Hukumu ya kunywa bia

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kunywa bia

Question

Ni ipi hukumu ya kunywa bia?

Answer

Ni haramu kisharia (Kisharia) kutumia kitu chochote kinacholevya akili ya mwanadamu na kuiondosha katika ufahamu wake; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na masanamu, na kutafuta bahati kwa mishale, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa} [Al-Maidah: 90].

Na pombe inajumuisha vileo vyote bila kujali asili yake; imepokelewa kutoka kwa Umar bin Al-Khattab (R.A.) alisema: "Hakika uharamu wa ulevi umeshuka, nao unatokana na vitu vitano: Zabibu, tende, ngano, shayiri, na asali...". Na kwa sababu hiyo, bia inayotokana na shayiri na mfano wake ni haramu kuitumia kwa sababu inasababisha ulevi, na Mtume (S.A.W.) amesema: “Kila chenye kulevya ni ulevi, na kila ulevi ni haramu”. Na uharamu hapa unajumuisha kutumia kiasi kingi au kidogo; kutoka kwa Jabir bin Abdullah (R.A.), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Kile ambacho kiasi chake kikubwa kinalevya, basi kiasi chake kidogo pia ni haramu”.

Maelezo

Ni haramu kisharia kutumia kitu chochote kinacholevya akili ya mwanadamu na kuiondoa katika ufahamu wake, sawa iwe kiasi anachotumia mtu ni kidogo au kingi; Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: {Enyi mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na masanamu, na kutafuta bahati kwa mishale, ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo ili mpate kufanikiwa. Hakika Shetani anataka kutilia kati yenu uadui na chuki kwa ajili ya ulevi na kamari, na akuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kuswali. Basi je, mtaacha?} [Al-Maidah: 90-91].

Na kutoka kwa Abdullah bin Umar (R.A.), kwamba Mtume (S.A.W.) amesema: “Kila chenye kulevya ni pombe, na kila ulevi ni haramu” [Imepokelewa na Muslim].

Pia kutoka kwa Abdullah bin Umar (R.A.), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) amesema: “Mwenyezi Mungu amielaani  pombe, na mnywaji wake, na mnyweshaji wake, na muuzaji wake, na mnunuzi wake, na mkamuaji wake (wa matunda), na mwenye kukamuliwa, na mbebaji wake, na yule anayebebewa” [Imepokelewa na Abu Dawood].

Hivyo basi, dalili hizi na matini za kisharia zinaonyesha uharamu wa kutumia pombe na vileo vyote ambavyo huondoa akili na kuifanya ipoteze ufahamu wake. Lakini kuna baadhi ya watu hunywa bia kwa hoja kwamba haijaharamishwa; na hiyo ni kwa sababu zifuatazo:

Kwamba ulevi ulioharamishwa na Mwenyezi Mungu ni ule unaotokana na tende, na bia inatokana na shayiri; na wakatoa ushahidi wa hilo kupitia hadithi ya Anas bin Malik (R.A.): "Ulevi umeharamishwa, na ulevi kipindi hiko ulikuwa ni tende pevu[1] na tende iliyoiva"

Kwamba kunywa bia kwa kiasi fulani hakupelekei kulewa na akili kupoteza ufahamu wake, bali mwanadamu anakuwa na uwezo wa kutambua yanayotokea sehemu alipo.

Yafuatayo ni  majibu ya watu hao: Hakika maneno hayo ni batili, na hayafai kwa upande wowote ule; na hiyo ni kwa sababu zifuatazo:

Hadithi ya Anas bin Malik (R.A.): “Pombe iliharamishwa, na Pombe siku hizo ulikuwa ni tende mbivu  na tende zilizoiva”. Hii haionyeshi kuwa ulevi uliharamishwa umedhibitiwa tu kwa kile kinachotokana na tende, bali inaonyesha kuwa hiyo ilikuwa ni miongoni mwa aina za pombe katika wakati huo. Kwani neno "Khamr" pombe linajumuisha kila kinywaji kinacholevya, kiwe kimetokana na tende au kitu kingine, na hili ndilo walilo nalo jamhuri ya wanazuoni wa fiqhi. Ushahidi wa hilo ni hadithi ya Abdullah bin Umar (R.A.) aliyesema: "Umar (R.A.) alitoa hotuba juu ya mimbari ya Mtume (S.A.W.) akasema: “Hakika uharamu wa pombe umeshuka, nao unatokana na vitu vitano: Zabibu, tende, ngano, shayiri, na asali. Na pombe ni kile chochote kinacholewesha akili"[2].

2- Madai yao kuwa kunywa bia kwa kiasi fulani ambacho hakileweshi ni jambo linalojuzu; maneno haya yanapingana na maandiko ya Sharia yaliyokuja kuharamisha kila kinacholewesha, sawa kiasi anachotumia mtu kiwe ni kingi au kidogo. Kutoka kwa Jabir bin Abdullah (R.A.), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) amesema: “Kile ambacho kiasi chake kikubwa kinalevya, basi kiasi chake kidogo pia ni haramu”[3].

Tunapata faidia Kutokana na yaliyotangulia:

1- Pombe ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameiharamisha inajumuisha kila kinacholewesha kinachoondosha akili na kumfanya mtu apoteze ufahamu, iwe kimetokana na zabibu, tende, shayiri, au mfano wa hivyo.

2- Kutumia kinywaji cha bia ni jambo la Haramu kisharia, kwa sababu inalewesha akili.

3- Kutumia kileo chochote kwa kiasi kidogo ambacho hakumfanyi mwanadamu kupoteza akili yake pia ni jambo la Haramu; kwani imethibiti kisharia kuwa kile ambacho kiasi chake kikubwa kinalevya, basi kutumia kiasi kidogo chake pia ni haramu.

 

[1] "Busr": Ni tende katika hatua ya kwanza ya kuiva kabla haijawa 'rutab' (tende mbivu laini).

[2] Imepokelewa na Bukhari.

[3] Imepokelewa na Abu Dawud.

Share this:

Related Fatwas