Kufunua Uso wa Mwanamke

Egypt's Dar Al-Ifta

Kufunua Uso wa Mwanamke

Question

 Kufunua Uso wa Mwanamke

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema ni za Mungu, na Rehma na amani zimfikie bwana wetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu, na baada ya hayo ... Huu ni utafiti katika kufunua uso wa mwanamke.

 Neno la Kiarabu KASHFU (kufunua) katika lugha maana yake ni: kuondosha kitu kutokana na kile kinachoficha na kukifunika, na (kufunua) kitu  - kudhihirisha: kukiondoa humo kinachokifunika na kinachoficha. Imesemwa: amefunua jambo  juu yake: Alilidhihirisha, na Mwenyezi Mungu akafichua  huzuni yake: Akaiondoa, na fulani (amefunuliwa), sehemu ya mbele ya kichwa chake ikadhihirika na akashindwa katika vita, na mwanamke (akafunuliwa): Mwanamke alizidisha kudhihirisha mapambo yake, na jambo: lilifunuliwa kwa juhudi fulani, na jambo (lilifunguka): likaonekana [1].

Maana ya kiistilahi haitofautiani na maana ya kilugha, ambayo ni: kuondoa  kitu katika kile kinachokificha na kukifunika.

Neno la Kiarabu ALWAJHU (Uso) katika lugha: huchukuliwa kutokana na ALMUWAJAHA (makabiliano) (na ni mustakbali wa kila kitu. Uso unaweza kuelezea mtu, husemwa: umemkabili: ikiwa nimakabiliana naye: ukikutana naye uso wake na uso wako [2].

Katika istilahi: uso wa mwanadamu ni: ni shemu iliyopo kati ya mwanzo wa nywele wa kichwa na chini ya kidevu kwa urefu, na ni kati ya ndewe za masikio kwa upana [3].

Huu ni upambanuzi katika kuelezea sehemu ya mvutano:

Wanazuoni wamekubaliana kwamba vazi la Kiislamu linalohitajika kwa mwanamake wa Kiislamu lazima litimize masharti matatu:

kwanza: Lisioneshe maeno ya mvuto ya mwili wake.

Pili: Lisioneshe yaliyo chini.

Tatu: Liwe ni lenye kusitiri.

Kisha baada ya hayo wakatofautiana kuhusu sehemu gani ya mwili wa mwanamke inapaswa kufunikwa, na sehemu inayoruhusiwa kudhihirishwa, kuna wanaotofautisha sehemu za siri za mwanamke wakati wa Swala na nje ya Swala - yaani sehemu za siri kutokana na kutazama - na wapo ambao hawakutofautisha.

Ama katika Swala, makubaliano ya madhehebu manne yanayotegemewa ni kwamba sehemu za siri za mwanamke zinajumuisha mwili wake wote isipokuwa uso na viganja viwili, na hali hiyo hiyo inatumika anapokuwa katika Ihram (Hija).

Katika Al-Kanz na maelezo yake ya Az -Zayla’iy, kutoka katika vitabu vya wafuasi wa Hanafiy: “(Na mwili wa mwanamke huru ni uchi isipokuwa uso wake, viganja vyake na miguu yake), kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika}. [An Nuur: 31]. Yanayokusudiwa ni mahali pa pambo lao na yanayoonekana kwayo, uso na viganja viwili. Hayo yamesemwa na Ibn Abbas na Ibn Umar, na katika Al-Mukhtasar akatoa sehemu tatu kwa ajili ya kutahiniwa kwa kuzidhihirisha; na kwa sababu Mtume, Rehema na Amani zimshukie, amekataza mwanamke mwenye kuhirimia kuvaa glovu na nikabu, na ingekuwa uso na viganja ni sehemu za siri, asingeharamisha kusitiri kwa kitu kilichoshonwa, na kuna mapokezi mawili katika miguu, na mtazamo sahihi zaidi ni kwamba si sehemu za siri za kutahiniwa kwa kuifanya zionekane” [4].

Katika Kifayat At-Taalib Ar-Rabbaniy, miongoni mwa vitabu vya wafuasi wa Malik: “Katika Swala, mwanamke lazima afunike miguu yake, nywele, shingo na shore za nywele yake, na inajuzu kwake kuonesha uso na viganja vyake katika Swala kwa sifa maalumu” [5].

Na katika Ash-Sharh Al-Kabiir miongoni mwa vitabu vyao vile vile: “(Na) inachukizwa (kwa mwanamke kuvaa nikabu), yaani kufunika uso wake kwa nikabu, ambayo ndiyo inayofika macho katika Swala, kwa sababu ni kuzidisha, na mwanamume ni karaha zaidi - yaani zaidi ya mwanamke - isipokuwa awe ni miongoni mwa watu waliozoea kufanya hivyo” [6].

Na katika Al-Minhaj na maelezo yake ya Al-Ramliy, miongoni mwa vitabu vya wafuasi wa Shafi: “(Na) sehemu za siri za (mwanamke huru) (ni kisichokuwa  uso na viganja viwili) katika mwili wake nyuma na mbele kwenye vifupa vya mwanzo wa mkono; kwa mujibu wa kauli yake Mola Mtukufu: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika}. [An-Nuur: 31] .

Ibn Abbas na Aisha wamesema: Ni uso na viganja, kwa sababu lau kama zingekuwa sehemu za siri, zisingelazimika kufunuliwa wakati wa Ihram” [7].

Na katika Sharh Al-Muntaha kutoka katika vitabu vya Hanbali: “(Na mwanamke  huru na baleghe mwili wake wote ni uchi katika Swala) hata kucha yake kimatini (isipokuwa uso wake) kwa mujibu wa Hadithi: (Mwanamke ni uchi) ameipokea At-Tirmidhi, ambaye amesema: Ni Hassan na Sahihi. Na hukumu hii ni ya kawaida yaani kuacha Uso kwa mujibu wa Ijmaa [makubaliano ya Wanachuoni] : wote ni uchi isipokuwa uso. Ama Ibn Abbas na Aisha kuhusu kauli yake Mwenyezi: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika } [An Nuur: 31] Wakasema: (Uso na Viganja) Ibn Masud alikhitalifiana nao na akasema: “Nguo” na kwa sababu hakuna haja inayopelekea kufunua viganja kama kupelekea kufunua uso na kwa kulinganisha na miguu [8].

Ama nje ya Swala, kinachotegemewa ni kuwa sehemu za siri za mwanamke huru wa Kiislamu ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja, hivyo inajuzu kwake kufunua(uso na viganja). Na haya ni Madhehebu ya wanazuoni walio wengi miongoni mwa  Hanafi, Maliki na Shafi, na ni Madhehebu ya Al-Awzaiyi na Abu Thawr miongoni mwa Wanachoni wa Fighi wa Salaf, na ni kauli moja katika Madhehebu ya Ahmad. na Madhehebu hayo haikutofautisha sehemu za siri za mwanamke huru wakati na nje ya Swala, na hapa chini ni wametaja ushahidi waliotumia kama dalili.

Huu ni upambanuzi wa ushahidi wa wale wanaosema inajuzu kufunua uso wa mwanamke:

Wale wanaosema kuwa inaruhusiwa kufunua uso wa mwanamke wametoa ushahidi mwingi, ambao ni kama ifuatavyo:

Dalili ya kwanza:

Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika} [An-Nuur: 31] Ibn Abbas amesema: “Uso wake na viganja vyake” pia imepokewa kutoka kwa Ataa, Said Ibn Jubayr, Adh-Dahhak, na Al-Awzaiy, na Al-Hasan amesema: Uso na nguo. Imaam At-Tabariy ameipokea hii katika tafsiir yake kisha akasema: “Rai iliyo sahihi zaidi juu ya jambo hili ni kauli ya yule aliyesema: Alikusudia kwa hilo: uso na viganja vya mikono, basi hii inajumuisha : wanja, pete, bangili, na rangi.

Hivyo, tulisema kwamba maoni yanayofaa zaidi kuhusiana na jambo hili yanatokana na maelezo maalumu; kwa ajili ya maafikiano ya wote kwamba kila mwenye kuswali ni lazima afunike sehemu zake za siri wakati wa Swala yake, na kwamba mwanamke afunue uso na vigania vake wakati wa Swala yake, na afunike chochote cha mwili wake, isipokuwa kile kilichopokewa kutoka kwa Mtume S.A.W, kwamba alimruhusu aoneshe mkono wake hadi nusu. Ikiwa hili lilikubaliwa kwa kauli moja na wote, basi inajulikana kwamba ana haki ya kufichua sehemu ya mwili wake sehemu ambayo sio ya siri, kama ilivyo kwa wanaume, kwa sababu ikiwa si ya uchi, haikatazwi kuionesha, na kama anaruhusiwa kuonesha sehemu hiyo, basi imejulikana kuwa ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu Mtukufu amelivua katika kulitaja kwa kusema: {isipo kuwa unao dhihirika} kwa sababu yote hayo yanadhihirika kwake” [9].

Imam Al-Qurtubiy amesema: “Kwa kuwa ni kawaida nyuso na viganja hudhihirika kama kimazoea na kiibada, na hilo ni katika Swala na Hija, basi inafaa kuvivua  kwake kunarejea katika hayo” [10].

Al-Jassas mfuasi wa Hanafiy amesema: “Inaashiria pia kwamba uso na viganja si miongoni mwa uchi kwa sababu anasali wakati uso na viganja vyake vikiwa wazi, na vingekuwa uchi ingemlazimu avifunike, kama anavyopaswa kufunika uchi” [11].

Dalili ya pili:

Ilivyopokewa na Bukhariy ni kuwa Mtume S.A.W, amesema: “Mwanamke katika hali ya Ihram asijifunike uso wala kuvaa glovu” [12], na dalili ni kwamba ingekuwa kufunika uso na viganja vya mikono ni wajibu isingejuzu kuvifunua katika hali ya Ihram, na kuzifunika namna hii itakuwa ni miongoni mwa makatazo ya Ihramu, na lau kama uso na kiganja ni uchi isingekatazwa kufunika.

Wale wanaoharamisha (kufunua uso na viganja) wamejibu kuhusu kutolea dalili  Hadithi hii, na hata wakaitumia kuwa ni dalili ya  uwajibishaji kwa mwanamke kufunika uso wake, ufafanuzi wa hili utakuja wakati wa kujadili dalili zao wao.

Dalili ya tatu:

Ilivyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas RA, amesema: Al-Fadhl alikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, akaja mwanamke mmoja kutoka kwa Khath’am, na Al-Fadhl akaanza kumwangalia yule mwanamke, na mwanamke akamtazama, na Mtume S.A.W, akauelekeza uso wa Al-Fadhl upande wa pili, akasema mwanamke:  Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, faradhi ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake nayo ni Hija, imemdiriki baba yangu akiwa mzee sana na hawezi kupanda ngamia wake, Je! Naweza kufanya Hija badala yake, akasema: (Ndiyo). Na hii ilikuwa wakati wa Hija ya Kuaga [13].

Hadithi hii katika mapokezi yake mbalimbali ilikuwa katika Hija ya kuaga, kwa hiyo ni baada ya Aya ya kujiteremshia nguo, na sababu yake ni kwamba lau uso ungekuwa uchi na kutakiwa kufunikwa, basi Mtume S.A.W, asingeridhia kudhihirika kwake mbele ya watu, na angemuamuru kuweka nguo juu yake, na lau uso wake ungefunikwa Ibn Abbas asingejua kama mwanamkes ni mzuri au mbaya.

