Kumwombea Dua Asiye Muislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumwombea Dua Asiye Muislamu

Question

Mimi ni Muislamu Mjerumani, isipokuwa baba yangu aliyefariki hivi karibuni hakuwa Muislamu, lakini yeye alikuwa mtu mwema, na alikuwa daima akinuia heri na kuitenda, mpaka ninaweza kusema kwamba: Yeye aliishi maisha yake kama Muislamu katika matendo yake isipokuwa dini yake ilikuwa si Uislamu. Na kwani ninampenda sana na kumheshimu kwa tabia yake ya kupigiwa mfano, kwa hivyo mimi nataka kumwombea dua. Lakini baadhi ya watu wa kituriki wananiambia kwamba Qur`ani Tukufu imekataa kuwaombea dua wasio Waislamu. Lakini katika upande mwingine, Qur’ani Tukufu inawaelekeza Waislamu kuwa daima wawe waadilifu kwa wazazi wao, hata kama wao si Waislamu. Dua ni jambo bora kabisa ambalo Muislamu anaweza kumfanyia mtu. Pia nilisoma Hadithi isemayo kwamba Muislamu atakuwa Peponi, pamoja na yeyote ampendaye. Ningependa kuwa Peponi pamoja na baba yangu mpendwa, basi nifanye nini?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Ndugu yetu kipenzi chetu:

Mwenyezi Mungu ni mwenye rehema kwa waja wake kutokana na nafsi zao wenyewe, na Mwenyezi Mungu Amemsifu kipenzi chake Mtume Muhammad S.A.W. kuwa yeye ni rehema kwa walimwengu wote, na kwamba yeye ana tabia tukufu, na Mtume S.A.W.  alikuwa akipenda tabia njema, na alimsifia mtendaji wake japokuwa  si Muislamu; na walipoletwa matake wa Twayi, binti wa Hatim Al-Twayi alikuwa miongoni mwao na baba yake alikuwa maarufu sana kwa ukarimu na maadili mema; Na Mtume S.A.W. akasema :" Mwacheni, kwani baba yake alikuwa akipenda tabia njema, na Mwenyezi Mungu Anapenda tabia njema ", kisha mmoja wa Masahaba akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je? Mwenyezi Mungu anapenda tabia njema? Na Mtume S.A.W. akasema: "Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, haingii Peponi mtu yeyote ila kwa tabia njema " imepokelewa na Al-Baihaqy kutoka katika Hadithi ya Aly Ibn AbuTwalib R.A.

Na hukumu za Duniani zinatofautiana na hukumu za Akhera, huwenda akahukumiwa mtu duniani kuwa ni kafiri kwa kuwa yeye hakuingia katika Uislamu, na inawezekana kuwa mtu huyo hajawahi kuukadhibisha Uislamu. Na hukumu hii haiulazimishi Udharura wa aliyehukumiwa kwa ukafiri kwa matendo yake ya uwazi kuwa ataingia motoni, zaidi ya hayo kukaa humo motoni milele; na inawezekana akawa ni mwenye udhuru mbele ya Mwenyezi Mungu kwa kutofikiwa kwake na Uislamu kwa njia ya wazi, au kutosimamishiwa hoja kinaishi, basi atakuwa miongoni wa watu wa mtihani katika Siku ya Kiyama, na Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Haimpasii Nabii na wale walioamini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni} [AT TAWBAH 113]; basi katazo la kumwombea msamaha kafiri hapa ni kwa kuwa mwenye kuombewa imebainika kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa motoni, na kwa ufahamu huo ni kwamba hakuna ubaya wowote wa kumwombea msamaha mtu asiyejulikana kuwa ni miongoni mwa watu wa motoni, na pia inawezekana kumwombea dua ikiwa haujulikani ukafiri wake; kama njia ya kumpunguzia adhabu akiwa ni miongoni mwa watu wa  motoni, kwani imekuja katika Sunna kwamba baadhi ya watu wa motoni wanapunguziwa adhabu kwa baraka ya Mtume S.A.W; basi hakuna kizuizi juu ya tamaa katika ukarimu wa Mwenyezi Mungu, bali hilo ni jambo lililohalilishwa, na kwa hivyo hakuna kizuizi chochote cha kumombea dua baba yako, na huwenda Mwenyezi Mungu akamrehemu na kuyapokea maombi yako.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas