Mwenendo na Tabia yake nzuri.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mwenendo na Tabia yake nzuri.

Question

Mwenendo na Tabia yake nzuri.

Answer

Maisha ya Mtume (S.A.W) yalikuwa mfano wa pekee wa ukamilifu wa ubinadamu, na tabia yake na fadhila zake zilijulikana na kusambaa kwa wanadamu wote. Mtume (S.A.W) alikuwa akijulikana miongoni mwa watu wake kwa tabia njema, maadili mema, na sifa tukufu. Kama alivyosema mama wa Waumini Khadijah (R.A): "Wewe huwasaidia wenye shida, unawapa masikini, unawakaribisha wageni, na unasaidia katika matatizo ya haki." ([1])

Tukifuatilia maisha yake ya mwanzo, tunajikuta mbele ya mfano adimu na wa pekee, ambapo Mwenyezi Mungu alimkusanyia sifa za juu kabisa, fadhila tamu zaidi, na maadili safi zaidi. Hakutenda jambo baya, wala hakutafuta maovu. Alijiepusha na makosa madogo na makubwa, kabla na baada ya utume. Hivyo, alijulikana kama mtu mtukufu kwa watu, bila kujali Pamoja na kutoafutina matukoa yao na maeneo yao, kwa sababu ya tabia yake na mwenendo wake Mzuri.

Yeyote anayefuatilia mwenendo yake na maisha yake atagundua kwamba tangu mwanzo kabisa, Mtume (S.A.W) alijiepusha na kila kitu kinachoweza kudhoofisha ubinadamu au kuchafua ukamilifu wa utu. Na kwa nini isiwe hivyo? Mwenyezi Mungu alimtunza na kumlinda kutokana na uchafu wa kipindi cha ujinga, ili amwezeshe kwa ajili ya heshima na ujumbe wake, mpaka akawa mwanamume, na mtu bora zaidi miongoni mwa watu wake kwa tabia, mkarimu kwa ukarimu, mwenye subira zaidi, mkweli zaidi katika maneno, na mwenye amana zaidi. Alijiepusha na uchafu na tabia zinazochafua wanaume, mpaka akaitwa "Al-Amin" (Mwaminifu) miongoni mwa watu wake, kwa sababu ya mambo mema ambayo Mwenyezi Mungu alimkusanyia. ([2])

Hii inathibitishwa na aliyoyasema mwanazuoni Ibn Khaldun alipoelezea kuwa miongoni mwa ishara za Manabii waliochaguliwa na Mwenyezi Mungu ni "kuwa na tabia njema na usafi kabla ya wahyi (ufunuo), na kujiepusha na kila jambo baya na uchafu. Hii ndiyo maana ya isma (Kulindwa na dhambi), kana kwamba amezaliwa na tabia ya kujiepusha na mambo mabaya na kuyachukia, kana kwamba yanaenda kinyume na asili yake." ([3])

Mtume (S.A.W) alilindwa kutokana na matendo mabaya kabla na baada ya utume. Kwa sababu hii, hakufanya chochote miongoni mwa matendo au tabia za kipindi cha ujinga. Imesimuliwa katika sahihi mbili "Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alikuwa akibeba mawe pamoja nao (Maqurqysh) kwa ajili ya Kaaba, na alikuwa amevaa nguo yake. Ami yake, Abbas, alimwambia: 'Ewe mpwa wangu, waonaje ukiweka kikoi chako (nguo ya kujifunga chini) mabegani mwako?' akavua na kuweka mabegani, kisha akaanguka na kupoteza fahamu. Na baada ya hapo, haukuwahi kuonekana uchi wa (S.A.W)." ([4]).

Na ikiwa hii ndiyo kauli ya wanazuoni na wanahistoria, basi Mtume (S.A.W) anasimulia jinsi Mwenyezi Mungu katika utoto wake akisema: "Nimejikuta nikiwa pamoja na vijana wa Kikuraishi, tukibeba mawe kwa ajili ya baadhi ya michezo ya vijana, sote tukiwa uchi. Nikaichukua nguo yangu na kuiweka shingoni mwangu, na nikibeba mawe juu yake. Nikiwa katika hali hiyo, nilikuja na kurudi nyuma, ghafla nikapigwa na mtu ambaye sikumwona, na pigo lake halikuwa kali, kisha akasema: 'Funga nguo yako.' Basi nikaichukua na kuifunga, kisha nikabeba mawe shingoni mwangu nikiwa nimevaa nguo, tofauti na wenzangu." ([5])

Kama alivyosema Al-Mawardi, hili ni "kutokana na amri ya kulindwa, ili akue katika hali hiyo na aizoee." ([6])