Ikisemwa: Yeye ni yupo Iharmu na katika hali hii ni haramu kuvaa nikabu, tunasema: Ndio ni haramu kuvaa nikabu, lakini haikatazwi kufunika uso, na dalili ya uhalali wa kufunika uso ni kauli ya Asmaa binti Abi Bakr: “Tulikuwa tukifunika nyuso zetu mbele ya wanaume, na tulikuwa tukichana nywele zetu kabla ya hapo tukiwa katika Ihram [14], na ikiwa kufunika uso si wajibu katika Ihram  basi si wajibu katika hali nyingine isipokuwa Ihram, ambayo ndiyo inayotakiwa kuthibitika.

Ikisemwa: Alikuwa miongoni mwa wazee, tunasema: Imeelezwa katika mapokezi ya Hadithi kwamba alikuwa ni mwanamke kijana, na ikiwa alikuwa ni kikongwe, basi mwanamke huyo alikuwa na uso wa mvuto na kutamani ndoa, hivyo hajumuishwi miongoni mwa wanaoruhusiwa kuacha hijabu.

Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalaniy amesema katika Al-Fath: “Amesema Ibn Battaal: Katika Hadithi kuna amri ya kuinamisha macho kwa kuogopa fitna, na ina dalili ya kuwa wanawake wa waumini hawalazimiki kuvaa hijabu iliyolazimu wake wa Mtume S.A.W; kwani kama hilo lingetakiwa kwa wanawake wote, Mtume SAW,  angeliamrisha mwanamke huyo Khathamiyyah kujisitiri, na pale alipotupilia mbali uso wa Al-Fadhl, na kuna dalili kwamba mwanamke kufunika uso wake si faradhi.” [15].

Dalili ya nne:

Kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema: “Niliswali pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, siku ya Idi, alianza kuswali kabla ya khutba bila adhana  wala iqama, kisha akasimama akiwa ameegemea kwa Bilal, na akaamrisha kumcha Mungu na akawahimiza wamtii, akawatolea watu mawaidha, akawakumbusha, kisha akaendelea mpaka akawajia wanawake, hivyo akawausia na kuwakumbusha, na akasema: Mtatoa sadaka kwani wengi wenu ni kuni za Motoni, akasimama mwanamke miongoni mwao mwenye mashavu mabaya, akasema: kwa nini Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Kwa sababu mnalalamika sana na hamna shukurani kwa mwenzenu. Akasema: Basi wakaanza kutoa baadhi ya vito vyao, wakatupa baadhi ya hereni zao na pete katika nguo ya Bilal [16].

Sehemu ya dalili katika  Hadithi hii: Mpokeaji wa Hadithi bwana wetu Jabir bin Abdullah RA,  amesema (mwenye mashavu mabaya), maana yake ni yule mwanamke ambaye mashavu yake yalikuwa mekundu yakiwa na weusi, kwa hiyo Sahaba huyo mashuhuri aliuonaje uso wa mwanamke huyo na kuufafanua ikiwa hakuwa ameufunua?

Wale walioipinga wakajibu Hadithi hii: Hakuna chochote ndani yake kinachoashiria kuwa Mtume S.A.W, alimuona uso wake ukiwa wazi, na akamridhia kufanya hivyo, kila lililopatikana kuwa Jabir aliuona uso wake, na hilo halimlazimu kuufunua kwa makusudi, na wanawake wangapi hijabu zao zinaangukwa usoni mwake bila kukusudia, na baadhi ya watu wanauona katika hali hiyo, kwa hiyo mwenye kutumia Hadithi iliyotajwa hapo juu ni lazima athibitishe kuwa Mtume S.A.W, ameuona, na kuridhia jambo hilo, naye hana njia ya kuthibitisha hilo.

Hadithi iliyotajwa hapo juu ilipokewa na watu wengine asiyekuwa Jabir, na hawakusema kuwa mwanamke aliyetajwa kudhihirisha uso wake, na Imamu Muslim alitaja kwenye Sahih yake watu wengine asiyekuwa Jabir waliyopokea  Hadithi hii, akamtaja Abu Said Al-Khudriy, Ibn Abbas, na Ibn Umar, na wengine waliitaja kwa wengine. Hakuna yeyote aliyepokea Hadithi hii isipokuwa Jabir aliyesema kwamba aliona mashavu ya mwanamke huyo yakiwa ni mashavu mabaya, na hivyo inajulikana kwamba hakuna ushahidi wa kufichua uso katika Hadithi iliyotajwa hapo juu ya Jabir.

Hili linajibiwa kuwa lau bwana wetu Jabir alikuwa na nia ya kukifikisha Hadithi hii kwa undani wake; kiasi cha kumueleza mwanamke aliyeuliza kuwa ana mashavu mabaya, basi lau kitambaa chake (cha kuficha uso)  kingeanguka na uso wake ukaonekana, angelitaja hilo na kulielezea.

Baadhi yao [17] walikwenda kwenye Madhehebu mengine katika kuijibu Hadithi hii, wakisema kwamba kuna herufi iliyobadilishwa katika Hadithi, na wakayapa usahihi zaidi yale aliyoyapokea Al-Qadhi Iyaadh kwa mashekhe wake wakubwa kwamba: Maneno (Sitat An-Nisaa) ni kosa katika Sahiih Muslim, na kwamba jambo sahihi ni: (Mwanamke kutoka kwa tabaka la chini) - Kama ilivyoelezwa katika Sharh ya Muslim na An-Nawawiy, ambayo imepokewa katika Sunan An-Nasaiy [18].

Kisha akasema: “Kauli yake - yaani katika Hadithi - (mashavu mabaya) ina maana: kuna mabadiliko na weusi ndani yake, kauli yake: (mwanamke kutoka tabaka la chini na mwenye mashavu mabaya) maana yake : yeye si katika wanawake wa tabaka la juu. Lakini ni wa chini na mweusi, na usemi huu huonesha sana kwamba mwanamke alikuwa mtumwa na si mwanamke huru, na kwa hiyo hakuna ushahidi katika hili kwa yeyote aliyeitumia kama ushahidi kwamba inajuzu kufunua uso wa mwanamke, kwani kinachosameheka kwa watumwa wa kike ni jambo lisilosameheka kwa wanawake huru”.

Imamu An-Nawawiy alijibu hilo katika maelezo yake ya Muslim, akisema: “Na haya waliyadai kuna mabadiliko ya neno halikubaliki, bali ni sahihi, na kinachokusudiwa nacho si mwanamke wa juu, bali kile kinachokusudiwa ni mwanamke miongoni mwa wanawake waliokaa katikati yao, Al-Jawhariy na wanalugha wengine wamesema: neno (Sitat), maana yake kuwa mwanamke alikuwa akikaa katikati ya wanawake, na (mwenye mashavu mabaya) maana yake kuna mabadiliko na weusi ndani yake [19].

Tukichukulia kwamba tunakubali kuwa herufi imebadilishwa, neno (sifla: mwamamke wa chini) halioneshi kwa uhakika kwamba alikuwa mtumwa wa kike; bali ni uwezekano tu ambao una maoni kwenye uchunguzi. Katika kamusi na maelezo yake ya Az-Zubaidiy: (Sifla yaani watu wa chini au duni) [20].  Tazama, Sheikh alipokuwa akichunguza maana zilizomo katika lugha hiyo, hakutaja hata dalili kwamba neno hili linaweza kutumika kwa watumwa wa kike.

Mwisho: Hata kama dhana ya ushahidi huu itashindwa kuunga mkono madai yetu kwamba inajuzu kwa mwanamke kufunua uso wake, ubatili wa dalili maalumu hauoneshi ubatili wa maana maalumu.

Dalili ya tano:

Kutoka kwa Sahl Ibn Saad: Alikuja mwanamke kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., na akasema, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Nimekuja kujitoa kwako,  na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, akamtazama na kumuangalia sana, kisha akainamisha kichwa chake, mwanamke huyo alipoona kwamba hakuwa na uamuzi wowote juu yake, akakaa chini, hapo mtu miongoni mwa Masahaba akasimama na kusema, “ Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ikiwa huna haja naye, basi niozeshe mimi, akasema Mtume: Je! Unamiliki kitu chochote, akasema: “Hapana, Wallahi, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, akasema: “Nenda kwa jamaa zako na uone kama utapata chochote”. Akaenda na akarudi na kusema: “Hakuna, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, sikupata chochote”. Akasema: Tazama hata ikiwa ni pete ya chuma, akaenda na akarudi na kusema: “Hakuna, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata pete ya chuma, lakini hii ni nguo yangu.” - Akasema Sahl: nguo/msuli bila nguo ya juu - atachukua nusu yake. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., akasema: “Atafanya nini na nguo yako, akivaa hakuna chochote juu yake, na ukiivaa hakuna chochote juu yako ". Basi yule mtu akakaa mpaka kikao chake kikawa kirefu, kisha akasimama, na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, akamuona anaondoka, akaamrisha aitwe, na alipokuja, akasema: “Una nini katika Qur`ani? Akasema: "Nina Sura fulani na fulani na fulani, akazihesabu, na Mtume akasema: Je umezihifadhi kwa moyo, akasema: Ndiyo. Akasema: Nenda, kwani mimi nimekumilikisha kwa yale uliyonayo katika Qur`ani [21].

Tukio hili linaashiria kuwa mwanamke huyo alikuwa uso wake ulikuwa wazi, vinginevyo, ni ipi hekima ya Mtume S.A.W, kumchunguza kwa ukaribu?, na nini sababu ya Sahaba huyo kutaka kumuoa na hakuona chochote kutoka kwake?

Ikisemwa: Mahali hapo ni pahali pa kuoana na kuchumbiwa, tunasema: Tukikubali hilo, basi pokezi halina chochote kinachoashiria kuwa hakudhihirisha uso wake kisha akaufunua.

Na ikisemekana kuwa inawezekana hii ilikuwa kabla ya Hijabu, tunasema: Al- Hafidh Ibn Hajar katika Al-Fat-h amepokea hivi kutoka kwa Ibn Al-Arabiy na akajibu kusema: “Ibn Al-Arabiy alichukua njia tofauti katika kujibu na kusema: Inawezekana kwamba hii ilikuwa kabla au baada ya Hijabu, lakini alikuwa amevaa chenye kufunika, na muktadha wa Hadithi uko mbali na hilo [22].

Tukichukulia kuwa tunakubali kwamba hii ilikuwa kabla ya Aya kuhusu Hijabu, hii haiashirii chochote. Hakuna tofauti baina ya hili kutokea kabla ya Aya ya Hijabu au baada yake. Kwa sababu Aya kuhusu Hijabu ni malumu kwa wake za Mtume SAW, Mama wa Waumini - kama itakavyofuata -.

Dalili ya sita:

Iliyopokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A, kwamba Asmaa binti Abi Bakr aliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, akiwa amevaa nguo nyembamba, na Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, akamgeukia na kusema: “Ewe Asmaa: Mwanamke anapofikia umri wa kupata Hedhi, haifai kwa yeyote kuona chochote kutoka kwake, isipokuwa hivi na hivi” na akaashiria uso na viganja vyake. Abu Dawud alisema: Hii ni Hadithi Mursal ya Khalid Ibn Duraik ambaye haikumfikia Aisha RA, [23].

Imaamu Al-Baihaqiy amesema: “Ingawa Hadithi ni Mursal lakini kauli ya Masahaba waliopita R.A, katika kueleza yale aliyoyaruhusu Mwenyezi Mungu katika pambo la nje, kauli ikawa na nguvu, na Mwenyezi Mungu atuwafikishe” [24].

