kuzidisha atakuwa amefanya riba” ([44]).

Kutoka kwa Othman Ibn Affan R.A Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema:                                                 

“Msiuze dinar moja kwa dinar mbili, wala dirham moja kwa dirham mbili” ([45]).

Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa mtu mmoja katika washirikina aliuwawa siku ya vita vya Ahzaabu, wakaenda kwa Mtume S.A.W: Tupatie mwili wake na tutakupa dinar elfu kumi na mbili. Mtume S.A.W akasema: “Hakuna kheiri katika mwili wake wala thamani yake” ([46]).

Imepokewa kutoka kwa Omar Ibn Khattab R.A amesema:

“Hakika miongoni mwa Aya ya mwisho ya riba kuteremka, na Mtume S.A.W amefariki na wala hajaifafanua, basi acheni riba na sababu za riba” ([47]).  

Sura ya dalili: Ni kuwa adhabu kali na amri ya kuacha riba na kuwa nayo mbali imekuja moja kwa moja pasi ya kufungamanishwa sehemu pasi na sehemu nyengine, na dalili wala haijakuja na sharti, yenyewe imeonesha uharamu ni sawa sawa ndani ya nchi ya Uislamu au nchi ya vita ([48]).

Ama dalili za kiakili nazo ni:

Ni kuwa kila kilichoharamishwa kwa Waislamu nacho ni haramu kwa wengine, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake} ([49]). Na kauli yake Mola Mtukufu: {Na wahukumu kati yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu} ([50]). Nayo imejengwa juu ya asili kuwa makafiri wanaambiwa kwa sehemu ya Sharia.

Kila kilichokuwa haramu ndani ya nchi ya Uislamu, kimekuwa haramu ndani ya nchi ya vita, kama vile machafu mengine na maasi ([51]).

Ulinganishi kwa mtu aliyehakikishiwa amani ndani ya nchi ya Uislamu, mtu wa vita pindi anapoingia kwenye nchi ya Uislamu kwa amani na akauza dirhamu mbili kwa dirhamu moja hiyo haifai, vile vile Muislamu anapoingia nchi ya vita na akafanya kama hivyo pia kwake haifai ([52]).

Nchi ya vita ni kama nchi ya uovu kwa sababu Imamu hana nafasi kwenye nchi hizo, mtu muadilifu na muovu ni kama Muislamu na mtu wa vita, kwa sababu wote wawili hakuna anayeaminika na mali ya mwenzake, na wala hakuna hata mmoja aliyesema kuwa mali ya Muislamu inafaa kufanya kazi kwa riba kwa mtu muovu ([53]).

Dalili za wanaosema inafaa:

Wanaosema inafaa wametumia dalili za nukuu na kiakili.

Ama dalili ya nukuu Ni:

Haditi iliyopokewa na Makuhul kutoka kwa Mtume S.A.W amesema:

“Hakuna riba kati ya Muislamu na mtu wa kivita ndani ya nchi ya vita”. Na Abu Yusufu amesema: “Kwa hakika Abu Hanifa amesema haya kwa sababu baadhi ya Masheikh wametuambia kutoka kwa Makuhul kutoka kwa Mtume S.A.W amesema: “Hakuna riba kati ya watu wa vita” nadhani pia amesema: “Na Wislamu” ([54]).

Wanaosema haifai wameelezea pingamizi nyingi juu ya dalili hii, miongoni mwazo:

Kwanza: Usahihi wa upokezi wa Makuhul ni Hadithi ya ajabu na iliyokosa mpokezi mmoja katika Maswahaba, kutokana na hilo Imamu Shaafi R.A anasema: “Alichopinga Abu Yusufu kwa Abi Hanifa R.A sio kilichothibiti, hivyo hakuna hoja ndani yake” ([55]).

Watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa wamejibu pingamizi hili:

Sarkhasy amesema: “Makuhul ni Mwanachuoni anayeaminika, na Hadithi iliyopoteza mpokezi mmoja wa mfano wake inakubalika” ([56]).

Wengine wakasema: “Hadithi iliyopoteza mpokezi mmoja kwetu sisi ni hoja, na kutofahamika baadhi ya Masheikh si jambo lenye madhara, kwa sababu kutofahamika huko kwa upande wetu na wala si kwa upande wa Mwanajitihada” ([57]).

Pili: Hadithi ya Makuhul kama inakubalika inapingana na andiko hivyo haifai kuacha kilichopokewa na Qur`ani kuwa ni haramu, na Wanachuoni wamekubaliana juu ya uharamu wake kwa Hadithi isiyofahamika haijapokewa katika usahihi wala kwenye kitabu kinachoaminiwa, hivyo haifai kufunganishwa na maandiko ya moja kwa moja, mfano kauli ya Mola Mtukufu:  {Msile riba} ambapo haiongezwi Hadithi hata moja kwenye Kitabu, kuongezea na kuwa kwake Hadithi inayowezekana kukosekana mpokezi mmoja ([58]).

Hilo linajibiwa: Ni kuwa haina maana Hadithi ya Makuhul imepoteza mpokezi mmoja kuwa riba inafaa ndani ya nchi ya vita, bali maana yake ni kuwa: Haifikiwi riba kati ya Muislamu na mtu wa kivita, hakuna kinachopingana kati yake na jumla ya Hadithi zenye wapokezi wengi katika mambo ya riba, kisha si kwa Abi Hanifa na alionao kuhusisha Hadithi zenye wapokezi wengi na ile iliyopoteza mpokezi wake mmoja.

Tatu: Inachukuliwa kuwa kusudio la kauli yake: “Hakuna riba” ni katazo la riba na wala si kukanusha kama kauli ya Mola Mtukufu:

{Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija} ([59]).

Makusudio yake yanakuwa ni kuharamisha riba kati ya Muislamu na mtu wa vita kama ilivyoharamu kati ya Waislamu, na Imamu An-Nawawi anasema: “Lau ingekuwa sahihi tungesema maana yake: Si halali riba ndani ya nchi ya vita kwa dalili zote” ([60]).

Pingamizi hizi zinajibiwa: Kuwa katazo la riba kwao halifunganishwi na nchi ya vita, hivyo haifai kuhusishwa na katazo, na kinyume na hivyo basi ingelazimishwa riba kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya Uislamu, nayo ni hoja kwao.

Na inajibiwa kuwa: Sisi hatukusimama juu ya kauli ya wanaokubali kuhusisha maana ya katazo, na mwenye kudai hilo basi anapaswa kuleta ufafanuzi.

Pia asili mfano wa maneno kama haya ni kuelezea ukanushaji, katazo halihusishwi isipokuwa kwa dalili inayopinga, lakini kwa kuchukuliwa uwezekano tu bila ya dalili haidhuru katika kuleta dalili, kumekuwa na dalili ya uharamu wa kusema maneno machafu vitendo vichafu na majadiliano katika Hija na sehemu zingine, hivyo inafaa kuhusishwa na katazo katika Aya, wala hakuna aliyesema mfano wake juu ya uharamu wa riba ndani ya nchi ya vita, na utajo wa jumla haujapingana kwa asili na sehemu.

Ikiwa itasemwa, maana yake: Ni kuwa riba inapofikiwa ni haramu sehemu yeyote, ama kuwa imefikiwa sehemu zote hakuna dalili ya utajo wa jumla kwenye hilo ([61]).

Yaliyopokewa kutoka kwa Ibrahim An-Nakhai amesema: “Hakuna ubaya dinar moja kwa dinar mbili ndani ya nchi ya vita kati ya Waislamu na watu wa vita” mfano wake yamepokewa kwa Sufyan Thawry ([62]).

Anajibiwa kuwa: Ni kauli ya Taabii haipewi nguvu juu ya kupinga ujumla wa Aya na Hadithi.

Linajibiwa kuwa: Kauli ya Taabii katika yanayofahamika kwa rai ni imeondolewa kihukumu, hivyo ni shahidi mzuri wa Hadithi iliyopita ya Makuhuli, na kushikamana kila mmoja na mwenzake, bali ndani yake kuna jibu kwa mwenye kuizingatia Hadithi ya Makuhuli kwa maana ya katazo, kwani kauli ya Ibrahimu haichukuliwi kabisa, na Hadithi hujifasiri zenyewe kwa zenyewe.

Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Jabir Ibn Abdillah R.A kutoka kwa Mtume S.A.W amesema katika Hotuba ya siku ya kuaga akiwa katika viwanja vya Arafa: 

“Riba ya zama za ujinga ni batili, riba ya kwanza iliyowekwa kwenye riba zetu ni riba ya Abbas Ibn AbdulMutwalib yenyewe yote ni batili” ([63]). Kutoka kwa Sulaiman Ibn Amru kutoka kwa baba yake amesema, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W katika Hija ya kuaga anasema:

“Fahamu kuwa riba zote katika riba za zama za ujinga ni batili, kwenu mna mitaji ya mali zenu hivyo msidhulumu wala kudhulumiwa…..”([64]).

Sehemu ya dalili: Ni kuwa Abbas R.A baada ya kusilimu alirudi Makka – wakati huo mji wa Makka ulikuwa ni mji wa kivita – na alikuwa akifanya biashara za riba kabla ya kuteremka amri ya kuharamisha na baada ya kuteremka kwake mpaka katika zama za ukombozi wa Makka, hii inaonesha kuwa hukumu ya riba haifanyi kazi kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita ([65]).

Wakapinga dalili hii wale wanaosema imezuiliwa:

Kwanza: Inatosha kuchukuwa tamko la Hadithi kuwa Abbas R.A alikuwa mtu wa riba katika zama za ujinga kabla ya Uislamu, kwa sababu hakuna dalili ya wazi kuwa baada ya kusilimu kwake aliendelea na biashara za riba.

