Hukumu ya Utoaji Mimba (Aborsheni)

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Utoaji Mimba (Aborsheni)

Question

Nini hukumu ya kutoa mimba?

Answer

Wanazuoni wa Fiqhi wamekubaliana kuwa ikiwa umri wa kijusi tumboni mwa mama yake umefikia siku mia moja na ishirini (120) — kipindi ambacho roho hupuliziwa — ni haramu kutoa mimba katika hali hiyo; kwani huko huchukuliwa ni kuua nafsi. Ama ikiwa kijusi hakijafikisha siku 120, inaruhusiwa kutoa mimba ikiwa kuna haja au dharura; kama vile daktari anayeaminika anapoamua kuwa kubaki kwa kijusi tumboni mwa mama kuna hatari kwa maisha yake au afya yake. Katika hali hiyo, inaruhusiwa kukitoa iwe kabla ya siku 120 au baada ya hapo; kwa ajili ya kulinda maisha ya mama na afya yake iliyo thabiti, na kuipa kipaumbele kuliko maisha ya kijusi ambayo bado hayajathibiti.

Maelezo

Wanazuoni wamekubaliana kuwa ikiwa kijusi kimefikisha siku 120, haramu kukitoa; kwani ni kuua nafsi. Mwenyezi Mungu anasema: { Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao} [Al-An'am: 151], na anasema: {Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki.} [Al-Isra: 33].

Ikiwa kijusi hakijafikisha siku 120, Wanazuoni wametofautiana kuhusu utoaji mimba:

Baadhi ya Wanazuoni wamesema ni haramu.

Baadhi wamesema ni makruhu (haipendezi).

Baadhi wamesema inaruhusiwa kukiwa na udhuru.

Tunapata faida kutokana na yaliyotangulia:

Msimamo wa "Idara ya kutoa Fatwa" ya Misri kuhusu kutoa mimba katika hali hii ni kwamba: Ikiwa daktari mwaminifu ataamua kuwa kubaki kwa kijusi kuna hatari kwa maisha au afya ya mama, inaruhusiwa kukitoa iwe kabla ya siku 120 au baada ya hapo; kwa ajili ya kulinda maisha ya mama na afya yake. Na kuipa kipaumbele kuliko maisha yasiyotulia ya kijusi.

Share this:

Related Fatwas