Dalili ya saba:

Kwamba haja ya kufunua uso kwa ajili ya kununua na kuuza na kufunua kiganja kwa ajili ya kutoa na kuchukua, kwa hivyo hii haifanyi kuwa uchi.

Huu ni upambanuzi  katika maandiko ya wanazuoni wa Madhehebu manne kuhusu ruhusa ya kufunua uso wa mwanamke nje ya Swala:

Imamu Al-Mirghnaniy mfuasi wa Hanafiy amesema katika Al-Hidaya: “Mwili mzima wa mwanamke huru ni uchi isipokuwa uso wake na viganja vyake” [25].

Sheikh Ad-Dardir amesema katika Ash-Sharh Al-Kabir miongoni mwa vitabu vya Malikiy: “(Na) ni - sehemu za siri - za mwanamke huru (mbele ya) mwanamume (wa mbali) Muislamu ni mwili wake wote (isipokuwa uso na viganja)”  [26].

Imepokewa katika Asna Al-Matalib miongoni mwa vitabu vya Imamu Shafi na Sheikh Al-Islam Zakariya Al-Ansariy: “(Uchi wa mwanamke huru wakati wa Swala na mbele ya asiye Mahram) hata nje yake ni mwili wake wote isipokuwa uso na viganja)” [27].

Al-Mardawiy mfuasi wa Imamu Hanbaliy amesema katika Al-Insaf: “Mtazamo sahihi wa Madhehebu ni kwamba uso si sehemu ya siri, nayo ni maoni ya wanazuoni .. kuhusu viganja kuna mapokezi mawili” [28].

Huu ni upamambanuzi katika  kutaja wanazuoni miongoni gani anawajibisha kufunika uso:

Miongoni mwa wanazuoni ni wale waliotofautisha baina ya sehemu za siri za kutazama mwanamke - yaani nje ya Swala - na sehemu za siri ndani ya Swala. Wanazuoni wa sasa ambao wafuasi wa Imamu Shafi na Hanbali waliona kuwa ni wajibu kusitiri mwili mzima wa mwanamke, ikiwa ni pamoja na uso wake na viganja vyake - nje ya swala - na hivi ndivyo ilivyopokewa kutoka kwa Abu Bakr Ibn Abdir-Rahman at-Tabiiy.

Katika Al-Iqnaa fi Hall Alfadh Abi Shujaa cha Al-Khatib Ash-Shirbiniy, miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Imamu Shafi, anapozungumzia masharti ya Swala, akitaja kufunika sehemu za siri na akasema: “Sehemu za siri ya mwanamke huru ni visivyokuwa uso na viganja, nje yake na ndani hadi kwenye vilimbilimbia vya mkono”. Sheikh Al-Bujayrimiy katika Hashiya yake alielezea kauli yake (sehemu za siri za mwanamke aliye huru), akisema: “Yaani wakati wa kuswali. Ama sehemu zake za siri nje ya Swala, kuhusiana na mtu wa mbali kumtazama, ni mwili wake wote, hata uso na viganja, hata ikiwa kusalimika na fitna” [29].

Katika Sharh Ibn Al-Qasim Li Mtan Abi Shujaa katika Fiqhi ya Imamu Shafi: "Sehemu za siri za mwanamke aliye huru wakati wa Swala ni usio kuwa uso wake na viganja vyake, nje na ndani hadi vilimbilimbi vya mkono, ama sehemu za siri za mwanamke aliye huru nje ya Swala, ni mwili wake wote”. Sheikh Al-Baijuriy alitoa maelezo yake kuhusu hilo akisema: “Yaani mbele ya watu wa mbali” [30].

Sheikh Mansur Al-Bahutiy mfuasi wa Hanbaliy amesema katika Kashaf Al-Qinaa: “viganja (na uso) wa mwanamke huru aliye baleghe ni (sehemu zake za siri nje ya Swala (kuzingatia kutazama kama vile sehemu nyingine za mwili wake)” [31].

Huuu ni upamabanuzi  kuhusu ushahidi wa wale wanaowajibisha kufunika uso na majadiliano yake:

Wale ambao waliwajibisha wanawake kufunika nyuso zao - katika nyakati za zamani na za kisasa - walitaja yafuatayo:

Kwanza: Ushahidi kutoka katika Qur`ani:

Dalili ya kwanza:

Kauli yake Mwenyezi Mtukufu: {Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao}. [Al Ahzab: 53].

Sehemu ya ushahidi wa Aya juu ya ulazima wa kusitiri uso ni kuwa, hata kama iliteremshwa Aya kuhusu wake za Mtume SAW, Mama wa Waumini, basi lililo muhimu ni ujumla wa maneno, siyo sababu maalumu, na kwamba ikiwa wake za Mtume S.A.W,  wameamrishwa kufunika nyuso zao, basi wanawake wengine wa umma wameamrishwa hivyo hivyo. Zimepokewa nukuu za Wafasiri ambazo zinaonesha ulazima wa kujisitiri.

Abu Jaafar at-Tabariy amesema: “Na wauliza jambo wake za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W, na wanawake wa Waumini ambao si wake zenu, basi waulizeni nyuma ya pazia baina yenu na wao, na kuwauliza kwenu nyuma ya pazia ni safi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao kuliko athari za uovu zilizomo ndani ya vifua vya wanaume juu ya wanawake, na katika vifua vya wanawake juu ya wanaume, na ni dhahiri zaidi kwamba Shetani hatakuwa na njia juu yenu wala juu yao” [32].

Ibn Kathir amesema: “Kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia} maana yake: Na kama nilivyokukatazeni msiiwaingie ndani kwao, vivyo hivyo msiwatazame hata kidogo, na kama mmoja wenu anayotaka haja kuchukua kutoka kwao, asiwatazame, na wala asiwaombe haja ila kwa nyuma ya pazia” [33].[34]

Hili linaweza kujadiliwa kwamba Maimamu wote wawili Ibn Jarir At-Tabariy na al-Qurtubiy wamesema kuwa si wajibu kufunika uso katika kufasiri Aya ya Surat An-Nur: {isipo kuwa unao dhihirika} - kama ilivyotajwa hapo juu - hii inaweza kufasiriwa kuwa ni kusahau, au ikafasiriwa katika kile ambacho Aya hii ni maalumu kwa Mama wa Waumini na ambayo Surat An-Nur ni kwa ujumla kwa wanawake wa umma.

Aya hii ni maalumu kwa Mama wa Waumini, na anayesema kuwa mazingatio ni ujumla wa neno, basi kwanza athibitishe kuwa maneno hayo ni ya jumla katika kauli yake Mwenyezi: {Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia} [Al-Ahzab: 53] ili ipate kujumlishwa kwa wanawake katika Umma, basi tamko katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mnapo wauliza} ni maalumu kwa wake za Mtume SAW, na muktadha wa ushahidi katika Aya haujumuishi maneno yoyote ya jumla yaliyoainishwa katika vitabu vya Usuli.

Pamoja na hayo hapo juu, kuna Hadithi katika Sahihi Bukhariy inayoashiria kuwa kufunika (uso) ni wajibu kwa Mama wa Waumini. Kutoka kwa Anas RA,amesema: Mtume SAW, alikaa baina ya Khaybar na Madina kwa siku tatu, kwa ajili ya kumuoa mama Safiyya, hivyo nikawaalika Waislamu kwenye karamu yake, na hapakuwa na mkate wala nyama ndani yake, lililotokea alimuaru Bilal aitandaze mikeka, akaweka tende kavu, maziwa yaliyokaushwa, na samli, kisha Waislamu wakasema: “Je Bibi Harusi ni mmoja wa Mama wa Waumini, au mjakazi? Wakasema: Akimsitiri basi huyo ni katika Mama wa Waumini, na asipomfunika basi huyo ni mjakazi. Alipoondoka alitayarisha kipando kwa ajili yake, na akatandaza pazia [35].

Al-Hakim amesema: Makhlad Ibn Jaafar Al-Baqarhiy aliniambia, Muhammad Ibn Jarir amesem: Abu Ubaidah Maamar Ibn Al-Muthanna amesema: Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. wakati ulipofika Wajumbe kutoka wa Kinda ulipofika, akamuoa Qutailah binti Qays, dada wa Al-Ashath Ibn Qays, katika mwaka wa kumi, kisha akaugua katikati ya Mfungo tano, kisha akafa siku ya Jumatatu, siku mbili zilizopita katika Mfungo sita. na hakuwa amemfikia wala kumuingilia.

Baadhi yao waliweka wakati wa kumuoa, hivyo walidai kuwa alimuoa mwezi mmoja kabla ya kifo chake, na wengine walidai kuwa amemuoa wakati wa maradhi yake, na wengine walidai kuwa alipendekeza ampe Qutailah hiari kuolewa na anayemtaka, basi akachagua kuolewa, basi akamwozesha kwa Ikrimah bin Abi Jahl katika Hadhramaut. Abu Bakr alipojulishwa aksema: Nilikuwa karibu kuwachoma moto, basi Umar Ibn Al-Khattab akasema: Yeye si katika Mama wa Waumini, na Mtume S.A.W, hakumuingilia, wala hakuweka pazia juu yake, na baadhi yao walidai kuwa ameritadi [36].

Iwapo wale wanaokataza kufunua (uso) watasema: Na tukiwakubalia  kuwa maneno hapa ni maalumu kwa wanawake wa Mtume SAW, na kwamba wameamrishwa kuvaa Hijabu, na kwamba wao ni watakatifu na wasafi. basi si wanawake wengine wa umma hawanastahiki zaidi haya kuliko wao? Tunasema: Hili linajadiliwa katika njia mbili:-

Kwanza: Mambo yanayohusu Wake  wa  Mtume S.A.W, yanasisitizwaa mno kuliko wengine. Na mwenyezi alisema: {Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine}[Al-Ahzab: 32].

Pili: Kama ingekuwa hivyo, sisi Waislamu kwa ujumla tungedaiwa majukumu zaidi kuliko Mtume S.A.W;  kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu amemsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yajayo, pamoja na kuhifadhiwa kwake na madhambai Mtume S.A.W, , na sisi tumekabiliwa na madhambi na adhabu, lakini tumegundua kuwa Yeye S.A.W, aliteuliwa kwa ajili ya majukumu ambayo ni magumu na yenye shida zaidi kuliko yale waliyoyapata Waislamu wengine, kama vile kuswali Swala ya Usiku kwa mfano.

Dalili ya pili:

Kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na owazilinde tupu zao, wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo husu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa}. [An-Nuur: 31] [37].

Maana ya Aya hii kuhusu ulazima wa Hijabu ya mwanamke mbele ya wanaume wasiokuwa Mahram imeelezwa kwa njia zifuatazo:

Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamrisha Waumini wanawake kuzilinda tupu zao, na amri ya kuzilinda tupu zao ni amri ya kufanya hivyo na ni njia ya kufikia hilo, na mwenye akili hana shaka kuwa moja ya njia zake ni kufunika uso; kwa sababu kuufunua ni sababu ya kumtazama, kutafakari uzuri wake, na kufurahia hilo, na hivyo kufikia na kuwasiliana. Katika Hadithi: “Macho yanazini kwa njia ya kutazama” mpaka akasema: “tupu inathibitisha hilo au ikanushe” [38]. Ikiwa kufunika uso ni njia ya kuhifadhi tupu, inaamrishwa kufanya hivyo, kwa sababu njia zina hukumu sawa na malengo [39].