Pili: Ikiwa itakubalika aliendelea na biashara za raba, basi anaweza kuwa si mwenye kujua uharamu wake, hivyo Mtume S.A.W akataka kuanzisha kanuni hii na kuipitisha tokea hiyo siku ([66]).

Al-Juswasw alijibu hilo kupitia Hotuba ya Mtume S.A.W iliyotajwa akisema: “Ndani yake kuna dalili kuwa makubaliano yaliyofanywa ndani ya nchi ya vita, kwa mtazamo wa Imamu hayapingi kwa kuvunjwa hata kama yamefanyika kwenye uharibifu, kwa sababu inafahamika kuwa kati ya kuteremka Aya na kati ya Hotuba ya Mtume S.A.W Makka na kubatilisha kwake riba ambayo haikuwa makubaliano katika makubaliano ya riba Makka kabla ya ukombozi, wala hakuishilizia kwa kuivunja, na wala hakutenganisha riba iliyokuwepo kabla ya kuteremka Aya na iliyokuwepo baada ya kuteremka kwake ([67]). Na kama riba kati ya Waislamu na washirikina isingekuwa halali ndani ya nchi ya vita basi riba ya Abbas ingekuwa batili siku aliyosilimu na atakachopata kwa hiyo riba baada ya hapo ni chenye kukataliwa, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe} ([68]).

Atwahawi amesema: Dalili hii ni sahihi, kwa sababu Abbas alisilimu kabla ya ukombozi wa mji wa Makka kwa muda mrefu, lau riba ingekuwa haramu kwake alipokuwa Makka basi angetakiwa kurudisha kwa aliyofanya nao biashara za kiriba. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:ْ {Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu}, na Aya hii inaungwa mkono na Hadhiti iliyopokewa kutoka kwa Mtume S.A.W anasema:

“Kila mgao uliofanyika katika zama za ujinga basi huo ni mgao sahihi ndani ya wakati wa ujinga, na kila mgao ndani ya Uislamu huo ni mgao sahihi ndani ya zama za Uislamu” ([69]).

Kwa sababu ndani yake kuna wajibu kuwa mgao wa mirathi ndani ya zama za Makka lau utatokea utafanya kazi kwa hukumu ya zama za ujinga, hata kama utakwenda kinyume na mgao wa Uislamu, vile vile hukumu ya riba ambayo ilikuwa kati ya washirikina na Waislamu ni yenye kufaa kwao lakini haifai kwa Waislamu.

Miongoni mwa yanayoonesha kuwa hukumu ya riba haijavuka kwenda nchi ya vita lau itavuka ingewajibika kuwa batili katika hali zote zilizokuwa kabla ya kuharamishwa au baada ya kuharamishwa, kama inavyokuwa batili ndani ya nchi ya Uislamu kabla ya kuharamishwa au baada ya kuharahamishwa, kwa sababu ikiwa asili yake kabla ya kuharamishwa hubatilika kwa uharamu wake, na ikiwa baada ya kuharamishwa hubatilika, pindi Mtume S.A.W alipoelezea kuwa ameibatilisha siku ya ukombozi imeonesha kuwa haikuwa batili kabla ya hapo, na uharamu haukukutana na wakati wa ukombozi wala haukuvuka huo wakati ([70]).

Kwa hakika Ibn Rushdi miongoni mwa Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Malik alikubali dalili hii katika tangulizi zake. Mtume S.A.W alisema katika hotuba yake:

“Fahamu kuwa riba zote ndani ya zama za ujinga ni batili, na riba ya kwanza kubatilishwa ni riba ya Abbas Ibn Abdulmutwalib”, katika maelezo haya yanaonesha kufaa kufanya riba na watu wa vita ndani ya nchi ya vita kwa mtazamo uliofikiwa na Imamu Abu Hanifa, kwa sababu mji wa Makka ulikuwa ni mji wa vita, na Abbas Ibn Abdulmutwalib alikuwa Muislamu, ima ni kabla ya vita vya Badri kwa mujibu wa kauli ya Ibn Ishaq, au kabla ya ufunguzi wa Khaibar kama ilivyoonesha kwenye Hadithi ya Al-Hajjaaj Ibn Alaatw kutokana na Mtume S.A.W  kukiri kwa ujumbe na kukubali aliyoyahidi Mwenyezi Mungu, riba siku ya ufunguzi wa Khaibar ilikuwa haramu, na kwa vile haikupokewa kwa Mtume S.A.W yaliyokuwa riba baada ya Uislamu mpaka ilipokwisha zama za ujinga kwa ufunguzi wa mji wa Makka, isipokuwa yaliwekwa kwake yale yaliyokuwepo hayajazuiliwa, hivyo imeonesha kufaa kwake ([71]).

Baadhi ya wafuasi wa Imamu Abu Hanifa wameona kuwa Hadithi ya Abbas imepokewa mara mbili, mara ya kwanza katika ufunguzi wa Makka mwaka wa nane wa Hijiria, na mara nyengine imepokewa katika Hija ya kuaga, na hali ya riba katika utajo wa kwanza ilikuwa ni maalum kwa watu wa Makka, na katika mara ya pili ilikuwa ni maalum kwa watu wa Thaqiifi ambao Abbas alikuwa anafanya nao biashara kwa riba baada ya ufunguzi wa Makka kwa kuwazingatia ni watu wa Twaifu nayo Twaifu ni mji wa kikafiri wakati huo.

Mwenye kitabu cha iilaau Al-Sunan anasema:

Kauli ya Mtume S.A.W siku ya ufunguzi: “Riba ya kwanza kubatilisha ni riba ya Abbas Ibn Abdulmutwalib” kwa hakika amekusudia watu wa Makka hawakuwa na riba kwa kuwa kwao ndani ya mji wa Kiislamu kwa kukombolewa na wala haijakusudiwa riba iliyokuwepo kwa watu wa Twaaif waliokuwa Thaqiif na mfano wao miongoni mwa washirikina wasiokuwa wa Makka, hilo likawa limebakia mpaka waliposilimu Thaqiif, na Aya ikateremka:

{Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na achene riba zilizo bakia} kwa sababu hiyo – Mwenyezi Mungu Anajua zaidi – Mtume S.A.W alibatilisha riba ya zama za ujinga na riba ya pili ya Abbasi katika hotuba yake ya Hija siku ya Arafa, na akakusudia kubatilisha riba iliyokuwepo kwa watu wa Twaifu na wengine ambao waliingia katika Uislamu na kukombolewa miji yao baada ya ukombozi wa mji wa Makka ([72]).

4- Wayahudi wa Bani Nadhiir Mtume S.A.W pindi alipowahamisha wakasema: Kwa watu tuna madeni bado hayajalipwa, Mtume S.A.W akasema: “Lifanyeni la muda na harakisheni kulipa” ([73]).

Upande wa dalili: Mfano wa miamala kama hii haifai kati ya Waislamu, kwani mwenye deni la muda kwa mwingine kisha akamuondolea sehemu ya deni kwa sharti la kulipa haraka deni lilobaki haifai, amelichukia hilo Omar na Zaidi Ibn Thabit pamoja na Ibn Omar R.A, kisha Mtume S.A.W akapitisha hilo kwao, kwa sababu walikuwa watu wa mji wa vita ndani ya wakati huo na mji wao ni mji wa vita, ambapo Mtume S.A.W aliwazingira kwenye ngome yao, na kwa sababu hii aliwahamisha, kutokana na hayo tumefahamu kuwa inafaa kati ya mtu wa vita na Muislamu yale yasiyofaa kati ya Waislamu ([74]).

5- Yaliyopokewa kuwa Aba Bakri kabla ya kuhama pale Mwenyezi Mungu Alipoteremsha kauli yake: {Alif Lam Mim (A.L.M.) Warumi wameshindwa} washirikina wa Kikuraisha walimuuliza: Hivi mnaona kuwa Warumi watashindwa kwa Wafursi? Akasema: Ndio. Wakasema: Je unaweza kati yetu kuweka na wewe rehani, ikiwa Warumi watashinda utachukuwa rehani yetu, na ikiwa Wafursi watashindwa tutachukuwa rehani yako, ndipo Abu Bakri R.A akaweka rehani kwenye hilo, kisha akaenda kwa Mtume S.A.W na kumfahamisha ndio Mtume S.A.W akasema: “Waendee na ongeza rehani na achana na kuweka muda” Abu Bakri R.A akafanya na Warumi wakashindwa dhidi ya Wafursi ndipo wakaenda kwa Abi Bakri na kumtaka aje kuchukuwa rehani yake, akaenda na akachukuwa ([75]). Katika mapokezi mengine imeongezwa: “Abu Bakri alicheza kamari akaibeba na kuja nayo kwa Mtume S.A.W, na Mtume S.A.W akasema: “Hili ni chumo baya toa sadaka” ([76]).

Sura ya dalili: Kisa kinaonesha juu ya kufaa kucheza kamari na watu wa vita, ambapo kama hilo lisingekuwa linafaa basi Mtume S.A.W asingelikubali kati ya Abi Bakri Swiddiq na washirikina wa Makka, na Makka ulikuwa mji wa vita ([77]).

Wanaopinga dalili hii wameizungumzia kwenye pande mbili:

Upande wa Kwanza: Abubakri Swiddiq R.A pindi alipocheza nao kamari na kuchukuwa mali ndipo alipoenda nayo kwa Mtume S.A.W na Mtume akasema: “Itoe sadaka” ndipo akafanya hivyo, lau kama mali ile ingekuwa ni nzuri na halali kwake basi asingetakiwa kutoa sadaka.

Hoja hii inajibiwa kuwa: Kutakiwa kutoa sadaka hakuoneshi kuwa kinachotolewa sadaka si miliki yake, isipokuwa kinyume ndio sahihi zaidi, ambapo ikiwa hamiliki kwa njia hii basi asingetakiwa kuitoa sadaka ([78]).

