Hukumu ya kuwepo nchi nyingi za Kiislamu
Question
Qur`ani Tukufu inawaelezea Waislamu kuwa wao ni Umma mmoja na ni haramu kujitenga kati yao, je, kuwepo nchi nyigi kwa mifumo na katiba za kisiasa na Sharia mbalimbali ni jambo linalojuzu katika Fiqhi ya Kiislamu?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Sharia ya Kiislamu imeamrisha kuwa Uislamu ndio kiunganishi kinchowaunganisha, kiunganishi hiki kikubwa, hakizuii viunganishi vingine ambavyo vinawaunganisha wanadamu; kama nchi, kabila, ukoo, mazingira na lugha, na mengineyo miongoni mwa viunganishi amabvyo vinaweza kuwaunganisha Waisalamu na wasiokuwa Waislamu katika ubinadamu. Uislamu haujafuta viunganishi hivi wala haukukataza, bali Uislamu umekuja na kuunga udugu na kupenda nchi na kuimarisha uzalendo, bali umetahadharisha kuwa nchi ndio kiunganishi kikuu kuliko Uislamu, hili linafanana na kutofautiana kwa aina, na kutofautiana kwa migongano, kutofautiana kwa migogoro kumekatazwa, ama kutofautiana kwa aina hakujakatazwa muda wakuwa kunafikia masilahi mbalimbali, tofauti ya uaina ikigeuka kuwa tofauti ya mgogoro basi imekatazwa kisharia.
Kutokana na hilo: Kugawanyika Waislamu katika nchi hizi hakukatazwi na Sharia kukifikia Masilahi, kwa sharti kusivunje kiunganishi kikubwa ambacho ni kiunganishi cha Uislamu kwa kugombana.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
