Hukumu ya siku za kuzaliwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya siku za kuzaliwa

Question

Je, inaruhusiwa kwa Muislamu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa?

Answer

Kusherehekea siku za kuzaliwa kunaruhusiwa katika Uislamu, kwani huleta furaha na raha moyoni mwa Muislamu na kumkumbusha neema za Mwenyezi Mungu katika kumpa maisha haya, yote ni katika mambo ambayo yanapendekeza katika Uislamu. At-Tabarani amepokea kwamba Mtume (S.A.W) aliulizwa: Ni matendo gani bora zaidi? akasema: "Kumfurahisha Muumini kwa kumlisha anapokuwa na njaa, kumvisha anapokuwa uchi, au kutimiza mojawapo ya mahitaji yake."

Katika riwaya nyingine, amesema: "Amali bora zaidi baada ya yale ya lazima ni yale yanayomfurahisha Muumini."

Na lipoulizwa kuhusu kufunga siku za Jumatatu, akasema: "Hiyo ni siku niliyozaliwa, na siku niliyopewa utume - au niliopewa Wahyi." Kinachofahamika kutokana na Hadithi hii ni kwamba inaruhusiwa kusherehekea siku zote za neema, na siku ya kuzaliwa ni neema inayostahili shukrani. Kuonyesha furaha kwa kila neema ni aina ya kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kama Anavyosema: “Sema: "Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehma zake! Basi na wafurahi"

Maelezo

Siku ya kuzaliwa ni kumbukumbu ya kila mwaka ya kuzaliwa kwa mtu, na ni kawaida katika tamaduni nyingi kusherehekea siku za kuzaliwa kwa kukusanyika familia, jamaa na marafiki ili kumpa mtu husika zawadi ili kuufurahisha moyo wake.

Baraza la Fatwa la Misri (Ofisi ya kutoa Fatwa) limeeleza kwamba hakuna pingamizi la kisharia kwa kusherehekea siku za kuzaliwa, kwa sababu zifuatazo:

Kwanza: kwa sababu kunaleta furaha moyoni mwa Mwislamu, na hili linapendekeza katika Uislamu. Umar bin Al-Khattab (R.A) amesema: "Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa: 'Ni vitendo gani bora zaidi? ' Akasema: 'Kumfurahisha Muumini kwa kumlisha anapokuwa na njaa, kumvisha anapokuwa uchi, au kutimiza mojawapo ya mahitaji yake”.

Mtume (S.A.W) amesema: "Amali bora zaidi baada ya yale ya faradhi ni yale ni kumfurahisha Muumini."

Pili, inatukumbusha neema za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu katika maisha haya. Abu Qatadah R.A. amepokea kwamba Mtume  (S.A.W) aliulizwa kuhusu kufunga siku za Jumatatu, akasema: "Hiyo ni siku niliyozaliwa na siku niliyopewa utume - au niliyopewa Wahyi." Hadithi inaashiria kuwa inaruhusiwa kusherehekea siku zote zenye neema, na siku ya kuzaliwa ni neema inayostahili shukrani, Inapendekezwa kuonyesha furaha kwa kila neema kama njia ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa neema hiyo, kama Anavyosema: {Sema: "Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehma zake! Basi na wafurahi."} [Yunus: 59].

Tatu: Kusherehekea siku ya kuzaliwa ni bidaa ambayo hakuna andiko katika Qur`ani Tukufu au Hadithi linayoiharamisha au kuruhusu, na kanuni ya Fiqhi ni kwamba mambo kama hayo yanaruhusiwa hadi kutakapokuwa na ushahidi wa kinyume chake.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

 Hakuna  kizuizi cha kisharia katika kusherehekea siku ya kuzaliwa, kwa sababu inatukumbusha neema za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu katika dunia hii na huleta furaha katika mioyo ya Waislamu, jambo ambalo linahimizwa katika Uislamu.

Share this:

Related Fatwas