Pili: Limetokea hili kabla ya kuteremka Aya iliyoharamisha kamari ([79]), kwa sababu Aya ya kamari imeteremka ndani ya Suratul-Baqarah na Suratul-Maidah nazo zote ni katika Sura za Madina.

Tumesema: Hatukubali uhalali wa riba na kamari ndani ya Uislamu wakati wowote ule, si wakati wa Makka wala Madina, kwa dalili kuwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu} ([80]) imeteremka baada ya vita vya Uhdi ndani ya mwaka wa pili Hijria, Ibn Atia amesema: “Katazo hili la kula riba wakati wa kisa cha Uhdi, wala sifahamu sababu iliyopokewa juu ya hilo” ([81]), nina maanisha kwenye hilo yaliyokuja kwenye kauli yake Mola Mtukufu ndani ya Suratul-Ruum – nayo ni Sura ya Makka:

{Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao ndio wataozidishiwa} ([82]).

Huenda ongezeko katika Hadithi iliyopita nayo kauli yake: “Hiyo ni kabla ya kuharamishwa kwa riba” ikiingizwa katika Hadithi za baadhi ya wapokezi ikidhaniwa kuwa riba na kamari si halali katika nchi ya vita, kama ilivyo si halali ndani ya nchi ya Kiislamu, hivyo ikachukuliwa mali aliyopata Abi Bakri kwa washirikina kuwa ilikuwa ni kabla ya kuharamishwa kwake.

Ikiwa tutakubaliana na madai yao basi tunasema:  Makubaliano kufanyika kabla ya kuharamishwa kwake hakupelekei kuhalalisha kuchukuwa baada ya kuharamishwa, kwa sababu Uislamu hurudisha kilicho haramu kikiwa bado hakijakabidhiwa, hayo yameelezwa kwenye sherehe ya kitabu cha As-Sair” ([83]), na katika kitabu cha “Al-Mabsuutw” kinasema kuwa Uislamu unazuia kukabidhi kama unavyozuia kuanza makubaliano, ikiwa kuchukuwa baada ya kuharamishwa haifai kabisa, kama ilivyoonesha kauli yake S.A.W: “Mali hii ni haramu” kwa maana ni haramu kwa sura si kwa uhakika wake, na kama si hivyo basi angekataza kuchukuwa tokea mwanzo ([84]).

6- Yaliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas R.A kuwa Yazid Ibn Rukana alicheza mieleka na Mtume S.A.W na Mtume S.A.W akacheza naye mara tatu, kila mara moja mshindi anachukuwa mbuzi mia moja, ilipofika mara ya tatu akasema: Ewe Muhammad hakuna mtu yeyote aliyewahi kuniangusha na kuuweka mgongo wangu kwenye ardhi kabla yako, na wala hakuna yeyote ninayemchukia zaidi yako, na mimi ninashuhudia kuwa hakuna Mola wa haki isipokuwa ni Mwenyezi Mungu na hakika yako wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi Mtume S.A.W akasimama na akamrudishia mbuzi wake ([85]).

Upande wa dalili ni kuwa: Lau hilo lingekuwa ni jambo lenye kuchukiza basi Mtume S.A.W asingelifanya.

Dalili hii inajibiwa kuwa: Lau hilo lingekuwa ni jambo zuri basi Mtume S.A.W asingerudisha ([86]).

Hoja inajibiwa kuwa: Mtume S.A.W kurudisha kwake hakumaanishi kuwa hilo ni katika matendo yanayochukiza isipokuwa kurudisha kwake ni katika kumpendezeshia kwake Uislamu, mara nyingi alikuwa anafanya hivyo S.A.W kwa washirikina ili kuwazowesha wapate kuamini ([87]).

Hilo linajibiwa kuwa: Tukio hilo limetokea Makka kabla ya kuhama kwa Mtume S.A.W na hilo ni kabla ya kuteremka Aya za kuharamisha hilo ([88]).

Linajibiwa hili kuwa: Mwenendo wa Hadithi unaonesha ni baada ya kuteremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu} ([89]) nayo ni Suratul-Maidah ambayo imekuja na Aya inayoharamisha mchezo wa kamari.

Dalili za Kiakili:

Watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa na wale wanaokubaliana nao wametumia dalili ya kiakili katika kauli zenye nguvu za Madhehebu yao katika kupitisha mikataba isiyofaa ndani ya nchi isiyo ya Waislamu, miongoni mwa dalili hizi ni:

Mali za watu wa nchi ya vita ni halali bila ya makubaliano, kwa makubaliano yasiyofaa sharti bora ni kutokuwepo hiyana, na iwe kuchukuwa kwa ridhaa ([90]).

Na kuzingatiwa kuwa hukumu juu ya mkataba usiofaa ni kuangalia asili, kwa kuwa ni katika miamala mibovu kati ya Waislamu, na wala haikuwa mibovu kwa kuwa kati ya Muislamu na asiye Muislamu, hapa cha kuzingatiwa katika kufaa kwa watu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa ni kuwa Muislamu amechukuwa kwa ridhaa ya asiye Muislamu na kwa hiyari yake hata kwa makubaliano yasiyofaa, kisha hapa makubaliano si kwa umiliki bali ni kwa kupata sharti la umiliki nalo ni ridhaa, na hapa umiliki kwa Muislamu ni kwa kuchukuwa na kushikilia si makubaliano, na kwa msingi huo wamesema katika masuala ya riba ndani ya nchi ya vita, kisha haifikiwi maana ya riba kwa sababu riba ni jina la kilichozidi na kunufaisha ([91]).

Umiliki haukuwa kwa sura hii kwa makubaliano, kwa sababu sharti la kumiliki kwa makubaliano kwa watu wa madhehebu ya Abu Hanifa – vile vile ni katika masharti ya kupitisha riba – ni kuwa vitu viwili mbadala ambavyo wanashirikiana kwa vitu hivyo pande mbili za makubaliano: Ni vyenye kuzuiliwa, na viwe vyenye thamani, na kuthaminishwa kwa watu wa Abu Hanifa kunathibiti kwenye nchi ya Uislamu, na kwa watu wa Imamu Shafi kunathibiti kwa Uislamu, na wala visiwe miliki ya yeyote wenye kuuziana ([92]).

Pindi sharti moja katika masharti haya likikosekana haitakuwa riba wala miliki kwa makubaliano.

Watu wa Abu Hanifa pia wametoa dalili kwa kulinganisha kufaa kwa asiyekuwa Muislamu kuuza watoto wake na Waislamu kuwanunua ndani ya nchi ya vita, na wakachukuwa dalili ya hilo kwa kitendo cha Amru Ibn Al-Aas R.A kutoka kwa Abdillah Ibn Hubaira As-Sabai amesema: “Amru Ibn Aas alisuluhisha watu wa Intablis - nao ni mji Barka uliopo kati ya Afrika na Misri – juu ya malipo ya kuuza watoto wao kwa malipo wayatakayo” ([93]).

Sura ya dalili ni kuwa: Kuuza mtoto ni katika makubaaliano au mikataba mibaya ni katika haramu kama isivyojificha, kupitisha mkataba mmoja kwenye nchi ya vita kunapelekea kupitisha mkataba mwingine kwenye nchi ya Kiislamu.

At-Tahanawi amesema akisherehesha Hadithi hii:

Dalili ya kufaa watu wa vita kuuza watoto wao, na Waislamu kuwanunua, mtoto hawezi kuwa mtumwa kwa baba yake, hii inakuwa ni sawa na kumuuza mtu huru na kumnunua, na mfano wake haifai kabisa ndani ya nchi ya Waislamu, hata kama asiye Muislamu anayeishi kwa amani na Waislamu akamuuza mtoto wake haijapitishwa na Mwanachuoni yeyote na wala hatufahamu uwepo wa tofauti, Amru Ibn Aasi amepitisha hilo ndani ya nchi isiyo ya Waislamu, imeonesha kuwa mashirikiano yasiyofaa kati ya Waislamu yanafaa ndani ya nchi si ya Waislamu kati ya Muislamu na asiye Muislamu, na Imamu Sarkhasy anasema kuwa nchi ya makubaliano haiwi nchi ya Waislamu ni nchi ya vita, kama ilivyo kabla ya makubaliano, mpaka ikafaa kwa Muislamu kuuziana na watu wake dirhamu moja kwa dirhamu mbili, vile vile kununua watoto wao, watu wa madhehebu ya Abu Hanifa wametofautiana kuhusu ikiwa asiye Muislamu atauza mtoto wake wa kiume au wakike kwa Muislamu anayeishi nao kwa amani, wengi wamesema kuwa: Kuuza huko ni batili, na Karkhy amesema: Ikiwa wao hawaoni kufaa kuuza basi inakuwa ni batili, na ikiwa wanaona kufaa kwake basi itafaa, na kusahihisha kauli hiyo katika kitabu cha “Al-Ghiyaathiya” imesemwa nayo ni kauli iliyopitishwa yenye nguvu kwetu sisi kwa kukubaliana kwake na Hadithi.

Ikiwa itasemwa hivyo basi kufaa mtu wa vita kuuza mtoto wake na kununuliwa kwake kama Amru Ibn Aasw alivyofanya ni dalili ya wazi kuwa hakuna riba kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita, kwa sababu kumuuza mtu huru na riba katika uharamu ni sawa sawa, hivyo kufaa kimoja wapo ndani ya nchi ya vita kunapelekea kufaa chengine, haisemwi: Wapi umejifunza kuwa wao kwa maana ya watu wa Barka na Antablas walikuwa wanauza wanawake wao na watoto wao nchini mwao? Kwani huenda walikuwa wanawauza ndani ya nchi ya Waislamu, kwa sababu tunasema: Mfano wa uuzaji kama huu hakuna yeyote aliyeupitisha katika nchi ya Waislamu, hivyo ni lazima kusema kuwa walikuwa wanawauza ndani ya nchi yao, vile vile malipo yalikuwa yanachukuliwa kutoka kwa watu wa dhimma na watu wa usuluhishi ndani ya nchi yao, kama inavyofahamika katika kitabu cha Sair Al-Khalafau ([94]).

Watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa pia wamechukuwa dalili ya kufaa kufanya makubaliano mabovu na yasiyofaa ndani ya nchi ya vita kwa kulinganisha kuwa hakuna riba kati ya mtumwa na bwana wake, na hilo ni katika yaliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas “Alikuwa anamuuzia matunda mtoto wake kabla ya kumlisha, na alikuwa haoni kati yake na mtoto wake kuna riba” ([95]).

Yanaungwa mkono na yaliyopokewa na Ibn Hazmu kwa upokezi wake kutoka kwa Atwaa amesema: Ibn Abbasi alikuwa anawauzia wanawe tende za miaka miwili na mitatu, ndipo alipokuja Jabiri Ibn Abdillah na kumuuliza: Hivi unafahamu Mtume S.A.W amekataza kufanya hivi? Ibn Abbas akasema: Hapana, lakini hakuna riba kati ya mtumwa na bwana wake ([96]).

Sehemu ya dalili ni kuwa: Watu wa vita wote ni watumwa kwa Muislamu na mali zao ni haki ya Muislamu, kama vile mtumwa na anavyomiliki ni mali ya bwana wake.

Mwenye kitabu cha Ilaau Sunan:

Ndani yake kuna dalili kuwa makubaliano ya riba yanapokosa usahihi wake basi hakuna chukizo katika sura yake wala hakuna dhambi, hivi umeona Jabir alipinga hilo kwa Ibn Abbas kwa kuwa ni sura ya riba, na Ibn Abbas akasema: Hapana, kwani kati ya mtumwa na bwana wake hakuna riba, kwa maana hakuna ubaya kwa sura ikiwa itakosekana ukweli wake, na kuna dalili ya kufaa sura ya riba kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita, kwa kukosekana kwake uhalisia wake kama ilivyoelezwa, kwa sababu watu wa vita wote ni watumwa kwa Muislamu, kwani kauli ya huyu Ibn Abbas ni ushahidi mzuri usiofichika.

Haisemwi kuwa: Mali ya mtumwa kwa bwana wake tofauti na mali ya mtu wa vita, kwani si miliki ya Muislamu, tunasema: Mali ya mtu wa vita halali kwa Muislamu kama vile kuni na hashish uhalisia hazikuwa miliki za mtu wa vita hivyo ikafananishwa na mali ya mtumwa, tumekubaliana juu hilo – kwa maana hakuna riba kati ya mtumwa na bwana wake – kuanzia Imamu Al-Hassan Al-Baswary, Jabir Ibn Zaid, An-Nakhai, As-Shaaby, Sufian At-Thawri, Othman Al-Bataa, Al-Hassan Ibn Huyayyi, Al-Laithu na As-Shaafi ([97]).

Kauli yenye Nguvu:

Ni wazi kupitia maelezo ya dalili za pande mbili hupewa nguvu kauli ya waliopitisha uwepo wa makubaliano na mikataba isiyofaa ndani ya nchi isiyo ya Waislamu, hasa kwa kuwa wenye kuzuia wametoa dalili za jumla zisizokata dalili za watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa na wale wanaokubaliana nao, ni sawa sawa katika dalili za nukuu au za kiakili, kama tutakavyoeleza hilo katika majibu juu ya dalili za wenye kuzuia makubaliano haya.

Kuongezea juu ya hayo tunaweza kuyapa nguvu yale tuliyoyaelezea kwa sura nyingi:

Sura ya Kwanza: Ni kuwa dalili za Abi Hanifa na anaokubaliana nao ni kauli katika masuala kwa kuzingatia ameweka sharti la nchi ya vita iliyoelezewa katika baadhi ya mapokezi, kuongezea juu ya dalili zake zenye nguvu zaidi kimapokezi na kimtazamo, na wala si dalili zilizojengwa kwa maelezo tu peke yake kama Wanachuoni wengi walivyodhani, bali katika hilo Imamu Abu Hanifa ana dalili nyingi zenye nguvu, ni dalili za wazi juu ya usahihi wa alichosema, na anao waliomtangulia kama Imamu Ibrahimu An-Nakhai katika kuhalalisha riba ndani ya nchi ya vita, na kutoka kwa Ibn Abbas R.A katika kuhalalisha riba kati ya mtumwa na bwana wake na kukubaliwa yote hayo na Sufian At-Thawry, lau yasingekuwa yamethibiti kwenye Hadithi na kauli za Maswahaba na Taabiin basi Sufian asingekubali kabisa mfano wa kauli kama hii.

Sura ya Pili: Abu Hanifa na wale waliokubaliana naye hawakusema uhalali wa riba kati ya Muislamu na mtu wa vita, bali wamesema kuwa haifikiwi kati yao kwa uhakika ndani ya nchi ya vita, bali kwa sura tu, kwa kuwa nchi ya vita na watu wake ni sehemu ya kutawaliwa ([98]).

Sura ya Tatu: Kupatikana baadhi ya Hadithi zinazopingana kwenye maeneo mbalimbali kwenye vitabu vya Sharia na vya Hadithi, wala haiwezekani kukusanya kati ya vitabu hivyo vya aina mbili isipokuwa kwa maelezo yaliyofikiwa na Imamu Abu Hanifa katika masuala haya, miongoni mwa hayo:

Yaliyopokewa katika sababu ya uhalali wa kuchukuwa malipo kwa kusoma Qur`ani, na hayo yanapatikana katika Hadithi ya Abi Said Al-Khudry ambayo inaelezea Muarabu mmoja alifanyiwa rukia kwa kutumia Suratul-Fatiha kwa malipo na Abu Saidi alichukuwa malipo hayo na Mtume S.A.W alikiri na kukubali akisema: “Hakika katika haki mliyochukuwa malipo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu” ([99]).

Ibn Jawzy amesema katika kubainisha kufaa kwa hilo:

“Watu wetu wamejibu kuhusu Hadithi hii kwa majibu matatu, miongoni mwayo: Ni kuwa watu walikuwa makafari, hivyo ikafaa kuchukuwa mali zao – kwa maana ya ridhaa ya nafsi zao hata kama makubaliano yatakuwa hayakubaliki” ([100]).

Na huu ni muelekeo wake kwenye kauli ya Abu Hanifa katika utafiti wetu huu.

Imepokewa kuwa Mtume S.A.W alimtaka mmoja wa Swahaba anunue ngamia mmoja kwa ngamia wawili kwa malipo ya baadaye ([101]). Na Mtume S.A.W kukataza kwake kuuza mnyama kwa mnyama ([102]).

Wanachuoni wamekusanya kati ya vitabu vya Sharia na Hadithi kuwa maelezo ya kuhalalisha yalikuwa kabla ya kuteremka Aya ya riba, au yalikuwa ndani ya nchi ya vita, ambapo hufanyika riba kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita ([103]).

Sura ya Nne: Kauli ya Abu Hanifa na anaokubaliana nao kwa asili inapewa nguvu kwa kuzingatiwa ni hitajio na kuna wepesi.

Miongoni mwa sura za makubaliano yasiyofaa ambayo yameelezewa uhalali wake na watu wa kauli hii ndani ya nchi isiyo ya Waislamu:

Kuuza mzoga, kuuza pombe, kuuza nguruwe, kucheza kamari na riba ([104]).

Makubaliano ya mtu wa vita kumuandikia mtumwa wake Muislamu mkataba wa pombe na nguruwe, imesemwa ndani ya kitabu cha Al-Bahru Raaiq: “Ikiwa mtu wa vita amemuandikia mtumwa wake Muislamu ndani ya nchi ya vita mkataba wa pombe au nguruwe na kutekelezwa hilo, basi lililowazi ni kuwa anamuacha huru, ikichukuliwa kauli yao kwetu kumiliki mali ya mtu wa vita kwa sura yeyote iliyokuwa inaridhiwa na yeye, wala haijifichi kuwa nguruwe hapa ni kama pombe katika hukumu” ([105]).

Vile vile kilimo kwa makubaliano yasiyokubalika, amesema ndani ya kitabu cha Fatawa Al-Hindia: “Ikiwa Muislamu amemuwekea sharti mtu wa vita ya vipimo kumi, ni sahihi kwa kauli ya Abi Hanifa na Muhammad R.A na kwa upande wa Abi Yusuf R.A ni haifai, kwa sababu kwa upande wao makubaliano yasiyokubalika yanafaa kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita” ([106]).

Pia na mudharaba (Makubaliano ya kibiashara) kwa sharti lisilofaa kati yao. As-Sarkhasy amesema: “Pindi Muislamu na Dhimmiy wanapoingia ndani ya nchi ya vita kwa amani na wakatoa mali ya biashara kumpa mtu wa vita kwa faida ya Dirham mia moja, au mtu wa vita akatoa basi inafaa katika kauli ya Abi Hanifa na Muhammad, na faida kati yao wawili kwa mujibu wa masharti waliyojiwekea hata kama hajapata faida isipokuwa Dirham mia moja yote inakuwa kwa mwenye kuwekewa sharti na msingi wa mali unarudi kwa mwenye mali.

Na katika kauli ya Abi Yusuf R.A mudharaba usiyofaa na mwenye kufanya mudharaba ana malipo ya mfano wake, hali zao wote wawili katika hili ni kama hali zao ndani ya nchi ya Kiislamu, nayo ni katika masuala ya riba yenyewe haifanyiki kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita kwa kauli ya Abi Hanifa na Muhammad R.A, tofauti na kauli ya Abi Yusufu R.A, na makubaliano yote yasiyofaa ni katika maana ya riba ([107]).

