Kunyoosha safu (katika Swala)
Question
Je! Kuna Ushahidi wa maandiko kuhusu kunyoosha safu (katika Swala)?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Zimepokewa Hadithi nyingi za Mtume zinazozungumzia kunyoosha safu; miongoni mwazo ni Hadithi zilizokuja katika sahihi mbili na nyinginezo:
Hadithi zilizokuja katika sahihi mbili: Hadithi ya Anasa bin Malik R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Nyoosheni safu zenu, hakika katika kunyoosha sawa safu ni katika kutekeleza ibada ya sawa”.
Na Hadithi nyingine ya Anas R.A. kwamba Mtume S.A.W amesema: “Siamamisheni sawa safu zenu, hakika mimi ninawaona nyuma ya mgongo wangu”.
Na katika sahihi mbili pia: Hadithi ya Al-Nouman bin Bashir R.A. kutoka kwa Mtume S.A.W. amesema: “Mnyooshe safu zenu, au Mwenyezi Mungu Awafanye maadui wenyewe kwa wenyewe”.
Na Imamu Ahmad amepokea katika Hadithi ya Abu Masoud R.A.: “Mtume S.A.W. alikuwa anapangusa mabega yetu katika Swala anasema: Nyoosheni sawa safu wala msipindishe zikakosana nyoyo zenu”.
Na imepokewa kutoka kwa Imamu Abu Dawoud katika Hadithi zake kwa isnadi sahihi katika Hadithi ya Umar Allah Amuwie radhi yeye na baba yake, “kwamba Mtume S.A.W. amesema: Simamisheni sawa safu, na wekeni sawa mabega yenu, na zibeni uwazi, na kuweni wapole kwa ndugu zenu wanapoelekeza kunyoosha safu kwa mikono yao, wala msiache uwazi, kwani hilo ni katika kazi za Shetani, na mwenye kuunga na kunyoosha safu Mwenyezi Mungu Atamweka karibu na kumsamehe dhambi zake, na mwenye kuacha kuunga safu na kuinyoosha Mwenyezi Mungu humweka mbali na rehema zake”.
Na kunyoosha safu kuna maana mbili katika Hadithi zilizotangulia:
Maana ya kwanza: Kunyoosha kihisia: Nako ni Kusimama sawa na waliosimama kwa namna wasiwe baaadhi ya wanaoswali wamewatangulia wengine katika safu moja.
Maana ya pili: Kunyoosha safu kimaana: Nako ni Kuziba uwazi kwa namna hakupatikani uwazi.
Na Wanazuoni wamekubaliana kwamba kunyoosha safu ni katika Sunna zilizokokotezwa katika Swala ya jamaa, pia Madhehebu ya Hanafi yanaeleza wengineo wanaeleza kuwa ni wajibu kwa Imamu, isipokuwa inatakikana kuwa kunyoosha safu kwa umoja na upendo, hasa baada ya kuwepo uchache wa elimu; jambo hili linahitaji upole zaidi kwa watu ili kuwafundisha na kuwalemisha, lakini haya yote yasitoke nje ya makusudio asili ya Swala ambayo ni kuhudhurisha moyo kunyenyekea, na ukamilifu zaidi ni kufuata Sunna za Mtume za wazi na za ndani, na akishindwa kukusanya kati ya viliwili hivyo, achunge kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu katika Swala na kujenga upendo kati ya Waislamu ni bora kuliko uongofu wa dhahiri uliokosa uhalisia huu wa msingi unaokusudiwa, kwamba uongofu wa dhahiri unaokusudiwa kwa mwingine, kilichokuwa kinakusudiwa chenyewe ni bora kuliko kilichokusudiwa kwa kitu kingine wakati wa mwingiliano, na ukamilifu wa kuthibiti kwake kwa pamoja.
Mwanazuoni Kashmir Al-Hanafy anasema: “Kunyoosha safu ni wajibu kwa Imamu kama ilivyo katika Ad-Dar Al-Mukhtar, na kuliacha hilo ni karaha iliyo karibu na haramu, na Ibnu Hazm amesema kuwa kunyoosha safu ni faradhi, na kinachazingatiwa katika kunyoosha safu ni kubandanisha kisigino kwa kisigino, ama kilicho katika Bukhari katika kubandanisha kisigino kwa kisigino na baadhi ya watu wakadai kuwa ni uhalisia, wakati hilo ni katika yaliyozidishwa na mpokeaji, na sahihi ni kutoweka wakati katika hili, bali lililo bora ni lile linalokaribiana zaidi na unyenyekevu.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