Haya yanajadiliwa kwa kusema: kuinamisha macho kumeamrishwa kwa wanaume na wanawake sawa sawa, na kufunika uso wa mwanamke hakuna kitu kinachomzuia kumtazama mwanamume, hata hivyo wanaume hawakuamrishwa kufunika nyuso zao, na kama vile uso wa mwanamke ni fitina kwa mwanamume, vivyo hivyo uso wa mwanamume ni fitina kwa mwanamke. Kisha tunauliza: Je, zinaa kwa macho ni ya mwanaume kumtazama mwanamke pekee, au ni mwanaume kumtazama mwanamke, na pia mwanamke kumtazama mwanaume? Je, mwanamume mzuri, aliyepambika vizuri anapaswa kufunika uso wake kwa hofu ya wanawake kufitiniwa naye? Ikiwa utamlazimu mwanamke kufunika uso wake ili kulinda sehemu za siri za mwanamume, basi pia unamlazimu mwanamume kufunika uso wake ili kulinda sehemu za siri za mwanamke; kwa kuwa sababu ni moja, na ikiwa sharti halisihi basi hukumu haisihi pia, Na ikiwa mnalazimisha kufunika kwa wanawake lakini si wanaume, hii ni kupingana wazi; kwa sababu amri ya kulinda sehemu za siri ni kwa wanaume na wanawake wote.

kauli yake mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao}. Shungi ni kile ambacho mwanamke hufunika kichwa chake kama vile Hijabu, ikiwa ameamrishwa kuvaa cha kusitiri juu ya kifua chake, basi ameamrishwa kufunika uso wake, ama kwa sababu ni lazima kufanya hivyo, au kwa kipimo cha  uwiano (Qiyas); na ikiwa ni wajibu kufunika kifua na shingo, basi kufunika  ni bora zaidi, kwa sababu ni mahali pa uzuri na fitina. Watu ambao wanahitaji uzuri wa picha huuliza tu uzuri wa uso, ikiwa ni mzuri, hawaangalii kitu kingine chochote kutokana na umuhimu. Kwa hiyo, ikiwa wanasema kwamba fulani ni mzuri, hakuna kitu kinachoeleweka kutoka kwa maneno haya isipokuwa uzuri wa uso, kwa hiyo inakuwa wazi kwamba uso ni mahali pa uzuri unaotafutwa kwa kweli. Ikiwa ndio hivyo basi vipi inaweza kueleweka kwamba Sharia hii yenye hekima inaamuru kufunika kifua na shingo, kisha inaruhusu kufunuliwa uso [40].

Hili linajibiwa kuwa kuweka kuweka kitambaa kifuani hakulazimu kufunika uso, kwani katika lugha Khimar (kitambaa): kitambaa cha cha mwanamke: ni kile kinachositiri ambacho mwanamke hufunika kichwa chake [41]. Kwa hiyo, kuweka kitambaa ni kifuani wala  si kwenye uso.

Wanazuoni wa Tafsiri wamesema: Kilemba ni kinachoofunika kichwa, na kifua ni sehemu iliyo wazi juu  ya shati ambalo baadhi ya mwili huonekana. Maana yake ni: Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaamrisha Waumini wanawake kufunika mahali pa  vifuani kwa kinachositiri ili isionekane, na wanawake walikuwa wakifunika vichwa vyao kwa kinachositiri na kuinamisha nyuma ya migongo yao, kama walivyokuwa kabla ya Uislamu, hata mahali pa ufunguzi wa shati na baadhi ya vifua vyao vikaonekana. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu, Akawaamrisha kufanya hivyo ili kwenda kinyume na mila za wanawake wa zama za Jahiliya, kwani walikuwa hawafanyi hivyo [42].

Vile vile vinavyoashiria usahihi wa tafsiri ya shungi kuwa ni kitu ambacho kichwa kimefunikwa nacho ni yale yaliyopokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W, kuwa amesema: “Mwenyezi Mungu hakubali Swala ya mwanamke baleghe isipokuwa kwa Hijabu” [43], pamoja na makubaliano ya Wanazuoni kuhusu usahihi wa Swala ya mwanamke huku akiwa amefunua uso wake, kwani maana ya Hijabu ni sawa ndani ya Swala na nje yake.

Kisha kama amri ya kufunika uso kama ingehitajika kwa makusudi, basi Aya ingeiweka bayana.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amekataza kabisa kuonesha mapambo isipokuwa yanayodhihirika, ambayo ni ya kuonekana kwa kawaida, kama vile nguo, na kwa ajili hiyo akasema: {isipo kuwa unao dhahirika} na hakusema ila yale wanayodhahirisha. Kisha akakataza tena kujipamba isipokuwa kwa wale Aliowatenga, kwa hivyo hii inaashiria kuwa pambo la pili ni tofauti na pambo la kwanza.

Pambo la kwanza ni pambo la nje linalodhihirika kwa kila mtu na haliwezi kufichika, na pambo la pili ni pambo lililofichika analojipamba nalo, na lau kuwa pambo hili lingeruhusiwa kwa kila mtu, basi kujumlisha katika la kwanza na kutenga katika la pili hakuna faida yoyote inayojulikana [44].

Hili linajibiwa kuwa tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo: {isipo kuwa unao dhihirika} kwa maana ya nguo si sahihi kwa yafuatayo:

Kwanza: Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema katika Aya: {Isipo kuwa unao dhihirika} na hakusema: isipokuwa kile kilicho dhahiri, na kuna tofauti kubwa kati mawili hayo, lau kilichokusudiwa ni mavazi, Aya hiyo ingesema: isipokuwa yale yanayodhihirika. Ama neno “kudhihirika” lina maana ya kuonekana kwa kitu baada ya kufichika. Ibn Mandhur katika Al-Lisaan anaserma: “kuhdhihirika maana yake: kuonekana bila ya kufichika” [45], kwa hiyo kinachokusudiwa si nguo; kwa sababu ni dhahiri na haiwezi kufichwa, ama mahali pa mapambo inaweza kufichwa.

Pili: Kuvua katika Aya: {isipo kuwa unao dhihirika} baada ya kukatazwa kuonyesha mapambo, inaashiria aina ya ruhusa na wepesi, na kuonekana kwa nguo ya nje hakumaanishi ruhusa yoyote au kuondolewa aibu; kwa sababu kuonekana kwake ni wa dharura hakuna namna.

Tatu: Tunakiri kuwa pambo la pili ni tofauti na pambo la kwanza. La kwanza ni pambo la nje linalodhihirika kwa kila mtu na haliwezi kufichika, na la pili ni pambo lililofichika ambalo anajipamba nalo. Na lau pambo hili lingeruhusiwa kwa kila mtu, basi kujumlisha katika la kwanza na kutenga katika la pili haikuwa na faida inayojulikana, lakini hatukubali kwamba uso na mikono sio miongoni mwa mapambo ya kwanza, bali  sahihi ni kama ilivyoelezwa kwa ushahidi wetu.

Mwenyezi Mungu Ameruhusu kuoneshwa pambo la ndani kwa wafuasi wa kiume ambao hawana nasaba katika wanaume, yaani watumishi wasio na matamanio, na kwa mtoto mdogo ambaye hajafikia umri wa matamanio na hajaoneshwa sehemu za siri za wanawake, na hii inaashiria mambo mawili:

Moja: Haijuzu kwa mwanaume wa kando yeyote kuoneshwa pambo lililofichika isipokuwa aina hizi mbili.

Pili: Sababu na msingi wa hukumu ni kuogopa kufitina na mwanamke kushikamana naye, na hapanashaka kuwa uso ni sehemu kuu ya uzuri na pahali pa fitina, hivyo kuufunika ni wajibu ili wanaume wenye hamu ya wasifitinike[46].

Hili linajibiwa kwa kusema: hatukubali kuwa uso na viganja ni mapambo ya ndani, bali ni mapambo ya nje ambayo kuna uzito kwa mwanamke kuyaficha. Kama ilivyotajwa katika ushahidi wetu, katika kueleza maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu: {isipo kuwa unao dhihirika}.

At-Tahir Ibn Ashur amesema: “Wafasiri wote walieleza mapambo ya mwili mzima, na wakaeleza yale yanayodhihirika kuwa ni uso na viganja, na ikasemwa: pia miguu, na nywele. Kwa mujibu wa tafsiri hii, pambo la dhahiri ni lile ambalo Mwenyezi Mungu amelifanya lionekane kimaumbile, na kufichwa kwake kunazuia manufaa yake au kumsababishia mwanamke shida, na hilo ni uso na viganja, na wanazuoni wengi wa wanaona kuwa kuvua kudhihirisha uso na viganja vya mikono kunaingia katika katazo la kudhirisha mapamabo kunakolazimu uhalali wa kudhihirisha uso na viganja katika hali zote, kwa sababu suala ni kwamba kilichovuliwa ni hali zote za zilizovuliwa nayo [47].

Ibn Al-Arabiy mfuasi wa Malikiy amesema: “Kuna maoni matatu kuhusu mapambo ya dhahiri:

Kwanza: Kwamba nguo, ina maana kwamba nguo zao zinaonekana kwao hasa. Na Ibn Masuud alisema hivi.

Pili: Wanja na pete; Haya yamesemwa na Ibn Abbas na Al-Miswar.

Tatu: Ni uso na viganja. Na hii ni maana ile ile ya kauli ya pili, kwa sababu wanja na pete zinahusiana na uso na viganja, isipokuwa huelezwa kwa maana nyingine, ambayo ni kwamba mwenye kuona uso na viganja ni mapambo ya dhahiri  anasema hivyo maadam hakuna wanja au pete juu yake, na ikiwa kuna wanja na pete, basi lazima zifichwe, na zinakuwa miongoni mwa pambo la ndani. Na pambo la ndani ni kama vile: hereni, mkufu, bangili ya mkono, na bangili ya mguu (kikuku) , na mengineyo [48].

Abu Bakr Al-Jassas alijibu kauli ya Ibn Masuud kwamba kilichodhihirika kwake ni nguo: kwamba haikuwa na maana; kwa sababu inajulikana kuwa alitaja pambo na kinachokusudiwa ni kiungo ambacho pambo hilo huvaliwa juu yake, Je, huoni kwamba inajuzu kwake kuwaonyesha wanaume mapambo yote, kama vile vito na bangili, kikuku na mkufu [49] ikiwa hajayavaa? Basi tunajua kuwa kinachokusudiwa ni mahali pa pambo, kama alivyosema katika muktadha wa usomaji baada ya haya: {wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao} na kinachokusudiwa ni mahali pa pambo, hivyo kufasiri kwa maana ya nguo haina maana; Anaziona nguo alizokuwa amevaa bila sehemu yoyote ya mwili wake, kama vile anavyomwona kama hajavaa.

Ama kauli ya kuwa sababu ya hukumu na zunguko zake ni juu ya hofu ya kufitiniwa kwa mwanamke na kushikamana naye, hapana shaka kuwa uso ni sehemu ya uzuri na pahali pa fitina, hivyo ni wajibu ufunikwe ili wanaume wanaopenda sana wanawake wasijekufitiniwa nao.

Hili linanajadiliwa kuwa haioneshi kwamba mwanamke lazima afunika uso wake; kwa sababu yote haya yanahusu sababu ambayo wanaume na wanawake wako sawa.

Kauli yake mwenyezi Mungu Mtukufu: {Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyo yaficha.}.

Hii ina maana kwamba mwanamke asipige mguu wake, ili bangili za miguu alizozificha au mfano wa hivyo katika kile alichovaa kwa mwanamume. Ikiwa mwanamke amekatazwa kupiga miguu yake kwa kuhofia mwanamume kufitiniwa kwa yale anayoyasikia, kama sauti ya bangili za miguu yake na mengineyo, basi vipi kufunua uso?

