Hukumu ya Elimu kwa wasichana

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Elimu kwa wasichana

Question

"Kulitokea mjadala kati yake na kaka yake mkubwa kwa sababu alikuwa anawapeleka mabinti zake shule — na ni mabinti wanne. Kaka yake alimwambia kuwa si sahihi kwa msichana kupata elimu, na kwamba msichana anayesoma ni mbaya kitabia. Muulizaji anataka kujua hukumu ya Kiislamu kuhusu elimu ya msichana."

Answer

Kuhusiana na suala la kutafuta elimu, basi ni faradhi kwa kila Muislamu awe mwanamume au mwanamke, ambapo Uislamu umesawazisha kati ya wanaume na wanawake katika faradhi hiyo, kwa mujibu wa kauli yake Mtume (S.A.W.): “Hakika kutafuta elimu ni faradhi juu ya kila Muislamu wa kiume na wa kike”. Na kwamba Mtume S.A.W. alikuwa anawapokea wanawake wanaotaka kujifunza. Na katika hayo tunataja Hadithi ya Ummu Salama R.A. alipomuuliza Mtume S.A.W. kuhusu hukumu ya kuoga kwa mwanamke baada ya kupata manii wakati wa kulala akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je! Mwanamke anatakiwa kuoga akipata manii akiwa amelala? Mtume akasema: Ndiyo akiona manii”; hiyo kwa kuwa mwanamke akijifunza atafaidika mwenyewe na kufaidisha jamii yake anakoishi, lakini tahadhari tunayoitoa ni hatari ya kuchanganyika kwa wasichana na wavulana kama vile katika Vyuo Vikuu siku hizi, lakini msichana akiwa atasoma katika Chuo au shule ambako wasichana wanatengwa na wavulana, basi hakuna shida, bali ni jambo linalopendekezwa wala hamna haraja kisharia katika hali hii, kinyume binti na wazazi wake huwa wanastahiki malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Ama kuhusu aliyoyataja muulizaji kuhusiana na hukumu ya kutukanwa na ndugu yake, basi ni uhalifu wa kisharia na haikubaliki katika Uislamu, na hakuna sababu ya kutukana wala kutiana tuhuma kati ya muulizaji na nduguye, bali anatakiwa kumcha Mungu katika maneno na vitendo vyake na kuwajibika kwa adabu za Uislamu na mafunzo yake.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas