Kubaini jinsia ya mtoto kabla ya kuzaliwa
Question
Mimi ni mjane na nina watoto wawili wa kike kutoka kwa mume wangu wa zamani, na nimeolewa tena na mume mwingine. Nataka kuwa mjamzito tena, na madaktari wamesema kwamba ni vigumu kupata ujauzito sasa isipokuwa kwa njia ya mimba za watoto wa maabara (au chupa za maabara). Je, ni ipi hukumu ya kisheria kuhusu hili? Na nini hukumu ya kisheria kuhusu kuingilia kwa madaktari katika kubaini aina ya jinsia, kwani nataka mtoto wa kiume?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Kupata mimba kwa kutumia mbegu ya mume na yai la mke nje ya tumbo na kisha kurudishwa kwenye tumbo la mke hakuna kizuizi kisheria, ikiwa itathibitika kwa uhakika kwamba yai limetoka kwa mke na mbegu kutoka kwa mume, na kwamba yai hilo limetungishwa nje ya tumbo la mke na kisha kurudishwa kwa tumbo la mke huyo bila kuchanganywa au kuchukuliwa mbegu kutoka kwa mtu mwingine, na kama kutakuwa na dharura ya matibabu inayohitaji hivyo kama vile ugonjwa wa mume au mke unaozuia njia za kawaida za kupata ujauzito, au mke hawezi kupata ujauzito isipokuwa kwa njia hii, na hii ifanyike na daktari mwenye ujuzi na uaminifu katika matibabu.
Kuhusu suala la kubaini jinsia ya mtoto, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliumba viumbe kwa usawa, akawaumba wawili: mwanaume na mwanamke, na akaweka sifa maalumu kwa kila mmoja zinazolingana na majukumu aliyoweka kwao. Alieleza kuwa huu ni mpangilio wa asili unaohitaji kuendelea, kama alivyosema Allah katika Qur'ani Tukufu:{Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni} (Anisaa:1) Na pia amesema: {Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike 45 Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa 46} (Annajm (45-46) na {Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.} (Azzariyat 49]
Huu utofauti katika uumbaji na usawa katika asili ni jambo ambalo linatokana na hekima ya Mweneyezi Mungu Mtukufu, ambaye anajua kila kitu na anaye uwezo wa kila kitu, kama alivyosema: {Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume,49, Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye uweza 50} (Ashura 49-50) Katika suala la kubaini jinsia ya mtoto, tunaangazia mambo haya katika viwango viwili tofauti:
Hivyo, iwapo tukishughulikia suala hili kwa mtazamo wa kibinafsi (mtu mmoja mmoja), kiasili vitu vyote ni halali; kwa sababu binadamu anaweza kuoa au asiowe, na ikiwa ataoa au kuolewa, anaweza kupata watoto au asipate, na ikiwa atapata watoto, anaweza kudhibiti idadi ya watoto au asifanye hivyo, kulingana na hali na mazingira yake. Kama ilivyo halali kwa mtu kufanya juhudi za kuongeza nafasi ya kuchagua jinsia ya mtoto kwa kufuata ushauri wa wataalamu, kama vile kuchagua vyakula, au wakati wa tendo la ndoa kabla ya au wakati wa kupevuka au kuchuja mbegu za kiume, au mbinu nyinginezo zinazojulikana kwa wataalamu, kama ambavyo inavyohalalika kutumia mbinu za kimaabara kwa mchakato wa kromosomu na nyenzo za urithi (DNA) kwa lengo hilohilo. Kwa kuwa kisheria hakuna inayozuia hili kwa mtazamo wa kibinafsi, lakini hili linapaswa kufanyika kwa masharti kwamba hakuna madhara kwa mtoto atakayezaliwa katika maisha yake ya baadaye, na hili linapaswa kuthibitishwa na wataalamu wa afya; kwani haikubaliki kufanywa mwanadamu kuwa ni kipande cha majaribio au kuwa kipengele cha kuchezea chezea.
Ama iwapo tutalishughulikia suala hili kwa mtazamo wa umma (kitaifa), hali inakuwa tofauti; kwa sababu suala hili litahusiana na kuvuruga usawa wa kimaumbile ambao Mwenyezi Mungu aliuumba, na kuvuruga uwiano wa idadi kati ya wanaume na wanawake, ambao ni kipengele muhimu katika kudumisha uzazi wa binadamu. Hali hii inakuwa aina ya kupinga uumbaji wa Mweneyzi Mungu kwa kujaribu kubadilisha mfumo wake, kuharibu muundo wake, na kuathiri misingi aliyoweka kwa ajili ya kuendelea kwa maisha ya binadamu.
Hivyo basi, kuna tofauti katika hukumu kati ya kuainisha aina ya mtoto kwa mtazamo wa kibinafsi na kwa mtazamo wa kijamii; hii inatokana na kile kilichoamuliwa kisharia kuhusu tofauti ya Fatwa kulingana na jinsi hukumu inavyohusiana na mtu binafsi na jinsi inavyohusiana na jamii. Hii ni sawa na kile kinachopatikana mara nyingi katika vitabu vya Fiqhi, kama vile kuwapiga vita watu wa mji watakaokataa kutekeleza Sunna ya Alfajiri au Adhana, ilhali inaruhusiwa kuiacha kwa mtu binafsi.
Na kwa hivyo, katika suala lililoulizwa: Hakuna kizuizi cha kutumia mbinu ya watoto wa bomba (IVF) ikiwa bado wanandoa wakiwa katika ndoa yao, kwa sharti kwamba yai lililohifadhiwa liingizwe tumboni mwa mke. Vilevile, hakuna kizuizi cha kuchagua kuhamisha watoto wa kiume badala ya wa kike kulingana na matakwa ya wanandoa, isipokuwa kuchagua jinsia moja ya mtoto haitakuwa jambo la kawaida katika jamii. (maana ikigeuka kuwa jambo la kawaida kwa watu wote, linaweza kuwa na athari mbaya kijamii au kimaadili)
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