Ni fitna ipi kubwa kwa mwanamume kusikia sauti ya bangili za mguu wa mwanamke na hajui ni mtu gani au ana uzuri wa kiasi gani?! hajui kama ni kijana au mzee?! na hajui ni mbaya au mrembo?! Ni kishawishi gani kikubwa zaidi, hiki au kutazama sura nzuri, isiyofunikwa, iliyojaa ujana, uchangamfu, urembo, na uzuri unaoleta fitna na utamanisha kuutazama?! Kila mwanaume anaependa sana wanawake ili kujua ni vishawishi gani kati ya viwili hivyo ni vikubwa na vinavyostahiki zaidi kusitiri na kufichwa [50].

Hii linajadiliwa kuwa ni kipimo cha uwiano kisicho sawa; maana tuliamrishwa kuinamisha macho, lakini hatukuamrishwa kuziba masikio, na zaidi ya hayo sababu iliyotajwa hapo juu inashirikisha wanaume na wanawake, basi ni ipi sababu ya kuwahusisha wanawake tu  bila ya wanaume?

Dalili ya tatu:

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: {Na wanawake wazee wasio taraji kuolewa, si vibaya kwao kupunguza nguo zao, bila ya kujishaua kwa mapambo. Na wakijihishimu ni bora kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua}. [An Nuur: 60].

Ushahidi wa Aya hii tukufu ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliondoa dhambi za wanawake wasio na uwezo na wasio na matumaini ya kuolewa kwa sababu wanaume hawazitamani kutokana na uzee wao. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameondoa dhambi kwa wakongwe hawa wapunguze nguo zao kwa sharti kuwa lengo lao sio kudhihirisha mapambo. Inafahamika wazi kuwa kinachomaanishwa kwa kupunguza nguo si kubaki uchi, bali kinachokusudiwa ni kupunguza nguo zilizo juu ya gauni na mfano wa hayo, ambazo hazifuniki kile kinachoonekana kwa kawaida, kama vile uso na viganja. Nguo zilizotajwa hapo juu ambazo wanawake hawa wazee wanaruhusiwa kuzipunguza ni nguo za awali zinazofunika mwili mzima. Kuhusisha  hukumu kwa wanawake wakongwe hao ni ushahidi kwamba vijana wanaotarajia kuolewa wanatofautiana nao katika hukumu hiyo, na lau hukumu hiyo ni ingekuwa inajumuisha  wanawake wote katika uhalali wa kupunguza nguo, kuvaa gauni na mengineyo, basi kutenga kanuni maalum ya wanawake wazee isingekuwa na faida yeyote.

Na katika kauli yake Mola Mtukufu: {bila ya kujishaua kwa mapambo}. Kuna ushahidi mwingine kwamba Hijabu ni wajibu kwa msichana anayetarajia kuolewa; kwa sababu ni kawaida sana, ikiwa atafunua uso wake, anataka kuonesha mapambo na kuonesha uzuri wake, na wanaume watamtazama na kumsifu, na kadhalika, na kitu kingine chochote isipokuwa haya ni nadra, na nadra haina hukumu [51].

Hili linajibiwa kuwa Aya hii haikutaja kufunika au kufunua uso, achilia mbali kuwa ni ushahidi unaofaa juu ya wajibu wa kuufunika, bali inazungumzia jambo jingine ambalo matokeo yake ni: si wajibu kwa wanawake wazee kuvaa baibui, na maana ya mavazi hapa ni baibui na ni tafsiri iliyopokelewa kutoka kwa baadhi ya Masahaba, kama Ibn Abbas na Ibn Masuud RA. Abu Jaafar At-Tabariy amepokea kutoka kwa Ibn Abbas akisema: kauli yake Mwenyezi {Na wanawake wazee wasio taraji kuolewa} ni mwanamake ambaye hakuna ubaya kwake akikaa nyumbani kwake akiwa amevaa gauni na mtandio, na akapunguza baibui  ikiwa tu hajadhihirisha yale anayoyachukia Mwenyezi Mungu. Na imepokewa pia kutoka kwa Abdullah katika kauli yake: {si vibaya kwao kupunguza nguo zao} Akasema: yaani baibui au kilemba cha kufunika kifuani [52].

baibui ni nguo pana kuliko mtandio, na ndogo kuliko kilemba, ambacho mwanamke hufunika kichwa chake na kifua chake , na ikasemwa kuwa ni nguo pana na ndogo kuliko kanga ambayo mwanamke anaivaa, na ikasemwa: ni kanga [53].

Dalili ya nne:

Kauli yake Mwenyezi: {Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}. [Al Ahzab: 59].

Ibn Abbas R.. A, amesema: “Mwenyezi Mungu amewaamrisha wanawake wa waumini, pindi wanapotoka majumbani mwao wakiwa na haja, wafunike nyuso zao juu ya vichwa vyao kwa baibui na wadhihirishe jicho moja” [54]. Tafsiri ya Sahaba ni hoja, na baadhi ya wanazuoni wakasema hata kuwa ni katika hukumu iliyonasibishwa kwa Mtume S. A. W, na kauli yake R. A: “Na hudhihirisha jicho moja”. iliruhusiwa tu kwa ajili ya umuhimu na haja ya kuona barabara, lakini ikiwa siyo lazima, basi hakuna sababu ya kudhihirisha jicho.

baibui ni vazi kubwa kuliko mtandio , sawa na joho. Ummu Salamah R. A, ilipoteremka Aya hii alisema: “Wakatoka wanawake wa Ansaar kama kwamba juu ya vichwa vyao kuna kunguru, kutokana na utulivu, na wamevaa nguo nyeusi” [55]. Ubaidah As-Salamaniy na wengineo walisema kuwa wanawake wa Waumini walikuwa wakishusha baibui zao juu ya vichwa vyao ili macho yao tu yaonekane ili kuona njia [56].

Hii linajadiliwa kama ifuatavyo:

Kwanza: Kutolea ushahidi Hadithi ya Ibn Abbas kuhusu kufunika uso sio sahihi; kwa sababu ni dhaifu, imepokewa na Ali Ibn Abi Talha kutoka kwa Ibn Abbas, na huyu Ali alizungumziwa na Imam Ahmad [57], na kupokea kwake na Ibn Abbas ni Mursal [58].

Ikiwa tutakubali usahihi wa pokezi huu, basi maneno ya Masahaba sio hoja kwa yale yanayosemwa na ijtihadi halisi; kwa sababu mwenye jitihada anaweza kukosea, na haijathibiti kwamba Masahaba waliwajibisha wengine kufuata kauli zao, na daraja la usahaba hata ikiwa ni heshima kubwa, haimfanyi mmiliki wake kuwa wamelindwa kutokana na kukosa [59].

Tukichukulia kuwa kauli ya Sahaba ni hoja, imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas mwenyewe na Masahaba wengine watukufu R. A, kinyume cha ilivyoelezwa kutoka kwake hapa, kama ilivyoelezwa katika ushahidi wetu wa kuruhusu kufunua kwenye Aya ya Surat An Nuur, ambayo ndiyo aliyoithibitisha Imam At-Tabariy.

Pili: Hoja ya Sheikh inayoegemezwa kwenye pokezi la Ubaidah As-Salamaniy si sahihi, kwani pokezi hili ambalo amelipokea As-Suyutiy katika Ad-Dur Al-Manthur  nayo ni dhaifu [60]; kwa sababu ni Maqtuu’ na Ubaidah As-Salamanii ni Tabiina kwa makubaliano ya wengi, kwa hivyo hakuna hoja kwake.

Tukichukulia pokezi hili, basi hakuna ushahidi katika maneno ya Ubaidah As-Salmaniy. Kwani ni rai yake tu na tafsiri yake ya Aya, au ni habari yake kuhusu ukweli wa wanawake katika zama hizi na si zaidi ya hayo.

Tatu: Maana ya baibui haioneshi kuwa ni kifuniko cha uso - kama ilivyotajwa hapo juu.

Dalili ya tano:

Kauli yake mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu. }. [Al Ahzab: 55].

Ibn Kathir, Mungu amrehemu, amesema: “Mwenyezi Mungu alipowaamrisha wanawake kujisitiri mbele ya wanaume wa kando, alibainisha wazi kuwa ndugu wa karibu  si wajibu kujistiri mbele yao, kama alivyowatenga katika Surt An-Nuur, pale Mwenyezi Mungu aliposema: {wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao}.. Aya [61].[62]Hii inajadiliwa kuwa muktadha wa Aya unahusu Mama wa Waumini, na wala haiashirii uwajibibikaji wa kusitiri uso, kwa hivyo maana kuu ya jambo hilo ni kujisitiri ni mbele ya wanaume wa kando, na kwamba ndugu wa karibu waliotajwa katika Aya wamevuliwa katika hilo - na hili liko nje ya wigo wa mzozo.

Pili: Ushahidi kutoka katika Hadithi:

Dalili ya kwanza:

Kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S. A. W, amesema: “Mmoja wenu akimchumbia mwanamke, akiweza kuangalia kile kitakachomfanya aoe afanye hivyo” Akasema: Basi nikamchumbia kijakazi na ninajificha mpaka nikaona kinachonifanya nimuoe, nikamwoa  [63].

Ushahidi katika hadithi hii ni kuwa Mtume S. A. W, aliondoa dhambi ya mchumba hasa akimwangalia mchumba wake kwa sharti ya kuwa utazamaji wake ni kwa ajili ya kumchumba, na hii inaashiria kuwa asiye mchumba ni mwenye dhambi kwa kumwangalia mwanamke wa kando kwa vyovyote vile, na mchumba vile vile akiangalia kitu kingine zaidi ya uchumba, kama vile lengo lake ni Kutafuta raha, starehe na kadhalika [64].

Hii inajadiliwa kuwa hakuna kitu ndani yake kinachoashiria ulazima wa kufunika uso, bali ndani yake kile kinachoashiria kuwa inajuzu kwa mchumba kumwangalia anayetaka kumchumbia, kisha hakuna maandishi ndani yake kwamba autazame uso wa mchumba tu hasa; kwa sababu utazamaji katika Hadithi umeachwa uwazi na wala hakubainishwa, na Hadithi zinazohusu kumwangalia mchumba zimeachwa wazi na hazielezi kiwango cha mchumba kumtazama mchumba wake, kwa hivyo tunaona kuwa kauli za wanazuoni zinahitilafiana katika kiwango cha kumtazama mchumba, na hii haimaanishi kuwa ni wajibu kwa mwanamke kufunika uso wake katika hali ya jumla.

Dalili ya pili:

Mtume S. A. W, alipoamrisha wanawake watoke kwenye kiwanja cha Swala ya Idi, walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mmoja wetu hana baibui, Mtume S. A. W akasema: “Dada yake amvalisha katika baibui lake” [65]. Hadithi hii inaashiria kwamba ilikuwa ni desturi ya wanawake wa Masahaba, mwanamke hatoki nje isipokuwa kwa baiubui, na kwamba bila hivyo hawezi kutoka.