Jibu la dalili ya Wazuiaji:

Watu wa Madheheubu ya Abu Hanifa na wale wanaokubalika nao wamejibu dalili ya wazuiaji wa makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi si ya Waislamu, na sisi tunaeleza kwa kina tunasema:

Ama dalili zao za nukuu kutoka ndani ya Qur`ani na Sunna ni dalili za jumla hazisimami kwenye dalili za waliojuzisha.

Al-Kamal Ibn Al-Himam anasema:

Maneno ya jumla makusudio yake ni mali iliyozuiliwa ya mmiliki wake, na mali ya mtu wa vita si mali iliyozuiliwa, maelezo haya ni katika uhakiki unaopelekea kuwa lau isingepokewa Hadithi basi ingefaa kuangalia kilichotajwa, kwa maana: Mali yake kuwa halali ([108]).

Ama Hadithi ya Ibn Abbas R.A Mtume S.A.W kutouza mwili wa Nufal Ibn Abdillah Ibn Al-Mughirah pindi alipoulizwa na washirikina – swala hilo linajibiwa kuwa Hadithi haithibitishi kutofaa, kwa sababu inawezekana kujizuia kukawa kwa jambo lingine, kama vile kuwa kwake kinyume na murua au miongoni mwa zingine.

Ikiwa patasemwa: Imepokewa katika Hadithi walisema kumuambia Mtume S.A.W: Hakika sisi tutakufanyia jambo, Mtume S.A.W akasema: “Hilo ni jambo baya na baya zaidi”.

Tunaweza kujibu hilo kuwa, si dalili pia juu ya uharamu, kwa sababu inawezekana kubeba ubaya kwa uchafu wa asili kwa kuwa ni katika vitendo vichafu visivyo haramu.

Imamu Sarkhasy ameona maelezo mengine katika Hadithi yanayokubaliana na kauli za waliopitisha, ambapo amesema: “Maelezo ya Hadithi ya Ibn Abbas R.A kuwa Mtume S.A.W aliwakataza hilo pindi alipoona ndani yake kuna chuki kwa washirikina, na huenda walitudhania kuwa tutawashambulia kwa tamaa ya mali” ([109]).

Muhammad Ibn Al-Hassan As-Shaibany amejibu dalili ya Hadithi hii katika mlango huu, ambapo dalili hii si sehemu ya mvutano, kwani sura ya masuala ni kuwa Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita, Mtume S.A.W na Waislamu walikuwa katika kambi ya Uislamu, Muhammad Ibn Al-Hassan anasema: “Ikiwa itasemwa: Watu wa vita walikuwa ndani ya kambi yao, na wana hukumu katika ardhi ya vita, tumesema: Lakini Mtume S.A.W na Waislamu hawakuwa kambini kwao, bali walikuwa ndani ya mji wa Uislamu nyuma ya handaki, ikiwa Muislamu yupo katika zuio la Waislamu na akazungumza na mtu wa vita akiwa ndani ya ngome yake au kambi yake, na akawa mtu asiye na mahusiano mazuri na Waislamu, basi hilo halifai, kwa sababu kusimamia upande waliozuiliwa Waislamu ni kukiuka haya makubaliano, na makubaliano yanapoharibika upande mmoja basi inatosha kuharibika kwake” ([110]).

Ama Hadithi ya Umar Ibn Khattab R.A: “Aya ya mwisho ya Qur`ani kuteremka ni Aya ya riba, na Mtume S.A.W alifariki wala hakututafasiria basi acheni riba” hakika Aya ya mwisho ya Qur`ani kuteremka ilisisitiza kuacha riba, kwa sababu kusudio la kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na achene riba zilizo bakia} ([111]), na ambayo inayofuata: {Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu}[112], Aya ya mwisho ya kuteremka katika Aya zote za Qurani ilikuwa kati ya kuteremka kwake na kifo cha Mtume S.A.W kwa siku themanini na moja, au siku tisa, kutokana na tofauti ya wapokezi, kama Assuyutwi alivyosema ndani ya kitabu cha “Al-Itqaan” ([113]), na kusudio la kusisitiza: Ni kukutana kwa riba ya fedha na riba ya An-Nasiiah (ya zama za ujinga) katika uharamu, kwa sababu riba ya fedha ni ile ambayo Omar anatamani kuifafanua, na riba ya An-Nisiiah nayo ni riba ya zama za ujinga, halikuwa jambo la kufichika juu ya mfano wake, kwa kuwa kwake inafahamika kwa watu, hakuna yeyote asiyeifahamu kwa watu wa lugha ([114]).

Ama dalili za kiakili kwa wanazuia ni kama zifuatazo:

Dalili ya kuwa kila kilichokuwa haramu kwa Waislamu ni haramu kwa wengine kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu} ([115]), ni maalumu kwa nchi ya Kiislamu, kwa maana ikiwa watatujia na jambo lilotokea ndani ya nchi ya Waislamu tutahukumu kati yao kwa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu na tutarudisha walichoingia makubaliano yasiyokubalika, ama ikiwa watatujia na jambo limetokea ndani ya nchi ya vita tutawapuuza na kutoliangalia, kwa dalili ya kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Basi wakikujia, wahukumu baina yao au jipuuze nao} ([116]).

Ama kuasisi kwao dalili kunatokana na kanuni kuwa makafiri ni wenye kuambiwa na Sharia, tunasema: Hakika masuala ni yenye tofauti, na dalili ni zenye kuvutana ile yenye nguvu ni kuwepo kwa tofauti, na faida ya tofauti inaonekana kwa upande wa adhabu, kwani wanasema: Wanaadhibiwa kwa sababu ya kuacha kuamini na matawi yote ya imani, na wenye kukanusha wamesema: Wanaadhibiwa kwa kuacha kuamini tu ([117]). 

Na kwa hili lau kungekuwa na faida ya kuwa makafiri wenye kuambiwa kuhusu makubaliano yasiyofaa wanayofanyia kazi na kuyaamini tofauti na hukumu ya Uislamu wangelazimika kukubali uharamu wa kuuza nguruwe na pombe ndani ya nchi ya Waislamu, na ufungaji ndoa bila ya mashahidi pamoja na eda wanazokaa, na yule aliyeharamu katika Uislamu kumuoa, kama vile dada wa kunyonya na mfano wake, pamoja na hayo yote hiyo ni hoja kwa wenye kuzuia, basi mwenye kusema anasema: Hakika riba haramu katika Uislamu na makafiri wanaambiwa misingi yake na matawi yake, basi kilichoharamu kwetu kimekuwa haramu kwao, hivyo riba ni haramu kati ya Muislamu na mtu wa vita ndani ya nchi ya Uislamu na nchi ya vita kwa pamoja, kama vile haramu kati ya Waislamu ndani ya nchi ya Waislamu, na mwenye kudai kunatofauti basi anapaswa kuleta maelezo, na haya ni miongoni mwa yasiyomalizika kwa mwenye kudai kuwa faida ya kuwa makafiri ni kuambiwa kwenye mambo ya matawi yanayoonekana katika hukumu za dini wala si wenye kuhusika na hukumu za Akhera peke yake ([118]).

Ama kauli yao: Ikiwa yaliyoharamu ndani ya nchi ya Uislamu ni haramu ndani ya nchi ya vita ni kama vile machafu na maasi mengine tu.

Anajibiwa kuwa: Mali za mtu wa vita ni halali kwa Muislamu pasi ya makubaliano, basi kwa makubaliano ni bora zaidi.

Ikiwa itasemwa: Uhalali wa mali zao pindi wanapoingia kwa Waislamu kwa usalama, vile vile makubaliano yasiyofaa hata kama italazimishwa kuimairishwa usalama haitofaa kufanya dalili, kwa sababu mtu wa vita pindi anapoingia nchi ya Waislamu mali yake inakuwa halali pasi ya makubaliano, na wala haiwi halali kwa makubaliano yasiyokubalika, kisha sio kila kilichohalalishwa pasi ya makubaliano ni halali kwa makubaliano yasiyofaa.

Kwanza hujibiwa kuwa: Usalama hauzidishi chochote zaidi ya kuharamisha hiyana kwao, hivyo kuhalalisha mali zao kwa Muislamu katika hali yake kama ilivyokuwa kabla ya kutakiwa usalama, tofauti ni kuwa yenyewe imezuiliwa na hiyana, kwani wakati wowote atakapoishikilia bila ya hiyana basi inafaa kwake kuichukuwa, na mwenye kudai tofauti na hivyo basi anapaswa kuleta ufafanuzi, na mtu wa vita pindi anapoingia kwenye nchi ya Uislamu si kwa amani mali yake haiwi halali kwa yeyote atakayeichukuwa, bali yenyewe ni mali ya ghanima kwa Waislamu haifai kwa yeyote kuichukua bila ya kiongozi, katika sherehe ya kitabu cha “As-Sair” amesema: Katika asili ya Abu Hanifa R.A ni kuwa mtu wa vita pindi anapoingia nchini kwetu si kwa amani na mali yake ikachukuliwa na Muislamu basi inakuwa ni mali ya Waislamu, na katika wajibu wa fungu la tano kuna mapokezi ya aina mbili, tumeelezea, lakini kuzingatia upande wa nchi kwa maana nchi ya Waislamu ni uharibifu wa makubaliano haya, na makubaliano pindi yanapoharibika kwa namna moja basi inatosha kuharibika kwake, na imeelezwa kuwa kinachozingatiwa kwetu katika kufikiwa riba ni kwa nchi na wala si mwenye kuingia makubaliano ([119]).

