Kusaini katika muda wa kazi ambao si rasmi
Question
Ni ipi hukumu ya kisharia kwa mfanyakazi ambaye anakaa nyumbani kwake muda wa kazi rasmi na anatia Saini katika kitabu cha mahudhurio bila ya kufanya kazi, au anasaini baada ya kufika muda ambao si rasmi, pia zamu ya kazi anayoichukua mfanya kazi na anakaa nyumbani kwake, je, hili linajuzu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Wanaofanya waajiriwa kama kuchukua zamu na kutokwenda kazini, hukumu yake inakuwa kwa mujibu wa sharia ambazo ameziweka mwajiri, ambazo muajiriwa amekiri kuzifuata wakati wa kusaini mkataba wa kazi, na kunatakikana kwetu sisi tutofautishe kati ya mambo mawili:
Kwanza: Mfanyakazi kufanya zamu yake rasmi ambayo inakuwa kwa kujua kiongozi wake katika kazi, na hapa inakuwa kwa mujibu walivyokubaliana kwa kumruhusu au kutomruhusu kwa mujibu wa mfumo wa kazi na sheria zake.
Pili: Mtu kusaini kuingia kazini pamoja na kuwa hajafika kazini.
La kwanza linajuzu kisharia muda wa kuwa mfumo wa kazi unaruhusu hilo, la pili linazingatiwa ni uvunjaji Sharia, hakujuzu kulifanya kisharia.
Ama kiongozi kuruhusu kutofika kazini au katika zamu pasi na kupangilia mfumo wa kazi pasi na kuwafahamisha viongozi wakubwa, hili halijuzu: si kwa mfanya kazi wala wasimamizi wake ambao wanafanya hili pasi na kujua walio juu yao.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