Kwa hiyo wanawake hawa R. A, wakataja kizuizi hicho cha Mtume wa Mwenyezi Mungu S. A. W,   , alipowaamrisha watoke kwenda kiwanja cha Swala ya Idi, akawabainishia utatuzi wa tatizo hili kuwa dada yake amvalishe baibui lake, na kutowaruhusu kutoka nje bila baibui, ijapokuwa kutoka nje kwenda kiwanja cha Sala ya Idi inajuzu na imeamrishwa kwa wanaume na wanawake. Ikiwa Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, hakuwaruhusu watoke nje bila baibui kwa yale maamrisho, basi angewapaje ruhusa ya kuacha baibui kwa ajili ya kutoka nje kwa yasiyo maamrisho wala hayahitajiki?! Bali ni kuzunguka sokoni, kuchanganyika na wanaume, na kutazama tu, jambo ambalo ni bure. Amri ya kuvaa baibui ni ushahidi kwamba ni lazima kujifunika uso [66].

Hii linajibiwa kuwa hakuna ushahidi kwamba ni wajibu kufunika uso; kwa sababu maana ya baibui, kama ilivyotajwa hapo awali, siyo kwamba inafunika uso, bali ni kwamba mwanamke hufunika kichwa chake, mgongo na kifua chake.

Dalili ya tatu:

Ilivyopokewa kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha R. A, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu S. A. W, alikuwa akisali Swala ya Alfajiri na wanawake wa Waumini waliswali naye, wakiwa wamejifunika na nguo zao, kisha wanarejea majumbani mwao, na hakuna yeyote atakayewatambua kutoka.na na giza, akasema Aisha: Lau kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S. A. W, angeliona tuliyoyaona , basi angeliwazuia kuja katika misikitini, kama vile Wana wa Israili walivyowakataza wanawake wao [67], na hadithi kama hii hiki kimepokelewa na Abdullah Ibn Masuud RA.

Ushahidi wa Hadithi hii una mambo mawili:

Moja wao: Hijabu na kufunika ilikuwa ni desturi ya wanawake wa Masahaba ambao walikuwa zama bora zaidi na  watukufu zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, walikuwa wana wa maadili na adabu na wakamilifu zaidi katika imani, na bora zaidi katika ibada, walikuwa ni mfano wa kuigwa na Mwenyezi Mungu awawie radhi, na wale waliowafuata kwa wema, basi ikiwa hii ndiyo njia ya wanawake wa Masahabah, basi vipi sisi kuiacha njia hiyo, ambayo katika kuifuata kuna wema na radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ya pili: Mama wa Waumini Aisha na Abdullah bin Masuud R. A, na bila kusahau elimu yao, elimu ya Fiqhi, utambuzi wa dini ya Mwenyezi Mungu, na nasaha kwa waja wa Mwenyezi Mungu, walisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S. A. W,  angewaona wanawake walichokiona, angewazuia wasiende misikitini, na hii ilikuwa katika zama za karne zilizopendelewa, hali ilibadilika si hali ya zama za Mtume S.A.W., kwa kadiri inahitajika kupigwa marufuku kwenda misikitini. Basi vipi kuhusu zama zetu, wakati jambo limepanuka, staha imepungua, na dini imedhoofika katika nyoyo za watu wengi?! [68].

Hili linajibiwa kuwa haifai kutolewa ushahidi kwa uwajibikaji wa kufunika uso, kwani hakuna chochote ndani yake kinachoonyesha kufunika au kufunua, bali ni maelezo ya desturi ya wanawake wa wakati huo, ingawa hatukubali kwamba walikuwa wamefunika nyuso zao kwa sababu zifuatazo:

Kwanza: Kauli ya Bibi Aisha RA: (wanawake waliovaa nguo zao) maana yake ni: kufunikwa, na kujisitiri pamoja na kufunika kichwa, na huenda ikaja kwa maana ya kufunika kichwa [69].

Pili: Kauli ya Bibi Aisha RA: (Hakuna anayewatambua kutokana na giza) - mabaki ya giza la usiku - maana yake: Hawajulikani kuwa ni wanawake wala wanaume, ndiyo inayoonekana kwa mtazamaji kama kwamba mizimu hasa, kama alivyopokea Al-Hafidh Ibn Hajar kutoka kwa Ad-Dawudiy [70]. Inaashiria kuwa kinachowazuia kutambulika ni mabaki ya giza, sio kwamba wanafunika nyuso zao, Na lau Bibi Aisha RA, angetaka kusema maana hii angeibainisha.

Tatu: Kuna pokezi lingine ambalo ndani yake ilielezwa kuwa utambuzi unaohusu  nyuso hasa, si utambuzi kwa jumla; Abu Ya`la amepokea katika Musnad yake kwa Isnad Sahihi ya upokezaji, kutoka kwa Mama wa Waumini Aisha RA, kwamba alisema: Ikiwa Mtume wa Mungu SAW, lau angewaona wanawake kama tunavyowaona, angewazuia wasiende misikitini kama walivyokataza Wana wa Israili wanawake wao. Tulikuwa tukisali Sala ya Alfajiri pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW, katika nguo zetu, kisha tukaondoka huku tukiwa hatutambuani nyuso [71].

Ikiwa tunakubali kuwa walikuwa wamefunika nyuso zao, basi kinachoashiria hii ni kuruhusiwa kufunika, sio uwajibikaji.

Dalili ya nne:

Amesema Mtume S. A. W: “Mwenye kuburuza nguo zake kwa kiburi, Mwenyezi Mungu hatamtazama siku ya Kiyama. Ummu Salamah akasema: Wanawake wanafanyaje na nguo zao ndefu? Akasema: “Ishushe kwa inchi moja.” Alisema basi miguu yao itakuwa wazi. Akasema: “Ishushe iwe ndefu kiasi cha dhiraa moja na wasiiongezee zaidi yake” [72]. Hadithi hii ina ushahidi wa uwajibikaji wa kufunika miguu ya mwanamke, na kwamba ni jambo linalojulikana sana miongoni mwa wanawake wa Masahabah R. A, na mguu bila shaka hauna fitina mfano wa uso na viganja. Kutahadharisha kilicho chini ni kutahadharisha kilicho juu yake na kinachostahiki zaidi yake kihukumu, na hekima ya Sharia inakataa kuwajibisha kufunika yale ambayo ni fitina ndogo na kuruhusu kufichua iliyo fitina kubwa kuliko hayo, kwani huu ni mgongano na haiwezekani kwa hekima ya Mungu na Sharia yake [73]. Hili linajibiwa kuwa tunakubali kuwa miguu ya mwanamke ni uchi ambao lazima ufunikwe, lakini hatukubali kuwa ni wajibu kufunika uso na viganja, kwa kulinganisha  na  kufunika miguu  katika mlinganisho wa ubora zaidi, kwa sababu huu ni mlinganisho batili, na kwa sababu unapinga maandiko yanayoonyesha kuwa inajuzu kwa mwanamke kufunua uso wake.

Dalili ya tano:

Kauli yake Mtume S.A.W: "Ikiwa mmoja wenu (mwanamke) ana mtumwa Mukatab na huyu Mukatab ana uwezo wa kulipa na kujikomboa, basi mwanamke anapaswa kujifunika [74].

Ushahidi wa Hadithi hii ni kwamba inajuzu kwa mwanamke kufunua uso wake mbele ya mtumwa wake maadamu yumo katika milki yake, na kama akimuacha ni lazima ajifunike kwa sababu amekuwa mtu wa kando, na hii ikaonesha uwajibikaji wa mwanamke kujifunika mbele ya mwanamume wa kando [75].

Na hili linajibiwa kuwa jambo hilo liko nje ya wigo wa mzozo huu, kwani linaloonyesha kuwa mwanamke kujisitiri na wanaume wa kando, na hilo ni nje ya wigo wa mzozo, siyo mwanamke kujifunika uso mbele ya wageni.

Kisha Hadithi hii ni miongoni mwa Hadithi zenye utata; kwa sababu tukizingatia maana ya kauli yake, "Ikiwa mmoja wenu (mwanamke) ana mtumwa Mukatab na huyu Mukatab ana uwezo wa kulipa na kujikomboa... mpaka mwisho wake” yaani ana kile kinalotosheleza kilichobaki miongoni mwa fedha, basi mwanamke anapaswa kujisitiri. na bado hajaachwa huru, na anamiliki kiasi cha fedha na bado hajalipa kutokana na mkataba wa kuacha huru na mmiliki wake, na tukakuta Mwenyezi Mungu Mtukufu anataja aliyowaruhusu wake wa Mtume wake A.S,  waangalie wale aliowaruhusu kuwatazama miongoni mwa watu, na akawaruhusu wale aliowaruhusu kuwatazama hawa wanawake, kwa kauli yake Mwenyezi: {Hapana ubaya kwao kuonana na baba zao} hadi kauli yake Mwenyezi: {wala wale iliyo wamiliki mikono yao ya kulia}. [Al Ahzab: 55]. 

Jibu lake: Yeyote aliyekuwa Mukatab juu ya mwanamke miongoni mwa tuliowataja wameingia katika wale waliomiliki mikono yao ya kulia, kwa ushahidi wa Hadithi hiyo, na kinachoashiriwa na waliomfanyia Mkataba ikiwa atatekeleza  yaliyomlazimu, basi ataachwa huru na itaharamishwa kwake kumtazama bibi yake ambaye ni miongoni mwa wake wa Mtume A.S, na kucheleweshwa kwake hili ili aweze kumtazama kwa mujibu wa kumiliki kwake, hiyo imeharamishwa; kwa sababu alimnyima wajibu, ili yale yaliyoharamishwa kwake yabaki kwake ikiwa atatekeleza wajibu huo kwa anayemdai, na hii ni maana ya kauli yake S.A.W, kwa mke wake Ummu Salamah: "Ikiwa mmoja wenu (mwanamke) ana mtumwa Mukatab na huyu Mukatab ana uwezo wa kulipa na kujikomboa, basi mwanamke anapaswa kufunika ." [76].

Maana hiyo aliitaja Sheikh Muhammad Anwar Al-Kashmiriy katika kitabu cha Al-A’arf Ash-Shadhiy [77] na ameikubali, kutokana na maana ya Hadithi, na haina uhusiano kwa uwajibikaji wa kufunika uso.

Dalili ya sita:

Kutoka kwa Aisha RA, alisema: “Wapanda farasi walikuwa wakitupita tukiwa katika Ihram pamoja na Mtume S.A.W, wanapokuwa usawa wetu, mmoja wetu alikuwa akishusha baibui lake juu ya uso wake kutoka kichwani mwake, na wakitupita, tunafunua [78]. Katika kauli yake: “wakitupita” yaani wapanda farasi “Mmoja wetu alishusha baibui lake juu ya uso wake” ni ushahidi wa uwajibikaji wa kufunika uso; kwa sababu kilichowekwa katika Ihram ni kufunua, na lau kungekuwa hakuna kizuizi kikubwa cha kufunua basi ingehitajika kubaki wazi. Ufafanuzi wa hili ni kwamba kufunua uso katika Ihram ni wajibu kwa wanawake kwa rai ya wanazuoni wengi, na wajibu haupingani isipokuwa kwa wajibu mfano wake, na lau si wajibu kujifunika na kufunika uso mbele ya wanaume wa kando isingeruhusiwa kuacha kitendo cha wajibu cha kufunua wakati wa Ihram, na  Imethibitika katika Sahihi Mbili na kwingineko kwamba mwanamke katika Ihram amekatazwa kuvaa nikabu na glovu mbili [79].

