Hukumu ya Ndevu
Question
Ni ipi hukumu ya ndevu katika Uislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Ndevu ni: jina la nywele zilizopo katika mashavu mawili na kidevu.
Kuna Hadithi tukufu za Mtume zinazoashiria uhalali wa kufuga ndevu, ikiwemo: kutoka kwa Ibn Umar R.A., kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Tofautianeni na washirikina. Fugeni ndevu na punguzeni masharubu”. Hadithi hii imepokelewa na Al-Bukhari. Vile vile imepokelewa kutoka kwa Abu Hurairah R.A., kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Kateni masharubu na fugeni ndevu, tofautianeni na Majusi” Imepokelewa kutoka na Imamu Muslim. Miongoni mwa Hadithi hizo ni pamoja na Hadithi ya Aisha (R.A) kutoka kwa Mtume (S.A.W): “Mambo kumi na katika maumbile...” Akayahesabu miongoni mwake: “Kufuga ndevu”. Ibn Abidin, mfuasi wa Madhehebu ya Hanafi, amesema: “Kufuga ndevu ziote maana yake ni kuziacha mpaka ziwe nyingi”.
Baadhi ya Wanachuoni kama vile Al-Nawawiy Al-Shafiy, wamesema kwamba hairuhusiwi kunyoa hata kidogo. Baadhi ya Wanachuoni wa Hanafi na Hanbali wameruhusu kuzikata ndevu zinazozidi kiganja. Rai za Wanachuoni juu ya kunyoa ni kati ya kukatazwa na Kuchukiza. Wafuasi wengi wa Madhehebu ya Hanafi, Maliki, Hanbali, na Wafuasi Madhehebu ya Shafi waliotangulia wanaona kwamba ni haramu. Wafuasi Madhehebu ya Imamu Shafi waliokuja nyuma wanaona kuwa ni karaha, kwa kuzingatia kuwa amri ya Sunna, kutokana na uhusiano wake na desturi kama vile kula, kunywa, mavazi, kukaa na mapambo. Hilo wamelifananisha na amri ya kupaka rangi nywele, kuswali na kanda mbili, na kadhalika.
Miongoni mwa kanuni za kisharia zilizowekwa ni kwamba linalokemewa ni kufanya waliokubaliana wanachuoni juu ya Uharamu, au kuacha waliokubaliana wanachuoni juu ya wajibu wake, na kwamba waliyotofautiana hayakemewi, na kuepuka kutofautiana kunapendekezwa, na kwamba aliyepewa mtihani katika jambo lolote kati ya hayo basi afuate mfano wa Wanachuoni ambao wameruhusu hivyo.
Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