Imesimuliwa kutoka kwa Ali (R.A), amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akisema: "Sikuwahi kufikiria kufanya jambo baya lililokuwa likifanywa na watu wa kipindi cha ujinga isipokuwa mara mbili tu maishani mwangu, na katika zote mbili Mwenyezi Mungu alinilinda. Usiku mmoja, nilimwambia kijana mmoja kutoka Makka ambaye alikuwa akichunga mbuzi za watu wake: 'Angalia mbuzi wangu, ili niweze kulala usiku huu hapa Makka kama vijana wengine wanavyofanya.' Alikubali. Nilitoka, na nikaenda kwenye nyumba iliyokuwa karibu na Makka. Nikasikia nyimbo, dufu zikipigwa, na nai. Nikauliza: 'Hiki ni nini?' Wakasema: 'Fulani anamoa fulani.' Nikapumbazika na nyimbo na sauti hizo mpaka usingizi ukanichukua, na halikuniamsha isipokuwa joto la jua. Nikarudi, akaniuliza umefanya nini? nikamueleza. Usiku mwingine, nilimwambia vivyo hivyo, naye akafanya. Nilitoka, na nikasikia sauti kama hizo, na nikaambiwa kama nilivyokuwa nimeambiwa. Nikapumbazika na sauti hizo mpaka usingizi ukanishika, na na halikuniamsha isipokuwa joto la jua. Nikarudi kwa rafiki yangu, akaniuliza umefanya nini? nikasema: 'Sikufanya chochote.' Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akasema: 'Wallahi, baada ya hapo sikuwahi kufikiria kufanya jambo lolote baya katika yale wafanyayo na watu wa kipindi cha ujinga mpaka Mwenyezi Mungu aliponipa heshima ya utume.'"([7])

Simulizi na kauli hizi zinaonesha tabia njema na safari ya heshima. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimlinda na kumpa kinga. Al-Mawardi anasema: "Hizi ni hali za kinga yake kabla ya utume, na kumlinda kutokana na uchafu wa ujinga. Kwa hivyo, baada ya utume, atakuwa mtukufu zaidi na salama zaisi kutokana na uchafu. Hali hii inatosha kuthibitisha kwamba yeye ni miongoni mwa wasafi waliochaguliwa, na miongoni mwa wema, aliepushwa na kughafilika. Na yeye ni mmoja ya manabii wakubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Alichaguliwa tangu asili, na Mwenyezi Mungu alimtakasa kutokana na uchafu, ili watu wawe wepesi zaidi kumkubali na kumtii."([8])

Mtume (S.A.W) alikulia akiwa amepambika na kila tabia nzuri, akiepukana na kila sifa mbaya. Kila tabia njema alikuwa nayo kwa sehemu kubwa na fadhila kubwa zaidi, na kila tabia mbaya alijiepusha nayo. Kadhi Iyad anasema:

"Sifa zilizopatikana za tabia njema na maadili ya heshima, ambayo akili zote zimekubali kumsifia na kumtukuza yule ambaye ana tabia moja kati ya hizo, achilia mbali anayezidi, na ambazo sheria imezisifu zote, na kuamrisha, na kuahidi furaha ya kudumu kwa yule mwenye tabia hizo, na imezielezea baadhi yao kuwa sehemu ya utume, na ambazo huitwa tabia njema, yaani usawa katika nguvu na sifa za nafsi. Zote zilikuwa tabia za Mtume wetu (S.A.W) kwa ukamilifu wa hali ya juu na wastani hadi kufikia lengo lake kuu.” ([9])

Kuangalia hali ya Sayyidna Muhammad (S.A.W) tangu mwanzo wa maisha yake na Mwenyezi Mungu kumuandaa kwa ajili ya utume wake ni kama alivyosema Profesa Muhammad Rashid Rida: "Mwenyezi Mungu alimuumba akiwa na asili kamilifu ili kumtuma kwa dini ya asili. Alimuumba katika maumbile kamili ([10])  ili kumtuma kwa dini ya akili huru na yenye mtazamo. Alimkamilisha kwa maadili ya juu ili kumtuma kukamilisha maadili. Alimchochea kumchukia ushirikina na hadithi za uongo na uchafu wa watu wake tangu akiwa mdogo, na alimpendezeshea upweke, ili nafsi yake isizoee kitu chochote wanachoshindania kwa matamanio ya mwili au matendo mabaya, kama vile kumwaga damu, kuwaudhi watu, au matamanio ya dunia, kama vile kula mali za watu kwa njia isiyo halali; ili amtume kuwa mrekebishaji wa yale yaliyoharibika ndani ya wanadamu, na kuwatakasa kwa kumfuata, na kumfanya kuwa mfano bora wa binadamu ili kutekeleza sheria anazofunuliwa kutoka juu." ([11])