Hili linajibiwa katika pande mbili:

Kwanza: kwa upande wa Isnad, katika mlolongo wake wa upokezi yupo Yazid Ibn Abi Ziyad, ambapo wanazuoni waliona kuwa ni dhaifu, na wakasema kuwa Hadithi yake haiwezi kutumika kama ushahidi; kwa sababu haina nguvu, na si mahiri wa kuhifadhi. Al-Hafidh Ibn Hajar amesema kuhusu yeye katika Taqrib At-Tahdhib: Yeye ni “Dhaifu” [80], na Al-Hafidh alisema katika Al-Fat-h kuhusu Hadithi hii: “Kuna udhaifu katika mlolongo wake wa upokezi” [81], na Imamu An-Nawawiy alisema katika Al-Majmuu kuhusu mlolongo wa upokezi wa Hadithi hii: ni “Dhaifu” [82].

Kwa kuchukulia kuwa tunakubali usahihi wake, si sahihi kuitumika kama dalili ya uwajibikaji wa kufunika uso kwa wanawake wote wa Umma, na huu ni upande wa pili: Hadithi hii inaweza kuwa maalumu kwa akina Mama wa Waumini, na tukisema kutokuwa na umaalumu kwao, basi kitendo hiki cha wao au wengine hakioneshi uwajibikaji tu, kwani kitendo tu peke yake hakioneshi uwajibikaji, hata kama kimetoka kwa Mtume S.A.W, achilia mbali kama kimetoka kwa mtu mwingine; muradi wa Hadithi ni uhalali wa kufunika uso katika Ihramu bila kuvaa nikabu.

Ama ibara ya: “Wajibu haipingani isipokuwa kwa wajibu mfano wake”: ni maneno yasiyo sahihi, kwa sababu kupingana ni baina ya hoja na ushahidi, si baina ya hukumu. Ikiwa itasemwa: Tunamaanisha "wajibu hauachwi ila kwa ajili ya wajibu." Tutaasema: Makusudio hayaondoai  muktadha, na bado tunajibu na kusema: Si wajibu kufunua uso katika hali ya Ihram ili uachwe kufunikwa, hapo lililo wajibu ni kuacha nikabu, na yale yanayoashiria maneno ya Bibi Aisha ni kuruhusiwa na uhalali, sio wajibu.

Baada ya hayo, tunaweza kutolea ushahidi kwa Hadithi hii kwamba si wajibu kufunika uso, kwa sababu lau kufunika uso na viganja kungekuwa ni wajibu, isingejuzu kuvifunua katika hali ya Ihramu, na kuvifunika kwa namna hii kuwa miongoni mwa makatazo ya Ihramu, na lau uso ungekuwa sehemu za siri, usingeharamishwa kuufunika.

Dalili ya saba:

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Masud R.A, kutoka kwa Mtume S.A.W.,  amesema: “Mwanamke ni uchi, na anapotoka nje Shetani shetani humpamba katika macho ya wanaume” [83]. Hadithi hii inaashiria kwamba wanawake wote ni uchi, na hakuvua Mtume S.A.W.,  chochote kwake [84].

Hili linajibiwa kuwa Hadithi haimaanishi “ujumla” kama walivyotaja, bali kile  kinachomaanisha ni: kwamba kanuni ya msingi katika mwanamke ni kujilinda na kujisitiri, si kujifunua na uchafu [85], na maana yake ni: mwanamke akitoka nyumbani kwake Shetani humtamani ili amfitini au amfanyie fitina na wengine, si kwamba lazima afunike uso wake.

Tukichukulia kuwa tunakubali ujumla wa Hadithi hii, uso na viganja ni maalumu kwa ushahidi wa ujumla huu. Sharia ya imetenga uso na viganja, kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: {wala wasioneshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika} na dalili nyinginezo zinazoruhusu kufunua uso

Dalili ya nane:

Kitendo cha Mama wa Waumini Bibi Aisha R.A, katika kisa cha Al-Ifk (uzushi), ambamo amesema: “Aisha alisema: Safwan Ibn Al-Mu’atal As-Sulamiy, kisha Adh-Dhakwaniy alikuwa nyuma ya jeshi, hivyo alisafiri usiku na kwenda nyumbani kwangu asubuhi na kuona weusi wa mtu aliyelala, akanijia na kunitambua aliponiona, na alikuwa akiniona kabla ya Hijabu, hivyo niliamka kuniona kwake wakati alinitambua, kwa hivyo nilifunika uso wangu kwa baibui langu [86].

Ushahidi ni kwamba lau asingemuona kabla ya Hijabu, asingemtambua kwa kumuona, na Hadithi hii ni dalili ya kuwa Hijabu inajumuisha uso, na inaashiria kwamba Hijabu inazuia mtu kumtambua mwanamke kwa njia ya uso wake; kwa sababu uso umefichwa kabisa [87].

Hii inajibiwa kuwa Hadithi hii haiko wazi juu ya uwajibikaji wa kujisitiri kwa Mama wa Waumini; Hakuna amri ndani yake, bali ni kitendo tu kwa upande wake R.A, basi vipi itumike kuwa ni ushahidi wa uwajibikaji kufunika uso kwa wanawake wengine?! Na kitendo cha Mtume S,A,W, peke yake hakioneshi uwajibikaji, basi vipi kuhusu kitendo cha mtu mwingine?! Jambo muhimu tu kwake ni kwamba alifunika uso wake.

Wakichukulia kuwa inaashiria uwajibu, basi kwao wao tu wake za Mtume, kwani wao ni Mama wa Waumini, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine}. [Al Ahzab: 32].

Dalili ya tisa:

Kutoka kwa Aisha R.A,  alisema: “Sawdah alitoka baada ya kuvaa Hijabu kwa ajili ya haja yake, na alikuwa ni mwanamke mnene ambaye hakufichika kwa yeyote anayemjua, na Umar Ibn Al-Khattab akamuona na akasema: Ewe Sawdah, Wallahi hujifichi kwetu, basi tazama jinsi unavyotoka” [88]. Na Hadithi hii inaashiria wazi kwamba uso wake ulikuwa umefunikwa, na kwamba yeye R.A, hakumtambua isipokuwa kwa mwili wake [89].

Na hili linajibiwa kwamba kisa cha kitendo cha mmoja wa Mama wa Waumini, na kitendo ndicho kitu pekee kilichohalalishwa, kwa hivyo uwajibikaji hauchukuliwi kutoka kwayo.

Dalili ya kipimo cha Uwiano (Al-Qiyasi):

Watetezi wa uwajibu wa kufunika uso wametumia dalili ya kipimo cha uwiano (AlQiyasi), wakasema: Imebainika kuwa kufunua na kudhihirisha uso wa mwanamke mbele ya wanaume wasiokuwa Mahrim kunajumuisha maovu mengi, na ikiwa kuna masilahi yeyote ndani yake, basi ni madogo na yamezama ndani ya maovu. Miongoni mwa maovu  yake ni: 

Fitina, kwani mwanamke hujitia fitna mwenyewe kwa kupamba uso wake, na kuufanya uonekane wa kuvutia. Hii ni moja ya sababu kuu za uovu na ufisadi [90].

Hili linajibiwa kuwa ni kuzidisha sana katika kuzuia visingizio, na uzuri ni jambo lililokadiriwa na siyo wazi, na amri ya kuinamisha macho iko wapi?! Na hili linaweza kuwa ni suala la Fatwa, siyo suala la hukumu, na kadiri wakati unavyobadilika na kuwa na ufisadi, Fatwa hubadilika na siyo hukumu. Zaidi ya hayo, fitina inaweza kutokea kwa kuangalia tu mavazi na ukubwa wa mwili.

Pia, tatizo hili linashirikiana na wanaume na wanawake, kwani Wanawake wanaweza kuvutiwa na uso mzuri wa mtu, lakini wanaume hawajaamriwa kufunika nyuso zao.

Kuondolewa kwa staha kwa mwanamke, ambayo ni sehemu ya imani na mahitaji ya asili yake. mwanawake alikuwa mfano wa kuigwa katika staha. " ana Staha zaidi kuliko  mwanamke bikra katika nyumba yake" na kutoweka kwa staha kwa mwanamke ni upungufu katika imani yake, na kutoka katika maumbile yake aliumbwa nayo [91].

Hili linajibiwa kuwa hakuna uhusiano kati ya kanuni fulani ya mavazi na heshima.

Kuchanganyika kwa wanawake na wanaume. Iwapo mwanamke atajiona kuwa ni sawa na mwanamume katika kufunua uso wake na kutembea bila Hijabu, hataona aibu katika msongamano, na hilo linajumuisha fitina kubwa na ufisadi ulioenea. Mtume S.A.W, siku moja alitoka msikitini, na wanawake walikuwa wakichanganyika na wanaume njiani, Mtume S.A.W, akasema: “Bakieni nyuma kwani si sawa kwenu kutembea katikati ya barabara, ni lazima mshikamane na kingo za barabara” [92]. akawa Mwanamke anajibana ukutani hadi mavazi yake yana nasa kutokana na kujibana kwake. Ameitaja Ibn Kathir alipofasiri kauli ya Mola Mtukufu: {Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao} [93].

Na hili linajibiwa kuwa hakuna uhusiano baina ya kuchanganyika na kufunika au kufunua uso, zaidi ya hayo, staha ambayo ukweli wake ni sifa inayomhimiza mtu kuachana na mambo machafu na kuzuia kuzembea katika haki ya mwenye haki [94]- ni sifa ya wanaume na wanawake na haikomei kwa wanawake pekee, na madai ya kutoweka kwa sababu ya msongamano ni ya udanganyifu na hayawezi kuegemezwa kama hukumu ya kisheria.

Dalili ya kiada (Desturi):

Ushahidi wa uwajibu wa kufunika ni ada ya jumla ambayo Waislamu wameifuata kwa karne kadhaa, huku wanawake wakifunika nyuso zao barakoa, nikabu, na vitu vingine.

Imamu Al-Ghazaliy ametaja katika Al-Ihyaa kwamba: Kwa muda mrefu, wanaume wameendelea kufunua nyuso zao na wanawake wameendelea kuvaa nikabu[95] .

Al-Hafidh Ibn Hajar pia ametaja katika Al-Fat-h kwamba: Desturi ya wanawake katika zama zilizopita na za kisasa wameendelea kufunika nyuso zao kwa wanawake wa kando [96]. 

Na hili linajibiwa kwamba halioneshi wajibu wa kufunika uso, bali ni maelezo tu ya hali yao na kwamba ilikuwa ni desturi yao katika zama zao kufunika nyuso zao.

Shubha na jibu lake:

Wale wanaosema kuwa ni wajibu kufunika uso wanasema kuwa tumekubali ushahidi wa uhalali wa kufunua uso, na kwamba mwanamke katika zama za mwanzo hawakufunika nyuso zao isipokuwa katika matukio machache tu, lakini zama hizo zilikuwa bora na zama za usafi na uaminifu, na wakati huu tunaoishi ni wakati wa fitina na ufisadi, kwa hivyo ni bora kwa mwanamke kufunika uso wake.

Jibu la hili ni kama ifuatavyo:

Muda wa zama za fitina haudhibitiwi; Tangu zama za Tabiina kuna wanaosema: Wakati wetu ni wakati wa fitina, pia uzuri ni jambo la kukadiriwa.

kwamba hili linakuwa katika njia ya kujilinda na haramu, ambapo upeo wake ni mpana, na sisi tuko katika zama za mpaka kati ya halali na haramu, na  ikiwa fungua mlango huu na tukapita njia hii ngumu hukumu nyingi za Sharia zingefutwa kwa rai tu kwa kisingizio cha kujiondoa kwenye shubha na hadhari.

Muhtasari wa utafiti na matokeo:

Tunachohitimisha mwishoni wa utafiti huu ni yafuatayo:

kufunika uso wa mwanamke au kuudhihirisha ni mambo ambayo wanazuoni wametofautiana ambayo hayakemewi kwa kuyafanya au  au kuyaacha.

Rai yetu tuliyochagua ni kujuzu kufunua uso, na hii ni rai ya Wanazuoni wengi; kwa sababu ya nguvu ya madhehebu yao na kwa ushahidi wao kuwa wazi.

Mwanamke anayefunika uso wake ni fadhila, siyo faradhi, Mwenye kuufunika atalipwa, na mwenye kuudhihirisha hatapata dhambi.

Kusema kuwa kufunika uso si wajibu haimaanishi kuwa hairuhusiwi au ni uzushi.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Mwandishi: Mustafa Abdulkaerim Murad

(Mtafiti katika idara ya tafiti za Kisharia

Tarehe 22/5/2008

Imesomwa na kuruhusiwa kusambazwa na:

Prof/ Abdallah Rabii Abdallah (Mwalimuwa Usoul Alfiqhi chuo kikuu cha Al-Azhar)

 

[1] Al-Mujam Al-Wasiit: Kidahizo: (KA SHA FA) UK. 788; Lisaan Al-Arab na Ibn Mandhuur: Kidahizo (KA SHA FA) 9/300; taj Al-Aruus Min Jawahir Al-Qamuus na Az-Zabiidiy: Kidahizo: (KA SHA FA) 24/312.

[2] Al-Misbaah Al-Muniir na Al-Fayyumiy Kidahizo: (WA JA HA) Uk. 649.

[3] Fat-hul Qadiir na Al-Kamaal Ibn Al-Humaam: 1/15; Mughniy Al-Muhtaaj na Al-Khatiib Ash-Shirbiiniy: 1/173.

[4] Tabyiin Al-Haqaaiq Sharh Kanz D-Daqaaiq na Az-Zayla’iy: 1/96.

[5] Kifayat At-Taalib Ar-rabbaniy Alaa Risalart Abi Zaid Al-Qayrawaniy, na Ali Ibn Khalaf Al-Menufiy: 1/313.

[6] Ash-Sharh Al-Kabiir na Sheikh Ad-dardiir pamoja na Hashiyat Ad-Disuqiy: 1/218.

[7] Nihayat Al-Muhtaaj Sharh Al-Minhaaj: 2/7-8.

[8] Sharh Muntaha Al-Iradaat, na Al-Bahuutiy: 1/150.

[9] Jamii Al-Bayaan Fiy Taawiil Al-Quran, na At-Tabariy: 19/157, na baadaye.

[10] Al-Jamii Li Ahkaam Al-Quran: 12/229.

[11] Ahkaam Al-Quran: 3/460.

[12] Sahihi Bukhariy (1741).

[13] Muttafaq: Sahihi Bukhariy (1442); Sahih Muslim (1334). Al-Fadhl alikuwa akipanda kipando pamoja na mtume SAW. Khath’am ni kabila la Yemen.

[14] Al-Mustadrak Alaa As-Sahihain, na Al-Haakim: 1/623, na akasema; Hii ni Hadithi Sahihi, kwa masharti ya Sheikh wawili na hawakupokea hivyo hivyo; na Adh-Dhahabbiy amemkubali hivyo katika At-Talkhiis.

[15] Fat-hul Bariy Sharh Sahih Al-Bukhariy: 11/10.

[16] Sahih Muslim (885).

[17] Sheikh Mustafa Al-Adawiy katika Kitabu chake: Al-Hijab, Uk. 73, na baadaye.

[18] Sunan An-Nasaiy (1575).

[19] Sharh Sahih Muslim, na An-Nawawiy: 6/175.

[20] Taj Al-Aruus Min jawahir Al-Kamus, Kidahizo: (SA FA LA): 29/204-205.

[21] Muttafaq: Sahih Bukhariy (4742); Sahih Muslim (1425).

[22] Fat-hul Bariy Sharh Sahih Al-Bukhariy: 9/210.

[23] Sunan Abi Dawud (4104) 2/460.

[24] Sunan Al-Baihaqiy Al-Kubra: 2/226.

[25] Al-Hidaya: 1/258.

[26] Ash-Sharh Al-kabir na Sheikh Ad-Dardir: 1/214.

[27] Asna Al-Matalib Sharh Rawdh At-Talib: 1/176.

[28] Al-Insaf na Al-Mardawiy: 1/425.

[29] Tuhfatul habib Alaa Sharh Al-Khatib: 1/450.

[30] Hashiyat Al-Baijuriy Ala Fat-h Al-Qarib: 1/146.

[31] Kashaaful Qinaa An Matn Al-Iqnaa: 1/266.

[32] Jamii Al-Bayan (Tafsir At-Tabariy) 20/313.

[33] Tafsir Ibn Kathir: 6/455.

[34] Rejea: Adwaa Al-Bayan na Ash-Shanqitiy: 6/642-644; Ibraz Al-Haq was-Sawab na Al-Mubarakfuriy, Uk. 20-27; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 251-271; Al-Hijab na Mustafa Al-Adawiy, Uk. 10-20.

[35] Sahihi Bukhariy (3976).

[36] Al-Mustadrak Alaa As-Sahihain: 4/40.

[37] Rejea: Risalat Al-Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 44-46, pamoja na Rasaail Fi As-Sufuur Wal Hijab; Ibraaz Al-Haq was-Sawaab, na Al-Mubarakfuriy, Uk. 15-20; Adillat Al-Hijab na Al-Muqadam, Uk. 283-284-310-318; Al-Hijab na Mustafa Al-Adawiy, Uk. 44-62.

[38] Muttafaq: Sahih Bukariy (5889); Sahih Muslim (2657).

[39] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 44-45, pamoja na Rasaail Fii As-Sufur Wal Hijab.

[40] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 45.

[41] Tajul Arus Min Jawahir Al-Qamus na Az-Zabidiy, Kidahizo: (Kha Ma Ra) 11/214.

[42] Tafsiir Ibn Kathir: 6/46; tafsiir Ruh Al-maaniy na Al-Alusiy: 18/142.

[43] Sunan Abi Dawud (641); Sunan At-Tirmidhiy (377); Sunan ibn Majah (655).

[44] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 45.

[45] Lisaan Al-Arab, Kidahizo: (Dha Ha Ra) 4/520.

[46] Risalatul Hijab na ibn uthaimiin, Uk. 45-46.

[47] At-Tahrir Wat-Tanwir: 18/207-208, kwa mabadiliko machache.

[48] Ahkaam Al-Quraan: 3/380-382.

[49] Al-Misbah Al-Munir Fiy Gharib Ash-Sharh Al-kabiir na Al-Fayumiy. Kidahizo: (Qa La Ba) Uk. 512.

[50] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 46.

[51] Rejea: Tafsiir ibn Saadiy, Uk. 574; Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 46-47; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 318-328; Al-Hijab na Mustafa Al-Adawiy, Uk. 63-67.

[52] Jamii Al-Bayan (Tafsiir At-Tabariy) 19/216-217.

[53] Lisaan Al-Arab na Ibn Mandhuur. Kidahizo (Ja La Ba) 1/272.

[54] Ameitaja Ibn Kathir katika Tafsiir: 3/569.

[55] Ameipokea ibn Abi Hatim, kama ilivyotajwa katika Tafsiir Ibn Kathir: 2/569.

[56] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 47; Ibrazul Haq na Al-Mubarakfuriy, Uk. 27-46; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 191-237; Al-Hijab na Al-Adawiy, Uk. 26-38.

[57] Dhuafaa Al-Aqiliy: 3/234.

[58] Tahdhiibul Kamaal: 20/490; Jamii At-Tahsiil, Uk. 240.

[59] Usuul Al-Fiqh Al-Islamiy na Daktari Wahba Az-Zuheliy: 2/857.

[60] Ad-Dur Al-Manthur Fiy At-Tafsiir Bil Maathur na As-Suyutiy

[61] Tafsiir Ibn Kathir: 6/456.

[62] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk.48; Ibrazul Haq na Al-Mubarakfuriy, Uk. 50-51; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 352.

[63] Sunan Abi Dawud (2082); Musnad Ahmad: 3/334.

[64] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 45.

[65] Muttafaq: Sahih Bukhariy (3180); Sahih Muslim (890).

[66] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 45.

[67] Sahih Bukhariy (553), (829); Sahih Muslim (645).

[68] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 49-50.

[69] Fat-h Al-Bariy Sharh Sahih Aal-Bukhariy na Ibn Hajar: 1/183.

[70] Fat-h Al-Bariy Sharh Sahih Al-Bukhariy na Ibn Hajar,: 2/55.

[71] Musnad Abi Ya’la: 7/466.

[72] Sunan At-Tirmidhiy (1731) na akasema: Hii ni Hadithi Hassan Ssahihi; Sunan An-Nasaaiy (5336); Sunan Ibn Majah (3571).

[73] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 50-51; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 335-337.

[74] Sunan Abi Dawud (3928); Sunan Aat-Tirmidhiy 91261), na akasema: Hii ni Hadithi Hassan Sahih, na maana ya Hadithi hii kwa maoni ya wanazuoni ni kujiepusha na shubha, na wakasema: Mtumwa Mukatab hakuachwa huru pamoja na kumiliki lililolipwa hata atakwishalipa; Sunan ibn Majah (2520); Musnad Ahmad: 6/289.

[75] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 51; Adillatul Hijab: 341-242.

[76] Mushkil Al-Athar na At-Tahawiy: 1/275.

[77] Al-A’arf Ash-Shadhiy Sharh Sunan At-Tirmidhiy: 3/38.

[78] Sunan Abi Dawud (1833); Sunan Ibn Majah (2935); Musnad Ahmad: 6/30.

[79] Rejea: Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 51; Ibrazul Haq na Al-Mubarakfuriy, Uk. 49-50; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 350-351.

[80] Taqrib At-Tahdhib, Uk. 601.

[81] Fat-h Al-Bariy Sharh Sahih Al-Bukhariy: 3/406.

[82] Al-Majmuu Sharh al-Muhadhab: 7/266.

[83] Sunan At-Tirmidhiy (1173) na akasema: Hii ni Hadithi Hassan Gharib.

[84] Rejea: Kashaful Qinaa na Al-Bahutiy: 1/266; Adillatul Hijab na Al-Muqadam: 329-330; Al-Hijab na Al-Adawiy: 38-41.

[85] Fatawa Mua’asirah na Sheikh Aal-Qaradawiy: 2/329.

[86] Muttafaq: Ssahih Bukhariy (2518); sahih Muslim: (2129).

[87] Rejea: Ibrazul Haq na Al-Mubarakfuriy, Uk. 49; Adillatul Hijab an Al-Muqadam, Uk. 342; Al-Hijab na Al-Adawiy, Uk. 42.

[88] Muttafaq: Sahih Bukhariy (4517); Sahih Muslim (2170).

[89] Rejea: ibrazul Haq na Al-Mubarakfuriy, Uk. 48-49; Adillatul Hijab na Al-Muqadam, Uk. 361; Al-Hijab na Al-Adawiy, Uk. 23-25.

[90] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 52.

[91] Risalatul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 52.

[92] Sunan Abi Dawud (5272).

[93] Risaltul Hijab na Ibn Uthaimiin, Uk. 52-53.

[94] Sharh Sahih Muslim na An-Nawawiy: 2/6.

[95] Ihyaa Ulum Ad-Diin: 2/47.

[96] Fat-h Al-bariy Sharh Sahih Al-Bukhariy: 9/324.

Share this:

Related Fatwas