Pili: Kauli yao, “Tupu inahalalishwa kwa mwanamke muovu wa matendo, na wala haihalalishwi kwa makubaliano yasiyofaa” ([120]), amesema katika sherehe ya kitabu cha As-Sair: “lau ikiwa Washirikina wameliteka eneno la Waislamu, kisha ikaonekana miongoni mwao wanaoishi kwa amani ya Waislamu wameiiba basi watatolewa kwenye nchi ya Waislamu, kwani hawapaswi kufanya hivyo, kwa sababu katika wizi huo ni hiyana kwa Waislamu, na hiyana ni haramu, lau mshirikina atapenda kuuza pombe au nguruwe au mzoga inafaa kwake kufanya hivyo, kwa sababu anafanya kwa ridhaa yao, hivyo haifikiwi maana ya hiyana, na baada ya kumnunua mtumwa kwa pesa ya kuuza pombe, pindi anapolipia anakuwa ni miliki yake mpaka amuache huru, na akija mmiliki wake anaweza chukuwa thamani yake ikiwa atataka, kwa sababu anammiliki kwa ridhaa ya nafsi zao na wala si kwa kuuzwa, anakuwa katika nafasi ambayo lau angemtoa zawadi kwake na kumuachia huru ([121]).

Inawezekana kujibu pia maelezo ya mwisho kuwa, uzinzi haulinganishwi na riba, kwa sababu tupu haihalalishwi kwa kitendo kiovo, ni kwa njia maalumu, ama mali uhalalishwa kwa ridhaa ([122]).

Wanaopinga wametumia dalili pia kwa kulinganisha mtu anayeishi kwa amani katika watu wa nchi ya vita, si halali makubaliano yake yasiyofaa na Waislamu ndani ya nchi ya Waislamu.

Linajibiwa hilo kuwa, mali ya mtu wa vita anayeishi kwa amani ndani ya nchi ya Waislamu imekuwa ni yenye kuzuiliwa kwa mkataba na makubaliano ya amani, ikiwa Muislamu atachukuwa kinyume na njia halali inakuwa ni hiyana dhidi ya mkataba wa amani na hili tumelikataza,

Sababu ya tofauti ya hukumu ya makubaliano yasiyofaa ndani ya nchi mbili ni kupewa kwake kumiliki, kwani mashirikiano yakikosa maana ya umiliki yenyewe kwa upande wa mashirikiano ni sawa sawa kwa upande wa Muislamu ndani ya nchi ya vita na ndani ya nchi ya Waislamu, ama kwa upande wa kuwa kwake amesababisha kupatikana kutawala mali ya mtu wa vita kwa ridhaa yake basi inafaa ndani ya nchi ya vita, na wala haifai ndani ya nchi ya Waislamu, kwa kuwa hali ya kwanza ni sehemu ya umiliki tofauti na hali ya nyingine ([123]).

Uharamu wa mali ya mtu wa vita ndani ya nchi ya Waislamu ni ulinzi ambao ameupata kwa hiyo mali kwa mambo mawili: Nchi ya Uislamu, na Makubaliano ya amani, ikiwa yatakosekana mambo hayo mawili mali yake inakuwa ni halali kwa Muislamu kwa asili ya uhalali.

Hivyo watu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wameelezea tofauti kati ya mali ya mtu wa vita ndani ya nchi ya vita na nchi ya Waislamu, wakasema: Kwa hakika mali ya mtu wa vita si yenye kuzuiliwa, bali ni halali kwake, isipokuwa Muislamu mwenye makubaliano naye ya amani amezuiliwa kuimiliki pasi ya ridhaa yake hii ni kutokana na kuwepo ndani yake hiyana, ikiwa atabadilisha kwa hiyari yake na ridhaa yake basi maana hii itakuwa imeondoka, na kuwa kushikilia mali halali si kumilikiwa, tofauti ya Muislamu pindi anapomuuzia mtu wa vita aliyeingia katika nchi ya Waislamu kwa amani, kwani anakuwa amenufaika na zuio kwa kuingia kwake nchi ya Waislamu kwa amani na mali ni yenye kuzuiliwa haiwi sehemu ya kushikiliwa, hivyo uainishwa umiliki kwa makubaliano na sharti la riba ni katika makubaliano yasiyofaa ([124]).

Ama dalili yao kuwa nchi ya vita ni kama nchi ya uovu, ambapo Imamu hana sauti wala mkono, sharti la uhalali wa mkataba na makubaliano yasiyofaa kwa mtazamo wa watu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa ni kuwa ndani ya nchi ya vita na kuwa moja ya upande wake ni watu wa hiyo nchi, wametenganisha nchi ya uovu ambayo inakaliwa na Waislamu hata kama watakuwa ni watu waovu.

Utafiti wa Nne: Mambo yanayopaswa kuangaliwa katika utafiti huu:

Mwisho wa utafiti wetu huu – na baada ya kuangalia kauli za Wanachuoni na dalili zao pamoja na kauli yenye nguvu – inapaswa kuashiria mambo kadhaa, miongoni mwa hayo mambo:

Madhehebu ya Abi Hanifa na wale wanaokubaliana naye, ni kauli ya kufaa moja kwa moja katika masuala yetu bila ya kizuizi kilichowekwa na Al-Kamal Ibn Al-Himam cha kuwa ongezeko ni kwa Muislamu, ambapo amesema: “Haijifichi kuwa unahitajika ufumbuzi wa moja kwa moja ikiwa ongezeko analipata Muislamu na riba ni pana zaidi ya hilo ongezeko, ambapo inakusanya ikiwa ni dirhamu mbili kwa upande wa Muislamu na upande wa kafiri,  jibu la masuala ni pande mbili, vile vile kamari huenda ikapelekea mali kuwa ni hatari kwa kafiri atakaposhinda, uwazi ni kuwa uhalali unafaidisha Muislamu kupata ongezeko, imeelezewa katika tafiti kuwa kusudio lao la uhalali wa riba na kamari ni pale pindi linapopatikana ongezeko kwa Muislamu kutokana na sababu pamoja na jibu kutolewa kinyume chake” ([125]).  

Kukubaliana ibara zake za mwisho katika jibu, Sarkhasy amesema: “Ni sawa sawa ikiwa Muislamu amechukuwa dirhamu mbili kwa dirhamu moja au dirhamu moja kwa dirhamu mbili, kwa kuridhia nafsi ya kafiri kwa kile alichompatia, kikiwa kichache au kingi, na akachukuwa mali yake kwa njia halali kama tulivyoelezea” ([126]).

Sio maana ya maelezo ya kwenye kitabu cha “Al-Mabsuutw” kuwa inafaa kwa Muislamu kumpa mtu wa vita kingi au kichache kwa wema, bali maana yake kufaa hilo kwake ikiwa ndani yake kuna manufaa, ni kama vile kuchukuwa dirhamu mbili kwa dirhamu mbili kwa muda wa baadaye, au anachukuwa dirhamu mbili zilizomzuri kwa dirhamu mbili chafu na mfano wake, kwa sababu hali ya masuala ni katika mambo ya kuuza, na mambo ya bei au kuuza yamejengwa kwenye kuchuma wala si kusameheyana, hivyo kufaa kubadilishana kingi kwa kichache katika kuuza hakuwi katika mlango wa wema.

Tofauti kati ya hukumu ya Kifiqhi ucha-Mungu na kinga:

Tamko la Wanachuoni wamekubaliana kuwa ucha-Mungu ni mpana zaidi ya hukumu ya Kifiqhi, na hilo ni kuwa Muislamu anaweza acha kingi kilichohalali kwa ucha-Mungu, kama walivyokuwa Maswahaba R.A wanaacha kingi halali kiucha-Mungu, wakihofia wasije ingia kwenye haramu, lakini hii haina maana kuwa wao wanaharamisha halali, na ucha-Mungu ni mpana zaidi na mpaka inafikia mwanadamu kutoa mali zake zote kuliko kupata kitu kinachotokana na haramu.

Kutokana na hayo, kujikinga na makubaliano yasiyofaa hata kama na mtu wa vita ndani ya nchi ya vita ni bora zaidi ili kujitoa kwenye tofauti.

Uhalali wa makubaliano haya kwa watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa ni asili, wanakubaliana nao walio kinyume lakini wakati wa kuhitajika, nayo inafahamika kwao kama maswala yanayo lazimisha, Az-Zarkashy anasema: “Huenda ikafaa kuingia makubaliano yasiyo halalali kwa dharura kama vile mtu aliyetenzwa nguvu na kulazimika ananunua chakula kwa bei ya juu ya bei ya kawaida” ([127]).

Imekuja ndani ya kitabu cha Mughny Al-Muhataj: “Hupewa aliyeingia makubaliano yasiyofaa haramu ya riba na nyingineyo isipokuwa katika masuala ya kutenzwa nguvu yanayofahamika, nayo ni kuwa ikiwa mmiliki wa chakula hatouza isipokuwa kwa bei kubwa zaidi ya bei ya kawaida maana yake anatakiwa kununua ununuzi usiofaa ([128]).

Haina maana kwa watu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa na wale anaokubaliana nao kuhalalisha makubaliano yasiyofaa kwa Muislamu ndani ya nchi ya Waislamu kuhalalisha kwa Muislamu yote yaliyo haramu ndani ya hiyo nchi, bali wamehalalisha hayo kwa sababu ni katika yanayotofautiana hukumu kwa kutofautiana na nchi mbili, kwa maana nchi ya Waislamu na nchi ya vita.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad S.A.W pamoja na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba wake wote.

Dr/ Majdi Muhammad Aashur.

Mtaalamu wa Ofisi ya Mufti wa Misri na mjumbe katika jopo la Wanachuoni wa Baraza la kisayansi la tafiti za Qur`ani na Sunna.

 

[1] Kamusi ya Al-Muhiitwu. Kipengele cha mkataba.

[2] Kamusi ya Lisaanul-Arabi kipengele cha mkataba.

[3] Al-Maida: 1

[4] Al-Baqarah:235.