Kwa ujumla, pande za utukufu katika tabia ya Mtume (S.A.W) zilikuwa nyingi na za aina mbalimbali, na tabia, mwenendo na maisha yake yaikuwa moja ya pande hizi za utukufu, ambazo ziliwavutia watafiti na wasomi, na kuvuta akili zao na kushinda hisia zao. Walikiri utukufu wa hadhi yake, ukamilifu wa tabia yake, utukufu wa cheo chake, unyoofu wa akili yake, uzuri wa maneno yake, na uzuri wa kukutana naye, pamoja na sifa nyingine za kimaadili na fadhila za kitabia ambazo alipewa yeye peke yake, kiasi kwamba baadhi yao waliandika kitabu kinachoitwa: "Muhammad (S.A.W) Nabii wa Zama Zetu," kilichoandikwa na mwandishi wa Uingereza Karen Armstrong. Katika kitabu hicho, alifichua utukufu wa Mtume (S.A.W), hadhi yake, na cheo chake, na kwamba pande za utukufu katika tabia yake ndizo zinazomwezesha kuongoza ulimwengu katika wakati huu. Hakika, hali halisi ya ulimwengu na maumivu yake yasiyo na mipaka na dhulma, uadui, uharibifu, na ufisadi, inathibitisha haja ya tabia ya Mtume (S.A.W), ambaye aliweza kwa tabia yake nzuri, wito wake mzuri, na sifa alizopewa na Mwenyezi Mungu, kuuokoa ulimwengu kutoka katika dhambi, na kuukomboa kutoka kwa uchafu wa ushirikina na uchafu wa ujinga. Aliurudisha binadamu kwenye utu wao, na ulimwengu kwenye asili yake. Jambo ambalo linawajibisha upendo, heshima, na utukufu.

Hili lilibainishwa na maelezo ya Urwa bin Masud Ath-Thaqafi, akielezea jinsi Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) alivyokuwa miongoni mwa masahaba na wapenzi wake, akisema: "Wallahi, nimekwenda kwa wafalme, na nimekwenda kwa Kaysar, Kisra, na Najashi. Wallahi, sijawahi kuona mfalme ambaye masahaba wake wanamheshimu kama masahaba wa Muhammad (S.A.W) wanavyomheshimu Muhammad. Wallahi, hakukohoa chochote isipokuwa kilianguka katika mkono wa mmoja wao, akakipaka usoni na mwilini mwake. Na anapowaamrisha jambo, wanalikimbilia. Na anapotawadha, walikuwa wanakaribia kupigana wakigombea maji aliyotawadhia. Na anapoongea, wanashusha sauti zao mbele yake. Na hawamwangalii usoni kwa kumuheshimu." ([12])

 

 

 

 

 

 

 

 

 


([1])  Imepokelewa kutoka kwa  Al-Bukhari na Muslim: Sahih Al-Bukhari: Kitabu cha Tafsiri ya Qur’ani, Sura: “Mwanzo wa Wahyi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani,” (6/173), No.: (4953), Sahih Muslim: Kitabu cha Imani, Sura: Mwanzo wa Wahyi 19, Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, 19. Nambari: (160).

([2])  Sira ya Ibn Ishaq, uk. 78.

([3]) Historia ya Ibn Khaldun: Imehaririwa na: Khalil Shahada, (1/116), Dar Al-Fikr - Beirut, toleo la 2, 1408 AH - 1988 AD.

([4]) Imepokelewa kutoka kwa  Al-Bukhari na Muslim: Sahih Al-Bukhari, Kitabu cha Swala, Mlango wa kutokutamanika kuwa uchi wakati wa swala na nyakati nyinginezo, Na. (1/82).

([5]) Sira ya Mtume wa Ibn Hisham, kilichohaririwa na: Mustafa Al-Saqa, Ibrahim Al-Ibyari, na Abdul Hafeez Shalabi, (1/183), Kampuni ya Maktaba na Uchapishaji wa Mustafa Al-Babi Al-Halabi na wanawe katika Misri, toleo la 2, 1375 AH - 1955 AD.

([6]) Ishara za Utume: (1/211), Dar na Maktaba ya Al-Hilal - Beirut, chapa ya 1 - 1409 AH.

([7])  Ishara za Utume: (1/212).

([8])  Ushahidi wa Utume na Al-Bayhaqi: Kimehaririwa na: Dr. Abdul-Mutti Qalaji, (2/33), Dar Al-Rayyan for Heritage, 1st ed., 1408 AH - 1988 AD.

([9]) Al-Shifa bi-Ta’rif Huquq al-Mustafa cha Jaji Iyad: (1/96), Dar Al-Fikr Printing, Publishing and Distribution, 1409 AH - 1988 AD.

([10]) Machafuko         

([11]) Ufunuo wa Muhammad, Muhammad Rashid Rida, uk. 89, Dar Al-Kotob Al-Ilmiyyah - Beirut, toleo la 1, 1426 AH - 2005 AD.

([12])  Sahih Al-Bukhari: Kitabu cha Masharti, Mlango wa Masharti katika Jihad na Upatanisho na Watu wa Vita na Masharti ya Kuandika, (3/193), Na.: (2731).

Share this:

Related Fatwas