Operesheni za macho kwa mkopo kupitia Benki
Question
Uongozi wa kituo unaomba kutoka kwenu muelekeo wa hukumu ya kisharia kuhusu watu wenye udhaifu wa kuona kuelekezwa Benki wakiwa na ripoti kutoka kituo chetu inayoonesha kuwa wanahitaji upasuaji wa kurekebisha kuona kwa kutumia leza (Laser), kisha Benki kuwasaidia kwa gharama za upasuaji na kutoa hundi kwa kituo, na baada ya hapo wao waliipe Benki kwa awamu kwa riba kwa Benki. Tunaomba mfafanue hukumu ya kisheria kuhusu jambo hili, na sisi kama uongozi tutatangaza na kuonesha Fatwa hii rasmi kutoka kwenu kwa jamii; kwa ajili ya kutuliza nyoyo na nafsi!
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
"Operesheni" iliyoulizwa ambayo gharama zake zote zimeainishwa mapema na kwa uwazi kamili bila ya utata, na kunakuwa na makubaliano ya wazi kati ya pande mbili: upande wa taasisi inayotoa "operesheni" (kituo) kwa upande mmoja, na mgonjwa anayetaka kufanyiwa "operesheni" kwa upande mwingine, si chochote zaidi ya aina ya huduma ambazo inajuzu kufanyiwa mkataba kisharia..
Imeelezwa kisharia kwamba inaruhusiwa kuuza kwa bei ya papo hapo au kwa bei ya kuchelewa hadi muda fulani ulio wazi, na ongezeko la bei kwa ajili ya muda ulio wazi linajuzu kisharia kama ilivyokubaliwa na wengi wa Wanachuoni wa Fiqhi; kwa sababu ni aina ya mauzo ya faida ("murabaha," ) ambayo ni aina ya biashara inayojuzu kisharia ambapo inawezekana kuweka masharti ya ongezeko la bei kwa ajili ya muda, kwa kuwa ingawa muda hauhesabiwi kama mali kwa uhalisia, lakini katika biashara ya murabaha ongezeko la bei linaweza kuwekwa kwa ajili yake ikiwa muda unatajwa wazi kwa ongezeko la kuzidi kwa thamani. Kwa madhumuni ya kupatikana makubaliano ya pande mbili kwa jambo hilo na kwa sababu hakuna sababu ya kukataza, na kwa kuwa kuna haja kubwa ya watu kufanya hivyo iwe wauzaji au wanunuzi. Hii haitachukuliwa kama riba, kwa sababu kanuni ya kisharia inasema kwamba riba haipo ikiwa bidhaa ipo katikati, na huduma zinazokubaliana nazo –
kama vile "operesheni" iliyo na gharama maalumu - ni kama bidhaa, na inahitajika kuwa na maelezo ya kifedha na ya muda ambayo yameelezwa wazi kabla, kama ilivyo katika mkataba wa "salam" (Ni kuuza kitu kilichoelezewa kwa sifa maalumu katika dhamana (deni), kwa kutumia neno “kukopesha”) ambapo wanazuoni walikubaliana kuwa ni lazima kutaja mahali na wakati wa utoaji wa bidhaa iliyokubaliwa ingawa haipo wakati wa mkataba, ambapo ni kuuza kitu kisichokuwepo wakati wa mkataba, na asili yake ni kupigwa marufuku (kukatazwa), lakini sharia imeiruhusu kwa ajili ya haja na kupunguza madhara; ikimaanisha kuchunga haja za baadhi ya waliokalifishwa ya kudhamini uwepo wa bidhaa wakati maalumu na kwa bei maalumu. Na haja ya mwingine ya kupama mali kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao na kutumia vitendea kazi vyao vilivosimama kutofanya kazi.
kwa hiyo, hapa inahakikisha kutimizwa kwa manufaa ya pande zote: kituo, mgonjwa, na taasisi inayofadhili - ikiwa ipo - bila kuwepo kwa hatari au udanganyifu au chochote kinachoweza kusababisha mizozo kati ya pande za mkataba, ambayo ni lengo la sharia takatifu, kwani hapa pia mgonjwa anaweza kuhitaji "operesheni" mara moja, lakini pengine asiwe na fedha za kumlipa gharama zote, na pengine hakuna nafasi katika kituo atakachofanyiwa "operesheni" kukubali kuchelewesha malipo au kugawanya malipo, hivyo kuingizwa kwa taasisi ya tatu inayofadhili kunakuwa na manufaa kwa pande zote mbili, hata ikiwa kutakuwa na ongezeko kwenye gharama ya operesheni.
Hivyo, Inahitajika wakati huu kuwa kila malipo ya gharama ya operesheni yatakuwa yamewekwa wazi kiasi na muda wake wakati wa mkataba, na haitaruhusiwa kuongeza fedha kwenye malipo ya mgonjwa ikiwa atachelewa kwa sababu zisizoweza kuepukika, pia haitakuwa halali kwa mgonjwa kuchelewa kulipa malipo aliyokubali bila sababu zisizoweza kuepukika.
Na kutokana na hayo, basi, "operesheni" hii ni aina ya huduma iliyo wazi katika kiasi chake na taratibu zake, hivyo ina hadhi ya bidhaa katika uwezo wa kufanya mkataba juu yake na kuipatia kwa bei ya papo hapo au kwa malipo ya kugawanywa, (kulipa kwa vipindi) kwa kutanguliza au bila kutanguliza, na kwa ongezeko la bei katika malipo ya kugawanywa (kulipa kwa vipindi) au bila ongezeko, na inaruhusiwa wakati huu kuingizwa kwa taasisi ya tatu au zaidi kwa ajili ya ufadhili, uwakala au udalali, na malipo ya taasisi inayofadhili kufanywa mara moja na kisha kuidhinishwa kutoka kwa mfaidi wa operesheni kwa ongezeko la bei kwa ajili ya muda linaruhusiwa kisharia; kwa sababu huduma zinazojulikana kwa kiasi na wakati zinachukua nafasi ya bidhaa wakati huu.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
