Hukumu ya mwenye kuacha Swala kwa makusudi:
Question
Ni ipi hukumu ya kuacha Swala kwa makusudi? Na kafara yake ni nini? Na vipi ninaweza kuifanya imani yangu kuwa na nguvu? Naomba msaada kwani sielewi.
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:
Swala ni nguzo ya dini; mwenye kuisimamisha ameisimamisha dini, na mwenye kuiacha ameivunja dini. Ni ndio mpaka unaotenganisha baina ya ukafiri na imani. Wanazuoni wameafikiana kwamba mwenye kuacha Swala kwa makusudi kwa kuikataa na kuikanusha faradhi yake, basi huyo ni kafiri na murtadi.
Lakini mwenye kuiacha kwa uvivu na uzembe, si kafiri bali ametenda dhambi kubwa, hivyo anapaswa kujuta, kuomba msamaha na kutubu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kuimarisha imani kunapatikana kwa kuhudhuria kwa Wanazuoni na kusikiliza maneno yao, pamoja na kujifunza sehemu ya Qur’ani Tukufu na kuihifadhi. Pia, ni muhimu kujitahidi kuswali msikitini kadri ya uwezo, kushirikiana na vijana wema, kuamini kuwa furaha ya kweli ipo katika radhi ya Mwenyezi Mungu juu ya mja, kutekeleza amri zake na kujiepusha na makatazo yake, pamoja na kumuelekea Yeye kwa kusujudu na kuomba Dua katika kila jambo dogo na kubwa.
Unapaswa pia kusoma maneno ya Mtume (S.A.W) kadri uwezavyo, kwani ni nuru, uongofu, na mwangaza kwako katika giza la maisha ya dunia.
Na kwa yaliyotangulia jawabu limeshaeleweka.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