[5] Tafasiri ya Qurtwubi

[6] Kitabu cha Hukumu za Qurani cha Al-Jaswaswau 2/294 – 295.

[7] Marejeo yaliyopita.

[8] Tafasiri ya Ruuhul-Maaniy 6/48.

[9] Kitabu cha Taarifaat.

[10] Kitabu cha Al-Manshuur 2/397. Na angalia: Kamusi elezi ya kifiqhi, ya Wizara ya Waqfu nchini Kuweit, kifungu cha mkataba.

[11] Kitabu cha Bahrul-Muhitwi cha Zamarkashy 1/322.

[12] Angalia kitabu cha: Manaahiji Al-Ukuul 1/79, na kitabu cha Tashayyufi Al-Masaami 1/186. Tamhiidu cha Isnawi 60, Bahrul-Muhitwi cha Zamarkashy 1/321, sherhul-Kawkabul-Muniir 1/474. Na kitabu cha Al-Ashbaah wa Nadhwaair cha Assuyuutwi 479.

[13] Angalia kitabu cha: Kashfu Al-Asrar 1/381, na kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhwahir cha Ibn Najiim 337, kitabu cha Mizanul-Usuuli cha Samarkandy 39.

[14] Angalia kitabu cha Taysiir Tahariir 2/236, na kitabu cha Kashfu Al-Asiraar 1/381, kitabu cha Fawatih Rahmuot 1/122, na kitabu cha Usuulul-Shaashy 168, pamoja na kitabu cha Jaamii Al-Asraar sherhe ya Al-Manaar  cha Kaaky 256.

[15] Kitabu cha Al-Ashbahu wa Nadhwair cha Ibn Najiim 337, na kitabu cha Mizanul-Usuul 37 na kitabu cha Fawaihul-Rahmout 1/122.

[16] Kitabu cha Mizanul-Usuul 39.

[17] Kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhwair cha Ibn Najiim 337, na kitabu cha Taisiir Tahriir 2/236, na kitabu cha Usuulu cha Sarkhasy 1/106, na kitabu cha Usuulu Shaashy 124.

[18] Kitabu cha Al-Ashbaha wa Nadhwahir 337.

[19] Kitabu cha Badhlu Nnadhar fii Al-Usuul 149.

[20] Kitabu cha Al-Mustaswfi 1/95.

[21] Kitabu cha Rawdha Nadhiri na Jannaatul-Munadhir 191, na angalia kitabu cha Al-Ihkaamu cha Aamidiy 1/113, na kitabu cha Al-Ibhaaju sherehe ya Al-Minhaaji 1/69, na kitabu cha Al-Bahru Al-Muhitw 1/320.

[22] Kitabu cha Taisiir Tahriir 2/237, na kitabu cha Al-Muwafiqat cha Shaatwibi 2/502.

[23] Sherehe ya kitabu cha Fathul-Qadiir cha Ibn Al-Himam 6/401.

[24] Kitabu cha Al-Inswaf cha Mardawiy 4/273, na kitabu cha Kashafu Al-Qannai cha Al-Bahuty 3/245, na kitabu cha Fathul-Milki Al-Aziz sherehe ya kitabu cha Al-Wajiiz 3/561..

[25] Kitabu cha Al-Manshuur katika Sarufi cha Zarkashy 3/16, na kitabu cha Al-Ashbah wa Nadhwairi cha Suyuutwi 312.

[26] Kitabu cha Al-Manshuur fii Al-Qawaidi 1/452.

[27] Kuuza kitu: Ni mtu kununua bidhaa kwa mtu kwa malipo ya baadaye kisha akakiuza kwa fedha taslimu, tatizo la hilo kuuza kwa fedha taslimu kisha ananunua kwa mkopo, angalia kitabu cha Mashariqul-Anwar alaa Swahhah Al-Aathaar cha Qadhi Ayyaadh 2/107, na sherehe ya kitabu cha Sahihi Muslimu cha An-Nawawi 11/21, na kitabu cha Al-Miswbaahul-Muniir cha Fayyumi.

[28] Kitabu cha Badaaii Swanaaii cha Makaasaany 5/304, na kitabu cha Bahru Raaiq cha Ibn Najiim 6/103, na kitabu cha Al-Bannany cha Jam’uu Al-Jawaamii 1/106.

[29] Kitabu cha Al-Hawii Al-Kabiir cha Al-Maarudy 5/75, na kitabu cha Al-Majmuui sherehe ya kitabu cha Al-Muhadhabu 9/376, na kitabu cha Al-Mughny cha Ibn Qudama 4/47, na kitabu cha Ikhtilaafu Al-Fuqahau cha TWabary 83, na kitabu cha Madhaahibu Al-Jaliil 3/354.

[30] Al-Muhalla cha Ibn Hazmi 8/514.

[31] Kitabu cha Sherehe Mushakkal Al-Aathaar cha Twahawi 8/248, 249, na kitabu cha Mukhtasar Ikhtilaaful-Ulamaau cha Twahaawi 2/491, na kitabu cha Muutaswar minal-Mukhtaswar cha Abi Al-Mahaasin Al-Hanafi 1/342, na kitabu cha Al-Mabsuutw cha Sarkhasy 14/56, na sherehu ya Fathul-Qadiir cha Ibn Al-Himaam 7/38, na kitabu cha Al-Bahru Raiq cha Ibn Najiim 8/50.

[32] Kitabu cha Masaaiu cha Imamu Ahmad 2/89, na kitabu cha Al-Inswafu cha Mardawi 5/52, 53, na kitabu cha Matwalibu Aula An-Nahyi cha Ruhaibany 3/188, na kitabu cha Al-Mubdai fii sherhi Al-Muqnai cha ibn Muflihu Al-Hambaly 4/157.

[33] Kitabu cha Badaii Swanaaii cha Al-Makaasany 5/193.

[34] Kitabu cha Tabyiin Al-Haqaiq, sherhu ya kitabu cha Kanzu Daqaiq 6/340, na Hashiyatu Raddul-Muhtar cha Ibn Aabideen 5/672.

[35] Kitabu cha Al-Mabsuutw cha Sarkhasy 14/58, na kitabu cha Badaaii Swanaaii 7/131.

[36] Kitabu cha Al-Mabsuutw 14/59.

[37] Kitabu cha Ilaau Sunan cha Dhwaafir 13/6250.

[38] Kitabu cha Al-Mabsuutw 22/131.

[39] Al-Baqarah: 275.

[40] Al-Baqarah: 278, 279.

[41] Aal-Imraan: 130.

[42] Kitabu cha Al-Bahru Al-Zukhar, cha Ahmad Ibn Yahya Al-Murtadha 4/340.

[43] Imekubaliwa na Wanachuoni wa Hadithi: Tamko la Imamu Muslimu katika sahihi yake 3/1219.

[44] Amepokewa na Imamu Muslimu katika Sahihi yake, kitabu cha mambo ya umwagiliaji Hadithi nambari 3/1211.

[45] Imepokewa na Imamu Muslimu katika Sahihi yake 3/1309, na Shaafi katika Musnadi yake 2/57.

[46] Imepokewa na Baihaqiy katika kitabu cha Sunanil-Kubra 9/133.

[47] Imepokewa na Ahmad katika Musnadi yake 1/36. 49, na Ibn Abi Shaiba katika Maswanafi yake 4/448, na Ibn Maja katika Sunani yake 2/764, Al-Buuswiiry amesema katika kitabu cha Miswbahu Zujaajah 3/35: Ni upokezi sahihi na wapokezi wake ni watu wenye kuaminika.

[48] Kitabu cha Al-Haawi Al-Kabiir 5/75, na kitabu cha Al-Majimuui 9/376, na kitabu cha Al-Mughny cha Ibn Qudama 9/237.

[49] Aal-Imraan: 85.

[50] Al-Maidah: 49, na angalia kitabu cha Al-Muhalla cha Ibn Hazmi 5/81.

[51] Kitabu cha Al-Umu cha Imamu Shaafi 4/237, na kitabu cha Al-Majmuui cha An-Nawawi 9/391, na kitabu cha Al-Mughany 4/46.

[52] Kitabu cha Al-Hawiy Al-Kabiir 5/75, na kitabu cha Al-Majmuu cha An-Nawawi 6/376, kitabu cha Al-Mughny 4/47.

[53] Kitabu cha Al-Mabdii 4/157, na kitabu cha Matwaalibu Uulaa An-Nahyi 3/189.

[54] Kitabu cha Raddu Alaa Sair Al-Auzaai cha Abi Yusufu 97 na kupokewa na Zailay katika kitabu cha Nusubi Rayah 4/44.

[55] Kitabu cha Al-Ummu cha Imamu Shaafiy 7/359.

[56] Al-Mabsuutw 14/56.

[57] Kitabu cha Ilaa As-Sunan 13/6236.

[58] Kitabu cha Al-Majmuui 9/376, na kitabu cha Al-Mughany 4/46, kitabu cha Matwaalib Uli Nnuhaa 3/189.

[59] Al-Baqarah: 197.

[60] Kitabu cha Al-Majmuui 9/391, na angalia kitabu cha: Al-Mughny 4/46, na sherhu Muntahii Al-Iraadat 2/79.

[61] Kitabu cha Iilaau Sunan 13/6245.

[62] Imepokewa na Twahawi katika kitabu cha Mushakkal Al-Aathar 4/245, na akasema katika kitabu cha Ilaau Sunan 13/6257, upokezi wake ni sahihi.

[63] Imepokewa na Imamu Muslimu katika kitabu cha Shaklul- Aathaar 2/889, na Imamu Ahmad katika Musnadi yake 5/73, na Ibn Maja katika Sunani yake 2/1025.

[64] Imepokewa na Imamu Ahmad katika musnadi yake 5/73 na Abu Daud katika Sunani yake 3/244. Na Imamu Tirmidhy katika Sunani yake 5/273, na akasema ni Hadithi Nzuri na sahihi.

