Hukumu ya kufuga mbwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kufuga mbwa

Question

Ni ipii hukumu ya kufuga mbwa? Na je,  kuwepo kwa mbwa kunazuia Malaika kuingia ndani ya nyumba? Je, mbwa ni najisi / uchafu?

Answer

Inafaa kumiliki na kumfundisha mbwa kwa ajili ya ulinzi au uwindaji na matumizi mengine ya manufaa binafsi na ya umma. Pia inafaa kumiliki mbwa bila ya malengo ya uwindaji au ulinzi, kama kwa ajili ya urafiki kwa mtu aliye peke yake. Na wala mwenye kumlea hapunguziwi thawabu za mmiliki wake, mradi tu asikoseshe usalama wa wengine.

Mbwa ni msafi na wala si najisi; hivyo ni halali kuswali mahali pa mguso wa mbwa bila haja ya kupasafisha.

Iwapo mbwa ni wa ulinzi au uwindaji, haizuii Malaika kuingia katika nyumba, na wala haizuii Malaika wanaoandika matendo ya mwanadamu, Malaika wa kifo, na wengine ambao hawambanduki mwanadamu. Lakini kumiliki mbwa kwa ajili ya kutisha au kuwaogopesha  wengine ndiyo kizuizi cha Malaika kuingia katika nyumba.

Maelezo

Hakuna kizuizi cha kumiliki na kufuga mbwa kwa madhumuni yaliyo halali kisharia, kama kumfuga kwa ajili ya mawindo, ulinzi wa nyumba, kujikinga na wizi, au kufuata makosa ya wahalifu, kama polisi wanavyofanya wakati mwingine na mfano na mambo kama hayo katika yenye kunufaisha mtu mmoja mmoja na jamii. Hii inatokana na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

" Wanakuuliza wamehalalishiwa nini? Sema: Mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri na mlicho wafundisha wanyama kukiwinda. Mnawafundisha alivyo kufunzeni Mwenyezi Mungu. Basi kuleni walicho kukamatieni, na mkisomee jina la Mwenyezi Mungu. Na mcheni Mwenyezi Mungu; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu." [Al-Ma’ida: 4] "Na maana ya 'mukallibin' ni wale wanaowafundisha (wanyama) uwindaji, na hii inajumuisha wanyama wote, akiwemo mbwa.

Ama kuhusu kufuga mbwa kwa malengo yasiyo yenye manufaa ambayo sharia imeyahalalisha. Wanazuoni yamegawanyika kwa rai mbili:

Rai ya kwanza: Rai ya Wanazuoni, kwamba ni haramu.

Rai ya Pili: Maoni ya baadhi ya Wanazuoni (Madhehebu ya Malik) ni machukizo (makruh).

Rai iliyochaguliwa[1] kwenye Fatwa hii ni rai ya pili: kwa kuwa: Hakuna kosa katika kufuga /kulea mbwa bila madhumuni ya uwindaji au ulinzi na mfano wake, kwani si haramu. Lakini huchukiza kwa kufuata Madhehebu ya Imamu Malik.

Kuhusu mbwa kuzuia Malaika kuingia ndani ya nyumba: Kauli ya Mtume (S.A.W)  aliposema: "Malaika hawaingii nyumba iliyo na mbwa au picha za sanamu." (Bukhari)

Wanazuoni wameelezea kauli hii kama ifuatavyo;

Hii ni kwa mbwa wasioruhusiwa kumilikiwa, kama kwa ajili ya kuwatisha au kuwahofisha wengine.

Hali hii haijumuishi Malaika wanaoandika matendo ya mwanadamu, Malaika wa kifo, na wengine ambao hawambanduki kutoka kwa mwanadamu.

Ama kuhusu kupunguziwa thawabu kwa mmiliki wa mbwa: Hadithi iliyopokelewa na Ibn Umar (R.A): Yeyote anayemfuga[2] mbwa, asiyekuwa mbwa wa uchungaji au mbwa mwindaji , atapunguziwa qirat mbili kutoka katika matendo yake mema kila siku.[3]" (Bukhari). Na mapokezi ya Abu Huraira ni qirat moja. Na Wanazuoni wametafautiana  juu ya maana yake pia.

Wanazuoni  wengi wanaamini kwamba maana iliyokusudiwa ya kupungua kwa thawabu ni kwamba dhambi inayotokana na kufuga mbwa ni sawa na Qirat moja au mbili za matendo mema.

Na Wanazuoni wengine – Madhehebu ya Imamu Malik - wanaamini kupungua kwa thawabu ni tu pale mbwa anapokuwa hatarishi au kutishia wengine. Kinyume chake hakupunguzi thawabu.

Hukumu ya kisharia: Kufuga mbwa hakuna kosa na hakupunguzi thawabu mradi tu asitishie au kuogofya wengine.

Ama kuhusu usafi wa mbwa na unajisi wake, Wanazuoni wamegawanyuika katika kauli tatu; kauli ya kwanza: Mbwa ni msafi.

Kauli ya pili: Ni najisi.

Kauli ya tatu: Mate / madenda yake pekee ndio najisi.

Fatwa iliyochaguliwa ni kuwa kati ya kauli hizi ni rai ya kwanza, yaani: usafi wa mbwa na kutokuwa najisi; na hii ni kwa sababu ifuatayo:

 Kwanza, mbwa hutumika katika uwindaji, na kama mbwa angekuwa najisi basi na windo aliloliwinda kwa mdomo wake lingekuwa ni najisi pia, lakini kwa kuwa Sharia imekuruhusu kumtumia mbwa na kula kile alichokishika kwa mdomo wake, hii inaonyesha usafi / utwahara wa mate yake.”

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Inafaa kumiliki na kumfundisha mbwa kwa ulinzi, uwindaji, au kumtumia kwa matumizi mengine ya manufaa binafsi au ya umma.

Inafaa kufuga mbwa bila ya dhumuni la uwindaji au ulinzi, kama urafiki kwa yule aliye peke yake, bila kupunguza thawabu mradi tu asitishie wengine.

Mbwa hazuii  Malaika kuingia katika nyumba kwa mujibu wa rai za Wanazuoni wengi.

Mbwa ni msafi na wala si najisi.

 

[1] "‘Al-Mukhtār lil-Fatwā’ ni kauli ambayo imepewa uzito kati ya maoni mbalimbali ya wanasheria wa Kiislamu."

[2] kumiliki / kumtumia.

[3] Amepokea Imam Bukhari.

Share this:

Related Fatwas