[65] Angalia: Kitabu cha Al-Mabsuutw cha Sarkhasy 10/28, 14/57.

[66] Kitabu cha, Takmilatul-Majmuui 10/439.

[67] Kitabu cha Ahkaamil-Quran cha Jaswaswa 1/471.

[68] Al-Baqarah 270, na angalia kitabu cha: Al-Jauhar Al-Muntaqy cha Ibn Turkumani 9/106.

[69] Imepokewa na Maliki katika kitabu cha Al-Muwatwaa 2/746, na kuendelezwa na Ibn Abdulbarr katika kitabu cha Tamhiid 2/48 kutoka kwa Ibn Abbas, na pia imepokewa na Abdulraziq katika kitabu cha Al-Muswannif 7/166, na Baihaqy katika kitabu cha Al-Kubra 9/122.

[70] Kitabu cha Al-Mukhtasar minal-Mukhtasar cha Twahawi 1/341 – 343.

[71] Kitabu cha Mukaddimaat Al-Mumahidaat 3/602.

[72] Kitabu cha Iilaaul-Sunan 13/6239.

[73] Imepokewa na DarQutwni katika Sunani yake 3/46, na Twabraniy katika Muujamu Al-Ausatw 1/249, 7/29, na Al-hakim katika kitabu cha Mustadraku 2/61 na akasema: isnadi ni sahihi, na kulkubaliwa na Adhahby, na kupokewa na Baihaqy katika kitabu cha Al-Kubra 6/28.

[74] Kitabu cha Sairul-Kubraa cha Muhammad Ibn Al-Hassan Al-Shaibany  3/228,  229 kitabu cha Al-Bahru Raqy /135, na angalia: Kitabu cha Al-Inswafu cha Mardawy 5/53.

[75] Imepokewa na Imamu Tirmidhy katika Sunani yake 5/343 na akasema: Hadini mzuri sahihi, na angalia kitabu cha Al-Mabsuutw cha Sarkhasy 14/56 na sherehe ya kitabu cha Sair Al-Kubra 4/1411 pamoja na sherehe ya kitabu cha Fathu Al-Qadiir 6/178…

[76] Imeelezwa ongezeko hili kwenye kitabu cha Maalim Tanziil 3/476 na Suyuutwi akainasibisha katika kitabu cha Adduru Al-Manshuur 6/480 cha Abi Yaalaa na Ibn Abi Hatim pamoja na Ibn Mardawi na Ibn Asaakir.

[77] Kitabu cha sherhu Fathul-Kadiir 6/178,

[78] Sherehe ya kitabu cha Sairul-Kabiir 4/1411, na kitabu cha Imamu Suyutwy 14/57, pamoja na kitabu cha Ruuhul-Maany cha Imamu Al-Aluusy 21/18.

[79] Kama ilivyopokewa na Tirmidhy katika kitabu chake 5/344 na akasema: Ni Hadiithi sahihi nzuri ni katika Hadithi ya Niyaar Ibn Makram, na Ibn Kathiir amesema katika tafasiri yake 3/424 imepokea kwa maelezo na kundi la Taabiin kama vile Akrama, Shaaby, Mujahid, Qatada, Sadiy na Zahriy.

[80] Suratul-Aal Imran:130

[81] Kitabu cha Muharrir Al-Wajiiz 1/506. Angalia tafasiri ya At-Tahriir wa at-Tanwiir ya Ibn Ashuur 4/85.

[82] Suratul- Ruum: 39.

[83] Sherehe ya kitabu cha As-Sair Al-Kabiir 3/225.

[84] Kitabu cha Al-Mabsuut cha Sarkhasy 14/59.

[85] Ibn Hajar ameinasibisha kwenye ufupisho wa Al-Hubair 4/162 na Abdiraziq, na Ibn Kathiir amesema katika kitabu cha Al-Bidaya wa An-Nihaya 3/104 imepokewa na Abubakri Shaafy kwa upokezi mzuri kutoka kwa Ibn Abbas.

[86] Kitabu cha Takmilatul-Majmuui 14/28, na angalia kitabu cha: Al-Mabsuutw 14/57, na sherehe ya kitabu cha As-Sair Al-Kabiir 4/1411.

[87] Kitabu cha Al-Mabsuutw 14/57, na sherehe ya Sairul-Kubiir 4/1412.

[88] Kitabu cha Al-Bidaya Wainnihaya cha Ibn Katheer 3/103.

[89] Maidah: 67, na angalia kitabu cha: Al-Khaswaisw Al-Kubra  cha Imamu Assuyutwi 1/129, 130.

[90] Kitabu cha Tabyiin Al-Haqaiq 4/97, na kitabu cha Al-Majmuu 9/376.

[91] Kitabu cha badaai Swanaai 5/192 na kitabu cha Hashiyatu Ibn Aabideen 5/426.

[92] Kitabu cha Badaaii Swanaaii 5/193, 7/131.

[93] Maelezo yamepokewa na Abu Ubaid katika kitab cha mambo ya mali 146 na Tahaanawi amesema katika kitabu cha Iilaai Sunani 13/6254 wapokezi wake ni watu wanao aminika, Suhail Ibn Aqiil hakufahamu haya lakini Laithu Ibn Saad alipokea kutoka kwa mtu asiyepingwa naye ni Imamu mwenye jitihada….

[94] Kitabu cha Iilaau Sunan 13/6254. 6256, na angalia pia 11/5281.

[95] Imepokewa na Shaafii katika Musnadi yake 84, Tahanawi amesema katika kitabu cha Iilaai Sunan 13/6252 upokezi wake ni sahihi.

[96] Kitabu cha Al-Muhily cha Ibn Hazmu 8/514.

[97] Kitabu cha Iilaa As-Sunan 13/6251, na angalia kitabu cha Al-Mahallah cha Ibn Hazmi 8/514.

[98] Kitabu cha Iilaau Sunan 13/6274.

[99] Imepokewa na Imamu Bukhary katika Sahihi yake 2/795 kutoka kwa Abi Said Al-Khudry, na 5/2166 kutoka kwa Ibn Abbas R.A naye hapa ni shahidi.

[100] Kitabu cha Tahkiik fii Ahaadiith Al-Khalaf cha Ibn Jawzy 2/219, na kitabu cha Tanqiih Tahkiik Ahaadiith maelezo ya Ibn Abdul-Haadiy Al-Hambaly 3/68. Na kitabu cha Naswbu Raayah cha Zailaii 4/139, na kitabu cha Umdaatu Al-Qaary sherehe ya kitabu cha SAhihi Al-Bukhary cha Ainy 12/96…

[101] Tamko hili limepokewa na Baihaqy katika kitabu cha Maarifatu Sunani wal Aathaar 4/300, na mfano wake kitabu cha Rabii katika Musnadi yake 230 kutoka kwa Ibn Abbas, na limepokewa na Imamu Bukhary katika Sahihi yake 2/776 kutoka kwa Raafii Ibn Khadiij, na kwa Imamu Shaafiy katika Musnadi yake 141.

[102] Imepokewa na Abu Daud katika sunani yake 3/250 na Imamu Tirmidhy katika Sunani yake 3/538, na Imamu An-Nisaai katika kitabu cha Al-Mujtaba 7/292, na Imamu Ahmad katika Musnadi yake 5/12, 19, 99 wote kutoka kwa Samrah Ibn Janabi, na Ibn Hayyan katika Sahihi yake 11/401 kutoka kwa Ibn Abbas.

[103] Kitabu cha Tabyiin Al-Hakaaik 4/112.

[104] Angalia kitabu cha: Al-Ikhtilaafu Al-Fuqahau cha Twabary 82, na kitabu cha Al-Mabsuutw 14/56, na kitabu cha Al-Bahru Raaq 6/147, 148, na Fatwa Swafdiy 1/495…

[105] Kitabu cha Al-Bahru Raaiq 8/50

[106] Kitabu cha Al-Fatawa Al-Hindia cha Sheikh Nidham na kundi la Wanachuoni wa India 5/276.

[107] Kitabu cha Al-Mabsuutw 22/131.

[108] Sherehe ya kitabu cha Fathu Al-Kadiir 7/39.

[109] Kitabu cha Al-Mabsuutw 14/58.

[110] Kitabu cha sherehe ya Sairul-Kabiir 3/226.

[111] Al-Baqarah: 278.

[112] Al-Baqarah: 281.

[113] Al-Itiqaan 1/28.

[114] Kitabu cha Imlaau Sunan 13/6265, 6266.

[115] Al-Maidah: 49.

[116] Al-Maidah: 49.

[117] Kitabu cha Fawatih Ar-Rahmuun, cha Ibn Abdulshakuur 1/115.

[118] Kitabu cha Ilaau As-Sunan 13/6272.

[119] Sherehe ya kitabu cha Sair Al-Kabiir cha Sarkhasy 3/226.

[120] Kitabu cha Al-Majmuui 9/376.

[121] Sherehe ya kitabu cha As-Sair Al-Kabiir cha Sarkhasy 3/227.

[122] Sherehe ya kitabu cha Fathul-Qadiir 7/39.

[123] Kitabu cha Badaai Swanaai 5/192, na kitabu cha Haashiyatu Ibn Aabideen 5/426.

[124] Badaai Swanaai 7/131.

[125] Sherehe ya kitabu cha Fathul-Qadiir 7/39.

[126] Kitabu cha Al-Mabsuutw 14/59.

[127] Kitabu cha Manthuur katika kanuni. 1/351.

[128] Mughny Al-Muhtaaj kwa sherehe ya Al-Minhaaj, cha Khatibu Sharbiny 2/30, na angalia kitabu cha Hawaashy As-Sharwaany kwenye kitabu cha Tuhfatul-Muhtaaji 4/291.

Share this:

Related Fatwas